Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Kipondo kikubwa hata kwa kosa dogo. I hate my dady

Sent using Jamii Forums mobile app
duh!! yupo hai bado baba yako?

mimi nimekula fimbo sana kwa baba yangu yani nilikua napigwa hivo hivo kosa dogo stiki lakini nilivyoenda secondary tu baba alikua my best friend sikupigwa hata kibao Mungu ampe kauli thabiti baba yangu,
 
I have a lot to say about my Father..

Ingawa ana uwezo wa kawaida tu kimaisha lakini thamani ya anayoyaonyesha ni zaidi ya uwezo alionao.. Huwa naomba Kila siku, Mungu amjaalie miaka mingi, abariki jitihada zangu zikazae matunda, nirudishe fadhila zangu japo kiuhalisia hazitofikia kile alichokifanya kwetu

LIVE LONG MY FATHER ✊✊
 
Mungu ampe maisha marefu baba yangu kipenzi na afya njema.

Nakumbuka mwaka 2018 nilijifungua binti yangu nyumbani kwa mchumba wangu mtoto alipotimiza mwezi mmoja nikampeleka nyumbani kwetu ili ndugu zangu pia wamsalimie. Nilifika nyumbani kipindi mama amesafiri kikazi so tukawa mimi na baba na kichanga wangu tuu.

Baba yangu alikuwa anaamka saa 11 ananipikia chai ya rangi anajaza chupa, ananipikia maziwa anajaza pia chupa anapika na uji ukiamka unakuta mezani kaweka yeye ameondoka. Mchana anarudi ananipikia chakula, na jioni hakutaka niingie jikoni kupika zaidi ya kujihudumia mimi na mtoto. Alikuja dada yangu kunisaidia lakini still baba hakuacha kunipikia kuanzia asubuhi mpaka usiku.

Yaani naamka asubuhi kila kitu kipo siku nyingine amepika supu sufuria nzima kwa ajili yangu. Nilikaa mwezi mzima nikarudi kwa baba mtoto wangu ila baba yangu alinihudumia vizuri kuliko hata nilivyohudumiwa ukweni baada ya kujifungua.

Namshukuru sana na ninamwombea heri, bond aliyo nayo na mjukuu wake mpaka sasa inatoka moyoni kabisa. Nakupenda baba yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daima nitamkumbuka mzee wangu kwa kujitolea kila alichonacho kuhakikisha watoto wake hawakosi. Kanipa elimu bora kadri ya alivyoweza japo yeye mwenyewe hakulijua hata darasa moja. Inasikitisha tu kuwa hakuishi kuja kuona japo kidogo ya matunda ya jitihada zake kwangu. Wengi wetu tulichukulia poa kila tulichopewa na wazazi , kutokutambua ni jinsi gani walijihini ili sisi tupate.
Rest in peace pa, Allah akuweke katika daraja lillo bora zaidi huko ulipo. Amiin.
Allahuma Amin
Ukipata wasaa mtolee sadaka
 
MI MZEE WANGU STICK PRIMARY LABDA ILA SEHEMU YOYOTE NILIYOSOMA SIJAWAHI KUWA NA SHIDA YA SCHOOL FEES WALIOLIPA ADA NILIKUWA MIONGONI MWAO SIJAWAHI KUTOLEWA CLASS KISA AXA ,VITABU KATIKA KILA LEVEL NILIJUWA NAVYO R .I.P TO HIM AMENIFU ZA ATA MIMI NIKIWA NA WATOTO WASIPATE SHIDA IZO
 
Huu Uzi ni wa kutiana machungu tu.

Huu Uzi pia unakumbusha upendo wa baba ni upendo wa Mungu.

Huu Uzi unatutaka wababa Vijana kumbuka nafasi zetu bila kutaka sifa.

Huu Uzi unatukumbusha baba ndiye mwenye uwezo wa kubaliki kizazi chake.

Huu Uzi unatukumbusha Wacha wamama wasifiwe kwa sababu ndio asili inavyotaka.

Huu Uzi unatukumbusha nafasi ya baba ipo toka milele na haiwezi kubadilishwa.

Huu unatukumbusha mtoto akikosa malezi ya baba basi atakuwa na chuki nawe mpaka siku aingiapo kabulini.
 
Binafsi nakumbuka siku moja hivi tuko kijijini na mzee tumepanga kesho yake tukamtembelee babu, baba yake mdogo baba ambaye alikuwa anaishi kilometa kadhaa kutoka tulipo (KM 7).

Wakati huo nilikuwa na Miaka 6, mkubwa kabisa, Sasa wakati wa safari tumetoka vizuri mimi na mzee mtu Bee (wawili) tu pale nyumbani kuelekea kwa babu.

Wakati tuko njiani nilikuwa namdekea sana baba yangu, Sasa baada ya kama Nusu safari hivi nikamrukia mzee na kumwambia nimechoka anibebe.

Mzee alinitazama usoni na kutabasamu kisha akasema unataka nikubebe mpaka wapi,mi nikamjibu mpaka kwa babu.

Mzee kweli akanichukua na kuniweka begani mpaka tumefika kwa babu, huku tukipiga story. Huwezi amini mzee alinibeba tena begani mwake wakati wa kurudi mpaka nyumbani.

Wala sikuwaza kwamba nilikuwa namuumiza mzee wangu na wala sikuwaza kwamba ipo siku nitakumbuka na kumisi moment ile.

Nakupenda sana Baba yangu, Nakuombea kwa Mungu akujalie Afya na Nguvu ili uweze kuishi miaka mingi hapa Duniani.

CC Zero IQ
Endelea kupumzika kwa amani baba angu.
Sa hii nina mtoto mrembo lkn nkiitizama picha ako anafanana na ww pia.
Sikuwai kufikilia kukupoteza maumivu nlonayo hayajawai kua na ahueni
Ndugu zako wamechukua mali zote nilichoambulia mim ni t-shirt zako mbili ambazo nikikukumbuka hua navaa, picha zako na kumbukumbu yako moyoni kwangu.

Nakuombea kwa Mungu kila siku azidi kukupunguzia adhabu ya kaburi Amen
 
Chukua hiyo Fridge ndogo, Jiko la gas na vyombo kahdaa vya kupikia, kitanda na godoro pia, Kodi tutakulipia ya miezi 6, ikawa mwanzao wa kuanza maisha ya kujitegemea. Nawashukuru sana washua kwa hili kwa kweli sikuanza vibaya maisha ya kujitegema!!!
 
Mimi na mdogo wangu kuna siku tulitwangana makonde vikali sanaaa..mzee alikuwa zake ndani si tulikuwa sebleni.

Aliposkia akatoka kuja sebleni,alituuliza chanzo cha ugomvi nikamueleza”dogo amemaliza msosi wake akaanza kulazimisha kula chakula cha mama,anataka mama asile ale yeye”.

Mi namkataza yeye akanitukana nikamzibua kichwa,akanirushia stuli.

Mzee akamzabua dogo kofi akarudi zale ndani.

Dogo sasa kujenga bifu na mimi kisa mi sjapigwa kapigwa yeye peke ake.

Mzee akanotice kuwa mi na dogo haziivi kwa simu kama mbili hivi,siku moja akarudi jioni,akatuchukua tukatoka kwenda kutembea,tukiwa huko akatushika mikono ye akiwa katikati..

Akawa anatukumbusha sisi ni ndugu ma hatupasi kununiana hata kqa sababu yoyote ile.

Tuliongea mengi sana usiku ule tuliwa njiani,tulipofika home tukaanza tena kupiga story na dogo.

MZEE WANGU ALIKUWA ANAPENDA NDUGU TUWE WAMOJA.

R.I.P mzee[emoji1488][emoji26]
 
Kuna kitabu kinaitwa "SOMA KWA HATUA".
kitabu sikipendi Kileee kimeniliza sanaa
Dingi akitoka kazini anaanza kunifundisha.
Nikikosea tu bakora za maana..
Kipindi hicho baba kanunua TV na deki..
Nikirudi mchana mimi tv tu nacheki mikanda.
Phantom solder,eastern condors,Rambo anold baba jeni..
Ila usiku ukianza kuingia nakuwa mpole maana najua baba akirudi ataniita anifundishe na bakora juu

Sent using Jamii Forums mobile app

Ulikuwa unakisoma chá nin??
 
