Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Mimi kama Tupac

They say I'm wrong and I'm heartless, but all along
I was looking for a father he was gone
I hung around with the thugs
And even though they sold drugs
They showed a young brother love
I moved out and started really hangin'
I needed money of my own, so I started slangin'
I ain't guilty, 'cause even though I sell rocks
It feels good putting money in your mailbox
I love paying rent when the rent is due
I hope you got the diamond necklace that I sent to you
'Cause when I was low you was there for me
 
nawapenda wazazi wangu wote wawili..mama amesimamia majukumu yake kutulea vyema na baba amesimamia majukumu ya kutunza familia yake pasi na ubaguzi..kinachoniuma ni kuona tu nashindwa kuwasapport kutokana na kipato changu kidogo nipatacho,nachofurahi ni ile hali ya wao kuendelea kunitia moyo katika utafutaji...Nawapenda san wazazi wangu Mungu awape maisha marefu
 
Binafsi nakumbuka siku moja hivi tuko kijijini na mzee tumepanga kesho yake tukamtembelee babu, baba yake mdogo baba ambaye alikuwa anaishi kilometa kadhaa kutoka tulipo (KM 7).

Wakati huo nilikuwa na Miaka 6, mkubwa kabisa, Sasa wakati wa safari tumetoka vizuri mimi na mzee mtu Bee (wawili) tu pale nyumbani kuelekea kwa babu.

Wakati tuko njiani nilikuwa namdekea sana baba yangu, Sasa baada ya kama Nusu safari hivi nikamrukia mzee na kumwambia nimechoka anibebe.

Mzee alinitazama usoni na kutabasamu kisha akasema unataka nikubebe mpaka wapi,mi nikamjibu mpaka kwa babu.

Mzee kweli akanichukua na kuniweka begani mpaka tumefika kwa babu, huku tukipiga story. Huwezi amini mzee alinibeba tena begani mwake wakati wa kurudi mpaka nyumbani.

Wala sikuwaza kwamba nilikuwa namuumiza mzee wangu na wala sikuwaza kwamba ipo siku nitakumbuka na kumisi moment ile.

Nakupenda sana Baba yangu, Nakuombea kwa Mungu akujalie Afya na Nguvu ili uweze kuishi miaka mingi hapa Duniani.

CC Zero IQ
Nimependa Andiko lako limenigusa sana, Tumefanana kias.
Hakuna kama Baba.
 
nawapenda wazazi wangu wote wawili..mama amesimamia majukumu yake kutulea vyema na baba amesimamia majukumu ya kutunza familia yake pasi na ubaguzi..kinachoniuma ni kuona tu nashindwa kuwasapport kutokana na kipato changu kidogo nipatacho,nachofurahi ni ile hali ya wao kuendelea kunitia moyo katika utafutaji...Nawapenda san wazazi wangu Mungu awape maisha marefu
Amina Kubwa
 
Eeeeh Jah endeleaa kumtunza baba angu!!! Nizidi kufaidi na kushuhudia mengi mazuri na makuu kwake.

Baba angu ni kiongozi wa maisha yangu, ni mlezi wa mambo yangu, ni kila kitu kwangu, siwezi elezea yote kwan sitamaliza.

Kikubwaa baba angu, wakati wa lile suala ambalo sio zuri na jema machoni Pa watu au jamii, lililokuwa kwangu, lakini wee hukujali jamii na watu wa nje watakuonaje au watakutazamaje km mzazi, lakini ulisimama na mie.
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Baba nakumbuka maneno haya,
"mwanangu kila mtu ana madhaifu na mapungufu yake, usionee unanyooshewa kidolee hata wao wana yao ambayo yakijulikana vidolee vitageukia kwao kabla havijakugusaa wee, najua inauma mnoo km mzazi ila haitobadilisha kuwa wee sio mwanangu, wee ni mwanangu na utabaki kuwa mwanangu milele, kikubwa nacho kuomba epuka madhaifu na mapungufu yako kuwa kikwazo kwa wengine, epuka kujipa umuhimu kwenye maisha ya watu au pasipostahili, najua wee ni msomi na unaelewa, ishi maisha yako binafsi, mimi, mama yako na ndugu zako wote tunakupendaa sanaaa na tupo pamoja na wee"

Baba maneno haya ndo msingi na nguzo kwangu, ndo kanuni na taratibu ya maisha yangu. Ubarikiwe sanaaaa baba yanguu.

NAKUPENDAAA SANAA, [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimba za shuleni
 
Mda mfupi kabla hajafariki "mwanangu ujue maisha ni mchezo, cheza vizuri kwa amani" akafunga macho. Lala kwa amani baba. Mengi nimeyaona na hakika maisha ni mchezo.
 
Back
Top Bottom