Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Naweza kujua kwa uhakiki wa kimantiki kwamba hicho kitu hakipo na hakikuwahi kuwepo zaidi ya hadithi,hakuna matendo bayana wala misikiko ya sauti na muonekano wa aina yeyote sifa zake zote zimebakia kuwa hadithi na vihisishi,KIKIWEPO KWA UWEPO ITAKUWA VYEMA ZAIDI*
Hebu nisaidie ni vp uliweza kujua kuwa hakuna Mungu?
 
Wakuu hamjambo!

Kama kichwa cha Uzi huu kinavyouliza, Mimi nikiri kuwa naamini uwepo wa Mungu mmoja aliyeumba vyote vinavyoonekana na visivyoonekana pia.

Katika vitabu mbali mbali vya dini, tunaelezwa kuwa dhambi ilitokana na uasi alioufanya shetani dhidi ya Mungu, biblia inaenda mbali kwa kudai kuwa vita vilipiganwa huko mbinguni na shetani alishindwa na akatupwa duniani akiwa na theluthi ya malaika wakawa upande wake.

Maswali:

1. Ikiwa kabla ya shetani kuasi hakukuwa na dhambi yoyote ile, tena alikuwa mbinguni kwenye utakatifu wa MUNGU, je shetani alishawishiwa au alitoa wapi mawazo ya uasi Ikiwa hakukuwa na shetani yeyote mwingine?

2. Kama MUNGU hujua mwanzo hata mwisho wa viumbe vyake, INA maana alikuwa anajua kuwa shetani atakuja kuasi baadae na kusababisha dhambi, kwanini alimuumba?
Jambo la kufikiria hapa ni kuona kwamba MUNGU alimuumba shetani/Lucifer ( dhambi) mahususi ili kuja kuwa upande maovu. Dhana hii inadhihirisha kuwa MUNGU ndie aliyeumba dhambi.

3. Je, lengo la MUNGU lilikuwa mwanadamu aishi milele bila kufa?
Hapa kuna mazoea yalishajengeka hasa kwa wakristo na waislamu kuamini kuwa isingekuwa Eva/Hawa kudanganywa na Shetani basi Leo hii wanadamu wasingekuwa wanakufa ( immortal). Hii dhana haina mantiki hasa ukiwaza kuwa wanadamu wangezaliana na kuishi milele bila kufa nadhani dunia ingekuwa imejaa mabara na visiwa vyote.
Hivyo MUNGU akaamua kuleta mauti ili kudhibiti ( control) idadi ya wanadamu duniani isizidi uwezo wa rasilimali zilizopo, fikiri Leo hii watu wanauwana kugombania ardhi je ingekuwaje akina Adam na bibi yetu Eva wangekuwepo wote?

4. Je, Dini ni matokeo ya mwanadamu kumhofia shetani?
Tunaishi katika jamii ambazo kila MTU ana juhudi za kujikwamua kuondokana na shida Kama magonjwa, njaa, vita, ambazo Mara nyingi wanadamu wanahesabu kuwa hayo yote ni sababu ya shetani, na dini wanaona ndio kimbilio ili kumkwepa shetani asiwadhuru.
Lakini wao wanaamini kuwa wanasali ili kumtukuza MUNGU, lakini kiukweli dini ni hofu ( fear of unknown) isiyo na ithibati yoyote.

5. Je, Mungu anawapenda wanadamu? Hapa jibu laweza kuwa ni ndiyo, bahati mbaya sana ukiangalia uhalisia toka zamani kuna ugumu wa kusema ndiyo au hapana.
Tunaambiwa kuwa mbinguni kulikuwa na vita Kali sana, mwaishowe malaika aitwaye Mikaeli alimshinda shetani, Mungu akamtupa ibilisi huyo huyo duniani kwa wanadamu anaowapenda sana. Mungu hakuona sehemu nyingine ya kulitupa hilo joka ila duniani ambako ndio wanadamu aliwaweka. Hii ni sawa na kuwarushia watoto wako furushi lenye nge wengi huku umewafungia chumbani na kuwataka wajikinge wasing'atwe hata kidogo.

Nimekuja kuamini kuwa: MUNGU yupo ila dini zote ni michezo ya kukamata fikra za wanadamu tu, inawezekana kabisa kuwa dini ziluletwa na shetani mwenyewe ili kuwachonganisha wanadamu wasiishi kwa upendo na amani.
Angalia jinsi Palestine na Israel, syria , Iraq n.k wanavyouana kwa misingi ya dini.

Niishie hapo, naomba waumini/maswahaba mje mtueleze hizi hoja.

Cc: Mshana Jr
Cc: Kiranga
Na wanajamvi wote karibuni.
Niliwahi kuwailiza wachungaji na mashekhe kuhusu maswala haya nilionekana kama muasi, na hawana majibu zaidi ya kukwambia Akili ya mwanadamun
inapoishia ndipo ya Mungu inapoanzia. Umeeleza na kudafanua vizuei kwa mytindo wa maswali. Thanks.
 
Nahitimisha mjadala kwa kusema "Kama Mungu angemuua Shetani baada ya kuasi je siku mtakapopata hizo habari mngeamini vipi kwamba shetani alikuwa muasi hivi???

Je mngeamini vipi kwamba Mungu ana upendo kwa wema na wabaya???

Ila niwashauri tu tusitende dhambi Kwa makusudi tujitahidi hat zile za bahati mbaya tuzitubu upesi tujuapo.
Sote tungejifunza kuwa Mungu si wakichezea. Na dhamhi tungeziepuka.
Yaani mtu anampiga risasi mwezake au anamchoma visu mwenzake au kwa mateso mengine yogote makali. Halafu unasema wewe ni Mungu na kwamba mtu huyo mwenye kumtesa na kunyanyasa wengine kwa makusudi kabisa akitubu uamsamehe?? Huyo Mungu ni wa ajabu sana.
 
Space haiumbwi. Labda nitumie neno lingine ni kwamba kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, Mungu alikuwa anaishi kwenye sehemu iliyowazi/tupu (hakukuwa na chochote kile zaidi ya yeye mwenyewe tu)
Kwahiyo hapa unakubali kwamba kuna vitu Mungu hakuumba, kama vile space.

Na kama unakubali au kuamini kuwa space haiumbwi, kwanini usiamini au kukubali pia kuwa ulimwengu hauumbwi?

Na pia swali lingine, kwa kabla ya kuumba ulimwengu huu(ambao kitheologia unakadiriwa kuwa na umri wa miaka 6000 tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa). Hapo kwenye space Mungu alikuwa anafanya nini kwa makarne na makarne?!
 
Hebu nisaidie ni vp uliweza kujua kuwa hakuna Mungu?
Mkuu Tz mbongo, kwa nilivyomuelewa huyo mdau ni kwamba, kadiri ya mahubiri na hadithi zinazomuhusu huyu Mungu, akizichanganua kimantiki, anagundua kuwa Mungu huyo hayupo. Hata mimi hapo namuunga mkono.

Binafsi ninaamini kuwa yawezekana Mungu ni kweli yupo ila si wa sifa hizi tunazohubiriwa na Abrahamic Religion (hasa ukristu na uislamu).

Ni vigumu sana kuamini kuwa Mungu huyu anaupendo mkuu usiomithirika ilihali watu wasiokuwa na hatia(mfano watoto wachanga) wanakufa kwa majanga ya asili kama vile tsunami nk.
 
Nitajie kinachokufanya uone kuwa inawezekana Mungu kuwa yupo? Unapinga sifa zinazoelezwa kumuelezea Mungu ila unadhani kuwa Mungu anaweza kuwepo,hebu nieleze ni yapi yenye kukufanya uone kuna uwezekano wa kuwepo Mungu?
 
