Je, wapinzani ni wakombozi?

Nimeirudisha mada hii kwa maana inaendana na majibu ya Mhe. Zitto kuhusu utayari ywa Chadema kupewa nchi na kuiweza kuingoza vizuri. Mhe. Kabwe amesema kuwa Chadema wakipewa nchi sasa hivi wanaweza kuiongoza, lakini kuiongoza vizuri hawataweza!! Hayo yalikuwa ni maoni yangu pia mwanzoni mwa mada hii. Je chama cha CUF kikipewa nchi sasa hivi kitaweza kuiongoza nchi vizuri? Haitoshi tu kutaka CCM itoke madarakani wakati hatuna Chama mbadala ambacho kinaweza kukabidhiwa nchi na sisi tukaendelea kulala usingizi mnono bila ya kushangaa nini kitatokea. Kama Chama chenye uzoefu wa karibu miaka 50 kinaweza kuvurunda kiasi hiki, hivi vyama vya miaka 15 vinataweza kufanya vizuri kweli?
 
MKJJ:
Sina uhakika kuwa umri wa chama ni kigezo kizuri cha kuona kuwa kitaweza kuongoza vizuri au la. Angalau mifano haituambii hivyo. Chama cha John Kufour nadhani kilikuwa na umri mdogo sana ukilinganisha na cha Rawlings kilichoshindwa. Lakini ni ukweli kwamba chama cha Kufour kimeweza kuleta maendeleo ya ajabu kama vile Ghana ndiyo kwanza ilipata uhuru katika miaka kumi aliyoongoza. Vilevile kilichokuwa chama tawala Senegal kabla ya chama cha Rais Wade kiliongoza ile nchi kwa zaidi ya miongo minne, lakini maendeleo yaliyopatikana katika miaka kumi ya utawala wa chama cha Wade kila mtu ni shahidi. Mfano mwingine wa karibu zaidi ni Kenya. Pamoja na matatizo yote ya chama cha NARC, ni ukweli usiopingika kuwa wakenya wengi leo wasingependa warudi katika enzi za KANU. Kwa hivyo umri wa chama cha siasa katik hili sidhani kwamba ni hoja.

Sikubaliani na Zito anaposema kuwa chadema ikipewa nchi sasa hivi haitaongoza vizuri. Bahati mbaya sijasikiliza mazungumzo yako na Zito, lakini kama kweli alisema hilo na kama viongozi wote wa chadema wanafikiri hivyo, basi kuna tatizo. Kuna ugonjwa unaitwa hypochondriasis. Huu ni ugonjwa lakini sio wa kimwili bali wa kisaikolojia. Ni pale mtu anapohisi anaumwa wakati haumwi, na madaktari wakimwambia haumwi haamini kuwa haumwi. Sasa huenda Zitto na viongozi wengine wa chadema wana huu 'ugonjwa'. Lakini mimi kama mwanachama wa kawaida wa chadema najua kabisa tunaweza kuongoza tena vizuri sana kuliko hao ccm kwa sababu chadema ina dira na sera bora zaidi kuliko CCM na ina watu wenye elimu ya kutosha na uzoefu wanoweza kuongoza serikali. Yeye mwenyewe Zito ana uwezo wa kushika nafasi yeyote katika serikali ikiwemo ya urais; bahati mbaya inaonekana hajui au ana-underestimate uwezo wake.

Nafikiri pia kuna tatizo la kufikiri kuwa chama kingine kikiingia madarakani basi kila kitu kitabadiliko. Kinachobadilika ni sera (policies) na baadhi ya sheria na viongozi wa kisiasa. Watendaji wengi wa serikali watabaki kuwa walewale. Jeshi litabaki kuwa lilelile. Polisi ni walewale. majengo na ofisi zilezile. magari yaleyale isipokuwa yatapunguzwa, n.k. Sasa sijui hii dhana kwamba tutashindwa kuongoza inatoka wapi.

Tatizo kubwa la vyama vya upinzani so kukosa uwezo wa kuongoza kwa maana ya dira, sera na mikakati ya kuongoza nchi. Isipokuwa ni kukosa taswira ya kuweza kuchagulika. Na bahati mbaya katika nchi zetu taswira ya chama ni kigezo kikubwa cha kuweza kuchaguliwa kuliko sera na mikakati ya chama ya kuongoza. Ingekuwa wananchi wanaangalia sera na uwezo wa viongozi CCM ingekwishafukuzwa madarakani siku nyingi. Ni katika Tanzania pekee ambapo Rais anaweza kusema uongo zaidi ya mara tatu na wananchi wakaona ni jambo la kawaida. Hili ndio jambo la kufanyiwa kazi na vyama vya upinzani. Kuwafanya wananchi waanze kujali mambo makubwa kama sera za maana dhidi ya mundane issues kama sura za viongozi na ukongwe wa chama.

It was practically wrong and politically damaging for Zito to say that we (chadema) cannot lead the country better than CCM, if he truly made this remark, which I doubt!!!! Clearly, there are things you can't say in politics however true they may be!
 
It was practically wrong and politically damaging for Zito to say that we (chadema) cannot lead the country better than CCM, if he truly made this remark, which I doubt!!!!

Majibu haya niliyatarajia tu! But mwanasiasa, assuredly I tell you, watanzania wengi wana doubt na vyama hivi vya siasa; wamechanganywa mara nyingi na hoja zenye kugubikwa na mikanganyiko toka kwa viongozi wa vyama hivi.

Yes, mimi sio CCM lakini si CHADEMA, na pia ni kwamba sio mwanachama wa PPT Maendeleo; ni kwakuwa nina wasiwasi na uwezo wa vyama hivi ambavyo tulitarajia viwe mbadala vinavyoongozwa na majibu yanayotofautiana toka kwa viongozi wa vyama hivi.

Mifano ni mingi sana; CUF wana experience ya suala hili na naamini kama kungekuwa na msemaji mwenye kuangukia CUF ningemdondoshea data alizowahi toa Tambwe kabla hajarejesha majeshi yake Nambari Wani. Ebana tunahitaji kuhakikishiwa uwezo wa vyama hivi kuiongoza taifa tusije jutia maamuzi ya kumg'oa CCM bila kuwahoji mara mbilimbili.

Sibishi; umri wa chama si hoja kubwa na wala haisumbui akili, kinachotakiwa kwa chama chochote ni viongozi wa chama husika (hata kampuni au NGO) kuhakikisha majibu yenu daima yanafanana au hata yanashabihiana.

Ni vema kuna ile thread inayowahusu CHADEMA na suala la majimbo etc; Mnyika is doing great and Eric Ongara. Hawa wametoa majibu mengi kwa maswali ya Mkandara hadi wananivuta. Lakini... Hebu kupitia kule au hapa tutoe wasiwasi juu ya uwezo wenu kuiongoza Tanzania iwe yenye neema.

Mpaka kieleweke!
 
MKJJ:
Sina uhakika kuwa umri wa chama ni kigezo kizuri cha kuona kuwa kitaweza kuongoza vizuri au la. Angalau mifano haituambii hivyo. Chama cha John Kufour nadhani kilikuwa na umri mdogo sana ukilinganisha na cha Rawlings kilichoshindwa. Lakini ni ukweli kwamba chama cha Kufour kimeweza kuleta maendeleo ya ajabu kama vile Ghana ndiyo kwanza ilipata uhuru katika miaka kumi aliyoongoza. Vilevile kilichokuwa chama tawala Senegal kabla ya chama cha Rais Wade kiliongoza ile nchi kwa zaidi ya miongo minne, lakini maendeleo yaliyopatikana katika miaka kumi ya utawala wa chama cha Wade kila mtu ni shahidi. Mfano mwingine wa karibu zaidi ni Kenya. Pamoja na matatizo yote ya chama cha NARC, ni ukweli usiopingika kuwa wakenya wengi leo wasingependa warudi katika enzi za KANU. Kwa hivyo umri wa chama cha siasa katik hili sidhani kwamba ni hoja.

Sikubaliani na Zito anaposema kuwa chadema ikipewa nchi sasa hivi haitaongoza vizuri. Bahati mbaya sijasikiliza mazungumzo yako na Zito, lakini kama kweli alisema hilo na kama viongozi wote wa chadema wanafikiri hivyo, basi kuna tatizo. Kuna ugonjwa unaitwa hypochondriasis. Huu ni ugonjwa lakini sio wa kimwili bali wa kisaikolojia. Ni pale mtu anapohisi anaumwa wakati haumwi, na madaktari wakimwambia haumwi haamini kuwa haumwi. Sasa huenda Zitto na viongozi wengine wa chadema wana huu 'ugonjwa'. Lakini mimi kama mwanachama wa kawaida wa chadema najua kabisa tunaweza kuongoza tena vizuri sana kuliko hao ccm kwa sababu chadema ina dira na sera bora zaidi kuliko CCM na ina watu wenye elimu ya kutosha na uzoefu wanoweza kuongoza serikali. Yeye mwenyewe Zito ana uwezo wa kushika nafasi yeyote katika serikali ikiwemo ya urais; bahati mbaya inaonekana hajui au ana-underestimate uwezo wake.

