Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Pumzika kwa amani Baba

"Hamuwezi pata shida nikiwa Hai labda nife"
Na alikuwa mpambanaji aase Mama amekuwa akinambia kila siku ,Hata mtaa niliolelewa watu wamekuwa wakinambia..ila alivoukata ndugu wakafanya Mali zake shamba LA bibi ...na kweli Tunateseka akiwa hayupo...
Alikufa nikiwa na miaka minne...I miss you Dad
 
The hustles! Vile mzee alipambana kuhakikisha anaweka msosi mezani, ada zinalipwa, tunalala pazuri na mengineyo. Wakati tumeshiba tunaimba 'nani kama mama', mzee yuko maporini huko usiku wa manane analinda mipaka ya nchi ili tukipate hicho chakula. Fathers are the most underrated humans!
Hii kitu mimi kama mtoto wa kiume huwa inanigusa sana, yaan nikimuona mwanaume ana hizo mambo za nani kama mama au sijui hakuna kama mama huwa nakosa kumwelewa kabisa yaan, (sina maana kwamba hawana umuhimu but overrated)

Madingi huwa wanapambana sana sema ni kimya kimya na kama tujuavyo wanawake always ndio waongeaji hivyo ukimya wa Baba wakati mwingine katika familia anaweza kuonekana kama hana impact yoyote hili ni suala linalotakiwa kueleweka sana, kwamba wapo na umuhimu wao sio wa kuupimia kabisa. Kosa ni kuweka bajeti yote ya kila kitu mikononi mwa mama kwahyo watoto tunadhani kila kitu ana-provide mama..
Kwa baba yangu mpendwa, kamanda, mwamba , jembe muhimu la wakati wote kumbukumbu zake kwangu ni Maisha yangu yote hata hapa nilipo sasa, Mungu mtukufu amsamehe madhaifu na mapungufu yake yote kama mwanadamu wa kiume azidi kumpa Afya na riziki daima mpaka pale atakaporudisha namba....MUNGU ASIMAME NAWE BABA!!
 
Nakumbuka mimi nikiwa form one na mdogo wangu grade 2 tumeshuka kwenye school bus tunatembea kuelekea nyumbani. Ghafla njiani akatokea mkaka jirani yetu akaanza niambia kwanini unanikataa huku ananipiga akinituhumu najisikia sababu sisi tunapelekwa shule na gari.

Mdogo wangu akakimbia hadi nyumbani kumwambia baba na mimi nilifanikiwa kumchomoka yule kijana nikakimbilia nyumbani kufika nalia baba akinichukua hadi nyumbani kwao yule kijana, ile tunaingia tu na yule kijana kafika kwao aiseeeeee alipigwa makofi na mshua nikajua yameisha tunaenda nyumbani.

Mara baba akasema tunaenda polisi kufika polisi nikaandika maelekezo na hivi nilikua underage ikachukuliwa defender pale kuja kumkamata yule kijana yeye alikua mkubwa tukaenda polisi alichapwa fimbo na polisi jamani baadae wakanipa fimbo na mimi nijirudishie hehehehe. Tangu siku ile hakuna kijana mtaani kwetu alitusogelea kuongea ujinga.

Nakupenda sana baba Mungu akupe maisha marefu.

Ooh asante sana mwanangu. Kumbe hii ndo ID yako. Baba anakupenda sana pia😘
 
Binafsi nakumbuka siku moja hivi tuko kijijini na mzee tumepanga kesho yake tukamtembelee babu, baba yake mdogo baba ambaye alikuwa anaishi kilometa kadhaa kutoka tulipo (KM 7).

Wakati huo nilikuwa na Miaka 6, mkubwa kabisa, Sasa wakati wa safari tumetoka vizuri mimi na mzee mtu Bee (wawili) tu pale nyumbani kuelekea kwa babu.

Wakati tuko njiani nilikuwa namdekea sana baba yangu, Sasa baada ya kama Nusu safari hivi nikamrukia mzee na kumwambia nimechoka anibebe.

Mzee alinitazama usoni na kutabasamu kisha akasema unataka nikubebe mpaka wapi,mi nikamjibu mpaka kwa babu.

