Je, nyumba zisizo na umeme zimesamehewa kodi ya jengo?

Waliosamehewa Kodi ya nyumba ni wamiliki, watakaolipa ni wapangaji. Hii nchi imekosa watafiti kwa kweli.

Wamiliki wa nyumba wanaweza kuwa asilimia 30 tu nchini waliobaki ni wapangaji na wanalazimika kujilipia umeme

Unampelekea deni mwenye nyumba unamkusanyia
 
Serikali inapendekeza Kukusanya kodi za majengo kwa kutumia Luku.najiuliza tuu,vipi nyumba zisizo na umeme,je zimesamehewa kodi ya majengo?
Mimi naona wanarejesha service charge kwa jina jingine la kodi ya wameunga huu umeme mpaka vijijii kwa hivyo hata wale nyumba za nyasi kule kijijini wanahusika ipo siku tutalipa kodi ya macho kama unaona chochotehapa tanzania basi wewe ni mtalii inabidi ulipie shilingi 100 kwa mwezi kuimarisha utalii wa ndani (au ndo tunalipia nguzo za 27000)
 
Tuipende nchi yetu,Kodi ndiyo hujenga nchi!
Ni muda wa kuijenga nchi yetu kwa mikono yetu
Asante mama SSH,Asante DR MWIGULU kwa kufikiria vizuri.

Niko tayari kulipa Kodi ili barabara na huduma zungine za jamii ziimarishwe🙏🙏🙏
 
Hayo ni matusi sasa,wengine wako vijijini na umeme wa luku huko hauko,wana umeme wao kama sola na majenerato maisha yanasonga.Kwa hiyo hao hawahusiki

Kuna viwanja vimepimwa vina hati, na vingine hati za kimila na serikali za mitaa. Ukishakuwa na hati tu ujue kodi hukwepi, itajilimbikiza utadaiwa baadae.
 
Hayo ni Mapendekezo yake Mwiguli, bado hayajawa rasimi, Napendekeza wadau walioko karibu na hawa viongozi Wawape taarifa kuwa hatupendezwi hata kidogo na hayo Wanayotaka.
 
Serikali inapendekeza Kukusanya kodi za majengo kwa kutumia LUKU, najiuliza tuu, vipi nyumba zisizo na umeme.

Je, zimesamehewa kodi ya majengo?
Kuna mtiririko maalum wa ufanyaji na utekelezaji wa maamuzi ya serikali.
1.Waziri husika hupeleka mapendekezo kwenye baraza la mawaziri baada ya mijadala kati ya watendaji na wadau wa sekta husika.
2. Baraza la mawaziri hukubali au hukataa au hurekebisha. Likikubali tunakuja hatua ya 3. Likikataa basi linaishia huko huko kwa siri kuu. Kwa hiyo kuna mengi huwa yanakataliwa ila kwa kuwa ni siri, hatujui.
3. Waziri husika au atakayeagizwa na baraza la mawaziri hupeleka maamuzi hayo bungeni kupitia taarifa za kawaida za serikali, mswada wa sheria au bajeti kuu kama ilivyokuwa kwa case hii.
4. Bunge linaweza kujadili na kukubali au kurekebisha au kukataa(at least theoretically). Likikubali basi tunaenda hatua ya 5, likikataa linarudi kwa waziri na BLW kufanya mabadiliko.
5. Waziri huandaa kanuni au miongozo ya utekelezaji wa maamuzi hayo.
6. Waziri huweka hadharani kanuni hizo na kuwapa watendaji wakuu wa wizara, idara au taasisi za serikali zinazopaswa kutekeleza maagizo hayo.
7. Watendaji wakuu wa MDAs kila mmoja kwa capacity yake huandika waraka kwa watendaji walioko chini yao na pengine kwa wadau wakuu wa sekta husika kuelezea namna ya utekelezaji wa sheria, miongozo au maamuzi au maagzio hayo ya serikali.

Kwa hiyo hotuba ya bungeni haitekelezwi moja kwa moja kama ilivyo wasilishwa na waziri. Yaweza pia kutekelezwa kama haihitaji muongozo.
 
Serikali inapendekeza Kukusanya kodi za majengo kwa kutumia LUKU, najiuliza tuu, vipi nyumba zisizo na umeme.

Je, zimesamehewa kodi ya majengo?


Yaani kama hata umeme huna wa Tsh 27,000 kuunganishwa kodi utaweza kulipa!
 
Waliosamehewa Kodi ya nyumba ni wamiliki, watakaolipa ni wapangaji. Hii nchi imekosa watafiti kwa kweli.

Wamiliki wa nyumba wanaweza kuwa asilimia 30 tu nchini waliobaki ni wapangaji na wanalazimika kujilipia umeme
hii imekufa kabla haijaanza!!!!! HUYU ALIYELETA MPANGO HUU NI mtz KWELI?!!!?
 
Hapana, mita zilizopo kwenye majengo tajwa ya serikali zinapewa msamaha wa makato ya kodi hii. Ni rahisi kulitekeleza hili kwa sababu kila mita ina "anuani yake" (namba ya mita).
Na vip kuhus nyumba zisizo na umeme? au ndo zimesamehewa kodi hivo
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom