Kwa hiyo unata kusema kuwa akili/utashi tuliopewa ni makosa ya MUNGU MWENYEZI?
Yaani kama ingewezekana asingeweka kabisa kitu utashi?
Huoni kuwa angekuwa hajakutendea haki ya kukupa Uhuru?Sasa si tungekuwa kama robots ambazo hazina hiari ambazo ukiziamrisha zikafanye chochote haziwezi kuhoji kama kuna madhara au faida?
Yaani unavyosema angemset ibilisi kwa namna ambayo asingeasi ina maana hapo neno hiari kwa ibilisi lisingekuwepo.Maanake ibilisi angekuwa kama robots.
Sasa MWENYEZI MUNGU hapendi kulazimisha.Ndio maana akakupa hiari ili ujichagulie mwenyewe.
Tena unatakiwa umshukuru sana maana utashi aliokupa ndio unaokusaidia kuchagua eidha kumwabudu au kutokumwabudu,kuhoji au kutohoji,kupuuza mambo au kuyatilia maanani.
Akaona haitoshi,amekupa na sheria za kufuata ili uishi maisha yasiyo na madhara kwako na kwamba ukizikiuka utaishia pabaya.Tena amekupa na nafasi ya kutubu endapo utakosea kwa bahari mbaya.
Sasa iweje ukikiuka hayo maagizo useme eti yeye ana makosa wakati kila kitu amekupa?Huo si utakuwa uzembe wa kiwango kikubwa?Yani ufanye makosa alafu umlaumu MUNGU MWENYEZI?
Tatizo letu ni kwamba tunapofanya makosa tunatafuta pa kuzitupia lawama (Kwa kesi hii utasema isingekuwa utashi nisingekosea) badala ya kuomba msamaha. Wakati huo tunsahaukuwa huo utashi tunaoulaumu ndio pia umetuwezesha kujua kuwa tumefanya makosa.
Nakushauri usitafute kisingizio mkuu.MUNGU MWENYEZI NI MKAMILIFU NA AMEKUFANYIA MEMA MENGI.
EE MUNGU MWENYEZI TUSAMEHE WAJA WAKO MAANA SI KWA HIZI KUFURU TUNAZOKUTENDEA.
Sent using
Jamii Forums mobile app