Mzee kweli akanichukua na kuniweka begani mpaka tumefika kwa babu, huku tukipiga story. Huwezi amini mzee alinibeba tena begani mwake wakati wa kurudi mpaka nyumbani.

Wala sikuwaza kwamba nilikuwa namuumiza mzee wangu na wala sikuwaza kwamba ipo siku nitakumbuka na kumisi moment ile.

Nakupenda sana Baba yangu, Nakuombea kwa Mungu akujalie Afya na Nguvu ili uweze kuishi miaka mingi hapa Duniani.

CC Zero IQ
Duh, safi sana! Hii story inabidi umkumbushe halafu umshukuru. Usichoke ku-express love yako kwake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namkumbuka kwa mambo 3:...1;....fimbo zilikuwa ni jadi kwetu...ilipasa kabisa tuliwa wengi mno (9), ilitusaidia kuongeza bidii ktk masomo...2;...nikiwa std 3 au 4,,,its long...tulikuwa tunaenda mlimani( sorry wachagga mtanielewa hapa) niko mbele yake natembea,,,, ghafla ninasikia "Nosspass" nikaitikia naam baba,,,dingi kwa hasira kabisa akasema...nanukuu " nani kakufundisha kutembea hivyo" nikajibu vipi.....nanukuu.." unatingisha tingisha matako pumbafu wewe .. umejifunzia wapi ?"..😀😀😀😀 nguvu ziliishia kabisa.....simsahau kabisa....3;......nikiwa mahabani na binti wa KIMARANGU (Mhanjo), dingi aliambia hapo "SIPO" dogo unapotea...nikaziba masikio......aiseeee....... siwezi msahau dingi wangu......R.I.P Mangi....🙁🙁.....alikuwa kiongozi haswaaa......
 
Namkumbuka kwa mambo 3:...1;....fimbo zilikuwa ni jadi kwetu...ilipasa kabisa tuliwa wengi mno (9), ilitusaidia kuongeza bidii ktk masomo...2;...nikiwa std 3 au 4,,,its long...tulikuwa tunaenda mlimani( sorry wachagga mtanielewa hapa) niko mbele yake natembea,,,, ghafla ninasikia "Nosspass" nikaitikia naam baba,,,dingi kwa hasira kabisa akasema...nanukuu " nani kakufundisha kutembea hivyo" nikajibu vipi.....nanukuu.." unatingisha tingisha matako pumbafu wewe .. umejifunzia wapi ?"..😀😀😀😀 nguvu ziliishia kabisa.....simsahau kabisa....3;......nikiwa mahabani na binti wa KIMARANGU (Mhanjo), dingi aliambia hapo "SIPO" dogo unapotea...nikaziba masikio......aiseeee....... siwezi msahau dingi wangu......R.I.P Mangi....🙁🙁.....alikuwa kiongozi haswaaa......
[emoji16][emoji16][emoji16] Dingi aliona unakoelekea soon wahuni watakuomba,
Dingi yako nimemkubaliiii


CC Zero IQ
 
Huwa natofautiana na dhana ya malezi ya viboko kwasababu me ni muhenga niliyelelewa pasipo viboko. Kila ukifanya kosa au mzee akisikia kitu, jioni hiyo hiyo mnakaa mezani,.. zile meza ndogo na viti vya ngozi ya ng'ombe vya kukunjwa.. anakuuliza uelezee situation ilivyo.. anakuelekeza (siyo kugombeza) uelekeo ulio mzuri.

Nilipokuwa std six na seven.. ananipa mitihani ya hesabu na science nipractise.. wakati mwingine ananipa week nzima niwe nimrmaliza.. wakati mwingine anakaa hapo kunisimamia (muda ulioainishwa ukiisha anachukua karatasi).. Baada ya week tunafanya masahihisho.

Nakumbuka mzee amewahi kunipiga mara moja tu (mara ya pili wakati anataka kunipiga nikakimbia, tukaanza kukimbizana kuzunguka nyumba.. Jioni ile nilienda kukaa na kula kwa shangazi)..

