Yule Dr. Mwaka nilimuona siku 1 anahojiwa Clouds Tv akasema yeye alikua anafanya shughuli za kuwawekea wanawake dawa za 'kalikiti'kichwani na shughuli kama hizo nikasema tu hiiiiiiiiiiiiiiii,mwafaa ila hapo nje ya nyumba yake kuna hummer 3,Range rover,V8 nikajua jamaa wanapiga pesa sana hawa no wonder Hamisi Mikopo 'kigwa' aliona ka wivu kiaina hahah.Hafu Hawa kina Dr ndondi waliibuka enzi za kina Jakaya, Mara Dr Rahabu, Mara Dr. Mwaka Yani mtu anajiita Dr na hajaenda kusoma bachelor ya medicine Muhimbili na serikali Ina mchekea tu.
Kuna kipindi yalitangazwa mafuta ya ubuyu kua ni mafuta bora saana watu wakayanunua balaa mpk mafuta ya alizeti yakaanza kukosa soko maaara paap mkemia mkuu anakuja kutangaza mafuta ya ubuyu yana sumu.Sumu ya Aflatoxin inatokea tu ikiwa mahindi yalivunda, kama yalikauka vizuri na hayakuingia maji mahindi hayana shida kabisa. Pia sumu hiyo inaua haraka, otherwise ungeona watu wanaanguka kila mahali kwa sababu ya kula ugali.
Sawa inabidi tuchukue tahadhari lakini sio kweli kuwa unga wa dona una sumu.
Jamaa anakwambia Ukichukua Coca-cola ukaichemsha kuna vitu vinabaki kwny sufuri,zile ni sumu.Ndodi bhana alikuwa bonge la tapeli unauziwa unga hata hautibu.
KAMA YUPO AJE HUMU,Dokta Ndodi hajafariki...yupo chimbo tu anaendeleza tiba mbadala.
Ndiye aliye promote matumizi ya unga wa dona badala ya sembe.
Si ndie alikuwaga na kipindi redio free au sie yeyeNakumbuka miaka ya kumi iliyopita huyu jamaa alikuwa anatangaza Sana Tiba mbadala. Maana alikuwa na swaga sio za nchi hii?
Anakwambia:
Matumizi ya sukari siyo mazuri. Hizi soda tunazokunywa na sukari tunazoweka kwenye chai zinaharibu afya zetu badala yake inatakiwa utumie asali.
Kwanza asali siyo tamu kama unabisha lamba asali halafu sikilizia ule utamu wake mwishoni utaona asali ni chungu.
Kwahiyo jitahidini kutumia asali, achana na sukari achana na soda.
Kuna member humu akasema akiwa mgahawani mkoa fulani bwana ndodi akiwa na kitambi kimeiva alinunua ugali wa sembe(unga anaokataza), kuku nusu (wa kizungu na kaungwa mafuta anayokataza), alivyomaliza akashushia na fanta baridi.
GoodMmmmmmhmn so mababu na bibi zetu ambao wamekula dona maisha yao yote hiyo Aflatoxin haikuwapo au ndio mzungu ni kama MUNGU anachosema na asikilizwe?!
Unajua madhara ya kula masembe wewe?!
Unga wa dona unbalance virutubisho na ndio maana hata wagonjwa wa kisukari wanatakiwa kutumia huo na sio ule wa sembe. Sembe sio nzuri kwasababu inasababisha mwili kuzalisha kiwango kikubwa sana cha sukari inayotokana na wanga wake. Na mwishowe ndio watu wanakuwa na mifuta mwilini na haieleweki inatokea wapi.
Mkuu mlilipa hiyo gharama ama?NENDA PALE MAGOMENI MWEMBE CHAI ALIKUWA NA KITUO CHAKE KIKUBWA TU
Tulimpeleka mtoto kwake akiwa anasunbuliwa na minyoo akatuambia matibabu yake ni laki tisa......yani 900k au kwa jina lingine mia tisa elfu
Mkuu mlilipa hiyo gharama ama?
yupo eneo la Mawambamawili kituo kinaitwa Ndondi kama jina lake lilivyo..Nakumbuka miaka ya kumi iliyopita huyu jamaa alikuwa anatangaza Sana Tiba mbadala. Maana alikuwa na swaga sio za nchi hii?
Ni yeyeSi ndie alikuwaga na kipindi redio free au sie yeye
Alitangaza kutibu kisukari..aliwapiga watu hela
Now atakuwa anahesabu pesa zake kimya kimyaa..
Kisukari kikizidi kushika Kasi
haaahaaahaa du we jamaa ndio umekuja na ushahidi wa picha kabisa. hapo katumia urefu lkn kamaanisha ufupi ndio maana aliweka alama hii '....'Jamani watanzania hebu tuacheni UONGO uliotukuka, ndodi ni mfupi wa kimo hizi hadithi mnatoa wapi kudanganya wanaJF?
View attachment 1592014View attachment 1592015
haaaahaaaahaaa hapo sasa unachemsha unataka nn kama sio umbea. mwee kama kuliwa tumeliwa sn na ndodiJamaa anakwambia Ukichukua Coca-cola ukaichemsha kuna vitu vinabaki kwny sufuri,zile ni sumu.
Sasa unajiuliza unachemsha Coca ili upate nini?Maana haikutengenezwa ili ichemshwe.
Pili inayobaki chini kwny ile sufuria si ni ile sukari ya kiwandani 'industrial sugar' au?
Ndodi anakwambia hio ndio ile sumu niliyokua nakwambia na ndio maana ukichukua msumali ukauweka kwny Coca baada ya siku kadhaa utaukuta na kutu au ukimimina Coca kwny choo kilichojaa inaenda inasafisha vzr kabisaaa.
Hahah jamaa aliwezaga kutupiga Saundi sana aisee.
mwenyewe huyoSi ndie alikuwaga na kipindi redio free au sie yeye
Sio kweli mkuu. Unapotosha watuUnga wa dona ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).
Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.