Mimi hadi leo, sipitwi na amka na bbc, sauti ya ujerumani(saa saba na 12 jioni), bbc jioni, sauti ya amerika, na hekima yake hii.

Siku moja Mother sijui alizingua nini, akawa amemfokea mbele yetu, sijui alinotice nini, akaitisha kikao na sisi , akatueleza Mama yenu alifanya moja na mbili that's why nilifoka ila mambo yapo sawa.
 
Nakumbuka mambo mengi ila zaidi mzee wangu hakuwa mtu wa kupenda kufanyiwa chochote. Mpaka anafariki akiwa na 77yrs alikua anafua mwenyewe, anapika mwenyewe, chumba anacholala anasafisha mwenyewe anasema hajazoea kumtegemea mtu kumfanyia chochote. Shida moja alikua mkali yule mzee sijapata ona ila namshukuru sababu kupitia ukali wake watoto wake hadi tumekuwa wakubwa ujinga tuliweka pembeni vinginevyo moto utakuwakia.

R.I.P dear father, miaka 9 sasa bila wewe. Namshukuru Mungu kwa kila kitu.
 
Munaraha sana munao sifia baba zenu.

Wengine hatukuwahi kupata mapenzi ya Baba,Mzee alikuwa Kitombi balaa,Majukumu yote ya nyumbani alimuachia mama(Bahati nzuri mama alikuwa muhangaikaji).Tulikuwa tunasikia tu sifa za mzee wetu huko nje anavyo nufaisha Wanawake wengine na watoto wao.

Tulisoma kwa Tabu na ndugu yangu,Mama alikanyaga sana charahani kuhakikisha watoto wake tunafikia ndoto zetu(Ahsante Mungu tumefika si Haba).
Mbaya zaidi mzee alifanya umalaya na hakutujali lakini alikuwa MTU wakumrudisha Nyuma mama yetu,Yaaani akiwa amefulia alikuja kumuhadaa Mama na anaondoka na akiba ndogo ya pesa ambayo mama alijitunzia(Mama alimpenda sana mzee).

Hii hali ilitufanya Mimi na ndugu yangu kuanza maisha yakuhangaika na biashara tukiwa wadogo sana,nakumbuka miaka ya 90,Mama alikuwa fundi cherehani,basi alikuwa akishona vi chupi vya watoto vya mikojo,Akimaliza tunagawana njia,yeye kaskazini Mimi na ndugu yangu kusini kwenda kutembeza(kuuza),kisha tunarudi ndio tunapata chakula cha siku hiyo.

Kipindi chote sikuwa mzembe na shule,na Mungu alinibariki haswa darasani,Japo sikwenda na viatu shule nilivaa ndala,na pia sikuwahi kutumia bag wakati wote nikisoma primary na hata secondary mwanzoni,lakini nilibidiika na masomo.

Baada ya dhiki zote na kusoma kwa shida,Mama alipata tenda yakushona sare za kwaya kanisani,hapo ndipo mwanzo wa mafanikio ya familia yangu ulianzia,

Mama alitusua,namimi nilifaulu kote nilipopita,kuanzia primary, secondary na kisha chuokikuu.

Mzee alianza kuwa mpole nakujirudi baada yakuona mafanikio ya mama na walau watoto wanakuwa.

Sasa tunamtunza mzee wetu japo yeye hakufanya hivyo,lakini ni Baba yetu ni Damu yetu,tunampenda na tunafarijika walau tunaye Baba,Naamini anamajuto moyoni na amekwisha kutubu.

Wakati mwingine maisha hutokea hivyo ili kukupa msingi bora wa maisha,Mana Ile biashara yakutembeza nguo mtaani ilinijenga sana kiakili,sikuwaza kuajiriwa ktk maisha yangu hata baada ya masomo ya vyuo vikuu,Mimi ni Biashara na Biashara.

Nampenda Baba lakini kwasababu ya jina lake sio kwa Malezi kama wengine mulivyofaidi kwa Baba zenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenitoa machozi Mkuu,I have gone through the same steps...ila ni Maisha I love that Woman,she sacrificed everything to make us a living
 
Back
Top Bottom