Nafikiri pia kuna tatizo la kufikiri kuwa chama kingine kikiingia madarakani basi kila kitu kitabadiliko. Kinachobadilika ni sera (policies) na baadhi ya sheria na viongozi wa kisiasa. Watendaji wengi wa serikali watabaki kuwa walewale. Jeshi litabaki kuwa lilelile. Polisi ni walewale. majengo na ofisi zilezile. magari yaleyale isipokuwa yatapunguzwa, n.k. Sasa sijui hii dhana kwamba tutashindwa kuongoza inatoka wapi.

Tatizo kubwa la vyama vya upinzani so kukosa uwezo wa kuongoza kwa maana ya dira, sera na mikakati ya kuongoza nchi. Isipokuwa ni kukosa taswira ya kuweza kuchagulika. Na bahati mbaya katika nchi zetu taswira ya chama ni kigezo kikubwa cha kuweza kuchaguliwa kuliko sera na mikakati ya chama ya kuongoza. Ingekuwa wananchi wanaangalia sera na uwezo wa viongozi CCM ingekwishafukuzwa madarakani siku nyingi. Ni katika Tanzania pekee ambapo Rais anaweza kusema uongo zaidi ya mara tatu na wananchi wakaona ni jambo la kawaida. Hili ndio jambo la kufanyiwa kazi na vyama vya upinzani. Kuwafanya wananchi waanze kujali mambo makubwa kama sera za maana dhidi ya mundane issues kama sura za viongozi na ukongwe wa chama.

It was practically wrong and politically damaging for Zito to say that we (chadema) cannot lead the country better than CCM, if he truly made this remark, which I doubt!!!! Clearly, there are things you can't say in politics however true they may be!
MWANASIASA!
Zito amelitamka hilo tena kwa Bahati mbaya mwishoni katika kufunga mahojiano,ninasema kwa Bahati mbaya kwani inaelekea muda ulikuwa anakimbizana nao na angeweza kujibu swali la MKJJ kwa kifupi kwamba si kweli au kweli Lakini alitoa na ufafanuzi,Kama unavyosema kuna vitu katika siasa huwezi kuongea nje bali unatakiwa ufanye marekebisho mkiwa wahusika tu,Hii sijui itapokelewaje na viongozi wake wajuu na wanachama wengine,kwa nielewavyo mimi wewe ni moja kati ya wanachama waliowengi watakaolipokea kwa mtazamo tofauti.
Halafu anaposema hawakuwa tayari kuongoza Nchi vizuri sasa kwanini walipoteza gharama nyingi Kufanya kampeni kwa ajili ya mgombea wao?Kama hilo walilijua kwanini hawakuunganisha nguvu na vyama vingine ili kuleta changamoto ya kweli katika kinyang'anyiro hicho cha mwaka 2005? maneno ya Mh. Kabwe yanapingana na ya mwenyekiti wake kwamba walishinda Lakini waliibiwa kura Hivi kama hawakuwa tayari kuwaongoza watanzania vizuri na kwa ufanisi hawaoni kwamba watanzania walio wengi nao waliliona hilo ndiyo maana waliwanyima kura zao?Sijui wenzagu mtaielewaje kauli yake hiyo?
 
MKJJ!
Mahojiano yalikuwa mazuri na hata yeye Mh.KabweZitto ameeleza vizuri tu lakini nafikiri kuna maswali mengine yanayofikishwa kwake awe muangalifu kuyajibu kwani yanaweza badala ya kukijenga chama chake yakakibomoa na kwenda kinyume na dhamira yake.Siasa ni Vita na Adui wanatumia udhaifu na mapungufu ya kila chama ,sera za chama na wahusika wa chama husika(pinzani au mbadala) kushinda vita hiyo.Utumiaji mzuri wa mapungufu ya mpinzani wako (Chama,sera na mgombea kama binaadamu)kisiasa ni silaha kubwa ya maangamizi katika anga la siasa.
 
Mwanasiasa,

Nakubaliana na wewe mia kwa mia. Kuna kitu kinamsumbua Zitto nje ya yote aliyoyasema. I mean kila statement yake inazidi kunitia wasiwasi zaidi. Na hasa mahojiano yake na MJJ kuna vipande kaboronga kama vile mtu anayetafuta support ya wananchi zaidi ya Chadema. Nina mashaka kama hayakutokea yale yaliyomkuta Harper.
 
Mkandara!
Mbivu na mbichi ziatajulikana na wakati utasema, kinachotakiwa ni kuvuta subira.
 
Mwakijiji,

Nakushukuru tena kwa kurejesha hii hoja ya "wapinzani ni wakombozi".

