ha ha ha, yaani hapo umenikumbusha uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam, kipindi kile Ditopile ni RC wa Dar, kitu kama 1994 au 95 hivi, Lutta Nelson alipogombea, Ditopile akaenda kupoiga kampeni akasema sio mnachagua watu hata Dar hawaijui, yaani hata tongotongo za kijijini kwao hazijawatoka, basi Lutta zengwe likamkuta akatoswa kwenye uchaguzi
sijawahi ona kiongozi yeyote toka Saigoni aliyepata kutuletea maendeleo iwe Dar, Mpirani au kitaifa, angalia KK alikuwa meya wa jiji miaka mingi na hakuna la maana alilofanya, Ditopile yeye ni uzinzi mpaka akawa anaitwa ukimuona mzurimzuri mtupie, angalia Ismail Aden Rage, tangu katibu TFF mpaka kwenye timu yangu niipendayo ya Simba, hamna jipya, sana sana atajifanya yeye mtoto wa njini anajua fitina wakati hamna maendeleo, JK nadhani sina la kusema, wote mnajua amekuwa rais wa aina gani,
kifupi members wa Saigon wamefanikiwa sana kupata vyeo mbalimbali hapa bongo na wanajua sana kuwafanyia fitina wenzao na kuwachafua majina lakini inapokuja kwenye sual la uongozi, wameprove failure vibaya