Eeeeh Jah endeleaa kumtunza baba angu!!! Nizidi kufaidi na kushuhudia mengi mazuri na makuu kwake.
Baba angu ni kiongozi wa maisha yangu, ni mlezi wa mambo yangu, ni kila kitu kwangu, siwezi elezea yote kwan sitamaliza.
Kikubwaa baba angu, wakati wa lile suala ambalo sio zuri na jema machoni Pa watu au jamii, lililokuwa kwangu, lakini wee hukujali jamii na watu wa nje watakuonaje au watakutazamaje km mzazi, lakini ulisimama na mie.
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Baba nakumbuka maneno haya,
"mwanangu kila mtu ana madhaifu na mapungufu yake, usionee unanyooshewa kidolee hata wao wana yao ambayo yakijulikana vidolee vitageukia kwao kabla havijakugusaa wee, najua inauma mnoo km mzazi ila haitobadilisha kuwa wee sio mwanangu, wee ni mwanangu na utabaki kuwa mwanangu milele, kikubwa nacho kuomba epuka madhaifu na mapungufu yako kuwa kikwazo kwa wengine, epuka kujipa umuhimu kwenye maisha ya watu au pasipostahili, najua wee ni msomi na unaelewa, ishi maisha yako binafsi, mimi, mama yako na ndugu zako wote tunakupendaa sanaaa na tupo pamoja na wee"
Baba maneno haya ndo msingi na nguzo kwangu, ndo kanuni na taratibu ya maisha yangu. Ubarikiwe sanaaaa baba yanguu.
NAKUPENDAAA SANAA, [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Sent using
Jamii Forums mobile app