Je, Vyoo vya Shule za Serikali vinajengwa hivi?

Hata mimi ndio nilivyokuwa nafikiri, hapo ni kama kujenga Vyoo vya shimo kwa mtindo tofauti.

Wakati nasoma kwenye shule moja kongwe ya serikali tulikuwa na Vyoo vya aina mbili, vile vya kuflash na vile vya shimo ambavyo tulivipa jina na kuviita 'mapambano'....kutokana na changamoto ya maji ilikuwa ni salama na rahisi zaidi kutumia choo cha mapambano.
 
2947116_BB4E79CF-0516-445A-AD1F-8A08FF4FEFF9.jpeg.jpg

Haya ndio mafanikio ya sera ya Force Account ya Awamu ya Tano.
Kila mtu anaruhusiwa kutotumia akili, toka kwa Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, ma DED wa Halmashauri.

Ila wanatakiwa wamuamini fundi Maiko, na hapo kafanya vitu vyake.
 
Inasikitisha sana. Ina maana tozo tunazolipa ndiyo zinatumika hovyo kiasi hicho??!!
 
Tena hiyo imejengwa na mkandarasi chini ya usimamizi wa mhandisi mwenye Phd
 
Mara mia wangekuwa wanatupa kwenye hiyo miradi vijana waliomaliza vyuoni wamehitimu mambo ya ujenzi ingesaidia sana kuliko huo upuuzi...

Kazi za force account n KIAZI CHA MOTO kwa serikali
 
Mnachanganya. Kujenga nyumba binafsi ambayo ina choo kimoja au viwili ni tofauti sana na kujenga yenye vyoo tisa vilivyojipanga. Sio sehemu zote Tanzania zenye uzoefu wa manholes, septic tank na soak pit.

Hata wale ambao wana vyoo vinavyotumia maji wengi hawajui namna vilivyounganishwa kwenye septic tank maana mabomba yanakuwa yamefikiwa. Na sio wote wanaojenga nyumba zao. Wengi tuu ni wapangaji.

Huyo mtu atakayejenga hivi kwa makusudi ili apige fedha atakuwa punguani kweli. Hapa ni ignorance tu na sio ufisadi.

Amandla...
Bongo kila mtu msemaji kaka....
Kiukweli force account ni upuuzi
 
Mnachanganya. Kujenga nyumba binafsi ambayo ina choo kimoja au viwili ni tofauti sana na kujenga yenye vyoo tisa vilivyojipanga. Sio sehemu zote Tanzania zenye uzoefu wa manholes, septic tank na soak pit.

Hata wale ambao wana vyoo vinavyotumia maji wengi hawajui namna vilivyounganishwa kwenye septic tank maana mabomba yanakuwa yamefikiwa. Na sio wote wanaojenga nyumba zao. Wengi tuu ni wapangaji.

Huyo mtu atakayejenga hivi kwa makusudi ili apige fedha atakuwa punguani kweli. Hapa ni ignorance tu na sio ufisadi.

Amandla...
Mkuu wewe unsona septic tank pale?
 
Tatizo siyo kufukia pekee. Hakuna chemba ndogo za kupokea mzigo na kuunganisha kwenye chemba kubwa. Hapo harufu itawasumbua sana na ikitokea kumeziba sijui watayakata hayo mabomba kuzibua na kuyaunga tena?

Mitano tena kwa mkandarasi
Kuna jambo hujalijua ila inajifanya kujua swala la ujenzi waachieni wajenzi wao ndio wanajua kwa mazungira yapi kijengwe nini.
 
Ndio shida ya force account. Wote hao hawajui lolote kuhusu miundo mbinu ya maji taka kwenye vyoo na mabafu mengi. Kuwatumbua itakuwa sio haki.

Ni kuwaletea mtaalamu atakae waelekeza namna ya kujenga inspection chambers, septic tanks, soak pits au French drains. Sio makosa yao. Na michoro mengi inakosa michoro ya hii miundo mbinu.

Amandla...
Hivi kweli hata kama hujui kusoma hata picha huioni< hao unaowatetea wanaweza kujenga vyoo vya namna hiyo majumbani kwao? Je huyo Mkandarasi na mafundi wake hawaoni hata aibu kwa kitendo hicho?
 
Waziri Ummy na DED wa hiyo Wilaya tunaomba maelezo..

Hata hivyo tunamshukuru uhuru wa kutoa maoni na kuibua uozo maana awamu ya Mwendazake ulikuwa marufuku kuonyesha madhaifu ya serikali bali sifa za bwana Magu kiongozi wa malaika na wanyonge.
Wanafunzi wanakua na kuona utendaji wa kazi wa namna hii unadhani unawajengea utamaduni gani
Mambo kama haya tena shuleni ndio baadae tunaendelea kupata viongozi wanaojijali wao tu
 
Kuna jambo hujalijua ila inajifanya kujua swala la ujenzi waachieni wajenzi wao ndio wanajua kwa mazungira yapi kijengwe nini.
Receiving mini-chamber ina umuhimu mkubwa sana kwa sewarge system yeyote.

Mimi siyo mtaalam wa ujenzi lakini kwa kuangalia tu hapo wamemchukua fundi gereji kufanya huo ujenzi.
 
Back
Top Bottom