Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Kuna kitabu kinaitwa "SOMA KWA HATUA".
kitabu sikipendi Kileee kimeniliza sanaa
Dingi akitoka kazini anaanza kunifundisha.
Nikikosea tu bakora za maana..
Kipindi hicho baba kanunua TV na deki..
Nikirudi mchana mimi tv tu nacheki mikanda.
Phantom solder,eastern condors,Rambo anold baba jeni..
Ila usiku ukianza kuingia nakuwa mpole maana najua baba akirudi ataniita anifundishe na bakora juu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi pia ndio kitabu nilifundishiwa na mzee kwa makonzi mengi sana 🤣🤣🤣
Baada ya kutiwa makonzi napewa hela ya toffee au pipi kifua. Dingi alikuwa hataki ujinga. Watu walishangaa sana kabla sijaanza std one naweza kusoma gazeti vizur kabisa😆😆😆😆😆
 
Daaah!! I miss him too much my best friend. Pacha wangu alinidekeza sanaaa, hakuwahi hata kunifinya.
Nilikuwa nikikosea akapewa kesi basi atasema "mama yangu hawezi kufanya hilo kosa" halafu atanigeukia na kuniuliza "si ndio mama?" basi naona aibu na kuanza kulia.
Then ananiambia "usilie mama yangu, najua ulipitiwa tu ila usirudie tena". This worked kuliko viboko, maana nilikuwa nampenda na kumheshimu sanaa.

RIP my love.
Hakika alikudekeza. Huyo baharia kazi anayo, maana ukishazoea kubembelezwa.
 
Yule mzee, kwanza amewahi nipiga mara 2 tu katika maisha yangu, nikiwa chekechea baada ya kuiba hela ndani na nikiwa darasa la sita baada ya kefeli darasani. Tofauti na mama ambaye anilinipiga fimbo mpaka akachoka na akaacha rasmi nikiwa darasa la 5.


Kikubwa hakuwa muongeaji sana kitu ambacho nimerithi kwake, Ila alipenda kunifundisha vitu hasa kuhusu maisha kwa vitendo badala ya maneno. Mifano ambayo naikumbuka mpaka kesho.

Mzee alinipambania na kuhakikisha napata elimu iliyo bora.

Ni miaka zaidi ya 8 anaumwa sasa, Ila bado hajaacha kupambana kwa ajili ya maisha yake na ya wane. Nakuombea maisha marefu mzee wangu.
 
Nadhani baba ngu ananielewa kuliko mtu yoyote chini ya jua kuliko hata mama japo I love them both.
Tukio moja kati ya mengi ambalo najivunia [emoji3] Nikiwa chuo mwaka wa kwanza UD palitokea mgomo wanachuo wote tukafukuzwa.Nikarudi zangu home kuskilizia.
Baadae tukatakiwa kurudi lakini kujisajili upya kulikua na mafomu ya kujaza serikali za mtaa.
Kufika kule kuna mbaba sijui mtendaji yule au m.kiti akagoma mpka nitoe hela eti mchango wa shule akanisema na maneno kibao kua badala ya kusoma tunafanya fujo so hajazi form hadi nitoe hela .Hapo niko o innocent first year sina nnacho elewa jamani.

Nilimpigia mzee nikashindwa hata kuongea nalia tu alivyorudi nikamweleza, akanambia panda kwenye gari akachoma mafuta hadi ofisi ya mtaa.
Kufika nikamuonyesha "baba nilileta form kwa huyu ndo kazizuia hadi ulete hela" The next thing I knew yule mzee amekunjwa baba anamkoromea kunichelewesha kwa sababu zisizo na mashiko.
Ilibidi watu waamulie mie hapo nimekimbilia kwenye gari nachungulia tu. Nikajaziwa form nikaenda posta kutuma with my hero [emoji1][emoji1] Isingekua baba na uwoga wangu ningekwama kurudisha form kwa wakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana Mushi hupaswi kuendelea na kazi kutokana na hali uliyo nayo..yafaa uwe nyumbani na familia ...Jibu la mzee Wanangu hawastahili shida labda niwe nimekufa...
Hapo ni baada ya kupata ajali na kupata hitilafu kwenye uti wa mgongo...nachokumbuka ..ilifika hatua hawezi kutembea still alitaka kwenda kupambana..
Tulikuwa hatununuliwi pipi ila mifuko ya pipi, Kama ni sikukuu Atanunua kila kitu in bulk, crates za soda mavazi, chakula, nk, , , Alikuwa na moyo wa kutoa ... Vitu hivyo havikuw vyetu peke yetu...Akifika utasikia Mama juma njoo chukua hivi ,mama fulani, , , , Then Wewe J chukua hizi wapelekee marafiki zako.......
KIZURI HAKIDUMU
Moment ambayo naipenda Alikuwa ananuka sana miguu so kazi Yangu kama sijalala akija Tuuu naanza kumwambia baba vua viatu hapo mlangoni unawe ...atacheka ataniita mwanangu J njoo univue viatu then ataninusisha...[emoji28]
....Nina mengi juu ya mshua ila alipendwa zaidi...
Rest in peace father