Siku zote jambo likishakuwa la imani basi lazima watawepo wenye kuamini na wasioamini,hakuna jambo la imani lenye kuaminiwa na watu wote.

Lakini ambacho hadi sasa sijapata majibu ni madai ya kwamba hakuna Mungu,sijajua ni vp wameweza kujua hakuna Mungu?
Mkuu, imani ni kukubali ukweli wa jambo lisiloweza kuthibitika.
Rejea maana ya imani katika Wikipedia.

Kwahiyo, kwa ujumla kusema kwamba Mungu yupo au hayupo zote hizo ni imani kwa sababu hakuna anayeweza kuthibitisha.

Tatizo linakuja, wale waaminio kuwa Mungu yupo, wanapochanganua sifa za Mungu huyo, ndio hapo wanapoibuka watu na kusema logically Mungu wa sifa hizo hayupo. Kwa sababu sifa zile zinakuwa zikijichanganya kimantiki.

Ni sawa na mimi niseme, ninapenda kunywa kinywaji ambacho ni cha baridi sana (mpaka sentigrade -30), na wakati huo huo ni cha moto sana (mpaka sentigrade 100). Kwa kweli kinywaji hicho hakipo, hata kama hamjawahi kukiona!!
 
Nitajie kinachokufanya uone kuwa inawezekana Mungu kuwa yupo? Unapinga sifa zinazoelezwa kumuelezea Mungu ila unadhani kuwa Mungu anaweza kuwepo,hebu nieleze ni yapi yenye kukufanya uone kuna uwezekano wa kuwepo Mungu?
Lakini pia yawezekana hayupo.

Tunapozungumzia uwezekano, maana yake ni kutokuwa na uhakika. Sina sababu hasa za kibinafsi zinazonifanya niamini au nisiamini kuwa Mungu yupo au hayupo. Kwa sababu sijui ukweli ni upi.

Lakini kwa nyie mnaosema kuwa yupo, na kuzitaja sifa zake ndipo hapo ninaposema kuwa wa sifa hizo mnazozitaja hayupo.
 
Mkuu, imani ni kukubali ukweli wa jambo lisiloweza kuthibitika.
Rejea maana ya imani katika Wikipedia.

Kwahiyo, kwa ujumla kusema kwamba Mungu yupo au hayupo zote hizo ni imani kwa sababu hakuna anayeweza kuthibitisha.

Tatizo linakuja, wale waaminio kuwa Mungu yupo, wanapochanganua sifa za Mungu huyo, ndio hapo wanapoibuka watu na kusema logically Mungu wa sifa hizo hayupo. Kwa sababu sifa zile zinakuwa zikijichanganya kimantiki.

Ni sawa na mimi niseme, ninapenda kunywa kinywaji ambacho ni cha baridi sana (mpaka sentigrade -30), na wakati huo huo ni cha moto sana (mpaka sentigrade 100). Kwa kweli kinywaji hicho hakipo, hata kama hamjawahi kukiona!!
Hao watu tatizo lao lingekuwa ni sifa tu za Mungu ndio wanazopinga basi haya majadiliano yangepata hitimisho,ila kilichopo ni kwamba wao wanasema hakuna Mungu kabisa hivyo wao hawaamini kabisa Mungu wa aina yeyote yule,hizo hoja za kwamba maelezo ya kuhusu sifa za Mungu yanajipinga hutumia tu kutetea msimamo wao na si kwamba ndio sababu za wao kutukuamini Mungu.
 
Lakini pia yawezekana hayupo.

Tunapozungumzia uwezekano, maana yake ni kutokuwa na uhakika. Sina sababu hasa za kibinafsi zinazonifanya niamini au nisiamini kuwa Mungu yupo au hayupo. Kwa sababu sijui ukweli ni upi.