Mzee aliacha kufanya shughuli zake za kujichanga na maisha, akaamua kila atakachokipata atuendeleze sisi wanae sita kielimu..
.
.
Baada ya haya yote, ile nimemaliza chuo, nimekaa miezi miwili kitaa, nimeanza tu kazi, mwezi wa kwanza hauna salary.. mwezi wa pili ndo salary ilitoka.. My father could not live to witnes my first salary.. Sikupata nafasi ya kumnunulia hata suruali😭😭😭😭😭😭😭.

My father was a living holy spirit. Najitahidi kuishi maisha yake, ni ngumu lkn najaribu.

Roho ya Baba yangu iendelee kupata kibali na kupumzika ktk amani ya Milele. Nakupenda sana.
 
Daaah!! I miss him too much my best friend. Pacha wangu alinidekeza sanaaa, hakuwahi hata kunifinya.
Nilikuwa nikikosea akapewa kesi basi atasema "mama yangu hawezi kufanya hilo kosa" halafu atanigeukia na kuniuliza "si ndio mama?" basi naona aibu na kuanza kulia.
Then ananiambia "usilie mama yangu, najua ulipitiwa tu ila usirudie tena". This worked kuliko viboko, maana nilikuwa nampenda na kumheshimu sanaa.

RIP my love.
 
Miaka Fulani ya utoto tuliishi na babu home kama mlezi wetu. Baba na babu walikuwa wanakaa kwenye boma moja, baadaye mzee akasepa zake Dar kusaka maisha, tukabaki na babu
Kuna siku watu wote walitegeana kwenda kuchunga nikabaki mwenyewe nyumbani. ilipofika muda wa mifungo kwenda machungani nikajikuta niko mwenyewe hom😡 umri miaka 4 . Ng'ombe kama mia 2 hivi wakavunja zizi wakatoka kwenda mbugani-kulikuwa na sehemu maalum ya kuchungia, hakukuwa na shughuli ya kilimo hapo.
Mimi huyo nikafuata nyuma
Hadi babu anakuja mida ya saa 6 hivi mifugo imeshiba. Akanipenda kutokea siku hiyo. Akaahidi kunisaidia na ndiye kanifiksha hapa
 
Munaraha sana munao sifia baba zenu.

Wengine hatukuwahi kupata mapenzi ya Baba,Mzee alikuwa Kitombi balaa,Majukumu yote ya nyumbani alimuachia mama(Bahati nzuri mama alikuwa muhangaikaji).Tulikuwa tunasikia tu sifa za mzee wetu huko nje anavyo nufaisha Wanawake wengine na watoto wao.

Tulisoma kwa Tabu na ndugu yangu,Mama alikanyaga sana charahani kuhakikisha watoto wake tunafikia ndoto zetu(Ahsante Mungu tumefika si Haba).
Mbaya zaidi mzee alifanya umalaya na hakutujali lakini alikuwa MTU wakumrudisha Nyuma mama yetu,Yaaani akiwa amefulia alikuja kumuhadaa Mama na anaondoka na akiba ndogo ya pesa ambayo mama alijitunzia(Mama alimpenda sana mzee).

Hii hali ilitufanya Mimi na ndugu yangu kuanza maisha yakuhangaika na biashara tukiwa wadogo sana,nakumbuka miaka ya 90,Mama alikuwa fundi cherehani,basi alikuwa akishona vi chupi vya watoto vya mikojo,Akimaliza tunagawana njia,yeye kaskazini Mimi na ndugu yangu kusini kwenda kutembeza(kuuza),kisha tunarudi ndio tunapata chakula cha siku hiyo.

Kipindi chote sikuwa mzembe na shule,na Mungu alinibariki haswa darasani,Japo sikwenda na viatu shule nilivaa ndala,na pia sikuwahi kutumia bag wakati wote nikisoma primary na hata secondary mwanzoni,lakini nilibidiika na masomo.

Baada ya dhiki zote na kusoma kwa shida,Mama alipata tenda yakushona sare za kwaya kanisani,hapo ndipo mwanzo wa mafanikio ya familia yangu ulianzia,

Mama alitusua,namimi nilifaulu kote nilipopita,kuanzia primary, secondary na kisha chuokikuu.

