Je tuhahitaji tena Ze Utamu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je tuhahitaji tena Ze Utamu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gembe, Apr 23, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Heshima Mbele,

  Jana nilipata ujumbe wa simu toka kwa Mpwa wangu ambaye yuko chuo kikuu cha dar es salaa,Safari hii alikuwa akiniambia jambo la kusikitisha. Aliniandikia kuwa ile tovuti al maarufu ze utamu kuwa wamemtoa mhe rais kwa picha mbaya isiyo na heshima katika jamii, Na kwa haraka sana mie nilienda kuchungulia kujua nini kilichomo na kukuta mambo ya jabu na kinyume na maadili ya kitanzania.

  Nilisikitika sana na kwa haraka zaidi nikawasiliana na mzee Mwanakijiji na Invisible kuonesha kusikitishwa kwangu kwa jambo hilo, Hata kama kuna sehemu mhe. Rais kashindwa siyo jambo zuri kufika hapa
  Kumkosea heshima na kumdharirisha mhe rais mie naona ni utovu wa niahdnamu na kukosa maadili.

  Nimefikira sana juu ya jambo hili na sas anaomba mnipe ushauri wa nini cha kufanya ili tuiomeshe tabia hii na ninavyoona naona hatuihitaji tovuti hii.No way!

  Nampa pole Mheshimiwa Rais na Familia nzima ya mkuu wa nchi na naomba vyombo vya sheria vichukue jukumu lake kufuatilia ni nani alifanya jambo hilo!

  It is so sad and am very angry about this
   
 2. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha na hiyo picha imekuwa inasambaa haraka kwenye e-mail za watu....Ni kitendo Kibaya na kinyume kabisa na Maadili yetu ya kitanzania.......Gembe si wewe tu,nafikiri Binadamu yeyote Muungwana na mwenye akili Timamu hawezi kukubaliana na mambo anayoyafanya huyu Mmiliki wa hii website (Utamu).....Haitochukua muda naona 40 zake zimekaribia.
   
 3. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2009
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Je picha hiyo ilimwanika kiasi gani mkuu wa kaya?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Apr 23, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Hii inanikumbusha suala la shamba la wanyama; kwa kweli ni aibu na kitendo cha kulaaniwa na kupingwa.
   
 5. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  duuu! Jambo hili linasikitisha sana nami nimeona, hii siyo tabia jema kwani picha inaonyesha ni kama imetengenezwa sasa sijui aliyetengeneza alikuwa na lengo gani. Inabidi hatua za makusudi kukomesha hali hii zichukuliwe ili jambo kama hili lisije rudia
   
 6. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Wewe nae....
  ....siku hizi JF kuna vi thread vya ajabu ajabu vya kujikomba komba.....

  ......hebu tuletee kidhibitisho cha kuchafuliwa raisi
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Maadili unayaona leo?
  mbona hapa yanabadikwa mapicha machafu machafu hamuoni kama ni kinyume na maadili yatu watz......
   
 8. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchngu, watu kibao wamechafuliwa kule. Ila siku itakapokuwa zamu yako ama ya ndugu wako wa karibu ndio utajua kuwa ile web haifai.
   
 9. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  WORDS fail me,shocked and awed,utamu has overstepped the little morality he/she had.its time the resources of the state were used to hunt down this menace to society
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Apr 23, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  nimeshasema hili na kuandika kwenye Cheche na hata Tanzania daima; huwezi kuwa na standards tofauti ndio maana watu wanapush the envelope. Ile habari ya kusagana iliyoandikwa kwenye Ijumaa endapo ingekuwa na kichwa cha habari "Waziri x afumwa Geto akisagana au Akiliwa uroda" na ikawa describe vile nadhani serikali ingechukua hatua.

  Kuna mtu haelewi maana ya uhuru wa maoni.
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Yo yo hapa si kujikomba. Lazima tuwe na mipaka katika kuharibu personality za watu. Rais ni mkuu wa nchi, ni baba wa familia ya watanzania, (penda usipende) ukweli ndiyo huo. Kinachotakiwa kuandikwa ni mapungufu ya utawala na kukosoa ile aweze kubadilika (maana kuna watu wanaompelekea taaarifa zetu hapa). Jua kuwa JF hapa ni FASIHI, fasihi ni kioo cha jamii, kinaelimisha na kinakosoa kwa manufaa ya jamii husika. Private life ya mtu wa heshima kama baba ni lazima iheshimiwe, tena sana. Huwezi kumchafua rais kwa personal and private life yake, give me a break here.

  Mimi siku zote nakubaliana na mapungufu yake kiutendaji, na sifurahii wakati mwingine, pia nikijua kuwa maamuzi mengine ya rais wa nchi si lazima ya mfurahishe kila mtu, so here I remain objective. Hata siku moja sitaweza kujadili his private affairs, that will make me cheap like bidhaa za Yeboyebo kutoka China. I hate to be cheap to avoid being labeled "Cheap mind discussses people..."
   
 12. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  wapi nimesema web ile inafaa?
  nimesema watz wanafiki mnalia lia maadili wakati nyie ndio wa kwanza kukiuka....humu humu JF kuna mapicha machafu machafu yanayokiuka maadili mbona hamyasemi?
   
 13. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Yoyo,
  Ndiyo nimeamua kujikomba kama unavyofikiri,ila ni watu ambao naamini ni masaada kwangu,Naona unaona Wivu sababu ulidhania nitakutafuta wewe kwanza siyo!Go to hell

  Mwanakijiji ni mpiganaji mkubwa na nakubaliana naye kwa hoja ambazo ni z masingi na wakati mwingine nampinga na kujikomba kwake siyo dhambi!

  Invisible ni kijana ambaye ni mtaalam wa mambo ya teknolojia,na kuwasiliana naye ni kuomba ushirikiano wake katika kutatua hili..

  as the matter of the fact wewe ni yoyo,brazemni na bishoo chukua time!

  kwa wengine wenye nia njema tuendelee kujadili hapa,It is totally ashame kumjadili Mkuu wa nchi kwa Picha za ovyo sababu anawakilisha sura ya nchi yetu,i have said and Yes am syaainga gain hata kama ameshindwa kutupa tunachotaka ila kwa hili No Way
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  .........duh ebwanee hao UWT wapo hivi kweli na hao wanao jiita intelejinsia vp hawajaamuka bado........nimechungulia mmmh hakufai hali ya hewa imechafuka.
   
 15. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Umeshaanzisha thread au kuwaambia hao ma comrade wako kuhusu picha chafu humu JF?
   
 16. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #16
  Apr 23, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Naona picha imetengenezwa na kubandikwa pale hiyo sasa zeutamu wanakosa heshima na maadili hata kama wanasema ukweli kwa vingine watu wajirekebishe kwa kile walichoonyesha kwa raisi sasa huo ukweli wao wote kama kuna ambao walikuwa wanauamini sidhani kama leo wataendelea tena na hadidhi zile zile -- kuna aina ya kufanya marketing ya tovuti la blogu lakini njia hii sio halali ni haramu na inachafua kabisa maadili ya tovuti au blogu husika
   
 17. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Hizo picha ziko wazi kw akila mtu au kwa wanaotaka?Je zinamdhalisha Mkuu wa Nchi?Je zinahusiana na mtu mwenye heshima na hazipatikani kokote?

  Usilete voroja kwa utetezi wako wa kipuuzi!shame on you!
   
 18. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  Mipicha kama hiyo ipo tele, kuanzia ya Bush na Mkewe, Bush ana pumuliwa na Osama, Saddam, Clinton na Mkewe, clinton anakandamizwa na Arafat, juzi hapa nimeona Obama na Michelle kwenye ile nembo ya nanilii, na kadhalika na kadhalika........ni maji-picha ya kipuuzipuuzi tu!! Ila kibongo bongo naona utamu wameenda mbali kweli na kama ndio hilo tembo, basi wao wamelitia mimaji ya mfereji wa Msimbazi (Mto Msimbazi).

  Ila haya yote yameanzia hapa hapa (ktk forums hii)............ndio maana yake hiyo!!
   
 19. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waungwana this is so sad is unexpected to our society and shame to our culture.We allow western influence to our society.About a month ago nilitextiwa picha ya President Obama inayofananafanana na hiyo and I was so sad and now am seeing this kind of behavior in my own society.I can only express my great sadness to that behavior and I dont know how much Mr.President will react.Remember one thing Mr.President Keep up a good work and don't let the foolishness stress your image.

  SAHIBA.
   
 20. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  wazee,
  acheni ufinyu wa mawazo/akili. hayo maadili mnayoyaongelea nyinyi ni ya namna gani ? ina maana upupu wote uliokuwa unawekwa mule ulikuwa unaendana na maadili ? hayo maadili yamekiukwa baada ya kuwekwa JK ? kwa nini sympathy hii iwe kwa JK pekee ? wengine je haiwagusi ? BINAFSI NAPINGA KABISA KITENDO HICHO NA HIVYO VILIVYOTOKEA HAPO AWALI KWA WATU WA KAWAIDA KABISA AMBAO HAWANA MAJINA KTK SERIKALI AU/NA KTK JAMII.

  Ingekuwa busara kama huruma hii pia tungeionyesha kwa wale wengine ambao walipatwa kuhusishwa na yaliyohusishwa kwa rais pia, lkn NIMESHANGAZWA MNO tena SANA kuona kwamba huruma hii ipo kwa watu wenye majina tu. Je kufuata maadili NI LAZIMA KUWE KWA WATU WENYE MAJINA/VYEO TU ?

  AGAIN, POLE MH. RAIS NA WOTE WALIOWEKWA MULE NDANI BEFORE maana sio kitendo cha kiuungwana, bali ni kuchafuana majina na kutokutendeana haki!!

  Na lingine, ina maana yale mapicha machafu ambayo yalikuwa yanatundikwa humu ndani ya jamiiforums pia ni maadili yetu ? au ndo tumeamua kukurupuka ili kuonekana na sisi tumo ? Acheni uzushi wazee ! Hata humu mapicha machafu yalikuwemo na sikusikia yoyote akilalamika, bali watu walikuwa wakijazana kana kwamba ni maadili mema!

  JE MNALO HAPO ?
  (Utetezi Kwa Wote)
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...