Nimesoma hoja za mwanasiasa, nakubaliana nami. Lakini kwa bahati mbaya nami sijasikiliza mahojiano ya Zitto. Huku nilipo ni ngumu ku-down load mahojiano. Nitachangia hoja hii nikishayasikiliza mahoajiano husika.

Lakini dhana ya kwamba wapinzani hawana uzoefu wa kuungoza sikubaliani nayo kabisa. Nitachambua kwa facts baada ya kusikiliza!

Dhana hii ilitumika sana pale Ubungo katika hatua za awali ikisemwa kwamba Mnyika hana uzoefu Keenja ana uzoefu.

Kwa kweli wakati ule nijibu dhana hii kwa maswali ambayo naamini yanaweza kutumiwa pia katika muktadha wa Taasisi(ikiwemo CHADEMA)

1. Hivi tunataka UZOEFU au UZEEFU? Uzoefu is a very subjective term. Watu wengi wanafikiri uzoefu ni miaka! Unaweza kuwa na miaka michache ukawa na uzoefu zaidi ya mwenye miaka mingi(wachambuzi wajadili)

2. Hivi tunahaja ya kuwa na UZOEFU au MZOEFU wa KUHARIBU? Kati ya mzoefu wa kuharibu na asiyekuwa na uzoefu wa kuharibu yupi bora? Je CCM wana uzoefu wa nini?

3. TANU iliingia madarakani ikiwa na miaka michache kuliko serikali ya mkoloni, je TANU ilipaswa kuachwa ili MZOEFU mkoloni aendelee? Miaka ya serikali ya TANU takribani 15 na ile ya MZOEFU CCM ya kuanzia 1977 mpaka 2007(30) ipi ilikuwa bora? Kwa nini uzoefu wa CCM usiwe mzuri kuliko TANU kimaadili, kukua kwa uchumi, elimu na tofauti ya pengo kati ya masikini na matajiri?

4. Hivi UZOEFU haupandi na kuanza kuporomoka? (In other words is experience not subjective to the law of diminishing return?)

5. UZOEFU hauzai URASIMU na UHAFIDHINA wa kukataa mabadiliko na fikra mbadala? Je uzeofu hauleti ugonjwa wa kufanya mambo kwa mazoea?(Matokeo ya ugonjwa huu ni kulindana na kurudia rudia-rejea dhana ya mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale wa chama kile kile wakiendeleza yale yale kwa ari,kasi na nguvu mpya).

6. UZOEFU sio kitu mahususi? (is experience a specialization?) Mathalani CHADEMA ina uzoefu na falfafa ya nguvu ya umma ama inauzoefu na sera ya “Majimbo”, je kama unayataka haya si afadhali uipe fursa CHADEMA badala ya kuwashauri CCM kuyafanya haya kwa kuwa hawana uzoefu nayo?

7. UZOEFU sio chanzo cha ubinafsi?(the feelings of only me can because only me can!). Matokeo yake ni kutengeneza kikundi cha watawala wachache wale wale.(closed cycle). Lakini ukichagua kikundi ambacho kiko tayari kufungua macho nje kitachukua hata watu walio nje ya vyama ama mfumo wa utawala na kuwaingiza kwenye mkondo wa uongozi.

8. Chama ni uongozi, hivi ukichukua wakuu wa wilaya, mikoa, baraza la mawaziri mmoja mmoja je wote wana UZOEFU wa miaka mingi unaosemwa? Kama hapana ni kwanini wamewekwa? Je, ukongwe wa chama ni sababu ya yoyote yule kuvikwa uzoefu ili mradi tu anatoka chama husika?

9. Je, Mtu au taasisi inazaliwa na UZOEFU? Kama hapana, kwa nini hatuwi na watu au taasisi hizo hizo milele? Wengine wanaingiaji? Lazima kuna mwanzo Fulani. Je, UZOEFU ni sawa na kibao cha kukopa kesho ambacho kila siku kinasomeka hivyo hivyo na kila siku kumzuia mtu kukopa?

10. Mambo ya Msingi ya uongozi-sifa za asili za uongozi zinahitaji UZOEFU, mathalani UADILIFU, KUCHUKIA UFISADI? Je, yanahitaji uzoefu wa asili au uzoefu wa miaka?

11. Je, ni bora aliye muaminifu katika mambo madogo hastahili kupewa mambo makubwa ?(UZOEFU BORA KATIKA MAMBO YA NJE YA UTAWALA MATHALANI KUENDESHA VIZURI CHA CHA SIASA)

Haya ni maswali ya kuchokoza mjadala. Mengine yanajichanganya yenyewe kwa yenyewe. Ni chakula cha fikra tu(food for thought).

Nitachangia rasmi mada hii baada ya kusikiliza mahojiano ya Zitto.

