Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!

Hio Public parties labda kama kungekuwa hamna ruzuku. Public ni kwa maskini as always. Private ni kwenye hela so ishi na hio kama hutaki shari na mwenyekiti wa Mboga mboga.
 
Ujinga umewajaa mpaka mnakera sasa, si mlisema hamtaki upinzani unakwamisha maendeleo? ndio mana mkaiba kura zote na kuwafanyia unyama ili muwe pekee yenu, ni nini kimewasibu saa hizi mnaanza kufukua sheria,ambazo mmezikanyaga kwa makusudi?
 
Kuiba kura, na NEC na TISS kuvuruga haki ya kikatiba ya wananchi kuchagua viongozi wao ndiyo inaitwa public Interest?
Hiyo siyo public interest ni Jiwe's and his croonies Interest
Tunahitaji kujenga taifa la watu wanaoaminiana na kuheshimiana bila kujali itikadi zao. Watumishi wa uma ambao nafasi zao siyo za kisiasa, mfano NEC, TISS, majeshi yote, wataalam kata wizara mbali mbali hawatakiwi kuwa mashabiki wa chama fulani kwa uwazi. Ikionekana hivyo ni sababu tosha ya kuwaondoa kwenye ofisi za uma kwa nchi inayofuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi.
Tatizo linaanzia hapo.

Maadui wa uma au taifa ambao ni hatari na watasambaratisha taifa ni hao watumishi wanaodhihirisha mapenzi yao kwa chama wazi wazi ambacho ni kinyume kabisa na sheria na katiba.

Lazima kujenga misingi ya kuaminiana kwanza. Hata hivyo, changamoto ya umasikini wa fikra/akili na kiuchumi kwa watumishi wengi huwafanya wajipendekeze kwa wanasiasa hadi kufanya upendeleo ambao labda hata hao waliopendelewa wanaweza kushangaa.
Kulaumu viongozi au chama fulani pekee hakuondoi tatizo.
 
Public interest haikuzingatiwa raia walipotaka kuandamana kwa kutoridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi mkuu.
Hayakuwa maandamano ya amani hata kidogo. Mr Mzungu alishawaambia, Atakuwa halali yetu; Hawatatuua wote, etc. Kwa hiyo hata maandamano hayo hayakuwa maslahi ya umma, ila dirisha tu la vurugu, ghasia & machafuko.
 
Mkuu huoni kwamba kukubali kupeleka viti maalumu itajenga mazoea ya miaka yote ya kushiriki uchaguzi "HURU NA HAKI " Na chama kimija kinabebelea kura zote bila aibu..

Mkubwa pascal huoni kwamba tunatengeneza mfumo mpya wa demokrasia ya vyama vingi wa kupigiwa kura za kutosha na zisihesabiwe zikahesabiwa zile ambazo hazijapigwa.
 
Who decides what is public interest and what is not?

On what criteria?

CHADEMA wakisema it is in the public interest for them to not participate in parliament, to protest the grotesquely fraudulent election, how could you dispute that?
 
Ulitakiwa uje na hoja juu ya uhalali wa uchaguzi kabla ya kuandika hizo rubbishes.

Yale mabegi ya kura feki yalitoka wapi?

Waliyokutwa nayo kwa nini hawakushtakiwa?

Kwa nini mawakala wazuiliwe kuingia vituoni?

Kwa nini Zanzibar yenye wapiga kura laki 7 wapige kura siku 2 tofauti na bara?

Otherwise unataka kutukanwa hapa ukimbilie polisi.
 
Hoja hapa CCM wamepora kura waziwazi...

Hapa ndipo pa kuanzia...hamtaki basi chukueni Bunge, Dola, Mahakama tuone kama mtakuwa na furaha mioyoni mwenu.
CCM wamepora kura, wamekataza maandamano, halafu wanataka kulazimisha wapinzani washiriki bungeni?

Yani umepanda daladala, mtu kakukanyaga mguuni.

Unamwambia umenikanyaga, anakuziba mdomo usiseme.

Unasema sawa, basi nataka nishuke nikuachie nafasi uendelee mwenyewe kwenye basi, anakwambia hakuna kushuka, baki humu humu niendelee kukukanyaga!
 
Back
Top Bottom