Lakini kwa nyie mnaosema kuwa yupo, na kuzitaja sifa zake ndipo hapo ninaposema kuwa wa sifa hizo mnazozitaja hayupo.
Sasa mkuu mbona unajichanganya tu,wewe unasema inawezekana Mungu akawepo(huna uhakika) halafu hapohapo unasema huna sababu zilizokufanya uone huo uwezekano wa kuwepo Mungu!!!!!

Kama Mungu jinsi anavyoelezwa kumekufanya useme haiwezekani kuwepo,iweje tena uje kusema Mungu anawezakuwepo ila bila sababu ya kukufanya uone uwezekano huo?
 
Kwahiyo hapa unakubali kwamba kuna vitu Mungu hakuumba, kama vile space.

Na kama unakubali au kuamini kuwa space haiumbwi, kwanini usiamini au kukubali pia kuwa ulimwengu hauumbwi?

Na pia swali lingine, kwa kabla ya kuumba ulimwengu huu(ambao kitheologia unakadiriwa kuwa na umri wa miaka 6000 tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa). Hapo kwenye space Mungu alikuwa anafanya nini kwa makarne na makarne?!

Kila mtu ana uelewa wake kuhusu neno Mungu. Mungu maana yake ni kianzilishi/chanzo (source) cha ulimwengu kuwepo. Hata kisayansi huwezi kuambiwa ulimwengu umejitokeza bila kuwa na chanzo kama vile energy, n.k kwahiyo ile chanzo cha kutokea ndio inatumika neno Mungu kwa maana kilichosababisha/anzisha uwepo wa ulimwengu.

Swali lako la pili ni kwamba muda unaanza kuhesababika baada ya tukio na sio kabla ya tukio kwahiyo huwezi kusema kuwa imepita makarne na makarne wakati hakukuwa na hesabu yoyote ya muda. Inawezekana ikawa hata sekunde haikupita Mungu akaumba ulimwengu hapo hapo. Au mwenzangu unaweza kuniambia Mungu kakaa muda gani kisha ndio akaumba ulimwengu? Au ni karne ngapi zimepita ndipo akaumba ulimwengu?
 
Sasa mkuu mbona unajichanganya tu,wewe unasema inawezekana Mungu akawepo(huna uhakika) halafu hapohapo unasema huna sababu zilizokufanya uone huo uwezekano wa kuwepo Mungu!!!!!

Kama Mungu jinsi anavyoelezwa kumekufanya useme haiwezekani kuwepo,iweje tena uje kusema Mungu anawezakuwepo ila bila sababu ya kukufanya uone uwezekano huo?
Mkuu, mimi sijajichanganya sehemu yoyote. Kusema kwamba yawezekana mungu yupo, au yawezekana hayupo, huko si kujichanganya. Ila ni kuthibitisha jinsi gani sijui. Kwa kifupi mimi sijui kiuhakika kama Mungu yupo au hayupo.

Ila nyie ambao mnasema kwamba mna uhakika Mungu yupo ndio hapo tunahitaji mtuhakikishie au mtuthibitishie.

Mnaposema Mungu yupo na anaupendo mkuu kwa viumbe vyake, ilihali baadhi ya viumbe wake wasio na hatia wanaangamia kwa majanga ya asili yaliyo ndani ya uwezo wake kuyadhibiti, hapo ndio mnatuchanganya kabisa.

Mnaposema kaumba kila kitu kasoro space (rejea jibu la mmoja hapo juu), kumbe kuna vitu hajaumba, sasa ni nani kaumba space!? Bado mnatuvuruga!!

Tuthibitishieni na tuone kwamba Mungu ndio mwenye sifa hizo, ili wote tuamini kuwa yupo!!
 
Kila mtu ana uelewa wake kuhusu neno Mungu. Mungu maana yake ni kianzilishi/chanzo (source) cha ulimwengu kuwepo. Hata kisayansi huwezi kuambiwa ulimwengu umejitokeza bila kuwa na chanzo kama vile energy, n.k kwahiyo ile chanzo cha kutokea ndio inatumika neno Mungu kwa maana kilichosababisha/anzisha uwepo wa ulimwengu.

Swali lako la pili ni kwamba muda unaanza kuhesababika baada ya tukio na sio kabla ya tukio kwahiyo huwezi kusema kuwa imepita makarne na makarne wakati hakukuwa na hesabu yoyote ya muda. Inawezekana ikawa hata sekunde haikupita Mungu akaumba ulimwengu hapo hapo. Au mwenzangu unaweza kuniambia Mungu kakaa muda gani kisha ndio akaumba ulimwengu? Au ni karne ngapi zimepita ndipo akaumba ulimwengu?
Mkuu, unafahamu vizuri habari ya spacetime!?

Mi pia siifahamu kiundani lakini angalau inamaanisha kwamba space na time ni vitu pacha, vinaendana na havitenganishwi!!

Unapozungumzia space (ambayo kadiri ya jibu ni kuwa haijaumbwa) basi unazungumzia time(ambayo bila shaka nayo itakuwa haijaumbwa).

Sasa katika space hiyo, Mungu alikuwa anafanya nini kabla ya kuumba ulimwengu!?

Mungu mjuzi wa yote: inamaanisha alijua angetuumba, malaika wema wangemuasi na kuwa waovu, adam na hawa wangekula tunda na mwishowe hawa angempa adhabu ya kuzaa kwa uchungu na adam kuhangaishwa na maisha.

Anaweza vyote na anatupenda sana, Je hawezi umsamehe mara moja shetani na kumfanya kuwa mwema tena!?
 
Hao watu tatizo lao lingekuwa ni sifa tu za Mungu ndio wanazopinga basi haya majadiliano yangepata hitimisho,ila kilichopo ni kwamba wao wanasema hakuna Mungu kabisa hivyo wao hawaamini kabisa Mungu wa aina yeyote yule,hizo hoja za kwamba maelezo ya kuhusu sifa za Mungu yanajipinga hutumia tu kutetea msimamo wao na si kwamba ndio sababu za wao kutukuamini Mungu.
Nafikiri wanamaanisha zaidi Mungu wa sifa hizo mnazozitaja. Kama kuna Mungu wa sifa nyingine basi awekwe ili sifa zake zidadavuliwe.

Kama naye hayupo, inamaana Mungu hayupo!!

Kama Mungu yupo ni Mungu gani!?

Kama Mungu ndio chanzo cha ulimwengu, je bado yupo!? (Chanzo hicho bado kipo). Maana ulimwengu ulianza muda mrefu umepita
 
Mkuu, unafahamu vizuri habari ya spacetime!?

Mi pia siifahamu kiundani lakini angalau inamaanisha kwamba space na time ni vitu pacha, vinaendana na havitenganishwi!!

Unapozungumzia space (ambayo kadiri ya jibu ni kuwa haijaumbwa) basi unazungumzia time(ambayo bila shaka nayo itakuwa haijaumbwa).

Sasa katika space hiyo, Mungu alikuwa anafanya nini kabla ya kuumba ulimwengu!?

Mungu mjuzi wa yote: inamaanisha alijua angetuumba, malaika wema wangemuasi na kuwa waovu, adam na hawa wangekula tunda na mwishowe hawa angempa adhabu ya kuzaa kwa uchungu na adam kuhangaishwa na maisha.

Anaweza vyote na anatupenda sana, Je hawezi umsamehe mara moja shetani na kumfanya kuwa mwema tena!?

Nimekuuliza swali je unaweza kunitajia huo muda ambao Mungu amekaa ni wiki, miezi, miaka, au ni karne ngapi zimepita ndipo akaumba ulimwengu? Au imepita kipindi za miaka mingapi ndipo ulimwengu ukajitokeza? Haiwezekani nikakutajia shughuli gani alikuwa anafanya pasipo wewe kunitaji muda.

La pili ni kwamba mimi nazungumzia uwepo wa Mungu, usichanganye kati ya uwepo wa Mungu na sifa/tabia ya Mungu. Mimi sipo kwenye kuzungumzia sifa na tabia za Mungu ambavyo hivyo vitu utavikuta kwenye vitabu vya dini. Mimi ninaamini uwepo wa Mungu kama kisababishi cha kuwepo kwa vitu vyote vilivyomo ulimwenguni. Mimi sio mwamini wa vilivyomo kwenye vitabu vya dini na ndio maana kuna maswali niliuliza post namba 184 na 186 kwa mmoja wa mtu anayeamini Mungu wa kwenye vitabu.
 
Mkuu asante kwa jibu lako fikirishi lakini naweza kujibu kama ifuatavyo:

La kwanza, kama kweli Mungu amekuwepo milele na milele maana yake kabla ya kuumba kitu chochote amekuwepo hapo kwenye space(kadiri ya mdau mmoja hapo juu, kuwa Mungu alikuwa kwenye space kabla ya kuumba chochote) kwa muda infinity(maana yake hana mwanzo). Sasa swali linakuja kwa wanaomuamini, katika Muda huu infinity, Mungu alikuwa anafanya nink hapo kwenye space peke yake? (Kumbuka hiyo ni kabla hajaumba chochote hata malaika)

La pili, mkuu hauwezi ukasema kuwa Mungu yupo pasi na kutanabaisha sifa zake. Yaani sifa ni kama identity ya uwepo wake, kwa mfano, wewe unaamini kuwa mungu ni chanzo cha vitu vyoote. Tayari hiyo ni sifa unayoamini anayo, na hapohapo swali linazuka, Je kama Mungu ni chanzo cha vyoote, je Mungu ni chanzo cha shetani, dhambi na uovu uliomo duniani!?
Nadhani utaona ni jinsi gani watu wanatumia sifa wampazo Mungu kupinga uwepo wake!
 
Tatizo linakuja palepale haiwezekani kutaja shughuli gani aliyokuwa anafanya pasipo kupata muda halisi kabla ya kuumbwa vilivyomo ulimwenguni. Embu fikiria pengine labda kaumba vilivyomo ulimwengu baada ya sekunde moja tu au baada ya dakika moja tu je? Kwanza tupate huo muda halisi kisha ndio tupate kuona Mungu kapoteza miaka mingapi ndipo akaumba hivi vilivyomo, na ndipo tujadili sasa kwamba je ndani ya hiyo miaka kadhaa aliyopoteza alikuwa akifanya nini.

Hoja yako ya pili ni kwamba habari ya shetani na dhambi vinapatikana kwenye simulizi za vitabu vya dini kitu ambacho nilishakujibu ya kwamba mimi siviamini.
 
Mkuu wewe Unaweza kuwa ulisoma chuo kikubwa kama havard au Cambridge,,lakini ukija kutafuta kazi hapa tz au popote lazima ufanyiwe interview.

Swali ni je unapofanyiwa ile interview ina maana kile chuo kikubwa ulichosoma kilikupa cheti ukiwa hujakamilika??

Je, huyu anaekupa mtihani wa interview ana level inayostahili kukupa mtihani kumlinganisha hata na tutor wa pale havard au Cambridge?

Kitu kizuri hujaribiwa ili kuthibitisha ubora wake?

La sivyo wewe na cheti chako cha havard havard ungekuwa unaingia Kazini moja kwa moja maana uko 100% perfect
Hasa huyo mshindani anawapima binadamu au Mungu ndio anajipima yeye mwenyewe? Kwasababu yeye Mungu ndiye aliyemuumba huyo mshindani na ndiye yeye huyo huyo aliyeumba na binadamu, sasa kama binadamu ana mapungufu inamaana yeye ndio kafeli kuumba huyo binadamu akawa mkamilifu. Kwahiyo Mungu anampima binadamu ili ajue kakosea kumuumba kwa ukamilifu kwa asilimia ngapi?