Nimepitia mengi sana ila nilipo afadhali...Ipo siku nitashusha nondo za life langu humu.[emoji24][emoji24][emoji24]
Dada kabaki kusema KAMA BABA ANGEKUWEPO
Please fanya kushusha full nondo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nachapa sana kazi siku hizi. Nayaona matunda. Wengi wanasema role model wangu sijui fulani. Lakini mimi role model wangu ni baba yangu. Alinifundisha kuchapa kazi,na yeye alichapa kazi. Amezeeka namtunza na najisikia vizuri kwamba anafurahia matunda ya malezi yake.

Baba ni wa kuthaminiwa sana. Wakati mwingine hata kama alijisahau akakutelekeza. Wakristo tunafundishwa 'usilipe Ubaya kwa ubaya...bali lipa ubaya kwa wema'.

Mama ana innate value...lakini nafasi ya baba aliewajibika ipasavyo ithaminiwe pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah!! I miss him too much my best friend. Pacha wangu alinidekeza sanaaa, hakuwahi hata kunifinya.
Nilikuwa nikikosea akapewa kesi basi atasema "mama yangu hawezi kufanya hilo kosa" halafu atanigeukia na kuniuliza "si ndio mama?" basi naona aibu na kuanza kulia.
Then ananiambia "usilie mama yangu, najua ulipitiwa tu ila usirudie tena". This worked kuliko viboko, maana nilikuwa nampenda na kumheshimu sanaa.

RIP my love.
He was doing his level best on how to tackle and solve ur misdoings, something to note is, not everyone unaweza ku terminate kosa au tabia mbaya kwa njia hiyo, Pavlov mtaalamu wa wanyama anatuambia njia mbili za kutoa tabia isiyotakiwa ambapo kuna"positive reinforcement" kama ambavyo dady wako alikuwa anakufanyia and other bla bla of the same sort lakn pia kuna"punishment"

Hoja yangu ni kuwa unatakiwa kuwa makini kujua kama hiyo tabia itaondoka aidha kwa ile ya kwanza au ya pili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ile ukitembea nae au ukiwa unatoka home anachungulia dirishan akisisitiza ukitembea nyanyua mguu usiburuze viatu au ndala maana vinaisha haraka na yeye hana pesa za kununua viatu kila Mara..dahh!! Leo kwel nayaona pesa ni ngumu hivyo kila ulichonacho ni kukitunza
 
Binafsi nakumbuka siku moja hivi tuko kijijini na mzee tumepanga kesho yake tukamtembelee babu, baba yake mdogo baba ambaye alikuwa anaishi kilometa kadhaa kutoka tulipo (KM 7).

Wakati huo nilikuwa na Miaka 6, mkubwa kabisa, Sasa wakati wa safari tumetoka vizuri mimi na mzee mtu Bee (wawili) tu pale nyumbani kuelekea kwa babu.

Wakati tuko njiani nilikuwa namdekea sana baba yangu, Sasa baada ya kama Nusu safari hivi nikamrukia mzee na kumwambia nimechoka anibebe.

Mzee alinitazama usoni na kutabasamu kisha akasema unataka nikubebe mpaka wapi,mi nikamjibu mpaka kwa babu.

Mzee kweli akanichukua na kuniweka begani mpaka tumefika kwa babu, huku tukipiga story. Huwezi amini mzee alinibeba tena begani mwake wakati wa kurudi mpaka nyumbani.

Wala sikuwaza kwamba nilikuwa namuumiza mzee wangu na wala sikuwaza kwamba ipo siku nitakumbuka na kumisi moment ile.

Nakupenda sana Baba yangu, Nakuombea kwa Mungu akujalie Afya na Nguvu ili uweze kuishi miaka mingi hapa Duniani.

CC Zero IQ
ni muda wako sasa na ww kumbeba mzee kwa hali namali kama yeye alivyofanya kwako si kuanza kuchakata papuchi na kumsahau mzee kabisa. kula papuchi huku unakumbuka na yale mazuri ambayo mzee amekufanyia
 
Back
Top Bottom