KanyeWest_Tz
JF-Expert Member
- Jul 18, 2026
- 237
- 539
Je uchawi ni imani?Uchawi ni suala la kiimani tu. Shida ni kwamba imani za kijadi zimetengenezewa taswira mbaya na historia ya ukoloni.
Kuamini kwamba damu ya Yesu imekuponya na kwenda kwa mganga hakuna tofauti ukifikiria. Kote ni kutafuta miujiza.
Imani ni kama miwani. Tunaitazama dunia kupitia imani zetu. Kwahiyo kila mtu anoana kwamba imani yake ni halisi.
Ingawa wengi huwa wanachanganya Kati ya Uchawi na Saikolojia(Magonjwa ya kawaida kabisa ya akili) lakini haiondoi ukweli kwamba Uchawi upo na unaathiri Sana maisha ya watu kiafya, kiuchumi,kijamii n.k.Hello jamii intelligence 👋
Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an
Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:
Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi
Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi
kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana
Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje
Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.
Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla
Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa
Sasa najiuliza...
Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?
Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?
Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?
Kuna hii pia👇
Ooh, wachawi wanapaa usiku...
Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?
Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa
Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?
Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?
Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu
Basi kuna mtu akamwambia mama:
Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔
Heh! 🤔
Nikastuka
Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?
Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine
Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.
Usiku naogopa kulala mwenyewe.
Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja
Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo
Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha
So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo
Mara nione hiki...
Mara nisikie kile...
Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?
Asieee!
Nikakaa nikasema:
Hapana, hizi mbona kama fix?
Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win
Nikaacha kabisa huo upuuzi
Nikaamua ku-clean akili yangu
Kuanzia hapo nikiambiwa
Njoo kwenye visomo
Nawaambia
Mimi sina tatizo lolote
Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu
Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku
Nikatumia zangu dawa nikawa fresh
Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu
Sioni mauza mauza wala nini
Naishi vizuri kabisa
Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu
Wala hakuna cha uchawi wala nini
Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake
Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...
Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?
Mashetani wana migodi yao huko?
Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi
Je, uchawi ni nguvu halisi?
Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?
Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...
Kwanini usitumike kinyume chake?
Au kama wachawi wanaweza kupaa...
Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?
Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?
ShesRise_1 ✋️
Unajua mkanganyiko uko wapi mkuu ni kwamba ukiacha kuamini hizo issue za uchawi wala hutouona kabisa kwenye maisha yakoIngawa wengi huwa wanachanganya Kati ya Uchawi na Saikolojia(Magonjwa ya kawaida kabisa ya akili) lakini haiondoi ukweli kwamba Uchawi upo na unaathiri Sana maisha ya watu kiafya, kiuchumi,kijamii n.k.
Kama ipi share basi tujifunzeMifano ya matukio ya kichawi ni mingi sana ambayo mimi binafsi nimeishuhudia wazi wazi
Yeah, ...mtu anaamua ku ziba gap kwa kufikiria vitu vya kujazia kwa asichokifahamu.Mi naona uchawi ni theory tu
Hatari sana kakaYeah, ...mtu anaamua ku ziba gap kwa kufikiria vitu vya kujazia kwa asichokifahamu.
Miujiza ipo. Muujiza ni msamiati wa kiimani tu ila kimsingi ni kupata bahati nzuri. Ukitokewa na jambo zuri usiloweza kulifafanua basi utaliita muujiza.Je uchawi ni imani?
Na ukiamini kuna miujiza?
Hakuna uchawi , bali ukosefu wa uelewa juu ya jambo husika.Hello jamii intelligence 👋
Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an
Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:
Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi
Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi
kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana
Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje
Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.
Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla
Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa
Sasa najiuliza...
Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?
Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?
Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?
Kuna hii pia👇
Ooh, wachawi wanapaa usiku...
Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?
Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa
Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?
Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?
Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu
Basi kuna mtu akamwambia mama:
Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔
Heh! 🤔
Nikastuka
Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?
Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine
Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.
Usiku naogopa kulala mwenyewe.
Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja
Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo
Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha
So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo
Mara nione hiki...
Mara nisikie kile...
Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?
Asieee!
Nikakaa nikasema:
Hapana, hizi mbona kama fix?
Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win
Nikaacha kabisa huo upuuzi
Nikaamua ku-clean akili yangu
Kuanzia hapo nikiambiwa
Njoo kwenye visomo
Nawaambia
Mimi sina tatizo lolote
Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu
Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku
Nikatumia zangu dawa nikawa fresh
Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu
Sioni mauza mauza wala nini
Naishi vizuri kabisa
Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu
Wala hakuna cha uchawi wala nini
Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake
Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...
Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?
Mashetani wana migodi yao huko?
Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi
Je, uchawi ni nguvu halisi?
Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?
Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...
Kwanini usitumike kinyume chake?
Au kama wachawi wanaweza kupaa...
Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?
Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?
ShesRise_1 ✋️
Mimi naweza kuthibitisha kwa kusema haupo kwa sababu sijauonaWakuu, tukitaka kuelewa vizuri hili suala bila kupishana lugha, lazima tukubali kuwa uchawi na saikolojia ni vitu viwili vinavyotembea barabara moja lakini kwa mitazamo tofauti. Hakuna anayeweza kubisha kwa 100% kuwa uchawi upo, na hakuna anayeweza kuthibitisha kwa 100% kuwa haupo.
