Je, kama vyama vingine vya siasa Tanzania vina nia nyingine, kwanini haviondolewi kwenye usajili?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Kwa mujibu wa sayansi ya siasa, chama cha siasa kina nia moja tu, kukamata dola na kuwahudumia wananchi wote.

Mhe. Rais amesema kuna vyama vina nia tofauti. Je, ni tofauti na hiyo nadhalia ya sayansi ya siasa? Au tofauti na nia ya CCM?

Je, nia ya CCM inarandana na nia iliyopo kwenye sayansi ya siasa?

Halafu, kama vyama hivyo vinajulikana kuwa na nia ovu, kwa nini bado vipo kwenye usajili?

 
Vyama vingine vina nia ya kuungana kuisapoti ccm kwa kila namna!
Vyama hivyo vingeunganishwa tu pamoja na ccm!
 
Vyama vyenye Nia nyingine ni vile ambavyo havitakubali kuporwa ushindi wao na ccm. Kwa tafsiri ya kiccm, Chama kinakuwa na Nia njema iwapo kinaisujudia ccm, na kukubali kuongozwa na ccm kwa shuruti.
 
Kwa mujibu wa sayansi ya siasa, chama cha siasa kina nia moja tu, kukamata dola na kuwahudumia wananchi wote. Mhe. Rais amesema kuna vyama vina nia tofauti. Je, ni tofauti na hiyo nadhalia ya sayansi ya siasa? Au tofauti na nia ya CCM? Je, nia ya CCM inarandana na nia iliyopo kwenye sayansi ya siasa?
Halafu, kama vyama hivyo vinajulikana kuwa na nia ovu, kwa nini bado vipo kwenye usajili?


View: https://youtu.be/t0T79SW44mM?si=Pli28m7MgjbmceBn

Apuuzwe tu ameshachanganyikiwa
 
Back
Top Bottom