Je, ni wakati gani muafaka kwa mzazi kuwabariki watoto wake?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,989
28,126
Ndugu zangu,

Nimekutana na hii tafakuri juu ya baraka za mzazi kwa watoto. Tafakuri hii imejengeka kupitia mandiko ya vitabu vitakatifu kwa kile alichokifanya Isaka kwa mtoto wake Yakobo.

Kwamba Isaka alipokuwa Mzee sana na kuona siku zake za kuishi zinaelekea ukingoni, akamtaka mwanaye ampikie vinono ile ale kisha ambariki.

Maana yake alimtaka mtoto wake aliyemkusudia afanye jambo fulani la kumfurahisha, ndipo aachilie baraka zake.

Kwa msingi huo basi kukaibuka maswali mengine kama ifuatavyo:

1. Je, baraka hutolewa mara moja tu?
2. Je, baraka haziwezi kutolewa kwa watoto wote?
3. Je, mama anaweza kubariki watoto wake?

Kwa muktadha huu basi, huenda wengi wetu hatujui namna ya kubariki watoto wetu na wala hatujawahi kubarikiwa kama tunavyodhani.

Karibuni tujifunze.
 
Labda tuanze kwa mjadala wa kujua kua ''Baraka'' ni nini?

Unamfanyia nini/kitu gani mwanao ndio inatafsirika kua umembariki?
Baraka hutolewa kwa kumtamkia au kumnuia yale mema unayomtakia kwenye maisha yake, kwa mujibu wa historia za vitabu vitakatifu..... hii ilifanyika kama hafla maalumu na sio kujisemea tu moyoni au kila siku.
 
Baraka hutolewa kwa kumtamkia au kumnuia yale mema unayomtakia kwenye maisha yake, kwa mujibu wa historia za vitabu vitakatifu..... hii ilifanyika kama hafla maalum na sio kujisemea tu moyoni au kila siku.
Kwanini mpaka ifanyike hafla maalum ndio mtoto abarikiwe?

Hizo baraka za mzazi kwa mwanae anayezitimiza ni Mungu,baraka hapo inakua ni kama maombi kwa mzazi kumuombea mwanae mema kwa Mungu,sasa inakuaje isiwe baraka ya kujisemea tu moyoni? kwani ukijisemea tu moyoni Mungu hawezi kukusikia? kingine ni kwamba kwanini isiwe kila siku kumbariki mwanao? kwani ikiwa kila siku inakua kuna tatizo gani?

Naomba ufafanuzi zaidi.
 
Anayebariki ni Mungu, mtendaji anapeleka tu ombi mfano; nimemsaidia mtu halafu ananiambia "Mungu akupe maisha marefu"
Mungu lazima amsikie kutokana na uzito wa jambo na ombi

Baraka hazitolewi kiholela ni ngumu kupewa baraka kila siku.
 
Kwanini mpaka ifanyike hafla maalum ndio mtoto abarikiwe?

Hizo baraka za mzazi kwa mwanae anayezitimiza ni Mungu,baraka hapo inakua ni kama maombi kwa mzazi kumuombea mwanae mema kwa Mungu,sasa inakuaje isiwe baraka ya kujisemea tu moyoni? kwani ukijisemea tu moyoni Mungu hawezi kukusikia? kingine ni kwamba kwanini isiwe kila siku kumbariki mwanao? kwani ikiwa kila siku inakua kuna tatizo gani?

Naomba ufafanuzi zaidi.
Hiyo pengine ni vile tunavyotamani iwe, ila pamoja na maombi ya kila siku tumeona jambo likifanyika kwa ukubwa kwa siku maalumu.
Je tufuate maoni yetu au miongozo?
 
Anaweza! Yeye ni Mungu wa duniani tena baraka ya mama inashika kama ilivyo laana yake
Waefeso 6:2-3
Ukimtendea vyema mzazi na akafurahi unabarikiwa automatically
Sio kila baraka lazima itamkwe
Sahihi kabisa,kuna njia nyingi tu za mtu kupata baraka ''Kubarikiwa na Mungu''

Mfano unaweza kutoa msaada kwa wasiojiweza au kwa wenye uhitaji,furaha yao ndio baraka kwako,ukifanya mema utabarikiwa na Mungu wala haihitaji mtu akuombee baraka kwa Mungu,

Tenda mema kwa kila mtu na maisha yako yatakua ya baraka.
 
Kumbukumbu la torati 30:19
Mungu ameshaachilia baraka na laana duniani
Matendo yetu ndiyo yanayovuta baraka au laana

Sahihi kabisa,kuna njia nyingi tu za mtu kupata baraka ''Kubarikiwa na Mungu''

Mfano unaweza kutoa msaada kwa wasiojiweza au kwa wenye uhitaji,furaha yao ndio baraka kwao,ukifanya mema utabarikiwa na Mungu wala haihitaji mtu akuombee baraka kwa Mungu,

Tenda mema kwa kila mtu na maisha yako yatakua ya baraka.
 
Anaweza! Yeye ni Mungu wa duniani tena baraka ya mama inashika kama ilivyo laana yake
Waefeso 6:2-3
Ukimtendea vyema mzazi na akafurahi unabarikiwa automatically
Sio kila baraka lazima itamkwe
Ni vizuri mkuu kwa kufanya marejeo ya mandiko.

Lakini tumeona jinsi Isaka alivyoishiwa baraka zote kwa mtoto mmoja tu, hakuweza kumbariki yule mwingine.

Na wakati huo tunaona mama hakuhusika na baraka zozote ukiachana na zile figisu alizofanya.
 
Back
Top Bottom