Twin issue ni kwamba mbona ambao hawaamini uchawi hawapati hayo mazingaombwe🤔Ukiangalia upande unaounga mkono kuwa uchawi upo, huwezi kupuuza shuhuda za watu mbalimbali, kuna mambo yanatokea kwenye jamii zetu ambayo sayansi haina majibu nayo kabisa mpaka sasa, na hata sayansi yenyewe imeshakubali kuwa kuna nguvu za asili na nishati katika ulimwengu huu ambazo bado hatujazielewa kikamilifu, kama nishati ya mawimbi ya simu ipo na hatuioni kwa macho lakini inatuwezesha kutuma jumbe sehemu tofauti, ni nani anayejua kama kuna negative spiritual energies ambazo wachawi wanazitumia kuathiri maisha ya watu?
Hapa hapa yaani whyUkiangalia upande unaosema uchawi haupo, napo utaona wazi kuwa mambo mengi tunayoyasikia ni kama propaganda, hadithi za kufikirika, na uoga tu wa kurithi. Hii habari ya kwamba mchawi anaweza kupaa kwa ungo, au anaweza kumgeuza genius kuwa kilaza, kwanini isifanye kazi kinyume chake?
Kama uchawi ni sayansi thabiti, kwanini hauna kanuni zinazotabirika kama zilivyo sayansi nyingine? Mbona nguvu zake zinaonekana tu gizani au pale mtu anapokuwa na uoga?
Naunga mkono hoja yakoHapa ndipo suala la saikolojia linapoingia, iko hivi binadamu ana asili ya kutaka kutafuta sababu ya kila kitu kinachomtokea, mtu akifeli sehemu yoyote au biashara yake ikienda tofauti ni rahisi sana kisaikolojia kutoa lawama kuhusu uchawi kuliko kukubali kuwa pengine alifanya maamuzi mabaya.
Hapa kuna kituMwisho wa siku, mijadala ya aina hii huwa inabaki kuwa neutral kwamba uchawi upo kama nguvu halisi ya kiroho, lakini hiyo nguvu inafanya kazi kwa kutumia udhaifu wa saikolojia ya binadamu. Usipoamini na ukiiweka akili yako sawa, hiyo nguvu huwa inakosa nguvu kwa mtu husika lakini ukiamini na kuingia uoga, unaifungulia mlango hiyo nguvu mwilini wako kukuathiri.
Hiyo mifumo inayoshirikiana kufanya dunia iende sawa, yenyewe ndio uchawi au miujiza yenyewe?Miujiza ipo. Muujiza ni msamiati wa kiimani tu ila kimsingi ni kupata bahati nzuri. Ukitokewa na jambo zuri usiloweza kulifafanua basi utaliita muujiza.
Dunia ni dhahania(abstract) sana. Kuna vitu viiingi sana vidogo vidogo vinavyoshirikiana kufanya dunia iende sawa. Mfano mwili wako; Kuanzia zile molecule za protini zinazounda seli, mpaka viungo ulivyonavyo, hiyo yote ni mifumo inayoshirikiana kukuweka hai.
Sasa kukaa chini na kuchambua tuweze kujua nini kinasababisha nini ni kazi ngumu hivyo tunaishia kukisia majibu yetu wenyewe. Huko kukisia ndo kwenye imani huko. Maji yakibandikwa motoni yanachemka. Hii ni hakika, kila mtu anaona. Hutokaa usikie mtu akisema maji kuchemka ni uchawi. Lakini jambo gumu kuelewa mfano gonjwa la saratani, litahusishwa sana na uchawi kwasababu halifafanuliki kirahisi. Kuelewa tu mifumo ya seli hai inavyoleta saratani ni kamzozo.
Mfano umeenda kwa mganga kuhusu suala la ajira. Baada ya hapo ukaomba kazi na ukapata. Vigezo unavyo. Umehangaika kutuma maombi na kufanya saili. Kwa kuwa hujui waajiri wameona nini kwako(huenda ni vigezo, huenda ni haiba, huenda ni bahati tupu) utakisia kulingana na imani(hii ni miwani tu umevishwa tokea utotoni) zako. Labda ni Mungu, labda ni mganga, labda ni nyota nk nk. Miujiza inatokea kwa namna hii.
Shukran mkuu asante kwa maoniHakuna uchawi , bali ukosefu wa uelewa juu ya jambo husika.
Kwa muktadha huu, kitu/jambo lisipoonekana kwa macho maana yake halipo?Mimi naweza kuthibitisha kwa kusema haupo kwa sababu sijauona
Paragraph ya mwisho kabisa, umeisoma vizuri ukaielewa Twin?Twin issue ni kwamba mbona ambao hawaamini uchawi hawapati hayo mazingaombwe🤔
Ukilinganisha na hao wanaomini hizo mambo
Hapo ndo penyewe sasa. Hakuna ajuaye🤷🏾♂️Hiyo mifumo inayoshirikiana kufanya dunia iende sawa, yenyewe ndio uchawi au miujiza yenyewe?