Mzee alianza kuwa mpole nakujirudi baada yakuona mafanikio ya mama na walau watoto wanakuwa.

Sasa tunamtunza mzee wetu japo yeye hakufanya hivyo,lakini ni Baba yetu ni Damu yetu,tunampenda na tunafarijika walau tunaye Baba,Naamini anamajuto moyoni na amekwisha kutubu.

Wakati mwingine maisha hutokea hivyo ili kukupa msingi bora wa maisha,Mana Ile biashara yakutembeza nguo mtaani ilinijenga sana kiakili,sikuwaza kuajiriwa ktk maisha yangu hata baada ya masomo ya vyuo vikuu,Mimi ni Biashara na Biashara.

Nampenda Baba lakini kwasababu ya jina lake sio kwa Malezi kama wengine mulivyofaidi kwa Baba zenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba yangu mzembe sana. Niliishi nae kwa miaka mitatu niliyojitambua badae maisha kwake yakawa magumu naishi na mama wa kambo. Nikatoka nikaenda kuishi na watu tofauti mpaka leo. Mzee nakumbuka ashawahi ninunulia pair moja ya viatu vya shule na mkanda tu, hakuna kitu chochote alishawahi ninunulia tena wala kunilipia. Mengine niliyoomba binafsi tena ya muhimu hakunipa mfano bima, cheti cha kuzaliwa, na uhamisho wa shule.

Zamani nilikuwa na hasira na kinyongo nae lakini sio sasa. Najua hakutaka nisome na wala hana uhusiano na mafanikio yangu.
Mara ya mwisho kwenda kwake ni 2011 mara zote nakutana nae mtaani kwa kupanga kama maafisa usalama vile. Taarifa zangu anazipata kwa kusikia, taarifa zake siwezi zipata lakini najua hana maajabu.
 
Dah! Utotoni tulinyimwa fursa zote za kitoto tukapewa fursa ya kusoma tu.
Nyumba haikuwa na geti lakini tuliishi kama watoto wa getini!

Tuliona kama tunanyanyaswa na mzee, kumbe ndiyo yalikuwa malezi bora.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mara nyingi sana wazazi wanapotujenga huwa tunawaona kama wanoko ...lkn mwisho wa siku ndio tunajua walimanisha nini

sent from HUAWEI
 
Nakumbuka zamani sana nipo under 10 year mzee alikuwa na pambo la bastora ,lilikuwa linatumia hizi groli za baiskeki,alikuwa ananifundish jinsi ya kushout ,nikipiga ilikuwa inatoka sauti kubwa na cheche kiasi,sijui kama lilikuwa pambo kweli,nilipokuwa mkubwa hakuwahi kunionesha tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nakumbuka siku moja hivi tuko kijijini na mzee tumepanga kesho yake tukamtembelee babu, baba yake mdogo baba ambaye alikuwa anaishi kilometa kadhaa kutoka tulipo (KM 7).

Wakati huo nilikuwa na Miaka 6, mkubwa kabisa, Sasa wakati wa safari tumetoka vizuri mimi na mzee mtu Bee (wawili) tu pale nyumbani kuelekea kwa babu.

Wakati tuko njiani nilikuwa namdekea sana baba yangu, Sasa baada ya kama Nusu safari hivi nikamrukia mzee na kumwambia nimechoka anibebe.

Mzee alinitazama usoni na kutabasamu kisha akasema unataka nikubebe mpaka wapi,mi nikamjibu mpaka kwa babu.

Mzee kweli akanichukua na kuniweka begani mpaka tumefika kwa babu, huku tukipiga story. Huwezi amini mzee alinibeba tena begani mwake wakati wa kurudi mpaka nyumbani.

Wala sikuwaza kwamba nilikuwa namuumiza mzee wangu na wala sikuwaza kwamba ipo siku nitakumbuka na kumisi moment ile.

Nakupenda sana Baba yangu, Nakuombea kwa Mungu akujalie Afya na Nguvu ili uweze kuishi miaka mingi hapa Duniani.

CC Zero IQ
At least leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom