Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Me nakumbuka alinilipia ada ya mitihani ya kumaliza sec huku akiwa anaumwa hoi na akihitaji wa pesa pia ili aendelee na matibabu
Masikini Baba yangu saa chache baada ya kumaliza mitihani furaha yangu ikakatizwa [emoji24][emoji24][emoji24] baada ya kurudi home na kukuta msiba[emoji24][emoji24][emoji24]
Ulikuwa ni upendo wa ajabu sana kwa mzee, na kuna kitu alikugunza sidhani kama utasahau kujitoa

sent from HUAWEI
 
Sisi wengine tumelelewa na singo Mother tu kwa kuwa walishaachana. Nakumbuka mara yangu ya kwanza (na hiyo ikawa ya mwisho kumuona) ilikuwa pale ofisini kwake (Wizara ya Afya). Nilikuwa natakiwa kuripoti shule ya bweni baada ya kufaulu darasa la saba.

Nilimsumbua Mother kwenye kutaka kununuliwa baadhi ya mahitaji ya shule nae hakuwa na uwezo mkubwa, hivyo ilimlazimu anipeleke ofisini kwa Baba yangu japo walishaachana. Nakumbuka tulipofika pale ofsini, Wafanyakazi wenzake Mshua walivyoniona walifurahi sana kuniona maana tumefanana sana.

Tuliruhusiwa kuingia ofsini kwake na alipomuona Mother tu akanijua. Alifurahi kuniona ila Moyoni mwake niligundua alikuwa bado na hasira na Mother. Alipiga story na mimi nikamueleza maendeleo yangu na sababu za mimi kwenda pale. Alifurahi kusikia kuwa nimefaulu na alinipa fedha kiasi na kisha aliniambia nijitahidi sana kusoma masomo ya Sayansi ili nije kutoboa na kumsaidia Mama yangu. Akamgeukia Mama akamuuliza kwa nini umemleta kwangu huyu dogo wakati nilishakwambia huyu mtoto ni ZAWADI YAKO?. Mama alijiumauma pale akajitetea kuwa huyu mtoto mwenyewe ndiye kang'angania nimlete kwako anahisi labda utamsaidia.

Lile swali na maswali mengine aliyoulizwa yalinifanya nisimsumbue tena Mama na sikurudi tena kumtafuta Mshua. (Pia kupitia yale maswali ya Mshua, yalinisaidia kujua sababu halisi iliyofanya Mother aachike - Nilibaini Mshua alikuwa sahihi kumuacha Mother).

Kiukweli ilinifanya nijifunze kuishi maisha ya kupambana bila kuhitaji sapoti yake na MUNGU aliniongoza hadi nikafanikiwa.
 
Pole sana mkuu... mshua yeye yuko wapi?
Sisi wengine tumelelewa na singo mother tu kwa kuwa mshua aliachana na Mother. Nakumbuka mara yangu ya kwanza na ya mwisho kumuona ilikuwa pale ofisini kwake (Wizara ya Afya). Nakumbuka nilikuwa natakiwa kuripoti shule ya bweni baada ya kufaulu darasa la saba. Nilimsumbua mother kwenye kutaka kununuliwa baadhi ya mahitaji ya shule nae hakuwa na uwezo mkubwa, hivyo ilimlazimu anipeleke ofisini kwa Baba yangu mzazi japo walishaachana. Wafanyakazi wenzake Mshua walivyoniona walifurahi sana kuniona maana nimefanana sana na Mshua. Mshua alinipa fedha kiasi kwa ajili ya mahitaji ya shule, kisha aliniambia nijitahidi sana kusoma ili nije kumsaidia Mama yangu. Akamgeukia Mama akamuuliza kwa nini umemleta kwangu huyu dogo wakati nilishakwambia huyu mtoto ni zawadi yako baada ya kuachana?. Lile swali lilinifanya nisimsumbue tena Mama na sikurudi tena kumtafuta Mshua. Nilifanya vizuri kwenye masomo yangu na leo hii nafanya kazi kwenye wizara hiyohiyo ya Mshua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu anitunzie huyu Mzee kwanza Amenifundisha kunyoosha Nguo za Kiume.. Mara nyingi nguo zake nilikuwa Nampigia Pasi mimi.

Nakumbuka wakati nipo O Level nilisoma Boarding.. Ile shule ikifungwa tu.. nilikuwa sipandi yale magari... Baba yangu anakuja mwenyewe kunichukua. Siki za Visiting day sasa... Nilikuwa naacha gumzo..

Zaidi sana ambalo hadi leo na Ukubwa wangu nalimiss.. Wakati nikiwa mdogo Nilipenda sana kumuosha Baba yangu Miguu.. Ile akirudi kazini tu.. Akivua viatu mimi na Beseni langu.. Naanza kumuosha.. Hadi akazoea.. Akitoka kuoga ajisugui miguu.. anaacha nakuja kumuosha Mimi.

Ni mengi mno mno nakumbuka kutoka kwa Baba yangu.. Ikitokea nimeharibu sehemu alikuwa anaumia... Hadi sasa akisikia napitia Changamoto.. Anaumia[emoji24]
MUNGU akupe Maisha marefu Baba yangu Joe.. Nakupenda Mno mno.. Nina Deni kubwa sana kwako..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu... mshua yeye yuko wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Nilivyomaliza Shule nilipata nafasi ya kusoma Chuo - DAR. Niliwahi tena kwenda pale ofsini kwake kumsalimia, niliambiwa ameshastahafu kazi.

Sikumtafuta tena hadi leo, Japo Kuna ndugu yake aliniona huko Facebook aliwahi kuniambia kuwa Mshua anaishi Dar - Kigamboni na ana watoto watatu wote wakike.
 
Tangu kitambo alikuwa anaishi Dar - Kigamboni. Wakati nasoma Chuo Muhimbili niliambiwa ananitafuta sana, ila mimi sikumfuatilia tena. Nilijulishwa tu alishaoa mke mwingine na ana watoto watatu wote ni wa kike. Wa kiume nilikuwa mimi tu nilietelekezwa.
Dah aisee !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi wengine tumelelewa na singo mother tu kwa kuwa mshua aliachana na Mother. Nakumbuka mara yangu ya kwanza na ya mwisho kumuona ilikuwa pale ofisini kwake (Wizara ya Afya). Nakumbuka nilikuwa natakiwa kuripoti shule ya bweni baada ya kufaulu darasa la saba. Nilimsumbua mother kwenye kutaka kununuliwa baadhi ya mahitaji ya shule nae hakuwa na uwezo mkubwa, hivyo ilimlazimu anipeleke ofisini kwa Baba yangu mzazi japo walishaachana. Wafanyakazi wenzake Mshua walivyoniona walifurahi sana kuniona maana nimefanana sana na Mshua. Mshua alinipa fedha kiasi kwa ajili ya mahitaji ya shule, kisha aliniambia nijitahidi sana kusoma ili nije kumsaidia Mama yangu. Akamgeukia Mama akamuuliza kwa nini umemleta kwangu huyu dogo wakati nilishakwambia huyu mtoto ni zawadi yako baada ya kuachana?. Lile swali lilinifanya nisimsumbue tena Mama na sikurudi tena kumtafuta Mshua. Nilifanya vizuri kwenye masomo yangu na leo hii nafanya kazi kwenye wizara hiyohiyo ya Mshua.
Bado yupo hai?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zaidi sana ambalo hadi leo na Ukubwa wangu nalimiss.. Wakati nikiwa mdogo Nilipenda sana kumuosha Baba yangu Miguu.. Ile akirudi kazini tu.. Akivua viatu mimi na Beseni langu.. Naanza kumuosha.. Hadi akazoea.. Akitoka kuoga ajisugui miguu.. anaacha nakuja kumuosha Mimi.

Chozi limenidondoka [emoji22][emoji22][emoji22]
 
Mi nakumbuka baada ya kututelekeza nilikua nikienda kwa wale family friend wa zamani wakati baba yupo.nikiulizia marafiki zangu wa utotoni.unaambiwa tu ..yupo nairobi anasoma huko...ukienda huku unaambiwa yupo sekondari fulani kampala.hata levo za vyuo ni huko huko.

Nikawa nawaza mzee asingetutosa tungesoma vizuri.kwakuwa alikuwa na kipato kizuri.na hata ajira isingekuwa ishu ni mtu mwenye koneksheni ya kibabe sana.

Nikikumbuka wakati wa kuomba misaada ya ada kwa marafiki zake wakati uwezo alikuwa nao kuwazidi .machozi yalikuwa yanamwagika sana.nilijenga chuki isiyokwisha mpaka leo.kwakweli simpendi hata kidogo.yaani simpendi kwelikweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nakumbuka siku moja hivi tuko kijijini na mzee tumepanga kesho yake tukamtembelee babu, baba yake mdogo baba ambaye alikuwa anaishi kilometa kadhaa kutoka tulipo (KM 7).

Wakati huo nilikuwa na Miaka 6, mkubwa kabisa, Sasa wakati wa safari tumetoka vizuri mimi na mzee mtu Bee (wawili) tu pale nyumbani kuelekea kwa babu.

Wakati tuko njiani nilikuwa namdekea sana baba yangu, Sasa baada ya kama Nusu safari hivi nikamrukia mzee na kumwambia nimechoka anibebe.

Mzee alinitazama usoni na kutabasamu kisha akasema unataka nikubebe mpaka wapi,mi nikamjibu mpaka kwa babu.

Mzee kweli akanichukua na kuniweka begani mpaka tumefika kwa babu, huku tukipiga story. Huwezi amini mzee alinibeba tena begani mwake wakati wa kurudi mpaka nyumbani.

Wala sikuwaza kwamba nilikuwa namuumiza mzee wangu na wala sikuwaza kwamba ipo siku nitakumbuka na kumisi moment ile.

Nakupenda sana Baba yangu, Nakuombea kwa Mungu akujalie Afya na Nguvu ili uweze kuishi miaka mingi hapa Duniani.

CC Zero IQ

Ulikuwa mayai wewe, dingi wangu katika umri huo utaanzia wapi kumwambia akubebe??!!, atakuambia; "pumbavu, wewe ni mlemavu??, watoto wa siku hizi bure kabisa!!, tembea huko!!., mimi nilipokuwa kama wewe nilikuwa natembea km 20, kwenda km 10 na kurudi km10."

May God rest him in peace, my Father who made me who I am.
 
Back
Top Bottom