Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Mbunge, je sheria zinatungwa na Bunge au Serikali?

Ninachofahamu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Mbunge wa Katiba.

Kadhalika miswada ya sheria huletwa bungeni na AG ambaye ni Mbunge.

Sasa nauliza, Ni Bunge linalotunga sheria?

Majawabu tafasali.

cc: Pascal Mayalla, BAK
Kiuhalisia sheria zinatungwa na serikali. Miswada inayopelekwa bungeni huandikwa na serikali, na hata ikipitishwa bungeni haiwezi kuwa sheria hadi ipate kibali cha rais.

Labda ndio kujichimbia mhimili mmoja kama alivyosema Magu, maana hata mahakama ikitoa hukumu mtu anyongwe, hukumu haitekelezwi hadi rais aafiki.

Kuna mhimili unaingilia majukumu ya mihimili mingine.
 
Nimekuelewa sana
 
Ninachofahamu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Mbunge wa Katiba.

Kadhalika miswada ya sheria huletwa bungeni na AG ambaye ni Mbunge.

Sasa nauliza, Ni Bunge linalotunga sheria?

Majawabu tafasali.

cc: Pascal Mayalla, BAK
Mihimili Mitatu Muhimu ya Nchi imejikusanya vizuri sana kwa pamoja ndani ya muhimili moja, kwa maslahi mapana ya waTanzania wote.
 
Suala la mihimili ya dolla linaeleweka vizuri kama utalielezea kwa lugha ya asili ya haya mambo.

Kuna state =dolla ambayo inakuwa na mihimili mitatu;

Parliament=Bunge

Judiciary=Mhimili Kimahama

Government=Serikali

Parliament=Bunge lina sehemu kuu mbili;

1. National Assembly=Baraza la Kitaifa ambalo limesheheni Wabunge wote wa Majimbo, Viti Maalum, Wakuteuliwa na wale 5 kutoka Baraza la Wawakilishi.

2. Rais, the President pia ni sehemu ya Bunge. Sasa hapa ndipo AG=Mwanasheria Mkuu anaingia. AG, Waziri Mkuu wanamwakilisha Rais Bungeni.

Kwenye Kiingereza kuna Parliament na National Assembly ila Kiswahili kina Bunge peke yake ambapo mantiki yake ni National Assembly, na hii inafanya watu wanachanganya

Kwa hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni sehemu ya Bunge na anamwakilisha Rais na Serikali yake.
 
Kwahiyo Sheria miswada ya sheria inatungwa na Serikali kisha Bunge linajadili na kupitisha na mwisho Rais anaidhinisha itumike ama la?
 
Kwanza Serikali ndiyo mtekelezaji wa shughuli za kilasiku, kwa hiyo yenyewe ndiyo yenye utaalam wa kusema nini kinatakiwa, na ndiyo maana Mswada unaanzishwa na Serikali.

Mswada ukikamilika, unapelekwa Bungeni kujadiliwa. Hapa Bunge linatumia mamlaka yake kama msimamizi na mshauri wa Serikali kwamba hiki weka, na hiki ondoa na linafanya hivi kwa niaba ya wananchi. Hapa wa kujibu hoja za kisheria ni Mwanasheria Mkuu ambaye yupo humo ndani ya Bunge.

Sasa Bunge ndiyo linaamua kwa pendekezo ya Serikali lilivyo, je lipitishe au liache?

Mswada ukipita, basi rais anasaini inakuwa sheria.

Ila Bunge likikataa, basi litasema sababu na kuilekeza Serikali cha kufanya. Na mwakilishi anayeyapokea haya maelekezo ni Mwanasheria Mkuu.
 
Ninachofahamu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Mbunge wa Katiba.

Kadhalika miswada ya sheria huletwa bungeni na AG ambaye ni Mbunge.

Sasa nauliza, Ni Bunge linalotunga sheria?

Majawabu tafasali.

cc: Pascal Mayalla, BAK
AG sio mbunge ni ex official kama Katibu wa Bunge.
Serikali au mbunge anaweza kupeleka muswada, Bunge ndilo linatunga sheria, rais anasaini ndio inakuwa sheria.
P
 
Kwanza Serikali ndiyo mtekelezaji wa shughuli za kilasiku, kwa hiyo yenyewe ndiyo yenye utaalam wa kusema nini kinatakiwa, na ndiyo maana Mswada unaanzishwa na Serikali.

Mswada ukikamilika, unapelekwa Bungeni kujadiliwa. Hapa Bunge linatumia mamlaka yake kama msimamizi na mshauri wa Serikali kwamba hiki weka, na hiki ondoa na linafanya hivi kwa niaba ya wananchi. Hapa wa kujibu hoja za kisheria ni Mwanasheria Mkuu ambaye yupo humo ndani ya Bunge.

Sasa Bunge ndiyo linaamua kwa pendekezo ya Serikali lilivyo, je lipitishe au liache?

Mswada ukipita, basi rais anasaini inakuwa sheria.

Ila Bunge likikataa, basi litasema sababu na kuilekeza Serikali cha kufanya. Na mwakilishi anayeyapokea haya maelekezo ni Mwanasheria Mkuu.
Bunge likipitisha ni lazima Rais wa JMT asaini iwe sheria?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom