Heaven Seeker
JF-Expert Member
- May 12, 2017
- 478
- 1,047
Si Serikali wala Sekta binafsi, ukiangalia, kwa uhalisia, kwa watu walio wengi, wanapata mishahara iliyo chini na uhalisia wa gharama za maisha. Mfano unakuta mwajiriwa wa Serikalini, graduate, kwa walio wengi, ukiachilia watu wachache sana waliopo kwenye sekta chache, wanalipwa kuanzia 750K- 950K kama basic salary. Ukiondoa makato yote mtu anajikuta anabakiza kama 500K hivi.
Katika hiyo 500K, unajikuta gharama za maisha kwa mwezi, yaani ulipie kodi ya nyumba, chakula, usafiri na bills nyinginezo ni karibu ya 1M kwa mwezi.
Ukienda kwa wenzetu nchi zilizoendelea, hata ufanye kazi ya kiwango kile cha chini kabisa kama usafi, warehouse assistance, food delivery, housekeeping, caretaker, huwezi kukuta mshahara wake ni chini ya gharama za maisha. Yaani wenzetu wame-standardize kwamba kiwango cha chini cha malipo kwa mtu kiwe sawa au juu kidogo ya gharama za kawaida za kuishi kwa mtu kwa mwezi. Yaani unakuta kwa mfano mtu anayefanya kazi ya usafi nchi zilizoendelea kama Sweden, UK, Uholanzi n.k analipwa average Euro 1800 - 2000 kwa mwezi, ila gharama za maisha kwa mwezi ni kama Euro 1500 hivi. Na kumbuka hapa ni kwa non-professional jobs.
Sasa swali langu ni kuwa, nyie wataalamu wa Uchumi na sheria hapa kwetu hebu tuambieni, Je ni kwa nini waajiri wengi hapa kwetu wanalipa mishahara chini ya gharama za kuishi zile za hali ya kawaida, mfano tuchukulie maisha ya kawaida mtu aishi angalau kwenye nyumba ambayo kodi ni 250K kwa mwezi, chakula na bills nyinginezo alipie angalau 600K kwa mwezi, jumla iwe angalau 850K.
Swali la pili, Je, ni hii ni haki au tunanyonywa?
Karibuni kwa mjadala.