Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,990
Nyangumi, hicho ndicho CCM imejaribu kufanya.. nacho ni kushika hatamu na utamu wa nchi!! Wao wanajenga, wao wananunua, wanalima na kuvuna!! Mwananchi wa kawaida hahitaji kufanyiwa kila kitu. Tunachohitaji ni kujengewa mazingira mazuri ambapo soko linatuamulia nani afanye nini. Nimeshaeleza toka huko nyuma ni nini wapinzani wafanye. La kwanza, wawe majasiri kusema:
a. Upinzani ukichukua madaraka itaundwa tume huru itakayochunguza mali zote ambazo viongozi waliopita walichuma wakiwa madarakani na kuoanisha na mapato yao. Wale itaoonekana mapato yao hayawiani na mali zao basi mali zao zitafilisiwa! Wasema watalifanya hilo ndani ya miezi sita ya mwanzo ya utawala wao.
b. Wapinzani wawaambie wananchi kuwa kila kijana wa Kitanzania aliyefaulu kwenda chuo Kikuu Serikali itagharimia nusu ya ada zao na matumizi. Anayepata daraja la kwanza kila mhula analipiwa 75% Wanaoenda shahada ya uzamili watalipiwa 75% na wa shahada ya Udaktari 100% Hii ni kuonesha kuwa upinzani unatilia maanani elimu. Na kwenye hilo la Elimu Wapinzani waseme chini ya uongozi wao, Elimu ya Msingi hadi ya Sekondari (O'Level) itakuwa ni ya bure!
Pia waamue kusema kuwa yeyote anayetaka kusomea Udaktari (Utibabu) analipiwa gharama zote! (nafikiri CCM inafanya kitu kama hiki).
c. Wapinzani waweke wazi kuwa pindi wakichaguliwa, watasitisha mara moja mikataba yote ya Nishati na Madini na kurenegotiate na kampuni yoyote ambayo inataka kuendelea kufanya kazi Tanzania. Katika kufanya hivi wawaambie wananchi kuwa Serikali hiyo mpya itawachunguza viongozi wote waliohusika na mikataba hii na wale ambao walinufaika kwa namna yoyote ile watafikishwa mahakamani kwa ufujaji wa mali ya umma.
d. Wapinzani wawahakikishie wananchi kuwa Watadumisha Muungano wetu na umoja wetu wa kitaifa! Hakuna mabadiliko yoyote ya mfumo au utendaji kazi wa Muungano yatakayofanywa pasipo ridhaa ya wananchi.
Hayo ni machache ya kuanzia!
na Mwandishi Wetu
MWANDISHI wa habari mwandamizi nchini, Makwaia wa Kuhenga, ameukataa wadhifa wa Katibu Mwenezi wa Chama cha Ustawi Tanzania (CHAUSTA), kama ilivyotangazwa na mwenyekiti wa chama hicho, James Mapalala na kunukuliwa na gazeti moja la kila siku nchini.
Mimi ni mwanachama mwanzilishi wa CCM, na sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha ushindani mpaka leo, alisema Makwaia katika taarifa yake.
Aliendelea: Mwaka 1987 jina langu lilikubaliwa na CCM chini ya Uenyekiti wa Mwalimu Nyerere kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC). Aidha, chama katika ilani yake ya uchaguzi ndani ya chama mwaka huo, kilinitaja kuwa kada wake wa mstari wa mbele.
Nilipoingia CCM, niliingia kufuata madhumuni na itikadi yake. Ingawa CCM imelegalega kimsingi katika itikadi yake, sijaona sababu ya kukihama kwenda CHAUSTA au chama chochote kingine. Nitapambana ndani ya chama changu cha CCM kuhakikisha kinarejea katika itikadi yake asilia, ambayo ni kukidhi maslahi ya wananchi walio wengi wakulima na wafanyakazi wa nchi hii, aliongeza.
Makwaia alisema, alishtuka na kushangaa kusoma gazeti kuwa ameteuliwa na Mapalala kuwa Katibu Mwenezi wa chama hicho wakati kwanza si mwanachama wake na wala hakuwa na habari ya mkutano mkuu wa CHAUSTA hapo Magomeni.
Kama ninavyoandika wakati wote katika makala zangu, nchi yetu inahitaji vyama vya upinzani kupata ushindani na uongozi bora nchini. Lakini kama mwendo wa upinzani ni kuwateua watu katika nyadhifa za vyama, watu ambao kwanza siyo wananchama wa chama husika, basi hatufiki! alisema.
mwanasiasa nafikiri kwa maneno mengine ni kuwa tunajua tunahcokitaka (kwenda Dodoma) lakini hatutaki kupanda gari la kwenda Dodoma, na badala yake tunajitahidi kujipa matumaini kuwa gari la Mtwara linaweza kutufikisha Dodoma! Ni kweli tunaweza kufika Dodoma kwa kupitia Mtwara (inategemea tunatoka wapi) Ukweli wa mambo ni kuwa Dodoma itaendelea kuwa katikati ya nchi, na kama unatoka Dar kwenda Dodoma basi njia nyepesi bila ya shaka ni kupitia Morogoro!
Tunataka kujenga Taifa la kisasa, la kidemokrasia na lenye maendeleo lakini hatutaki kufanya vile vitakavyotufikisha huko!
Lunyungu, sijasema wapinzani hawakubaliki, nimesema hawajajifanya waonekane wanahitajika (relevance). Ndio maana swali la msingi la mada hii hapa ni "Wapinzani ni Wakombozi"? Ni mpaka wafanye watu wawaone kweli wanawahitaji wasitarajiekupata viti vingi bungeni. Jinsi gani wanajifanya kuwa wanahitajika?
Kwa maoni yangu, siyo kwa kuonesha mapungufu ya CCM au serikali yote, kwani kila mtu anayajua na matatizo ya wananchi chini ya serikali ya CCM ni dhahiri. Huhitaji kuwa mwanasayansi kuweza kuyafahamu.
Mimi na wengine ambao tunaangalia kutoka nje (ya CCM na Upinzani) bado hatujaona mvuto wa upinzani zaidi ya kuipinga CCM. Upinzani lazima uwe zaidi ya kupinga na kukosoa, lazima wawe wanatuonesha kuwa wanaweza kuongoza na kutawala. Hadi hivi sasa binafsi sijawa impressed kuwa Tanzania inaweza kuwapa uongozi wa nchi wapinzani na matatizo yetu yatakwisha. Matatizo ya Kenya yamekwisha sababu NARC wako madarakani? Je, matatizo ya Zambia yamekwisha? vipi Malawi? Wapinzani watafanya nini zaidi kuliko kile ambacho kinaweza kufanywa au kimefanywa na CCM.
Eric.. na wanaweza kupewa nchi? kusimamia taasisi zote? haya nipe line up ya serikali ya Wapinzani. Kama chama ni Chadema nani anaweza kuwa Rais, Waziri Mkuu, Makamu, Wakuu wa Mikoa, ma DCs, n.k.. just fill 100 positions..!