Kocha Jurgen Klopp atangaza kuachana na Liverpool mwisho wa msimu huu 2023-2024

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametangaza kuachana na timu hiyo mara baada ya msimu huu kwa kile alichosema kwamba ‘amechoka’.

Klopp alijiunga na Liverpool Oktoba akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani na mkataba wake wa sasa na timu hiyo unafikia mwisho mwaka 2026 lakini ameamua kuachana na timu hiyo kabla ya mkataba kufikia mwisho.

Akiwa na Liverpool, Klopp ameiwezesha timu hiyo kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019 na taji la Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2019-20 ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kubeba taji hilo baada ya miaka 30.

“Naelewa ni uamuzi unaoshitua watu wengi kwa wakati huu, pale unaposikia kwa mara ya kwanza lakini naweza kuelewa hilo au walau kujaribu kutoa ufafanuzi,” alisema Klopp.

“Napenda karibu kila kitu katika klabu hii, napenda kila kitu kuhusu jiji hili, napenda kila kitu kwa mashabiki wetu, naipenda timu, nawapenda maofisa, napenda kila kitu lakini bado nimeamua kuchukua uamuzi, hiyo ni kuwaonesha kwamba ni mimi mwenyewe ndiye niliyelazimika kuchukua uamuzi huu,” alisema Klopp.

“Hivyo ndivyo nilivyoamua, nawezaje kulisema hilo la kuishiwa nguvu, sina tatizo nilifahamu tangu awali kwamba kuna wakati nitalazimika kutangaza, lakini kwa sasa niko sawa,” alisema.

“Baada ya kuwa pamoja kwa miaka mingi na baada ya kushirikiana kwa muda mrefu na yale yote tuliyopitia pamoja, nimejenga heshima kwenu, mapenzi kwenu yamekuwa, huo ndio ukweli,” alisema Klopp.

Liverpool chini ya Klopp imefanikiwa kubeba karibu mataji yote makubwa kuanzia Ligi ya Mabingwa Ulaya, EPL, Uefa Super Cup na Kombe la Dunia la Fifa.
 
UINGEREZA: Kocha wa Klabu ya Liverpool, Jürgen Klopp (56) ametoa taarifa ambayo inaelezwa kuwashtua Mashabiki wake akieleza kuwa ataondoka Klabuni hapo baada ya kumalizika kwa msimu huu.

Klopp ambaye amekuwa Meneja wa Liverpool tangu mwaka 2015, amebakiwa na Mkataba wa kuitumikia Klabu hiyo hadi mwaka 2026, lakini amewambia Wachezaji ataondoka mapema kabla ya kufika tamati ya Mkataba wake.

Chini ya Klopp, Liverpool imewahi kutwaa Taji la Ligi ya Mabingwa, Ligi Kuu, Makombe ya FA, Ligi na Kombe la Dunia la Vilabu.

===========

Jürgen Klopp has stunned Liverpool and the world of football by announcing he is to leave the club at the end of the season. The 56-year-old attributed his shock decision to “running out of energy”.

Klopp has been Liverpool manager since 2015 and is under contract until 2026 but, in an announcement via the club’s media channel, has revealed he will stand down two years early. The players were told by Klopp before training on Friday.

The news will come as a devastating blow to Liverpool supporters – who idolise the charismatic German – and also to the squad and the owner, Fenway Sports Group, whose appointment of the former Borussia Dortmund coach transformed the club’s fortunes.

Liverpool insist no one has been approached about the possibility of replacing Klopp but the former midfielder Xabi Alonso, who has guided Bayer Leverkusen to the top of the Bundesliga, is likely to be under consideration.

Under Klopp Liverpool have won the Champions League, Premier League, FA Cup, League Cup and Club World Cup. They reached another Carabao Cup final on Wednesday and have a five-point lead over Manchester City at the top of the Premier League, albeit having played one game more.

Klopp said he had told the owners in November of his intention to leave. “I can understand that it’s a shock for a lot of people in this moment, when you hear it for the first time, but obviously I can explain it – or at least try to explain it,” he said.

“I love absolutely everything about this club, I love everything about the city, I love everything about our supporters, I love the team, I love the staff. I love everything. But that I still take this decision shows you that I am convinced it is the one I have to take.

“It is that I am, how can I say it, running out of energy. I have no problem now, obviously, I knew it already for longer that I will have to announce it at one point, but I am absolutely fine now. I know that I cannot do the job again and again and again and again.

“After the years we had together and after all the time we spent together and after all the things we went through together, the respect grew for you, the love grew for you and the least I owe you is the truth – and that is the truth.”

Klopp said there were no underlying health issues for his departure. “I am OK. I am healthy, as much as you can be at my age. I told the club already in November. I have to explain a little bit that maybe the job I do people see from the outside, I’m on the touchline and in training sessions and stuff like this, but the majority of all the things happen around these kind of things.

THE GUARDIAN
 
Yaani kama kuna wakati au siku mashabiki wa manchester zote mbili, man u na man city kuwa katika furaha kupita kiasi ni leo,

Baada tu ya kusikia uamuzi wa ghafla wa kocha wa Liverpool Jurgen klopp kwamba anaondoka Liverpool mwishoni mwa msimu, jiji zima limeripuka kwa furaha,
Kwanini lakini?
Au jamaa amewatesa sana kwenye kipindi cha miaka tisa?
 
Hata uwe mshabiki wa Everton, kama ni mpenzi wa kandanda safi na sio matokeo tu huwezi kufurahishwa na habati hii

Sent from my SM-A137F using JamiiForums mobile app
 
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametangaza kuachana na timu hiyo mara baada ya msimu huu kwa kile alichosema kwamba ‘amechoka’.

Klopp alijiunga na Liverpool Oktoba akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani na mkataba wake wa sasa na timu hiyo unafikia mwisho mwaka 2026 lakini ameamua kuachana na timu hiyo kabla ya mkataba kufikia mwisho.

Akiwa na Liverpool, Klopp ameiwezesha timu hiyo kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019 na taji la Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2019-20 ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kubeba taji hilo baada ya miaka 30.

“Naelewa ni uamuzi unaoshitua watu wengi kwa wakati huu, pale unaposikia kwa mara ya kwanza lakini naweza kuelewa hilo au walau kujaribu kutoa ufafanuzi,” alisema Klopp.

“Napenda karibu kila kitu katika klabu hii, napenda kila kitu kuhusu jiji hili, napenda kila kitu kwa mashabiki wetu, naipenda timu, nawapenda maofisa, napenda kila kitu lakini bado nimeamua kuchukua uamuzi, hiyo ni kuwaonesha kwamba ni mimi mwenyewe ndiye niliyelazimika kuchukua uamuzi huu,” alisema Klopp.

“Hivyo ndivyo nilivyoamua, nawezaje kulisema hilo la kuishiwa nguvu, sina tatizo nilifahamu tangu awali kwamba kuna wakati nitalazimika kutangaza, lakini kwa sasa niko sawa,” alisema.

Liverpool chini ya Klopp imefanikiwa kubeba karibu mataji yote makubwa kuanzia Ligi ya Mabingwa Ulaya, EPL, Uefa Super Cup na Kombe la Dunia la Fifa.
Kwa miaka aliyokaa hapo nadiriki kusema hana mafanikio makubwa aliyopata kama mwenzie pep
 
Back
Top Bottom