Nimeuliza pia kuwa Mungu anafaidika na nini kwa kumuumba huyo mshindani? Wewe tu kama mzazi hupendi wala hutafurahia kuona mtoto wako anapata matatizo kwahiyo la kwanza utajitahidi kumwekea mazingira ya mwanao kutopata matatizo yoyote. Sasa kwa Mungu kumuumba mshindani kwa makusudi huoni inapingana na dai la Mungu ni mwenye upendo?

La pili ni kwamba binadamu wote wanaumbwa na Mungu mmoja si ndivyo? kama ndivyo na je akili ya binadamu pia anajiwekea mwenyewe huyo binadamu au Mungu ndio anamwekea na akili? Unadhani ni Kwanini akili ya mtu X iende duniani kuchagua dhambi wakati akili ya mtu Y isichague dhambi wakati wameumbwa na Mungu mmoja? Wakati Mungu anamuumba mtu X si alijua fika kuwa akili yake itaenda kuchagua dhambi duniani, je kitendo kumpeleka duniania hivyo hivyo pasipo kurekebisha kwa mfanya awe mkamilifu inaashiria nini?
 
Mkuu Achimwene-Masasi ukihusisha ile miti na mapenzi au Mambo ya uchafu kama ulawiti unakuwa umeacha maswali mengi zaidi ya majibu.Ukipata kujua ile miti ikiwakilisha nini utapata majibu ya maswali mengi sana.
"DHAMBI" Ni kukiuka maagizo ya mwenyezi mungu,kwenda kinyume na sheria za mwenyezi mungu,kufanya mambo ambayo Ni chukizo mbele za mungu.hapo mwanzo hakukuwako na dhambi, Before human creation dunia ilikua inakaliwa na viumbe wanaitwa majini,majini wameumbwa na mwenyezi mungu na wapo wema na wabaya,majini Ni viumbe visivyoonekana Kwa macho Ila kutokana na maandiko matakatifu Ni kwamba wameumbwa Kwa moto,Kubwa lao ndilo Hili tunalisikia linaitwa "lucipher",yeye alipewa uwezo mkubwa Sana na mwenyezi mungu juu ya viumbe vyote vilivyokuwa duniani na mbinguni ambavyo mungu aliviumba, Kwahyo majini waliishi muda mrefu Sana Hapa duniani kabla ya Adam "binadamu wa kwanza"
MWANZO WA DHAMBI
viumbe hao wa Kwanza kuishi duniani walianza kufanya dhambi ya "kulawitiana" na walizidi Sana kufanya dhambi ndipo mwenyezi mungu akawaangamiza kabisa katika uso wa dunia lakini "lucipher" hakuangamizwa Kwa sababu hakushiriki katika dhambi ya kulawiti/kulawitiana.
Ndipo mwenyezi mungu akaamua kuumba kiumbe chenye ujuzi na akili kuliko viumbe vya mwanzo "majini "akamuumba Adam ili aje atawale dunia na vilivyomo lakini suala hili lilipingwa na Jini lucipher ndipo ilipozaliwa dhambi Kwa Mara ya Kwanza Kwa maana alipinga matakwa ya mwenyezi mungu ambaye anapoamua jambo hashauriani na yeyote.
Kwahyo mwenyezi mungu akamuumba Adam na akampa akili na uwezo wa kutawala vitu vilivyomo duniani,na akamweka edeni.
Lucipher Yule jini mkuu akalaaniwa na kutupwa duniani lakini Bado alikua na uwezo Ule ambao aliumbwa nao,
Baadaye mungu akaona si vyema Adam awe binadamu peke yake duniani akamfanyia "msaidizi" ili atawale pamoja Naye lakini akawapa masharti akawaamuru wale matunda yote katika Ile bustani ambayo aliwaweka isipokuwa tunda LA mti wa katikati mti wa ujuzi wa mema na mabaya (pale bustanini palikuwa na mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya)
Ndipo Yule jini aliyetupwa duniani akawaonea wivu Adam na Eva akaandaa mpango wa kuwashawishi watende dhambi ili asiwe peke yake katika laana ya mwenyezi mungu.
Yule jini ndiye Yule nyoka tunaemsoma katika HOLLY BIBLE wapendwa, akamtokea Hawa Wakati Adam akiwa usingizini akamshawishi kufanya dhambi ya kulawitiwa naye, kisha Adam kumlawiti mkewe Hawa, Hapa ndipo binadamu wa Kwanza alipofanya dhambi Kwa muumba wake. Kwa hivyo kuna mambo watu wanaumiza Sana vichwa kuyajua
1.bustani Ni mwili wa mwanamke
2.mti wa ujuzi wa mema na mabaya Ni tendo la kulawiti/kulawitiana/kulawitiwa
3.mti wa uzima Ni Ile njia ya tendo LA ndoa ambayo Ni imehalalishwa na mwenyezi mungu pale tu unapofanya ki utaratibu ambao mungu anaukubali
4.nyoka Ni Yule jini luciopher
Nikipata muda nitaeleza haya mambo vizuri ili tuyaelewe kutokea katika maandiko pia tukumbuke kwamba maneno ya mungu mtu yeyote anaweza kuyasoma lakini sio kuyaelewa
.....ngoja nifuatilie mkeka wangu....
 
Tatizo linakuja palepale haiwezekani kutaja shughuli gani aliyokuwa anafanya pasipo kupata muda halisi kabla ya kuumbwa vilivyomo ulimwenguni. Embu fikiria pengine labda kaumba vilivyomo ulimwengu baada ya sekunde moja tu au baada ya dakika moja tu je? Kwanza tupate huo muda halisi kisha ndio tupate kuona Mungu kapoteza miaka mingapi ndipo akaumba hivi vilivyomo, na ndipo tujadili sasa kwamba je ndani ya hiyo miaka kadhaa aliyopoteza alikuwa akifanya nini.

Hoja yako ya pili ni kwamba habari ya shetani na dhambi vinapatikana kwenye simulizi za vitabu vya dini kitu ambacho nilishakujibu ya kwamba mimi siviamini.
Asante mkuu kwa kujibu!

Kwanza kabla ya kutoa hoja zangu, namimi niseme kitu!
Unajua mkuu, haya mambo ukiyajadili bila kuegamia upande wowote yanaleta raha sana. Kwa kweli kwangu mimi ni burudani tosha hii ninapoona watu kila hoja inayotolewa lazima ihojiwe. Safi sana na huu ndio u great thinker, hakuna kukubali kirahisi rahisi.

Sasa niende kwenye hoja!
Hili la kwanza unalozungumzia, ni kuwa kadiri ya wanaoamini Mungu, ni kuwa Mungu hana mwanzo wala mwisho, maana yake ni wa milele. Yaani kabla ya kuumba hata kitu kumoja, tayari alishakuwepo kwa kipindi Infinity kurudi nyuma. Sasa atuwezi tukasema kipindi infinity ni muda gani kwa kutaja kwa namba!! Yaani ni muda usiotamatika!!. Ona ilivyongumu ku visualize!!

Hoja yako ya pili, mkuu kadiri ya imani yako ni kuwa Mungu ni chanzo cha vitu vyooote. Sasa hapa pia tutahitaji utuelezee, Je, chanzo cha chanzo hicho ni kipi!?
Ndio, kila chanzo kina chanzo, angalia mfano huu, labda tuseme Chanzo cha kifo cha John Doe ni ajali, chanzo cha ajalu hiyo ni mwendo kasi wa dereva, chanzo cha mwendo kasi huo ni kulewa, chanzo cha ulevi wa dereva ni stress, chanzo cha stress, ni usaliti wa mkewe, chanzo cha usaliti wa mkewe ni... chanzo chanzo chanzo mpaka mwisho, na kujirudia rudia humohumo.

Mambo haya yanafurahisha sana!!
 
Back
Top Bottom