Point yako si kuwa kila kitu kina chanzo?Miujiza ipo. Muujiza ni msamiati wa kiimani tu ila kimsingi ni kupata bahati nzuri. Ukitokewa na jambo zuri usiloweza kulifafanua basi utaliita muujiza.
Dunia ni dhahania(abstract) sana. Kuna vitu viiingi sana vidogo vidogo vinavyoshirikiana kufanya dunia iende sawa. Mfano mwili wako; Kuanzia zile molecule za protini zinazounda seli, mpaka viungo ulivyonavyo, hiyo yote ni mifumo inayoshirikiana kukuweka hai.
Sasa kukaa chini na kuchambua tuweze kujua nini kinasababisha nini ni kazi ngumu hivyo tunaishia kukisia majibu yetu wenyewe. Huko kukisia ndo kwenye imani huko. Maji yakibandikwa motoni yanachemka. Hii ni hakika, kila mtu anaona. Hutokaa usikie mtu akisema maji kuchemka ni uchawi. Lakini jambo gumu kuelewa mfano gonjwa la saratani, litahusishwa sana na uchawi kwasababu halifafanuliki kirahisi. Kuelewa tu mifumo ya seli hai inavyoleta saratani ni kamzozo.
Mfano umeenda kwa mganga kuhusu suala la ajira. Baada ya hapo ukaomba kazi na ukapata. Vigezo unavyo. Umehangaika kutuma maombi na kufanya saili. Kwa kuwa hujui waajiri wameona nini kwako(huenda ni vigezo, huenda ni haiba, huenda ni bahati tupu) utakisia kulingana na imani(hii ni miwani tu umevishwa tokea utotoni) zako. Labda ni Mungu, labda ni mganga, labda ni nyota nk nk. Miujiza inatokea kwa namna hii.
Kabisa. Japo vyanzo vingine havijulikani.Point yako si kuwa kila kitu kina chanzo?
Inawezekana ukawa sahihi lakini sio sana, maana kutokujua kwako majibu hakumaanishi kuwa hiyo mifumo haipo au haikuathiri Mkuu.Hapo ndo penyewe sasa. Hakuna ajuaye🤷🏾♂️
Majibu ya uhakika hayapo. Miungu, uchawi, mizimu, vyote vinapwaya.
Binafsi naamini tunaweza kuishi vizuri tu bila hayo majibu.
Basi hapo unakoseaKabisa. Japo vyanzo vingine havijulikani.
Hakika muujiza ni jambo ulilodhani ni gumu sana lakini likawa jambo rahisi kwa namna ulikua hutarajii naamini huo ndiyo muujizaMiujiza ipo. Muujiza ni msamiati wa kiimani tu ila kimsingi ni kupata bahati nzuri. Ukitokewa na jambo zuri usiloweza kulifafanua basi utaliita muujiza.
Najaribu kuelewa hapaDunia ni dhahania(abstract) sana. Kuna vitu viiingi sana vidogo vidogo vinavyoshirikiana kufanya dunia iende sawa. Mfano mwili wako; Kuanzia zile molecule za protini zinazounda seli, mpaka viungo ulivyonavyo, hiyo yote ni mifumo inayoshirikiana kukuweka hai.
Sasa kukaa chini na kuchambua tuweze kujua nini kinasababisha nini ni kazi ngumu hivyo tunaishia kukisia majibu yetu wenyewe.
Huko kukisia ndo kwenye imani huko. Maji yakibandikwa motoni yanachemka. Hii ni hakika, kila mtu anaona. Hutokaa usikie mtu akisema maji kuchemka ni uchawi. Lakini jambo gumu kuelewa mfano gonjwa la saratani, litahusishwa sana na uchawi kwasababu halifafanuliki kirahisi. Kuelewa tu mifumo ya seli hai inavyoleta saratani ni kamzozo.
🤔Mfano umeenda kwa mganga kuhusu suala la ajira. Baada ya hapo ukaomba kazi na ukapata. Vigezo unavyo. Umehangaika kutuma maombi na kufanya saili. Kwa kuwa hujui waajiri wameona nini kwako(huenda ni vigezo, huenda ni haiba, huenda ni bahati tupu) utakisia kulingana na imani(hii ni miwani tu umevishwa tokea utotoni) zako. Labda ni Mungu, labda ni mganga, labda ni nyota nk nk. Miujiza inatokea kwa namna hii.
1.Kijana A alimtukana kijana B halafu kijana A(Mtukanaji) akapindishwa mdomo on the spot na kijana B(Mtukanwaji) tena alimwambia kabisa "Mimi huwa situkanwi"Unajua mkanganyiko uko wapi mkuu ni kwamba ukiacha kuamini hizo issue za uchawi wala hutouona kabisa kwenye maisha yako
Huoni hapo kama kuna walakini?
Kama ipi share basi tujifunze