Watoto ni baraka au sadaka?

Wazo Langu

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
1,381
841
Habari wanajamvi
Kuna jambo nimekua nikisoma katika vyanzo mbalimbali. Kuhusu suala zima la watoto.

1. Je, watoto ni Baraka ama ni Sadaka? Hapa namaanisha ukizaa watoto wengi utakuwa na baraka nyingi kwamba kila mtoto anakuja na riziki yake wakiwa wengi utakuwa tajiri? Au ukizaa watoto wengi utakua umetoa sadaka sana ya kuwapa watu wengine uhai na kuwatunza ambapo baadae utapata thawabu?

Katika nchi zilizoendelea ambazo ni tajiri sana uwiano wao wa kuzaa upo chini kuliko nchi zetu za kimaskini.
Hii inanipa ukakasi sana.
1. Kuna Uhusiano wowote kati ya maendeleo na idadi ya watoto?

2. Nchi za kimaskini tunazaa watoto wengi ili kupata furaha na baraka zaidi?

3. Je, hawa hawa wasiotaka watoto wengi ni kwamba hawataki baraka nyingi? Au ni wachoyo hawataki kuwapa watu maisha na kuwahudumia bure?

Kama watoto ni baraka kwanini tunazuia mimba? Nani hataki baraka nyumbani kwake?
Kama watoto ni baraka kwanini wanaume wanakana mimba? Nani akatae Baraka hata ya kusingiziwa?

Kama watoto ni Baraka kwanini tunawaita 'mzigo'?
Kuna kauli za kila mtu ahangaike na mzigo wake hapo ikimaanisha kila mtu ahangaike na watoto wake.

Kuna mzazi hapendi kuona baraka zinakuja kwa mwanae katika umri mdogo?
Au hii baraka tunamaanisha nini?

Je, nani ambaye yupo Tanzania na hapendi kwenda Denmark, South Korea au Luxembourg kwa sababu ni nchi ambayo haina Baraka na furaha tele kama Tanzania, Somalia na Burkina
? Hapa tukichukulia kuwa watoto ni Baraka na furaha

Kuna ndoa zinakufa kukosa watoto, huenda walioana ili kupata hii baraka lakini mbona kuna ndoa zinaharibika kwa sababu ya hawahawa watoto?

Wakizaliwa watoto wenye tofauti unakuta mzazi mmoja anawatelekeza na kukimbia familia, watoto ni watoto. Au ndiyo kuogopa mafuriko yaliyokuja na baraka ya mvua?

Tukisema watoto ni Sadaka ni kwamba unatumika kuleta uhai na kuumwagilia lakini sadaka hii kama hukujaaliwa kuleta watoto kwanini isiwe kulea ambao tayari wapo? Ama inakua ni sadaka kamili ikiwa utawaleta wewe tu?
Nchi zilizoendelea hawataki kutoa sadaka ya kulea?

Tusemeje kwa anayepata mtoto halafu huyu mtoto akawa ni wa kuhudumiwa tu maisha yake yote?

Kama watoto ni Baraka au ni sadaka kwanini kuna watoto wapo mitaani bila makazi?
1680433359431.jpg
 
Aisee,inafikikirisha sana.ila Mungu alisema enendeni mkazaane mkaijaze dunia!kuwa na watoto wengi ni jambo jema mchoni pa Bwana!Tatizo kubwa ni ubinafsi umetawala kwa viongozi hasa wa Africa,kwa rasilimali tulizo nazo mfano Tanzania,inashindikana nini kuwapa raia wake wote wasio na kazi hata tsh.laki 3 kwa mwezi?
 
Back
Top Bottom