Ni sahihi mzazi kuwakataza watoto wake kuangalia TV hasa kwenye kizazi hiki cha dot com?

mr pipa

JF-Expert Member
Jul 26, 2021
2,330
4,854
Kuna jirani yangu mmoja amewawekea msimamo na katazo kwa watoto wake kutoangalia television, na mwanzoni popote anapowakuta wanaangalia huwatandika sana viboko.

Katika sababu zake moja wapo anasema zinaharibu uwezo wa kufikiri, na kumharibu mtoto kisaikolojia katika ukuaji wake.

Zaidi huyu jirani amewapa base kwenye kusoma vitabu yaani watoto wake muda wao mwingi wanasoma vitabu ambavyo vipo nje ya uwezo wao mfano mtoto wake wa darasa la tatu humletea vitabu vya chemistry na bioloji yaani anamuandaa mtoto kwa miaka ijayo na sio ampe masomo ambayo anasomea darasani kwake hapana na zaidi atampa vitabu vya kiuchumi nk, na nikiri kwamba wale watoto wa jirani yangu ukikaa nao unaweza sema umekaa na mtu mwenye degree wa Cuba maana anavyokuchambulia mambo kujua ni wadogo utajiona mjinga mbele ya hutu tutoto.

Narudi kwenu wakuu ni sahihi mzazi kumpa katazo la kutoangalia tv aina yoyote hasa kwenye kizazi hiki cha taarifa, na maarifa.
 
Kama anataka wasiangalie tv atoe hito tv ya nyumbani wasiamgalie wote hapo atakua amewasaidia. Otherwise ni kumtafutia mtoto lawama tu.

Mtoto always ana mu imitate mzazi wake. Kile ambacho mzazi anafanya basi na mtoto naye atafanya tu. Kwa hiyo hakuna ubaya ikiwa na mzazi naye haangalii tv, ikiwa na mzazi naye anasoma vitabu.
 
Kama anataka wasiangalie tv atoe hito tv ya nyumbani wasiamgalie wote hapo atakua amewasaidia. Otherwise ni kumtafutia mtoto lawama tu.

Mtoto always ana mu imitate mzazi wake. Kile ambacho mzazi anafanya basi na mtoto naye atafanya tu. Kwa hiyo hakuna ubaya ikiwa na mzazi naye haangalii tv, ikiwa na mzazi naye anasoma vitabu.
kwao hakuna tv wala smatphone
 
Sio sahihi kuwakataza, ila msingi wa malezi ya watoto ni maadili. Hivyo ni wajibu wako mzazi kuwafundisha watoto wako tabia njema na hofu ya Mungu.
 
Darasa la 3 vitabu vya chemistry na biology!! Mmh!, huyo jirani anawabembelezea vitabu vya nje ya uwezo kuupata usingizi.
 
Usiwakataze.. watengenezee mazingira ya wao kuona tv sio ishu. Viko vingi vya kuwazoesha kufanya.
 
Ushoga huwa hauzuiliwi kwa style hiyo, huyo mzazi anajisumbua na kupoteza muda bureee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom