Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 3,560
- 7,914
Kulingana na unabii kulikuwa na falme nne katika danieli 7 zilizotabiriwa kuwa baada ya hizo ufalme watapewa watakatifu na ndipo mwisho wa dunia. wafalme hao waliotabiriwa ni babeli, umedi na uhajemi, uyunani na rumi.
je, tawala hizi zina uthibitisho na ushahidi wa kihistoria nje ya biblia ili mambo haya yasiwe uzushi, jibu ni ndio vyanzo mbalimbali vya kihistoria vinakili kuwepo kwa tawala hizi zilizo tawala dunia yote na hata majengo yake ya kale baadhi bado yapo mpaka leo.
"Hivyo kwa yoyote mwenye hekima hawezi kupingana na unabii huu kuwa ni mambo ya uzushi tu bali ilikuwa ni kitu cha kweli."
NDOTO YA DANIELI HII HAPA
Danieli 7:1-14
1 Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danielii aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.
2 Danielii akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.
3 Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali.
4 Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.
5 Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.
6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.
7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.
8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang'olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
9 Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.
10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.
11 Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.
12 Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang'anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira.
13 Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
UFAFANUZI
Hii ndio ndoto ya danieli anasema aliona wafalme wanne na yule wa mwisho ni wakutisha sana naye angekuwa na pembe kumi lakini aliona pembe nyengine ndogo ikizuka katika ya zile kumi nayo ilikuwa ni ndogo yenye kinywa na macho ya binadamu na baada ya kuondokana kwa pembe hiyo danieli anasema aliona viti vya enzi vikiwekwa mbinguni na ujio wa mungu ukawadia.
Lakini je hiyo pembe ingetawala kwa muda gani baada ya mnyama huyo wa nne kuchukua mamlaka hapa ndipo panapo changanya watu na mada yangu itajikita zaidi kwenye hii pembe ndogo kwani baada ya hiyo unabii utakuwa umetimizwa lakini angetawala kwa muda gani na tunge mtambuaje kuwa ndie huyo majibu yapo hapo hapo
Danieli 7:25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
1, Angenena maneno kinyume na mungu.
2, angekuwa na vita na watakatifu.
3, angebadili majira na sheria.
4, tungekuwa chini ya mikono yake kwa wakati na nyakati mbili na nusu wakati.
Baada ya hayo danieli anasema aliona mzee wa siku akija na mawingu inamaana baada ya haya mungu angerudi wakati wowote hakuna kuongeza kitu wala kupunguza kitu ujumbe umekamilika.
SWALI JE UNABII HUU WA PEMBE HIYO UMESHATIMIA PIA AU BADO ? JIBU TAYARI!
Kulingana na historia katika ufalme wa nne wa dunia uliotawala karibia mabara matatu yani ufalme wa rumi, ni ufalme uliotimiza vipengele vyote vya pembe ndogo kwa wakati ule, kwasababu uliwatesa na kuwauwa wakristo, ulikuwa na mtu anayeitwa kaisari huyu alijiita yeye ni mungu, pia ulitawala ule ulibadilisha sheria amri za mungu, pia utawala ule ulidumu kwa miaka 1290 au 1260 kulingana na historia ambapo tunaweza kusema ni wakati na nyakati mbili na nusu wakati za kiunabii.
Mpaka hapo ni wazi kuwa unabii umeshatimia tayari kabla sijaongeza ushahidi mwengine wenye nguvu wa ufunuo naomba tuangalie maelezo ya wasabato na wanadini wengine mtizamo wao kuhusiana na unabii huu.
WASABATO WANASEMA UNABII HAUJATIMIA KWAMBA PEMBE NDOGO AU MPINGA KRISTO BADO HAJAJA
Mfano Wasabato wanasema kuwa unabii huu bado hujatimia kwamba wanasubiri ujio wa pembe ndogo katika wakati huu na wanamtaja atakuwa yani kiongozi wa roman katoriki ya hivi leo.
CHANGAMOTO ZA MTIZAMO HUU,
Zinapingana na unabii wa Daniel yeys alisema aliona pembe ndogo ukiibuka mapema katikati ya zile pombe kumi za utawala ule wa rumi ya kale. inamaana mpinga kristo angeibuka wakati ule wa dola hilo sio hivi leo.
Rejea;
Danieli 7:24 Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.
Fungu hilo hapo juu linaonesha pembe ndogo ingeibuka wakati wa dola lile tu, na unabii unaongeza angebadili sheria na nyakati naye angetawala miaka 1290 au 1260 au wakati na nyakati mbili na nusu wakati tu. na asinge tawala mara mbili kwani pembe ile iliibuka mara moja tu sio mara mbili kama tulivyoona kwenye mnyama yule wa nne.
rejea;

Hapo juu inaonesha matendo ya pembe hiyo na muda wake atakao yatekeleza ni kwa muda wa wakati na nyakati mbili na nusu wakati ambazo bila shaka zinalingana na muda wa kihistoria wa utawala wa rumi ulipoishia ni jumla ya miaka 1290 au 1260 tu. hakuna sehemu inayosema utawala huu ungeibuka mara ya pili badala yake ingetokea nini sasa ? hakuna kuongeza kitu majibu yapo wazi ni wewe tu kukubali ukweli
Danieli 7:26-27
26 Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele.
kumbe baada ya kuondolewa utawala wake utaangamizwa milele hata milele hauta rudi tena kutawala.
27 Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
Ndiyo hivyo hakuna kuongeza kitu hapo ni hatari kuongeza kitu danieli anasema aliona baada ya pembe ndogo kutawala miaka 1290 mwisho ule ungewajia na sio tena ujio wa mwengine wa pembe ndogo wakati huu, na mambo yote ya pembe ndogo yaliyotajwa ikiwemo kubadili sheria na muda, kuuwa, kuteka, kunena maneno makufuru tayari alikwisha yafanya kwanini unabii huo usitimie mpaka hapo wakati ushahidi wa kihistoriaunasema hivyo hivyo ? hebu tukatae upotoshaji na uongo.
HEBU TUANGALIE NDANI ZAIDI KATIKA MAONO MENGINE YANAYO ELEZEA MAMBO YA SIKU ZA MWISHO.
Ndoto ya nebukafneza;
Danieli 2:37-45
37 Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu;
38 na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.
39 Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote.
40 Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta.
41 Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.
42 Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika.
43 Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.
44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.
45 Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.
Kufupisha Unabii huu naomba niseme hapo juu ni tafsri ya ndoto aliyo iona nebukadneza mfalme wa babeli, yeye aliona sanamu kubwa sana yenye madini ya aina nne dhahabu, fedha, shaba, na chuma, baadae aliona miguu nusu chuma na nusu udongo na tazama jiwe lisilichongwa kwa kazi ya mikono likaipiga miguu ile ye nusu chuma nusu udongo na ndipo sanamu ile ikavunjwa vipande vipande.
UFAFANUZI.
Sanamu hii ya ndoto ya mfalme wa babeli inafanana na wale wanyama wanne alio waona danieli ambao wote wanazungumzia mambo ya siku za mwisho yani falme nne babeli, umedi na uhajemi, na rumi, lakini katika ndoto hii danieli anasema baada ya ufalme wa mwisho yani chuma kungekuwa na mgawanyiko wa mataifa madogo madogo na katika siku hizo jiwe yani mungu angerudi tena kama ulivyo liona lile jiwe lililo zivunja sanamu hizo ni kuondolews kwa ufalme wa dunia.
Hii inamaana gani kwa ndugu zangu WASABATO na wanadini wengine, ni kwamba sanamu hii inaonesha kwamba hakuna utawala ambao ungekuja mara mbili inamaana baada ya rumi kungekuwa na mataifa madogo madogo na katika siku hizo mungu angerudi ambapo ndio tupo hivi leo huo wakati wa mataifa mengi madogo madogo ya kujitegemea, kifuatacho sio pembe ndogo danieli anasema aliona jiwe likija kupiga sanamu na kuvunja vunja na kwamba pembe ndogo ingetawala tu miaka 1290.
Lakini danieli anasema kuwa katika mataifa hayo madogo madogo yani miguu ya nusu chuma na nusu udongo yasingeshikamana, inamaana kungekuwa na ugomvi, vita, chuki, ushindani n.k kama tunavyoona hivi leo mataifa hayashikamani hii inatimiza unabii na baadae danieli aliona jiwe likija kuvunja tawala hizi yani mungu angerudi upesi wakati huu
NDUGU ZANGU WASABATO NA WANADINI WENGINE, wanasubiri ujio wa pembe ndogo ambayo imekwisha kuwepo ije itawale dunia tena na wanasema watu hawatauza wala kununua wakati haya yote yalikwisha fanyika swali je nje ya unabii huu je papa wa kanisa katoliki anaweza kuwa mfalme wa dunia nzima kama zamani kipindi cha dola la rumi ?
Hapana jibu hawezi, na hii inaendana na maono ya danieli anasema mataifa yale madogo madogo haya yatakuwa ni nusu chuma na nusu udongo kama vile udongo usivyoshikamana na chuma kwamba hawatakuwa kitu kimoja hawatashikamana badala yake yesu angerudi.
Katika uhalisia hivi sasa Papa hawezi kushurutisha chochote hata kwa mgongo wa umoja wa mataifa kwani utakuwa unapingana na unabii pili hauwezi kutokea danieli anasema "hawatashikamana" ndio katika watawala wa hivi leo hawawezi kushikamana na roman katoriki haiwezi kutawala dunia kama hapo zamani, haina jeshi, haishikamani na baadhi ya nchi za kiislam, haimiliki teknolojia yoyote, hivyo sio tishio kwa namna yoyote ile kwa hali halisi ilivyo ni kitu kisicho wezekana.
Licha ya baadhi ya mataifa kwenye sanamu ile ya danieli kuonekana ni chuma yani yangekuwa na nguvu sana lakini bado anasema hayato shikamana hata kwa mashinikizo kutoka kwao inamaana hata marekani hawezi kushinikiza dunia ifuate shinikizo lake kivyovyote huu ni unabii ulivyosema angalia mtu asije kukudanganya.
Kwahiyo Kwasasa tupo kwenye dakika za lala salama huku wengi wakiwa wamepotoshwa na wengi wakiwa wamejitakasa na kujifanya weupe lakini haya yote yalikwisha tabiriwa sio mambo mageni nafikiri shetani hawezi kuwaacha mfikie ule mwisho kwa amani msishange mtakapo gundua kuwa njia mliyokuwa mkizani imenyooka kumbe ni ile iendayo upotevuni kwani wokovu sio rahisi.
Leo nasikitika kuona wakazi wa dunia wakitazamia ujio wa wa dola la rumi mara ya pili wakati tayari limekwisha kuwepo ikiwemo hawa wasabato, je watakuwa wamepotoshwa ?
Danieli 12:10 Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.
NAOMBA PIA NIWAAMBIENI TAFSIRI YA UNABII WA UFUNUO WA YOHANA ILI TUMALIZE. HAKUNA KUONGEZA KITU WALA KONA KONA MWENYE AKILI NA SIKIO NA ASIKIE.
" tupo kwenye dakika za lala salama. "
Ufunuo wa Yohana 13:1-9
1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.
3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
4 Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.
8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
9 Mtu akiwa na sikio na asikie.
UFAFANUZI
Hapa kwenye unabii huu unaongelea ndoto kama ile aliyoiona danieli ya kwamba inazungumzia siku za mwisho ikumbukwe danieli aliona mnyama akitoka katika bahari na yohana anasema aliona mnyama akitoka katika bahari pia.
Lakini huyu mnyama aliyemuona yohana anapembe zaidi ya saba na vichwa kumi bila shaka anafanana na yule mnyma wa nne mwenye kutisha sana aliye muona danieli.
Mnyama huyu anatisha kwa kweli hebu angalia anavichwa kumi vya simba, ana mwili wa chui, anamiguu ya dubu kwa kweli huyu sio mnyama wa kawaida anatisha hivyo anaendana na yule mnyma wa nne yani ufalme wa mwisho wa nne wa dunia " rumi" mpaka hapo tupo pamoja.
sasa tuendelee
Ufunuo wa Yohana 13:11-18
11 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.
12 Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.
13 Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.