Natabaruku

JJ
 
J.J.Mnyika,
Sikiliza mahojiano kisha turudie maana pongezi zaidi nampa mwanakijiji ambaye aliweza kumtoa nyoka pangoni bila kujijua!...

Lugha nzito sana katumia Zitto na sielewi kwa nini hakuwasiliana na nyie kwanza kabla hajaweka madai kama haya. Sijui ali panic au kitu gani baada ya kuongea na Mbowe na Ndesa!
Again another political blander!
 
JJ

Hilo ni darasa mdogo wangu; ahsante sana, endelea kubarikiwa! Sasa sijui watu wanatafuta sifa zipi za kiongozi zaidi ya uwezo kama unaouonesha wewe!
 
Mwakijiji,

Nakushukuru tena kwa kurejesha hii hoja ya "wapinzani ni wakombozi".

Nimesoma hoja za mwanasiasa, nakubaliana nami. Lakini kwa bahati mbaya nami sijasikiliza mahojiano ya Zitto. Huku nilipo ni ngumu ku-down load mahojiano. Nitachangia hoja hii nikishayasikiliza mahoajiano husika.

Lakini dhana ya kwamba wapinzani hawana uzoefu wa kuungoza sikubaliani nayo kabisa. Nitachambua kwa facts baada ya kusikiliza!

Dhana hii ilitumika sana pale Ubungo katika hatua za awali ikisemwa kwamba Mnyika hana uzoefu Keenja ana uzoefu.

Kwa kweli wakati ule nijibu dhana hii kwa maswali ambayo naamini yanaweza kutumiwa pia katika muktadha wa Taasisi(ikiwemo CHADEMA)

1. Hivi tunataka UZOEFU au UZEEFU? Uzoefu is a very subjective term. Watu wengi wanafikiri uzoefu ni miaka! Unaweza kuwa na miaka michache ukawa na uzoefu zaidi ya mwenye miaka mingi(wachambuzi wajadili)

2. Hivi tunahaja ya kuwa na UZOEFU au MZOEFU wa KUHARIBU? Kati ya mzoefu wa kuharibu na asiyekuwa na uzoefu wa kuharibu yupi bora? Je CCM wana uzoefu wa nini?

3. TANU iliingia madarakani ikiwa na miaka michache kuliko serikali ya mkoloni, je TANU ilipaswa kuachwa ili MZOEFU mkoloni aendelee? Miaka ya serikali ya TANU takribani 15 na ile ya MZOEFU CCM ya kuanzia 1977 mpaka 2007(30) ipi ilikuwa bora? Kwa nini uzoefu wa CCM usiwe mzuri kuliko TANU kimaadili, kukua kwa uchumi, elimu na tofauti ya pengo kati ya masikini na matajiri?

4. Hivi UZOEFU haupandi na kuanza kuporomoka? (In other words is experience not subjective to the law of diminishing return?)

5. UZOEFU hauzai URASIMU na UHAFIDHINA wa kukataa mabadiliko na fikra mbadala? Je uzeofu hauleti ugonjwa wa kufanya mambo kwa mazoea?(Matokeo ya ugonjwa huu ni kulindana na kurudia rudia-rejea dhana ya mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale wa chama kile kile wakiendeleza yale yale kwa ari,kasi na nguvu mpya).

6. UZOEFU sio kitu mahususi? (is experience a specialization?) Mathalani CHADEMA ina uzoefu na falfafa ya nguvu ya umma ama inauzoefu na sera ya “Majimbo”, je kama unayataka haya si afadhali uipe fursa CHADEMA badala ya kuwashauri CCM kuyafanya haya kwa kuwa hawana uzoefu nayo?

7. UZOEFU sio chanzo cha ubinafsi?(the feelings of only me can because only me can!). Matokeo yake ni kutengeneza kikundi cha watawala wachache wale wale.(closed cycle). Lakini ukichagua kikundi ambacho kiko tayari kufungua macho nje kitachukua hata watu walio nje ya vyama ama mfumo wa utawala na kuwaingiza kwenye mkondo wa uongozi.

8. Chama ni uongozi, hivi ukichukua wakuu wa wilaya, mikoa, baraza la mawaziri mmoja mmoja je wote wana UZOEFU wa miaka mingi unaosemwa? Kama hapana ni kwanini wamewekwa? Je, ukongwe wa chama ni sababu ya yoyote yule kuvikwa uzoefu ili mradi tu anatoka chama husika?

9. Je, Mtu au taasisi inazaliwa na UZOEFU? Kama hapana, kwa nini hatuwi na watu au taasisi hizo hizo milele? Wengine wanaingiaji? Lazima kuna mwanzo Fulani. Je, UZOEFU ni sawa na kibao cha kukopa kesho ambacho kila siku kinasomeka hivyo hivyo na kila siku kumzuia mtu kukopa?

10. Mambo ya Msingi ya uongozi-sifa za asili za uongozi zinahitaji UZOEFU, mathalani UADILIFU, KUCHUKIA UFISADI? Je, yanahitaji uzoefu wa asili au uzoefu wa miaka?

11. Je, ni bora aliye muaminifu katika mambo madogo hastahili kupewa mambo makubwa ?(UZOEFU BORA KATIKA MAMBO YA NJE YA UTAWALA MATHALANI KUENDESHA VIZURI CHA CHA SIASA)

Haya ni maswali ya kuchokoza mjadala. Mengine yanajichanganya yenyewe kwa yenyewe. Ni chakula cha fikra tu(food for thought).

Nitachangia rasmi mada hii baada ya kusikiliza mahojiano ya Zitto.

Natabaruku

JJ

Mimi sipendi sana kushabikia siasa maana sizijui, but post ya Mnyika inasomeka vyema sana. Na pia nakubaliana na Mkandara kwamba its another politaca blander, safari hii toka upinzani.

Mnyika sikiliza mahojiano, na urudi hapa kukata issue.

Hii issue ya bwana Zitto itatusaidia sana vijana kujua namna siasa za Bongo zinavyo-oparate. Vijana tutaendelea kuifuatilia mpaka tujue mwisho wake.
 
Noo!!! kama nimemuelewa mwana kijj vyema! naweza nikachangia kama ifuatavyo, Nchi kuongozwa na moja ya chama cha upinzani sio suluhu kabisa ya matatozo ya Tanzania, kwa muono wangu inawezkana pia ikawa ndio balaa, kwanza wapinzani wanaweza wakawa so EXITED na kuiburuza nchi sehemu nyingine ambayo ni mbaya zaidi.
Chama cha CCM kina maovu, na Udhaifu kama unavyofichuliwa na baadhi ya watu, lakini udhaifu huo uliopo katika CCM unawezekana pia ukawepo ndani ya vyama vingine, hivyo bado kutawaliwa na chama tawala sio suluhu na imani hii ambayo ni potofu tuiondoe vichwani mwetu.
Kwa kusema hivyo haina maana kabisa kwamba vyama vingine vife na turudi katika mfumo wa chama kimoja noooooooooo!!!! tunahitaji upinzani ulio bora, upinzani unaochochea maemdeleo ya kweli, upinzani ambao tuna uhakika nao kwamba ukichukua nchi kutakuwa na mabadiliko ambayo yalisahauliwa na chama tawala na wapinzani wanakuja kuendeleza pale walipoishia wenzao na kurekebisha makosa yaliosababishwa na wenzao, sio upinzani wa makelele tuuuu.
Ili tuyapate haya ni lazima upinzani ukae na kuleta mageuzi ya kweli, uhakikishe unashinda viti vingi iwezekanavyo katika serikali za mitaaa, ili iwe rahisi kwa wenyeviti wa serikali za mitaa kufanya kampeni katika uchaguzi wa madiwani na ubunge, kwani serikali sio Raisi peke yake, Bunge ndio mahali muhimu sana pa kuzoa viti vingi. na serikali za mitaa ni sehemu muhimu kwani ndipo wananchi walipo. sasa kukimbilia Kiti cha urais, na kuwekeza nguvu ningi pale ni sawasawa na kujenga nyumba bila ya msingi. na hii inafanya wananchi wakose imani na vyama vya upinzani
Chama hakijatawala hata mtaa, je kinaweza kutawala Taifa?
mie sio mwana CCM jamani ila najaribu kuchambua kadiri niwezavyo ili tufikie mahala tukubaliane na tuunde nguvu moja na tujue cha kufanya kwa ajili ya Taifa
Siku njema
 
SDM!
swala si kupata viti vingi bali swali la msingi watapata vipi viti vingi katika mazingira ya uendeshwaji wa chaguzi zetu kwasasa?Kutoka Katiba mpaka usimamizi na utekelezaji wa chaguzi(Tume ya Uchaguzi inavyoendeshwa na ilivyoundwa).
 
Son of a Dead Millionare,

ndugu yangu unapotosha hapa kidogo.. ni maoni yako lakini bob hata siwezi kuamini kama sii propaganda.
Kwa nini chama cha Upizani kisiweze kutawala ikiwa Nyerere ambaye hakuwahi kutawala hata kijiji zaidi ya kuwa mwalimu wa shule aliweza kutawala nchi UPYA toka mikononi mwa mzungu. tena bila wasomi wala miundombinu ya uzalishaji. We had nothing!
Kutawala nchi ni sawa na kuwa mzazi, kila mtu husema fulani hawezi kulea lakini akisha oa na kuzaa maisha huwa tofauti na yale ya Usera!..
Kuna kila uwezekano wa CUF ama Chadema kuwa viongozi wazuri kuliko CCM. Kwa sababu hiyo ndiyo itakuwa challenge na nafasi pekee ktk maisha yao kupata Uongozi kisha CCM wana nguvu na sauti kama wapinzani wazuri kuliko wao.
Ushindani halisi utaanzia hapo na SODM, trust ukiwa nje ya Utawala mshikaji usiombe. Pia kama utapewa madaraka ku- prove kwamba makosa yaliyokuwa yakitokea ni ya viongozi basi utawala tamu ya utawala huanzia hapo.
kama unakumbuka Zitto alimtolea mfano Harper wa Canada, huyu jamaa chama chake hakijawahi kutawala nchi zaidi ya serikali ya jimbo lao Calgary. Miaka yote calgary ilikuwa tajiri lakini wananchi wake hawakupata kabisa chochote cha kujivunia lakini bado walikichagua chama hicho miaka nenda rudi.
jamaa kashika nchi sasa hivi, na mshikaji uchumi wa jimbo hilo una boom kiasi kwamba inatisha. Kila unayemsikia anakimbilia huko na sasa hivi hakuna hata nyumba za kutosha...
Kila mtu domo wazi pamoja na kwamba watu wengi hawakipendi chama hicho nahasa huyu bepari mkubwa Harper. lakini jamaa ndio analeta ajira na utajiri pamoja na kwamba msimamo wake kisiasa haupendwi na watu.

Chagua mwenyewe kusuka ama kunyoa!
 
Ndugu yangu kwanza soma kisha elewa, halafu ndio ukimbilie keyboard, Kwanza kumbuka Mwl. Nyerere alikuwa akipigania uhuru, na alianza ku mobilize watu kuanzia ngazi ya mjumbe wa nyumba 10 na ndio maana aliweza kukubalika na kujulikana kwa urahisi. na hatimaye kufanikiwa.
Sasa ndugu yangu Upinzani haujaweza hata kuchukua viti vya seikali za mitaa, nani atavijua? ukizingatia wapiga kura wanaojua mambo ni wachache?
Una habari kuna watu wanapiga kura na hajui hata jina la chama? anafika sehemu ya kupiga kura anasema niwekeeni alama Chama cha Mapalala, au niwekeeni Alama chama cha Nyerere.
sasa unategemea kuna chama kitaweza kushika dola hapa? na point hapa ni kwamba Hata wapinzani wakishika Dola bado sio suluhu ya matatizo yetu.
 
SODM,

Nimekusoma vizuri , labda wewe ndio hukunielewa. Ku mobilize watu ni swala jingine kabisa na uwezo wa kutawala. Hivi vyama vya Upinzani navyo vina watu kila ngazi na sii kweli kwamba TANU ilikuwa na wajumbe wa nyumba kumi wakati ikipigania uhuru wetu. Kushindwa kuchaguliwa kuwa madiwani ama wabunge hakuna maana hawana watu huko vijijini.

TANU ilipopigania uhuru hadi siku inatangazwa kuchukua ushindi wa uchaguzi wa kwanza hakuna hata mwafrika mmoja aliyewahi kuwa kiongozi ktk serikali ya mkoloni tena afadhali hawa wapinzani wana wawakilishi wao bungeni. Mkoloni aliwatumia zaidi machief kuliko viongozi wa kisiasa na kama hujaambiwa vizuri Nyerere na waasisi wetu walikuwa akifanya mikutano ya siri sana tofauti na leo. Na sio kweli tanu ilijulikana kila kona kwa sababu ukitazama hata kura za kwanza ni watu wachache sana waliopiga kura.
Kwa maana hiyo basi Tanu hawakuwa na experience yoyote ya uongozi wa nchi kama walivyo wapinzani.
 
WARAKA HUU UMETUMWA KWANGU NA THOMAS NGAWAIYA USOMENI

NA MWENYE MAONI JUU YA WARAKA HUU ATOE.

ITACHUKUWA MIAKA 100 KWA WAPINZANI WA TANZANIA KUELEWANA NA KUELEWEKA NDANI YA JAMII.

Muungano wao ni danganya toto.
Uchu wa madaraka wengi wameficha makucha yao
Hata wakiungana hawatazidi 5%, hivyo ni vigumu kupata ushindi.

Kuna mambo mengi sana yanayofanya Watanzania kujiuliza kuhusu viongozi wa upinzani Tanzania, moja ni juu ya ubinafsi wao;

Hakuna uongozi uliobora ndani ya vyama vyao. (mfano kupeana madaraka kifamilia, mfano mzuri CHADEMA).
Wapinzani wengine uhubiri ukabila mfano; siasa ya u-majimbo.
Hakuna amani ndani ya vyama hivyo. (hoja ya jino kwa jino)
Hawana uwezo wa kujenga uchumi wa nchi kwani kwa miaka 16 wamekuwa wakitegemea ruzuku ya serikali kwa kuendesha vyama hivyo.
Vyama vingine vinatumia udini jambo ambalo linahatarisha amani.

Hoja zote hizi ni kati ya maswali wanayojiuliza wananchi kuhusu kama kweli haya yatatukomboa kisiasa na kiuchumi Tanzania.?

Jibu ni hapana; Kwani ni vyama hivyo hivyo vinavyozungumzia umajimbo Tanzania na hivyo inamaanisha ukabila kwa kutaka kutugawa..

Ni vyama hivyo hivyo vinavyohubiri ubinafsi kwa kuamua kugombea nafasi za uongozi kila mara au uraisi kwa watu walewale bila kupisha wengine hata kama uwezo wao umechuja na kwa hali hiyo inaonyesha kuwa hakuna demokrasia ya kweli ndani ya vyama vya upinzani. Wananchi wanajiuliza endapo hapana demokrasia ndani ya vyama hivyo ni vipi watajenga demokrasi baada ya kupewa madaraka ya nchi nzima?

Jambo jingine ni kuhusu kupanua na kujenga uchumi wa ndani ya nchi. Ili kupanua uchumi wa nchi utahitaji ubunifu wa hapa na pale. Vyama hivyo vimedumu kwa zaidi ya miaka 16 na hadi sasa vyama vyote hivi hutegemea ruzuku ya Serikali kwa kujiendesha kwani hakuna hata senti moja inayotokana na michango ya wanachama wao na wala miradi yeyote wananchi wanajiuliza ni vipi hapa napo vyama hivi vimeshindwa kujikwamua kiuchumi ndani yao na kutegemea ruzuku ya serikali muda wote je! Watajengaje uchumi wa nchi ikiwa wao kwao wameshindwa?

Tangu vyama hivyo vianzishwe viongozi huzua migogoro ya hapa na pale isiyokuwa na kichwa wala miguu, na kufukuzana kila kukicha na hivyo kufanya wananchi kujiuliza kama wangepewa nchi ingetawalika? Pia Watanzania wanaangalia migogoro mingine ilivyo ndani ya nchi nyingine za Afrika kama Somalia, Sudan, Kongo, Uganda, Kenya, Burundi nk. Na kulinganisha na amani iliyopo Tanzania. Ndio maana 95% ya wale waliokuwa upinzani wameamua kurudi kwenye chama tawala.

Kwa hali hii jamii ya watanzania wameona na kuamua kutounga mkono vyama hivi vya upinzani kwa kuwa hawana jipya na badala yake wanahubiri chuki tu ya kuyumbisha Taifa letu lenye amani na viongozi wenye busara .

Mwisho jamii inajiuliza juu ya viongozi waliopo kwenye upinzani kwani ni wale waliokuwa ndani ya CCM na kuchujwa kwa sababu ya kukosa sifa na wao wakaanzisha vyama hivyo kutokana na chuki binafsi na siyo kwa masilahi ya Watanzania kama walishindwa kuungana wakati wakiwa asilimia ishirini ni leo ambapo wamebakia asilimia tano ?

Hii ndio picha halisi tunayoona sisi Watanzania kuwa wapinzani hawana nafasi ndani ya nchi hii hadi baada ya miaka 100, yaani karne ijayo, ambapo kutakuwa na kizazi kipya na chenye mawazo na mtazamo mwingine.

Ningependa kuwahasa wapinzani kuwa badala ya kufikiria muungano wa unafiki ni vema kama wana mawazo mazuri wakayasema au kuyatenda sasa kwa manufaa ya wananchi na nchi kwa ujumla na pia wajue kuwa chuki,ubinafsi,ukabila na udini kamwe havitaweza kujenga amani ya nchi wala kuleta maendeleo ya kiuchumi zaidi ya kuleta vita na mfarakano. Wananchi wa Tanzania tuepuke upinzani tujenge nchi yetu kwa amani na utulivu daima ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI.

Muungano huu nafananisha na wagonjwa wawili kuungana na kupata mmoja mwenye afya bila tiba.

Thomas Ngawaiya

Waraka huu umetumwa kwa bwana Mroki Mroki. Unaweza kusoma habari nyingine na picha kwenye blogu yake hapa: Mroki Mroki
 
Back
Top Bottom