Je, nyumba zisizo na umeme zimesamehewa kodi ya jengo?

Ikitokea mtu yuko mjini akahamia kwenye Solar, waziri wetu kajipangaje kukusanya kodi kwa watu wa aina hiyo?

Kuna watu wana line za simu zaidi ya moja; nyingine huwa ni data na nyingine kupokea kama backup. Kama haiwekewi airtime itabaki kudaiwa kwa malimbikizo au itakuwaje?

Nadhani wabunge watakuwa na nafasi kujadili na kumshauri kwa weledi mhe. Waziri wetu wa Fedha Ng'wigulu Nchemba.
Wabunge gani unao wataka kuweka huo mjadala?Hawa wa bunge la ndugai!!
 
kodi ya mwaka inagawanywa kwa miezi 12,kwa hiyo hapa kama kila mwezi ni 1000,maana yake kwa mwaka ni 12,000/=.Mpangaji akikaa miezi sita atakuwa amenunua umeme wa miezi 6 ,hivyo amelipa 6,000/=.Inayobaki atalipa atakaye itumia hiyo luku baadaye.
Nikinunua umeme kwa mwezi mara 2 au zaidi inakuwaje?
 
kodi ya jengo inalipwa mara moja kwa mwaka, sasa ikitokea mpangaji ameishi miezi 6 tu akahama inakuwaje?
Utalipa 1000 kila unaponunua uneme, ukihama utaenda kulipa ukohamia, atakaehamia hapo ulipohama anaendelea kulipia. Sasa tunaonunua umeme wa elfu 2 sijui itakuwaje
 
Toka niimfahamu Dr Mwigulu Nchemba kwa hiyo hotuba kweli kaitendea kazi taaluma yake!!!
Hili la Kodi ya nyumba Nampa heko Sana,bonge la solution,kweli jamaa ni great thinker.

Bonge la bajeti hii,tusubiri utekelezaji Sasa!
 
Kwa mwezi naweka umeme wa buku 10
Kama ni buku katika 5000
Kwa mwaka watakula 20000

Sasa nyumba za kupanda wengi ambao matumizi yako juu itakua shughuli
 
Toka niimfahamu Dr Mwigulu Nchemba kwa hiyo hotuba kweli kaitendea kazi taaluma yake!!!
Hili la Kodi ya nyumba Nampa heko Sana,bonge la solution,kweli jamaa ni great thinker.

Bonge la bajeti hii,tusubiri utekelezaji Sasa!
Lakini maana yake kodi imeongezeka pia watu watakuwa wanaweka LUKU moja tu kwenye kiwanja kimoja hata kama kuna nyumba zaidi ya moja
 
Back
Top Bottom