Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

vipi mzee alikula kona nini? unaweza ukaona unamlaumu bure tu kumbe sio baba ako mama ako alimbambikia

Hittin Blunts And Bustin Nuts
No he's my real father na hakuwahi nikataa na alifanya hadi maboresho kwenye jina lake kwenye chet changu cha kuzaliwa liliandikwa vibaya na mm nikalekebisha kuanzia hapo skull nk..
 
Namkumbuka kwa mambo 3:...1;....fimbo zilikuwa ni jadi kwetu...ilipasa kabisa tuliwa wengi mno (9), ilitusaidia kuongeza bidii ktk masomo...2;...nikiwa std 3 au 4,,,its long...tulikuwa tunaenda mlimani( sorry wachagga mtanielewa hapa) niko mbele yake natembea,,,, ghafla ninasikia "Nosspass" nikaitikia naam baba,,,dingi kwa hasira kabisa akasema...nanukuu " nani kakufundisha kutembea hivyo" nikajibu vipi.....nanukuu.." unatingisha tingisha matako pumbafu wewe .. umejifunzia wapi ?"..😀😀😀😀 nguvu ziliishia kabisa.....simsahau kabisa....3;......nikiwa mahabani na binti wa KIMARANGU (Mhanjo), dingi aliambia hapo "SIPO" dogo unapotea...nikaziba masikio......aiseeee....... siwezi msahau dingi wangu......R.I.P Mangi....🙁🙁.....alikuwa kiongozi haswaaa......
huyo binti wa kimarangu bado upo naye?

Hittin Blunts And Bustin Nuts
 
Ila MUNGU awasamehe mama zetu wamekuwa mstari wa mbele kuwafitisha baba na watoto wao na kujiweka wao kuwa ndio waliplay role kubwa sana kumbe mzee ndie mshika usukani ambae amesababisha familia kufika mbali.

Ila wengi wa akina mama huwanza kuleta ajenda za kibaguzi ili kuwafitini watoto na baba zao ili wao waweze kupewa kipaumbele......!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila siku mzee wako anakupa malalmiko kuhusu baba ako lakini baba ako huwezi kusikia akiyasema madhaifu ya mama ako

Hittin Blunts And Bustin Nuts
 
Mi nakumbuka baada ya kututelekeza nilikua nikienda kwa wale family friend wa zamani wakati baba yupo.nikiulizia marafiki zangu wa utotoni.unaambiwa tu ..yupo nairobi anasoma huko...ukienda huku unaambiwa yupo sekondari fulani kampala.hata levo za vyuo ni huko huko.nikawa nawaza mzee asingetutosa tungesoma vizuri.kwakuwa alikuwa na kipato kizuri.na hata ajira isingekuwa ishu ni mtu mwenye koneksheni ya kibabe sana.nikikumbuka wakati wa kuomba misaada ya ada kwa marafiki zake wakati uwezo alikuwa nao kuwazidi .machozi yalikuwa yanamwagika sana.nilijenga chuki isiyokwisha mpaka leo.kwakweli simpendi hata kidogo.yaani simpendi kwelikweli.

Sent using Jamii Forums mobile app

nimeusoma huu uzi watu wanawapenda wazazi wao, wengine wanawakumbuka kwa kuwa wameshatangulia mbele za haki nimekosa furaha kabisa ,i feel sad
wengine waliishi maisha ya furaha utotoni sisi wengine hatukupata hiyo bahati , unakua na mzazi lakini huna tofauti na yatima !!!

Pole sana mkuu.
 
Mungu amuweke Mahali Pema peponi nafikiria kuandika kitabu khs maisha yke Kuna mengi sna amefanya juu yetu watt wake na Jamii yke kikubwa zaidi kauli yke. mie nmechukua mpira nmempiga chenga mpk goli kipa kazi kwenu kufunga au kutoa njee...R. I. P MWAMBA WA KIZARAMO...
IMG-20200402-WA0149.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ulikuwa unaishi kijiji gani?

Hittin Blunts And Bustin Nuts

Kwakweli mimi sikuwahi kuishi kijijini bali niliishi katika mjini fulani maarufu huko Kigoma hadi napata akili za kujitambua, na niliposema jambo hilo kuhusu baba yangu nilikuwa tu nafanya "imagination" kwa jinsi nilivyokuwa namfahamu baba yangu. Juu ya yote aliweza kutufundisha na kuishi katika hali zote za maisha, alikuwa ni mlezi mwema.
 
Ninachokumbuka tambo zake tuu oooh mimi nilioa na miaka 16 na blah blah kibao.Mke wake wa Mwanza kuniuzisha barafu ndio niende shule,siku mdogo wangu alipokunywa dawa afu yeye ,mkewe na ndugu wengine hawana habari mpaka mama jirani alipomuokoa (sababu ya njaa dogo akafikiri dawa ni msosi).Huyu mama nilishaenda kumuona na bado tunamjali ka mama yetu.Chakufurahisha dogo kaolewa mtaa wa mbele kidogo na huyo mama.Siku aliyoniambia mimi nina watoto wengi sitegemei uje unizike au unisaidie.Kwa kifupi hatuna stori kila mtu na mpango wake.
 
Ila MUNGU awasamehe mama zetu wamekuwa mstari wa mbele kuwafitisha baba na watoto wao na kujiweka wao kuwa ndio waliplay role kubwa sana kumbe mzee ndie mshika usukani ambae amesababisha familia kufika mbali.

Ila wengi wa akina mama huwanza kuleta ajenda za kibaguzi ili kuwafitini watoto na baba zao ili wao waweze kupewa kipaumbele......!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mama yetu yupo tofauti.huwa anapenda tushirikiane na baba yetu.lakini sisi ndio tuliamua moja kwamba " kila mtu ashinde mechi zake".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa na tabia ya kupigana na dada yangu tunayefuatana sasa Baba kila siku tukipigana alikuwa ananigombeza tu ila nadhani siku ile alichoka, basi baada ya kupigana akaniita na kunifungia chumbani kwao na kuanza kunipa bakora , sasa kule chumbani kwao kitandani kulikuwa na ile neti ya duara basi baada ya kuona fimbo zimezidi nikajikuta napanda kitandani na kujiviringisha na ile neti na hii ni katika hali ya kukwepa hapo ilikuwa imekunjwa basi nilijiviringisha huku anaendelea kunichapa mwisho wa yote nikaitaka ile neti na kudondoka nayo pale kitandani nahisi huyu mzee ndio akapata huruma nikaponea hapo akaishia kunigombeza tu halafu huyo akatoka zake.

Huwa nikikumbuka kile kichapo saa nyingine nasema yule Mzee ni balaa.
 
Acha tu Mkuu.. Wakati naandika nimekuta nakumbuka vitu vingi sana hadi nikaanza kulia..

Sent using Jamii Forums mobile app

Mliobahatika kuwa na wazazi hadi sasa, msi-assume tu kuwa wanatambua mnawapenda.... inua mdomo wako na umwambie kwa neno lako.

Hasa baba wengi wanachukuliwa poa sana eti hustles zote zile ilikuwa wajibu wake, no wonder baba anakufa mapema.... b’se in most cases watoto wakishakua tu hana chake kila siku utasikia ‘nani kama mama’.

Don’t take baba for granted.
 
Ni kweli Mkuu.. Niseme tu kuwa pengine sipati Wasaa wa kumueleza Baba yangu Upendo wangu kwake..Ila ndani ya moyo wake anatambua.

Baba yangu ni wa pekee jamani.. Haishi kunizungumzia kwa Watu.. kubwa kuna watu wananifahamu kwa kunisikia ila hawanijui.. Nimemkataza mno.. alichoniambia kwenye hilo nimsamehe ili hawezu kuacha... Ki binadamu namwelewa ila nachukia..

Yote kwa yote.. Aliwahi kuniambia.. Mwanangu naomba kama ni kifo mimi nitangulie.. Unizike.. Ukiondoka ukaniacha Maisha hayatakuwa na Maana tena kwangu.[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]Ndiyo maombi yake.. Na ndugu zake hadi Mama yangu anawaambia hivyo.. Mkuu Mungu alinipa Baba wa kipekee sana.. Hata neno Nampenda sidhani kama linamstahili..

Nakumbuka mimi nikiwa form one na mdogo wangu grade 2 tumeshuka kwenye school bus tunatembea kuelekea nyumbani. Ghafla njiani akatokea mkaka jirani yetu akaanza niambia kwanini unanikataa huku ananipiga akinituhumu najisikia sababu sisi tunapelekwa shule na gari.

Mdogo wangu akakimbia hadi nyumbani kumwambia baba na mimi nilifanikiwa kumchomoka yule kijana nikakimbilia nyumbani kufika nalia baba akinichukua hadi nyumbani kwao yule kijana, ile tunaingia tu na yule kijana kafika kwao aiseeeeee alipigwa makofi na mshua nikajua yameisha tunaenda nyumbani.

Mara baba akasema tunaenda polisi kufika polisi nikaandika maelekezo na hivi nilikua underage ikachukuliwa defender pale kuja kumkamata yule kijana yeye alikua mkubwa tukaenda polisi alichapwa fimbo na polisi jamani baadae wakanipa fimbo na mimi nijirudishie hehehehe. Tangu siku ile hakuna kijana mtaani kwetu alitusogelea kuongea ujinga.

Nakupenda sana baba Mungu akupe maisha marefu.
Umeshaolewa?
 
Ni kweli Mkuu.. Niseme tu kuwa pengine sipati Wasaa wa kumueleza Baba yangu Upendo wangu kwake..Ila ndani ya moyo wake anatambua.

Baba yangu ni wa pekee jamani.. Haishi kunizungumzia kwa Watu.. kubwa kuna watu wananifahamu kwa kunisikia ila hawanijui.. Nimemkataza mno.. alichoniambia kwenye hilo nimsamehe ili hawezu kuacha... Ki binadamu namwelewa ila nachukia..

Yote kwa yote.. Aliwahi kuniambia.. Mwanangu naomba kama ni kifo mimi nitangulie.. Unizike.. Ukiondoka ukaniacha Maisha hayatakuwa na Maana tena kwangu.[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]Ndiyo maombi yake.. Na ndugu zake hadi Mama yangu anawaambia hivyo.. Mkuu Mungu alinipa Baba wa kipekee sana.. Hata neno Nampenda sidhani kama linamstahili..

Sent using Jamii Forums mobile app
We ni kama mimi ,baba yangu hakuwa na uwezo lakini nafeel ule Upendo wake wa dhati kabisa kwangu ukizingatia mimi ndio mtoto wa kiume pekee katika familia

CC Zero IQ
 
Back
Top Bottom