14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.
15 Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.
16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Danieli alisema alimuona mnyama mwenye kutisha akiwa na pembe ndogo ambayo ilifanya vita na watakatifu, ili badirisha sheria, iliongea maneno makufuru lakini pia haikuwa yenyewe ndio yule mnyama wa nne ila iliota kama pembe yenye mamlaka katika mnyama yule wa nne.
lakini yohana wa ufunuo hapa hajaona hiyo pembe ndogo yeye amemuona ndio yule mnyama wa nne mwenye kutisha sana lakini baadae aliona mnyama mwengine akitoka katika nchi huyu anafanya yale yale ya pembe ndogo ikiwemo vita na watakatifu, kama ile pembe ndogo ya danieli inamaana huyu ndio ile pembe ndogo ya danieli.
Ikumbukwe danieli aliona mnyama mwenye pembe kumi baadae pembe ndogo ilizuka na tatu zikaangushwa tatu toa kumi inabaki 8, inamaana pembe ambazo zingebaki pale ni nane, hebu tuchungulie kumtambua huyu mnyama wa pili kama naye ni pembe kati ya zile nane za daniel.
Ufunuo wa Yohana 17:8-11
8 Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.
9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.
10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache.
11 Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.
Kwa kweli mnyama huyu wa pili wa Daniel angewakilisha pembe ndogo bali sio utawala mpya kwani watawala waliotabiriwa ni wanne tu baada ya hawo watakatifuwangepewa ufalme, hivyo huyu mnyama wa pili sio kitu kipya ni ile pembe ndogo juu ya mnyama wa nne.
VIPI MTIZAMO WA WATU WENGINE MAKANISA KUHUSU MNYAMA HUYU WA PILI.
Wengi ikiwemo wasabato wanadai mnyama huyu wapili ni marekani kwamba marekani angeweza kushinikiza wakaazi wa dunia wamuabudu yule mnyma wa nne yani roman katoriki. hiki ni kitu ambacho kama kingetokea kingeenda kinyume na unabii wa siku za mwisho kwasababu utawala wa kirumi ungekuwako mara mbili, pia uharibifu ungekuwako mara mbili na kwasababu huyu mnyma wa pili wa yohana anaenda kuchukua mamlaka inamaana danieli alikosea kuona wanyama wanne kama watwala pekee wa dunia wangetakiwa kuwa watano ukijumuisha marakani.
Lakini ukweli haufichiki Hebu tuchambue mnyma huyo wa pili ni nani kwa undani zaidi je, mnyams huyu ni nchi ys marekani kama wasabato na wengine wanavyosema. ?
Ufunuo wa Yohana 13:11 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.
unabii unasema mnyama "anatoka katika nchi" inamaana hakuwa yeye ndio hiyo nchi bali alikuwa ndani ya nchi unabii unasema "akipanda kutoka" inamaana alikuwa anatokea kwenye nchi flani na sio yeye ni nchi kama wasabato na wengine wanavyodai.
Mfano naweza kusema nilimuona mnyama akitoka katika gari, akitoka katika jamiiforums, akititoka ubungo, siwezi kusema huyu mnyama ndio hilo gari, au ndio hiyo jamiiforums ila alikuwa ndani yake sasa ndio "anapanda kutoka nje" hivyo tukisema ametoka katika nchi yeye hawezi kuwa ndio hiyo nchi bali angetokea katika nchi. tuendelee

Unabii unasema alikuwa na "pembe mbili mfano wa mwanakondoo" katika uhalisia hapa kila mmoja anajua kuwa yesu kristo alichinjwa msalabani kama "mwanakondoo" hivyo kama mnyama huyu ni "mfano wa mwana kondoo hatokuwa nchi bali atakuwa mtu ambaye atakaye jifanya ni mungu bila shaka anafanana na pembe ndogo ya agano la kale hivyo sio nchi ya marekani.

unabii unaongezea " akanena kama joka" joka anatafsiriwa kiunabii kama shetani inamaana angeongea kama shetani kama "anaongea" inamaana hatokuwa nchi bali ni mtu. sasa tumesha mtambua mnyama wa pili ni nani mpaka hapo. mwenye akili na afahamu hakuna haja ya kuongeza au kona kona hapo.
unabii unaongeza
Ufunuo wa Yohana 13:12-13

Mnyama huyu wa pili tafsiri yake thabiti ni hii, kuna mtu angetoka katika nchi angekuwa mungu handia angenena kama shetani na angewafanya wakaazi wote wa dunia wamsujudie mnyama wa nne. kwamba hatokuwa nchi au taifa huyu mnyama au hatokuwa kitu kipya.
lakini angetokea wapi mnyama huyu ?
Ufunuo wa Yohana 17:11 Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.
Inamaana mnyama huyu ni miongoni mwa zile zile pembe saba naye ndio wa nane inamaana angebadirika hapa kuwa pembe ndogo kutoka katika zile pembe saba.
katika danieli 7 Ikumbukwe iliibuka pembe ndogo kati ya kumi na tatu kati yake zikaangushwa nazo zikabaki pembe saba na hiyo ndogo yenye macho ni ya nane nayo ni ile ya saba, lakini hii ya saba haina macho wala haineni kama joka, inamaana ingekuwa ni ufalme juu ya mnyama wa nne wa kisiasa lakini kwasababu ingeibuka pembe nyengine ndogo ambayo pia ni ya saba hii inatafsiwa kama utawala wa ufalme wa saba kuwa wa kisiasa na kidini kama ulivyoona pembe ya saba haina macho lakini ya nane nayo ni yasaba ina itikadi za kidini.
mpaka hapo inaturudisha mpaka kwenye ufunuo 13
Ufunuo 13 unasema huyu mnyama ambaye ndio pembe ndogo ya danieli agano la kale, anapembe mbili.

Inamaana mnyama huyu wa pili angekuwa na mamlaka ya kisiasa na kidini na asingekuwa nchi bali ndio ile pembe ndogo na unabii unaongeza
Ufunuo wa Yohana 13:14-17

Je, mambo haya yamekwisha tumia je kuna mtu alishawai kuwako kwenye dola la rumi mwenye nguvu za kisasa na kidini ? jibu ni ndio
je kuna mtu aliwauwa na kuwatesa watakatifu katika dola hilo la rumi ? jibu ni ndio.
Je, kuna mtu aliwa kutumia chapa ya mnyama asiweze kuuza wala kununua kipindi cha dola la rumi jibu ni ndio. watu walikuwa hawawezi kuuza wala kununua pasipo kuwa na muhuri wa mamlaka ya kaisari.
je, kaisari alikuwa mfano wa mungu kwenye dola hilo ? jibu ni ndio kaisari alikuwa kama mungu.
je, kaisari alishusha moto mbinguni ? jibu ni ndio kaisari alikuwa akifanya ishara za miujiza ili kuwaaminisha watu kuwa yeye anafanana na mungu.
je, kaisari aliwahi kutia pumzi kwenye sanamu ikanena kama mwanadamu ?, jibu ni ndio kaisari alijenga sanamu nyingi zilizo nena kama wanadamu na kutoa amri kwa watu.
Huu ni uthibitisho wangu wenye nguvu sana kuwa unabii umekwisha timia wote watu hivi leo baaada ya kuutazamia ujio wa yesu wanatazamia ujio wa dola hilo la rumi ya kale mara ya pili kitu ambacho hakiwezi kutokea tena dola hilo na pbe ndogo ambaye ni mnyama wa pili angepaswa kutawala kwa wakati na nyakati mbili na nusu wakati yani miaka 1290 pekee baada ya hiyo watakatifu wangepewa ufalme waumiliki milele hata milele.
Msishangae kwanini mmedanganywa wazi wazi na kupofushwa dhidi ya ukweli imeandikwa hata wale wateule wangedanganywa. je, wewe ni mteule jiandae jiwe litakuja wakati huu na kuvunja falme hizi zote. tupo kwenye dakika za lala salama na wengi wamepotoshwa.
KWA WALE MSIO AMINI
Heri aaminiye ili wakati ule aokolewe kuliko asiye amini kabisa wakati ukawajia akahukumiwa.
asante sana
Ufunuo wa Yohana 21:1-8
1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.