Biashara ya kutoboa kirahisi Dar 2024

Mar 15, 2019
36
97
Habari za Asubuhi wakuu humu ndani natumahi mko poa.

Sasa kama mada inavyojieleza hapo juu, mimi nimekuwa nikifanya utafiti mbalimbali hapa Dar es Salaam kuhusu biashara ambazo mtu ukizifanya kwa sasa ni haraka tu unatoboa kimaisha. Miongoni mwa biashara hizo ni biashara ya kuuza nafaka kwa jumla na rejareja, kuuza chakula chenyewe hapa namaanisha restaurant pamoja na biashara ya simu na accessories.

Nina mchanganuo wa biashara zote tajwa hapo juu, kuanzia mtaji wa milioni 5 ili kuweza kufanikiwa kwa urahisi zaidi. Kwa yeyote mwenye mtaji ambao hana wazo wala mchanganuo wa biashara namkaribisha tuweze kushirikiana.
 
Ingekuwa rahisi watu wengi sana wangeshakuwa matajiri.... akili za kuambiwa changanya na za kwako. Wewe mleta mada hautaki kuwa tajiri?
Ninataka ndiyo manaa ninatafuta mtu wa kushirikiana mwenye hiyo pesa mimi sina mtaji nina mchanganuo wa namna ya kufanya .... akiona inafaa tutafanya
 
Habari za Asubuhi wakuu humu ndani natumahi mko poa.

Sasa kama mada inavyojieleza hapo juu, mimi nimekuwa nikifanya utafiti mbalimbali hapa Dar es Salaam kuhusu biashara ambazo mtu ukizifanya kwa sasa ni haraka tu unatoboa kimaisha. Miongoni mwa biashara hizo ni biashara ya kuuza nafaka kwa jumla na rejareja, kuuza chakula chenyewe hapa namaanisha restaurant pamoja na biashara ya simu na accessories.

Nina mchanganuo wa biashara zote tajwa hapo juu, kuanzia mtaji wa milioni 5 ili kuweza kufanikiwa kwa urahisi zaidi. Kwa yeyote mwenye mtaji ambao hana wazo wala mchanganuo wa biashara namkaribisha tuweze kushirikiana.
Hee!
 
mm nataka nfanye biashara ya laki moja wakuu nipeni ushauri serious
Biashara ya laki moja fanya hivi. Chukua 50k tafuta brenda ya kusagia juice ya matunda, 10k tafuta dumu la lita 5 na 20k tafuta cup ndogo za kuwekea juice za take away za buku na jero jero na hiyo 20k inayobaki tafuta matunda mbalimbali saga juice dumu moja weka juice ya aina moja ambayo inapendwa sana na dumu lingine weka juice ya mchanganyiko kisha mtafute dogo yoyote unayemuamini kama huwezi kutembeza mwenyewe, mkubalianae utampa Tsh ngapi kwa siku.

Au kama huwezi kabisa basi saga juice mpelekee mamalishe mmoja akuuzie wakati wa chakula. Hakikisha unapata mamalishe mwaminifu na ambaye hana tamaa, maana wengine wakiona unauza na yeye anatengeneza yakwake anauza.

All the best Mkuu
 
Back
Top Bottom