Je, unaweza kutoboa kimaisha (biashara) nje ya miji mikubwa kama Dar, Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,678
Tokea nizaliwe sijawai kusikia mtu anatoka mjini anaenda kutafuta maisha kigoma, sumbawanga, Gairo, Mara, Ruvuma, Mtwara, Singida n.k.

Simaanishi kwamba hakuna watu wenye pesa lakini naona kama huko mikoa ya pembezoni nguvu ya kuweza kuinua mtaji wa Kwa Kasi na kukua sio jambo jepesi ni kimbembe, nilifanikiwa kwenda maeneo kama kakonko, kibondo, Bariadi, Gairo, chemba, Bahi, Ruangwa, Songea, same, Mwanga na maeneo mengine ya vijijini, kwanza kila ndoto ya wakazi wa huko wanawaza kwenda daresalam na Mwanza kutafuta maisha.

Daresalam linabaki kama jiji muhimu sana kwa mtu kwenda kutafuta kipato kwa sababu ya mzunguko uliopo, ukiwa na mtaji, nidhamu,Mungu basi kwa mtaji wa million 5-10 unatosha kabisa kua wa tofauti kwa muda wa miaka 2 tu.

Lakini hata ukiwa na mtaji wa hiyo million 5-10 huko mikoani unaweza kukosa Cha kufanya maana unaweza anzisha biashara na ukakosa pia wateja.

Huko vijijini ni ngumu Sana kupata kijana mwenye pesa, mfano tokea alipoanza kuhustle mpaka kua na assets yoyote ya maana sio rahisi Kwa muda wa miaka 5, lakini Kwa daresalam mtu mwenye mtaji miaka 5 ni mingi sana lazima atakua na asset za maana na zinazoonekana, matajiri wengi huko mikoani na vijijini ni wazee.

Hivi mawazo yangu yapo sahii? Huko mikoani mtu anaweza kutoboa Kama ilivyo kwenye miji mikubwa?
 
Tokea nizaliwe sijawai kusikia mtu anatoka mjini anaenda kutafuta maisha kigoma,sumbawanga,gairo,Mara,ruvuma,Mtwara,singida n...
Una uhakika? Hawa matajiri wa Mikoani wao pesa wamezitoa wapi? 👇👇

IMG_20240203_173000_616.jpg
IMG_20240203_174048_562.jpg
 
Kwanza mtu alie toboa kimaisha unamtafsiri vipi??
Kila mtu yupo na definition yake kuhusu mafanikio, lakini Kwa upande wangu alietoboa kimaisha ni mtu mwenye asset anazomiliki, mtu mwenye uhuru wa kifedha anaeweza kufanya jambo lolote lile, mfano mtu anaweza kuumwa akafa kisa amekosa million 10 ya matibabu, kwangu mtu alietoboa no yule Ambae kafika hatua ya kua na uhuru wa kifedha.
 
Tokea nizaliwe sijawai kusikia mtu anatoka mjini anaenda kutafuta maisha kigoma,sumbawanga,gairo,Mara,ruvuma,Mtwara,singida n.k

Simaanishi kwamba hakuna watu wenye pesa lakini naona kama huko mikoa ya pembezoni nguvu ya kuweza kuinua mtaji wa Kwa Kasi na kukua sio jambo jepesi ni kimbembe, nilifanikiwa kwenda maeneo kama kakonko,kibondo,bariadi,gairo, chemba,bahi,ruangwa, songea, same,mwanga na maeneo mengine ya vijijini, kwanza kila ndoto ya wakazi wa huko wanawaza kwenda daresalam na Mwanza kutafuta maisha.

Daresalam linabaki kama jiji muhimu sana kwa mtu kwenda kutafuta kipato kwa sababu ya mzunguko uliopo, ukiwa na mtaji, nidhamu,Mungu basi kwa mtaji wa million 5-10 unatosha kabisa kua wa tofauti kwa muda wa miaka 2 tu.

Lakini hata ukiwa na mtaji wa hiyo million 5-10 huko mikoani unaweza kukosa Cha kufanya maana unaweza anzisha biashara na ukakosa pia wateja.

Huko vijijini ni ngumu Sana kupata kijana mwenye pesa, mfano tokea alipoanza kuhustle mpaka kua na assets yoyote ya maana sio rahisi Kwa muda wa miaka 5, lakini Kwa daresalam mtu mwenye mtaji miaka 5 ni mingi sana lazima atakua na asset za maana na zinazoonekana, matajiri wengi huko mikoani na vijijini ni wazee.

Hivi mawazo yangu yapo sahii? Huko mikoani mtu anaweza kutoboa Kama ilivyo kwenye miji mikubwa?
Mkuu, Maswali na majibu yote ushaatoa.
Huo ndio mchango wangu.
 
Sasa mkuu biashara Huwa ni common kwa mikoa yote sioni kama Kuna biashara mpya.

Zinaweza kuwa zinajirudia

Ila ili biashara ikulipe inategemeana na sehemu ulipo, na kitu gani kinapatikanika na kipi hakipatikaniki, kisha unacheza na gap.

Ukiwa Tunduma kuna biashara zake

Ukiwa maeneo ya migodi kuna biashara zake

Ukiwa znz kuna biashara zake

The same for Tanga, Arusha,Mwanza
 
Back
Top Bottom