JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
wandugu,
..Jenerali angeweza kutumia mfano wa kijiwe chochote kile maana viko vingi, lakini ameamua kutaja kjiwe cha Saigon.
..kama mnavyoelewa JK amejitambulisha kama mwanachama wa kijiwe hicho.
..sasa katika makala hii, reading btn the lines, utaona Jenerali anadai nchi haisongi mbele kwasababu JK anaongozwa na mawazo na mitizamo toka kijiweni Saigon.
..kwa kweli JK anapaswa kujitafakari ktk kipindi hicho cha kuelekea mwisho wa utawala wake.
..Jenerali anaendelea zaidi hapa:
makala nzima ipo hapa:
http://raiamwema.co.tz/tumekuwa-watu-wa-‘fasta-fasta’-tunafundishwa-‘kuwa-wajanja’

Katika mahojiano ya kipindi cha KITIMOTO nilikumbana na mashabiki waliotoka Saigon ambao walikuwa wamekuja studio kusema upuuzi ule ule : Leta kocha wa kizungu, waweke vijana kambini miezi sita, tunawachapa hawa Waganda na Wakenya bila taabu yo yote, kisha tunakwenda kucheza Kombe la Dunia.
Nilichokuwa nashauri ni kwamba hatuna budi kufanya maandalizi katika ngazi kadhaa tukianzia na watoto wa umri wa miaka mitano na kuendelea kadri umri unavyopanda (U-14 ; U-17 ; U-21 na kadhalika) kwa kuwawekea madaraja hadi wawe wapevu, tukiwekeza bila kuchoka, tukitaraji kwamba vijana tulioanza nao wakiwa na miaka mitano watakuwa na miaka 20 baada ya miaka 15, na hawa wawe ndio tumaini la kwenda Kombe la Dunia.
Mashabiki wa Saigon wakapiga kelele : nani angojee miaka 15, bwana wewe ? Wewe leta kocha mzungu, weka vijana kambini…
Ajabu ni kwamba walikwisha kusahau kwamba tulikwisha kuwa na makocha wazungu (akina Celebic, Trautmann, Hudson nk) ambao hawakutupa matokeo kama ya akina Marijani Shaaban, Paul West Gwivaha na Joel Bendera). Kumbukumbu mara nyingi huwakimbia watu wasiojisumbua kuzitafuta.
..Jenerali anaendelea zaidi hapa:
Rais Jakaya Kikwete alipomuuliza Leodgar Tenga kama iwapo yeye (Kikwete) angemleta kocha wa kigeni na kumlipa, Tenga angetupeleka Ghana (mashindano ya CAN) na Tenga akajibu ‘Ndiyo'. Tulichokuwa tunakishuhudia ni ushabiki wa mkuu (kuamini kwamba kocha wa kigeni ndilo suluhisho) na soni ya mdogo (kulazimika kuitikia jambo asiloliamini kwa sababu kamera za TV zilikuwa zinatiririka).
Kocha mgeni alikuja, na mkuu akalipa, lakini hatukwenda Ghana, na inavyoelekea kwa muda mrefu ujao tutakuwa tunawasikia na kuwatazama wenzetu wanaokwenda CAN.
Hapa ndipo wanapokutana wale mashabiki wangu wa Saigon na wakuu wa nchi wanaoamini kwamba mambo yanaweza kufanywa haraka haraka na yakazaa matunda wakati hakuna mkakati endelevu wa kujenga hatua kwa hatua.
Tumekuwa watu wa " fasta fasta " na watu wa kuambiwa " kuwa mjanja " badala ya watu wa tafakuri na mipango inayolenga mbali.
makala nzima ipo hapa:
http://raiamwema.co.tz/tumekuwa-watu-wa-‘fasta-fasta’-tunafundishwa-‘kuwa-wajanja’