Je napotaka kuagiza gari ni sawa kupata ushauri wa Fundi? Nini kifanyike kushawishi mafundi kuongeza ujuzi zaidi?

Je napotaka kuagiza gari ni sawa kupata ushauri wa Fundi? Nini kifanyike kushawishi mafundi kuongeza ujuzi zaidi?

Livanga

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2010
Posts
475
Reaction score
156
Kutokana na uzoefu na kwa kuzingatia changamoto tunazopitia sasa kadri muda unavyogea tutakuwa tuna uhaba mkubwa wa mafundi wajuzi wa kutatua matatizo ya magari kwa ufasaha ni kutokana na ukweli kwamba mafundi wengi hawana tabia ya kupenda kuongeza ujuzi wao na wanaamini kile wanachokijua kinatosha.
Mfano: Mafundi wengi hapa Tanzania hujikita katika kutengeneza magari ya aina fulani, ambapo Toyota ndio inayopendwa zaidi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wanakuwa confortable kutengeneza magari ya Toyota ikilinganishwa na mengine. Hivyo basi, unapowauliza kwa ushauri kuhusu gari la kuagiza, wengi wao watapendekeza Toyota na hata hivyo mafundi mara nyingi hupendelea version za zamani zaidi kuliko zile za kisasa. Sababu kuu ya hili ni ukosefu wa uelewa wa kutatua changamoto mpya zinazoweza kutokea kwa magari ya kisasa as mengi ni sofisticated.

Kwa kuzingatia haya, ningependa kuuliza:
  1. Je, ni sawa kuomba ushauri kwa fundi kabla ya kufanya uamuzi wa kuagiza gari?
  2. Nini kifanyike kuwashawishi vijana wengi ambao ni mafundi kwa sasa kuongeza ujuzi na wale ambao wanategemea kujiunga na fani hii?
  3. Je kuna vyuo vinavyotoa elimu fasaha na ya kisasa kwa ujuzi huu muhimu?
  4. Shule za msingi na sekondari ambazo sasa zinakuwa na Elimu amali zimewezeshwa kitaaluma na vifaa kwa ajili ya kufundishia kiasi ya kwamba watoto wakitoka hapo wanakuwa confotable kufanya kazi as watakuwa wameelewa nasio kukariri?
 
Mafundi wetu wengi ni wale wa chini ya mwembe. Changamoto sana.
 
Lakini haiwqzuii wqo kujiongeza tatizo ndio lipo hapo na changamoto wanaziona as more advanced vehicles are coming year by year ambazo zinawawiq vigumu kutwtuq na hivyo kuwanyima kazi au kufanya kwa kubahatisha na hivyo kuwatia watu hasara kwa kuharibu bila kujua au kununu vifaa ambavyo wala sio vibovu.
Wakati huo mafundi hao mata nyingi ni wabishi sana kukubali gari ifanyiwe diagnosis.
 
Back
Top Bottom