Je, wajua umuhimu wa lishe bora katika makuzi ya watoto?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Wataalamu wa #Malezi wanatueleza kuwa Lishe bora ina mchango mkubwa katika ukuaji na ustawi bora wa mtoto kwani hujenga afya na akili ya mtoto.

Lishe bora hujumuisha mchanganyiko wa vyakula vya protini kama kuku wa kienyeji na mayai yake, vitamini yaani mboga za majani na matunda, wanga kama viazi na ndizi pamoja na maji safi na salama.

Baadhi ya wazazi huhisi kuwapa watoto wao fati kwa wingi kama chipsi, kuku wa kisasa wa kukaanga na vitu vya sukari kama pipi chokoleti ni ishara ya kuwapenda watoto na kuwapa afya bora jambo ambalo si sahihi kwani huongeza unene unaoweza kuwasababishia watoto magonjwa ya kudumu

Ni muhimu kwa wazazi na walezi kuwapa watoto chakula bora kwa ajili ya ustawi wao wa sasa na baadae.
 
Kizazi kipya malezi mapya. Enzi zetu hata kama ungekuwa unakula gudulia la pipi na kisado cha chips kusingekuwa na shida kwa sababu zile hekaheka za siku nzima tu zilitosha kuunguza calories zote ulizojikusanyia kwa siku hiyo. Sasa kizazi hiki cha mabroila wanashinda wanaangalia katuni na kucheza games huku wamekaa ni shida kwa kweli. Wazazi wawe waangalifu!
 
Back
Top Bottom