Je, nyumba zisizo na umeme zimesamehewa kodi ya jengo?

Serikali inapendekeza Kukusanya kodi za majengo kwa kutumia Luku.najiuliza tuu,vipi nyumba zisizo na umeme,je zimesamehewa kodi ya majengo?

Wabunge walipe kodi stahiki.

Mikopo na misaada kwa ajili ya miradi mikubwa si unyonge.

Miradi isiyo na tija kama ya ununuzi wa madege ni werevu.

Wajameni, tusiige kun*a kwa tembo!
 
Waliosamehewa Kodi ya nyumba ni wamiliki, watakaolipa ni wapangaji. Hii nchi imekosa watafiti kwa kweli.

Wamiliki wa nyumba wanaweza kuwa asilimia 30 tu nchini waliobaki ni wapangaji na wanalazimika kujilipia umeme
Wapangaji si ndiyo wanaishi humo? Ki-mantiki wapangaji wanamiliki hizo nyumba kwa kipindi cha kodi zao "right of use"
 
Ikitokea mtu yuko mjini akahamia kwenye Solar, waziri wetu kajipangaje kukusanya kodi kwa watu wa aina hiyo?

Kuna watu wana line za simu zaidi ya moja; nyingine huwa ni data na nyingine kupokea kama backup. Kama haiwekewi airtime itabaki kudaiwa kwa malimbikizo au itakuwaje?

Nadhani wabunge watakuwa na nafasi kujadili na kumshauri kwa weledi mhe. Waziri wetu wa Fedha Ng'wigulu Nchemba.
 
Wapangaji si ndiyo wanaishi humo? Ki-mantiki wapangaji wanamiliki hizo nyumba kwa kipindi cha kodi zao "right of use"
kodi ya jengo inalipwa mara moja kwa mwaka, sasa ikitokea mpangaji ameishi miezi 6 tu akahama inakuwaje?
 
Serikali inapendekeza Kukusanya kodi za majengo kwa kutumia Luku.najiuliza tuu,vipi nyumba zisizo na umeme,je zimesamehewa kodi ya majengo?
Mkuu hapa umenishtua, kuanzia sasa nitatumia solar na generator
 
kodi ya jengo inalipwa mara moja kwa mwaka, sasa ikitokea mpangaji ameishi miezi 6 tu akahama inakuwaje?
kodi ya mwaka inagawanywa kwa miezi 12,kwa hiyo hapa kama kila mwezi ni 1000,maana yake kwa mwaka ni 12,000/=.Mpangaji akikaa miezi sita atakuwa amenunua umeme wa miezi 6 ,hivyo amelipa 6,000/=.Inayobaki atalipa atakaye itumia hiyo luku baadaye.
 
sasa mtu atapangiwaje matumizi yake ya umeme, kuna watu wanabania matumizi ya umeme acha tu!

umeme wa elfu kumi atatumia kwa miezi hata 2.

na kama ni msela au mtu anayesafirsafiri anaweza asinunue umeme mara kwa mara
 
kodi ya jengo inalipwa mara moja kwa mwaka, sasa ikitokea mpangaji ameishi miezi 6 tu akahama inakuwaje?
Atakakohamia hatalipa, kwa hiyo imejibalance. Nadhani faida ya mfumo huu ni urahisi wa kulipa kwa mlipaji pamoja na uhakika wa serikali kupata kodi yake. Details nyingine nadhani zitaangaliwa kutokana na michango ya wabunge.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom