Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Bwana Mushi hupaswi kuendelea na kazi kutokana na hali uliyo nayo..yafaa uwe nyumbani na familia ...Jibu la mzee Wanangu hawastahili shida labda niwe nimekufa...
Hapo ni baada ya kupata ajali na kupata hitilafu kwenye uti wa mgongo...nachokumbuka ..ilifika hatua hawezi kutembea still alitaka kwenda kupambana..
Tulikuwa hatununuliwi pipi ila mifuko ya pipi, Kama ni sikukuu Atanunua kila kitu in bulk, crates za soda mavazi, chakula, nk, , , Alikuwa na moyo wa kutoa ... Vitu hivyo havikuw vyetu peke yetu...Akifika utasikia Mama juma njoo chukua hivi ,mama fulani, , , , Then Wewe J chukua hizi wapelekee marafiki zako.......
KIZURI HAKIDUMU
Moment ambayo naipenda Alikuwa ananuka sana miguu so kazi Yangu kama sijalala akija Tuuu naanza kumwambia baba vua viatu hapo mlangoni unawe ...atacheka ataniita mwanangu J njoo univue viatu then ataninusisha...😅
....Nina mengi juu ya mshua ila alipendwa zaidi...
Rest in peace father

Nimepitia mengi sana ila nilipo afadhali...Ipo siku nitashusha nondo za life langu humu.😭😭😭
Dada kabaki kusema KAMA BABA ANGEKUWEPO
 
NAOMBA UMAKINI WENU NA PIA TOENI PREJUDICES

Dada angu alivoolewa hakubahatika kupata mtoto mapema. nikiwa nakaribia kuanza darasa la kwanza, Shem akaja home kwa baba na mama akawaomba niende kuishi nae. Mzee alimsisitiza kuwa huyu mkorofi kama kuchapa chapa kweli.

Nimelewa na shem kama baba angu mzazi .Kanifundisha vingi kilimo na tabia njema .Sijawahai maliza tamka neno lolote kinywani kuhusu mahitaji yangu asinitimizie.lAinidekeza na kunionya sana.
Ladha ya viboko vyake haifanani na mtu mwingine aliyewahi kunichapa.

Yeye hunifundisha kimyakimya sio muongeaji. Kaniambukiza u introvertHata leo hii nikipata nafasi huwa naenda kumsaidiankazi zozote iwe nyumbani au hata shamba.Huku akinipa a to z kuhusu hiyo kazi tunayoifanya kiti ambcho nimepata maarifa mengi sana.
Hapendi uchafu ,Utotoni nimekula sana stick kisa nilikuwa sijui kufua.Aikuwa anaaka maji nayosuuzia nguoxmara mwisho yawe masafi masafi kama nilivyochota.

Anapenda niwe smart muda wote.Ana sikuxyake special ya kupiga pasi huo upanga wake nzi akijipitisha tu tu lazima akatike tu
Anapenda niwe sharp muda wote .Kanifanya nipende sana baiskeli mpk leo .Asa enzi hizo uende na baiskeli shamba afu irudi bila hata mzigo wa kuokoteza.

Kuna siku nikiwa likizo kipindi o level basi alini mind sana kwa kuwa nilikiwa tu kufanya kazi nachill geto basi akafoka eti wenzako wanafanya mazoezi ya mpira wewe umekaa hovyo tu.

Baba angu mzazi sijaishi nae sana ila na miss alikuwa akitupikia akipata time na malezi vile vile.

KiUFUPI NAJIVUNIA HAWA WARU WAWILI
 
stori nzuri ,lakini hujaimalizia kuna kitu unaficha , atakua alikuchapa ila upunguze kudeka
 
Alikuwa mtu mwema sana.

Siwezi kusahau, siku natoka mkoa na watoto wangu, tulikutana na baba njiani karibu na kanisani. Alinipokea akarudi nyumbani.

Baadaye kidogo alitoka tena nikajua anaenda kwenye ile safari yake, kumbe ameenda buchani kununua nyama. My God my Lord, alikuwa mtu mwema sana; they killed him.

Endelea kupumzika Salama huko Mbinguni Mzee Izaki, ipo siku tutakutana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah! Pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
-Nakumbuka trip za kunipeleka maktaba kusoma vitabu, then madrasa then tunaenda kumalizia home schooling. Nilivichukia sana vitabu vya English aid na atlas maana vilikuwa ndo vitabu vyake pendwa.

- alijitoa sana kuhakikisha napata elimu bora na kunitimizia mahitaji yote kwa wakati. Ilikua ukitaja kuhusu shule tu chap chap anakutimizia.

-lastly, na-miss swala za jamaa na trip zetu za kwenda msikitini. On his last days on this earth mi ndo nilikua imam wake[emoji24][emoji24] katika swala, until the day he couldnt pray no more due to sickness. Nikirudi home nikiingia chumba chetu cha kuswalia nabaki kulia tu. I miss you very much Big man.

.... he always insisted kuwa nikitaka kufa maskini basi niamke wakati jua limeshachomoza, early birds eat fresh worms. Mwenyezi mungu akusamehe makosa yako na akuweke peponi in shaa allah[emoji172].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wangu Jembe sana ni moja kati ya wazee wapole sana duniani alishawahi kunichapa mara mojaaa tuu katika maisha yangu ni mtu ambae nikifanya kosa atalibeba kama lake lakini tatizo likiisha atakuonya. Mungu ampe maisha marefu huyu mzee siku moja nataka nimfanyie kitu kikubwa sana ambacho kitamfanya afurahi sana He is really a fighter..warrior... My hero!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kunilipia ada..kunipeleka shule..kunipatia nilichokihitaji kilichopo ndani ya uwezo wake..alikuwa radhi kuchelewa kazini lakini Mimi nifike shule.

Wakati nipo kidato Cha nne ile siku mvua ilinyesha kubwa Sana niliwahi kutoka shule kumbe nayeye alikuwa amenifuata shule..tukapishana baba wa watu alizunguka msimbazi na kariakoo yote kunitafuta..nimefika nyumbani saa tatu kasoro mzee wa watu kaingia saa nne..na wasiwasi mwingi masikini Baba yangu nilimuonea huruma..asubuhi akaniuliza Kama nipo salama ..akahakikisha kanipeleka shule nayeye akaenda kazini.


Namkumbuka sana



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Apumnzike kwa amani baba yangu huko aliko.
Japo nilikuwa mdogo sana nakumbuka baba alinipenda sana yaani kama mtu na mfuasi wake.Kila sehemu alikuwa kanibeba na alininunulia chochote niliçhopenda.
Bahat mbaya Vizuri havidumu Only nikiwa na 4yrs mzee wangu alifariki lakini mpaka leo hii anaishi kwenye kumbu kumbu Zangu.
Nakumiss sana Baba Yangu lakini ndio hivyo kazi ya Mola haina Makosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawai kuishi na wazazj wangu kwaiyo mengi ninayoyakumbuka ni nasaa nyingi wanazotoa juu yangu kuusu maisha na mahusiiano ila kaulii hii ya baba haijapotea akili mwangu nanukuu "ada siwezi kukulipia mwambie mama yako aliyekupeleka shule" aisee ni miaka mingi sana imepita ila sijawai isahau hii kauli ila Mungu ambariki maana ndyo wangu baba nafurahi kumuona akiwa na afya njema na namsifu kwa kupambania maisha yake maana kwa aliyopitia angekuwa mwingine saivi angekuwa kashapoteza muelekeo wa maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIKUMUONA SIKUMJUA NLIAMBIWA TU AMESHAFARIKI...sina upendo wowote kwa mzee wala sikumbuki chochote kuhusu yeye.,RIP
Inaonyesha asilimia kubwa wazee wetu hutangulia kuliko mama.
Binafsi sikumbuki vizur maneno ama malezi yake.Aliniacha nikiwa na miaka 6Ila kuna kitu kimoja huwa hakitok kichwani, mzee alikuwa mtu wa kupiga kambi huko kwenye shughuli zake, kuna kipindi niliumwa ilibidi arudi kwa ajili yangu na nakumbuka alikuja na zawad ya biskut(MARIE BISCUT),siku hiyo nilitamba sana hata kaka zangu ilibid wawe wapole ili niweze kuwapatia kidogo!!

"And the best that you can hope for
Is to die in your sleep."(Others ar usless)
 
Safi
Binafsi nakumbuka siku moja hivi tuko kijijini na mzee tumepanga kesho yake tukamtembelee babu, baba yake mdogo baba ambaye alikuwa anaishi kilometa kadhaa kutoka tulipo (KM 7).

Wakati huo nilikuwa na Miaka 6, mkubwa kabisa, Sasa wakati wa safari tumetoka vizuri mimi na mzee mtu Bee (wawili) tu pale nyumbani kuelekea kwa babu.

Wakati tuko njiani nilikuwa namdekea sana baba yangu, Sasa baada ya kama Nusu safari hivi nikamrukia mzee na kumwambia nimechoka anibebe.

Mzee alinitazama usoni na kutabasamu kisha akasema unataka nikubebe mpaka wapi,mi nikamjibu mpaka kwa babu.

Mzee kweli akanichukua na kuniweka begani mpaka tumefika kwa babu, huku tukipiga story. Huwezi amini mzee alinibeba tena begani mwake wakati wa kurudi mpaka nyumbani.

Wala sikuwaza kwamba nilikuwa namuumiza mzee wangu na wala sikuwaza kwamba ipo siku nitakumbuka na kumisi moment ile.

Nakupenda sana Baba yangu, Nakuombea kwa Mungu akujalie Afya na Nguvu ili uweze kuishi miaka mingi hapa Duniani.

CC Zero IQ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na mm kwa nini unanikataa
Nakumbuka mimi nikiwa form one na mdogo wangu grade 2 tumeshuka kwenye school bus tunatembea kuelekea nyumbani. Ghafla njiani akatokea mkaka jirani yetu akaanza niambia kwanini unanikataa huku ananipiga akinituhumu najisikia sababu sisi tunapelekwa shule na gari.

Mdogo wangu akakimbia hadi nyumbani kumwambia baba na mimi nilifanikiwa kumchomoka yule kijana nikakimbilia nyumbani kufika nalia baba akinichukua hadi nyumbani kwao yule kijana, ile tunaingia tu na yule kijana kafika kwao aiseeeeee alipigwa makofi na mshua nikajua yameisha tunaenda nyumbani.

Mara baba akasema tunaenda polisi kufika polisi nikaandika maelekezo na hivi nilikua underage ikachukuliwa defender pale kuja kumkamata yule kijana yeye alikua mkubwa tukaenda polisi alichapwa fimbo na polisi jamani baadae wakanipa fimbo na mimi nijirudishie hehehehe. Tangu siku ile hakuna kijana mtaani kwetu alitusogelea kuongea ujinga.

Nakupenda sana baba Mungu akupe maisha marefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulipokua wadogo baba yetu alikua mkali sana alikua anapiga kama anapiga magunia,
Alikua anatupenda sana alitupeleka kutembelea national parks enzi izo.,Ni baba bora sana

Na wakati huu ambao mama yetu anaumwa na inambidi awe hospital mda mwingi baba ndo anayebaki nyumbani na watoto,kuwaangalia,kuwapikia na kufanya kazi zote ambazo mama alikua anafanya.

Nakupenda Baba Bwana Yesu azidi kukutunza,akuweke kwa ajili yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom