tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,881
- 18,295
Inasikitisha sana kumkuta kijana mwenye nguvu chini ya miaka 40 ameingia kwenye uchawa na kushabikia vitendo vya uchawa. Mtu aliyechagua maisha ya uchawa anaweza kudhani kuwa amechagua maisha ya mteremko (kitonga) ama kwa kujitoa ufahamu au kuchukulia kirahisi madhara ya uchawa. Tatizo chawa huwa wanatangaza mafanikio yao tu lakini wanachelea kutangaza gharama wanazoingia kwenye kazi yao ya uchawa.
Ni rahisi, kwa mfano, changudoa au punda wa madawa ya kulevya kutangaza mafanikio yake kimaisha lakini kamwe hawezi kutangaza madhira anayoyapata. Kazi za aina hii ni mbaya sana kwani licha ya kumdhalilisha mtu kwenye jamii, humsababishia maumivu ya kisaikolojia ya muda mrefu ambayo hudumu nayo katika kipindi chote cha maisha yake.
Watu wanaoishi na chawa hawawezi kukubali kunyonywa bila kuweka masharti magumu. Na chawa ili aendelee kunyonya hana chaguo lingine zaidi ya kukubali masharti hayo, bila kujali ubaya au uzito wake. Utashangaa chawa mwenye umri wa miaka 30 hana mradi wowote lakini anamiliki mali za thamani kubwa. Kumbe ni shoga, msagaji, msagwaji au punda. Anakubali kutumikishwa kwenye ushoga, usagaji au upunda ilmradi mkono uende kinywani. Halafu anatoka hadharani kuwatangazia watu utajiri wake bila kutangaza utumikishwaji wake.
Tabia ya uchawa inawafanya vijana wawe wategemezi na kukubali kutumiwa na wamiliki wa chawa bila kuhoji. Pia linapelekea vijana kutoweka juhudi zozote kujitafutia mali kwa njia halali zinazokubalika kisheria na kijamii.
Vijana waliopo shuleni na vyuoni wanashindwa kuweka jitihata kwenye masomo baada ya kuona vijana wenzao wanafanikiwa kwenye uchawa hata bila kwenda shule. Aidha, vijana waliohitimu masomo na wakakosa kazi nao watajitumbukiza kwenye uchawa kwa kudhani kuwa watafanikiwa kwa haraka, hivyo kuwafanya wasitafute kazi halali kwa mujibu wa taaluma zao.
Matokeo ya haya yote ni kuongezeka kwa idadi ya watu wasiofikiri na wasiokuwa na ubunifu wowote kwenye kazi binafsi au za kuajiriwa. Na kibaya zaidi ni kuongezeka kwa idadi ya vijana wasiofaa katika jamii kama vile mashoga, wasagaji, waswagaji, changudoa, punda, n.k.
USHAURI
Serikali isipokuwa makini, hivi vitendo vya uchawa kwa vijana vilivyoshamiri hapa nchini vitasababisha madhara makubwa sana kwa vizazi vijavyo. Ni wakati muafaka sasa serikali ichukue hatua maridhawa kuupiga vita uchawa lakini pia viongozi na wanasiasa wanaotumikisha vijana kwenye uchawa yafaa waache tabia hiyo mara moja.
Kiongozi anaweza asione uchungu kumtumikisha mtoto wa mwenzake kwenye uchawa lakini atambue kuwa uchawa ni kansa ambayo ikisambaa kwenye jamii haiwezi kuwaacha salama watoto wake pia. Ubaya wa uchawa ni kutoridhika. Anaweza akadhani watoto wake wanaridhika na mali anazomiliki na kuwa hawawezi kuwa chawa. Anajidanganya sana. Ipo siku atawakuta watoto wake nao wakitumikishwa kwenye uchawa.
Haya mambo tumekuwa tukiyashuhudia hapa nchini kwa muda mrefu. Lazima tukubaliane kuwa uchawa una madaraja mengi. Ikiwa mwanao hatatumikishwa kwenye uchawa wa daraja la kwanza, lazima tu atakuja kutumikishwa kwenye uchawa wa daraja la pili au la tau. Tunashuhudia watoto wa vigogo nao wameanza kuingia kwenye uchawa wa daraja la juu.
Madaraja ya chawa
Hivyo basi, natoa rai kwa serikali kupiga marufuku vitendo vya uchawa na utumikishwaji kwani madhara yake yanaenea kwa haraka sana. Tusikubali kujenga ukuta wakati uwezo wa kuziba ufa tunao.
In short, chawaism has got detrimental and far-reaching consequences in the community. That is the reason I stress this habit to be banned forthwith before it destroys our society to an irreparable existent.
Nawasilisha.