Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

ManchoG

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,510
2,000
"Mimi nimesema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo. Sijasema vilivyomo kwenye ulimwengu vimejiumba vyenyewe".
Hii sehemu ya paragraph yako baada ya kuipitia imenipa tafakuri yenye kiulizo

Tuseme kama mtu wa dini akidai kuwa kuna chanzo ambacho wao huita Mungu chenye ujuzi wote lakini si chenye upendo wote unaweza kukubaliana nae katika hilo..?
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
52,502

You seem to be so slow. Yani miaka yote hii tunabishana ndiyo leo unafikiria swali hili?

For real? Nakuona unajongea Mzee wa Annunaki.

Kwanza nitamuuliza, anakubali kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo? Tulimalize la hiyo kabla ya kurukia lingine.

Akikataa hatuanzi kujadili lingine kabla ya kumaliza hilo.

Akikubali Mungu huyo hayupo, nitamtaka atoe ushahidi na uthibitisho wa kuwepo kwa huyo dubwana anayemsema yupo.

Zaidi, dubwana huyo si Mungu, kwa sababu ana mapungufu ya upendo. Mungu hana mapungufu yoyote.
 
Mfia dini

JF-Expert Member
Jun 20, 2019
308
250
Ukiwa hujui square root ya mbili ni nini, ni lazima square root ya mbili iwe kumi?
Nikikwambia mtoto wa miaka mitatu hawezi kuwa baba mzazi wa mtu wa miaka hamsini, ni lazima nimjue baba wa huyo mtu wa miaka hamsini?
Mimi nakwambia katuni mtoto wa miaka mitatu hawezi kuwa baba mzazi wa mtu wa miaka hamsini (kwa sababu ya timeline contradiction).
Wewe unaniuliza, kama hiyo katuni mtoto wa miaka mitatu si baba wa huyo mtu wa miaka hamsini, baba yake huyo mtu wa miaka hamsini ni nani?
Sijui, na sihitaji kujua baba yake mtu mwenye miaka hamsini ni nani ili nijue kwamba mtu mwenye miaka mitatu hawezi kuwa baba mzazi wa mtu mwenye miaka hamsini.
Ukweli kwamba simjui baba halisi wa mtu wa miaka hamsini, haunizuii kujua kwamba mtoto wa miaka mitatu hawezi kuwa baba wa mtu wa miaka hamsini. Kwa sababu ya timeline contradiction.
Ukweli kwamba sijui ulimwengu umeanzaje, haunizuii kujua kwamba haujaanzishwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa sababu Mungu huyu dhana ya kuwepo kwake inaji contradict yenyewe, na hivyo hawezi kuwepo.
umeandika upuuzi usio eleweka
anyways kama umeshindwa kuthibitisha Mungu hayupo sitaendelea kupoteza muda wangu kubishana na wewe kwani mpumbavu hawezi kuwa mwerevu wala mbuzi/nguruwe kuwa kondoo
endelea na upuuzi,upumbavu,umbuzi,na uzezeta wako salama
warning!!
Popote uonapo post yangu usidiriki kureply ,infact kama ungekuwa mwerevu usingeli ingia jukwaa la Dini/thread ya dini kwani ni jukwaa/thread ya/la watu waaminio uwepo wa Mungu ,jukwaa la watu kama wewe ni jukwaa la Mapenzi na si humu
 
Unaelewa kwamba, kama mimi kweli ni mpumbavu kama unavyosema, basi upumbavu wangu nao unathibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo?

Unaelewa kuwa Mungu huyo kuumba ulimwengu ambao wapumbavu wanaweza kuwepo, wakati ana uwezo wote wa kuumba ulimwengu ambao wapumbavu hawawezi kuwepo, ni contradiction?
 
Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Dec 1, 2013
1,196
2,000
Mkuu Kiranga nazingatia post yako No.526 nitaegemea kwenye mambo mawili kati ya kadhaa ulioyaongelea

1.Kwamba dini ilianza kwa watu kutaka kujipa majibu ya maswali ambayo hawakuwa na majibu yake

Sasa Mbona mpaka leo ambapo kuna technology,,innovation na design za ajabu bado kuna almost watu 5 billion wanasali.Hauoni hapo kuna jambo zaidi ya kukosa majibu ya maswali..Huhisi kusali ni natural characteristics aliozaliwa nayo binadamu na sio tabia alioikuta baada ya kuzaliwa.??? Hudhani kwamba unahitaji mda zaidi ujiulize kuhusu sala na ibada kwa Mungu kwamba na wewe inakuhusu ila umechelewa tu??

Huoni magharibi baada ya kuacha makanisa matupu wameamua kufanya Mambo machafu mno ndoa za jinsia moja,,beastility na upuuzi usiosemekana ambapo dini na sala vilipokuwepo waliogopa kuvifanya?

2.Sala ni therapy ya watu maskini wasio na therapist
Hivi Mbona kuna matajiri wengi sana wanasali,,,angalia Marekani ambayo bado kanisa lina nguvu uone ni matajiri wangapi wanasali,,,nenda kwa wayahudi wa ultra orthodox,,nenda Moscow utaona matajiri wakisali,,,majirani zangu waislam pitia Riadh,,tehrani mpaka Azerbaijani utaona matajiri wakisali,,njoo Africa ndio usiseme.Labda ungeniambia hao wasio na dini wanatafuta therapy artificial kwa kuwa hawajataka kujua natural ilio katika dini.
 
Hii technology unayoiona kubwa leo wewe, bado ni ndogo sana. Ndiyo kwanza tumeanza kugundua vitu. Einstein's Relativity imethibitishwa miaka 100 tu, na hata hiyo watu wengi mpaka leo hawajui inazungumzia kitu gani.

Ukienda Kariakoo usimamishe watu kumi, uwaulize mmoja baada ya mwingine, theory ya Relativity ya Einstein inazungumzia nini, wangapi wanaweza kukupa jibu sahihi angalau la jumla tu?

Watu wengi ni watumiaji tu wa hizo technology na innovation, hawaelewi zinavyofanya kazi. Watu hawaelewi Einstein's Relativity inavyo support GPS na Satellite na Internet, wanatumia tu hivi vitu bila kujua hata kwa juu juu vinavyofanya kazi.

Sasa hawa nao unawahesabu kwamba wanaelewa technology kiasi cha kuwafumbua macho wahoji habari za Mungu?

Inawezekana watu wakawa wanazaliwa na hali ya kutaka kusali au kuabudu, lakini hilo halitoshi kufanya Mungu awepo. Watu wanazaliwa na hali ya kujiona wanaona, lakini macho yao yamenyimwa uwezo wa kuona X-Rays, Gamma Rays, Ultraviolet Rays, Radio waves etc. Kutoiona hiyo miale hakufanyi isiwe muhimu au isiwepo.

Pia unaweza kuzaliwa ukaangalia kwa macho ukaona the earth is flat, naturally unaona the earth is flat, lakini kuona hivyo hakufanyi dunia iwe flat kama ni ya mviringo. Unahitaji uchunguzi zaidi kujua mambo magumu na mazito, si mambo yanayojulikana kwa kukubali vitu kirahisi tu.

Huoni magharibi baada ya kuacha makanisa matupu wameamua kufanya Mambo machafu mno ndoa za jinsia moja,,beastility na upuuzi usiosemekana ambapo dini na sala vilipokuwepo waliogopa kuvifanya?
Sala/dini, zaidi ya kuwa therapy kwa masikini, ina kazi nyingi sana.

1. Inatumiwa na matajiri na watawala kuwafanya masikini watumwa.
2. Inatumiwa na wabaguzi wa rangi kujitenga wao kundi hili ili wawabague wengine (ndiyo maana makanisa mengi Marekani unakosema watu wanasali sana yamegawanyika kwa ubaguzi wa rangi, ni social clubs za kubaguana kwa rangi)
3. Ni sehemu za watu kujionesha na kujitangaza, nani katoa sadaka kubwa, nani ana gari kubwa nani ana familia nzuri.
4. Ni sehemu ya hata wasioamini Mungu kwenda na kusema "Hata kama Mungu hayupo, dhana ya kuwepo kwake ni muhimu sana katika kuweka usalama, watu wengi, hususan masikini, wakijua Mungu hayupo, watafanya fujo sana.
5. Ni sehemu ya kwenda kutoa sadaka ili ujisikie umelipia mabaya yote uliyofanya. Ni therapy hata ya matajiri. Wezi na wauza madawa ya kulevya kibao wanaenda makanisani kutoa sadaka kubwa tu Mungu awabariki katika kazi zao. Angalia historia ya Mafia Mob na kanisa uone wakubwa wa Mafia walivyo Wakristo wazuri.
Mbona hayo mambo watu wanafanya mpaka kanisani huko Roma kila siku wana scandals?

Mbona kuna watu hawaamini uwepo wa Mungu na kwa kutoamini huko wanaishi Maisha yenye higher moral grounds?

Mimi nisipoamini kuwepo Mungu, naona mtu hawezi kunijaza ujinga nikaingia katika "holy war" na kumuua mtu kwa jina la Mungu. Hapo tayari kutoamini uwepo wa Mungu kumenisaidia kutoingia katika ujinga wa kulipua watu wenzangu kwa kisingizio cha mungu.

Huko Afrika watu wanapoamini Mungu sana mbona nako kuna ushenzi mwingi sana tu?

2.Sala ni therapy ya watu maskini wasio na therapist
Hivi Mbona kuna matajiri wengi sana wanasali,,,angalia Marekani ambayo bado kanisa lina nguvu uone ni matajiri wangapi wanasali,,,nenda kwa wayahudi wa ultra orthodox,,nenda Moscow utaona matajiri wakisali,,,majirani zangu waislam pitia Riadh,,tehrani mpaka Azerbaijani utaona matajiri wakisali,,njoo Africa ndio usiseme.Labda ungeniambia hao wasio na dini wanatafuta therapy artificial kwa kuwa hawajataka kujua natural ilio katika dini.
Sala/dini, zaidi ya kuwa therapy kwa masikini, ina kazi nyingi sana.

1. Inatumiwa na matajiri na watawala kuwafanya masikini watumwa.
2. Inatumiwa na wabaguzi wa rangi kujitenga wao kundi hili ili wawabague wengine (ndiyo maana makanisa mengi Marekani unakosema watu wanasali sana yamegawanyika kwa ubaguzi wa rangi, ni social clubs za kubaguana kwa rangi)
3. Ni sehemu za watu kujionesha na kujitangaza, nani katoa sadaka kubwa, nani ana gari kubwa nani ana familia nzuri.
4. Ni sehemu ya hata wasioamini Mungu kwenda na kusema "Hata kama Mungu hayupo, dhana ya kuwepo kwake ni muhimu sana katika kuweka usalama, watu wengi, hususan masikini, wakijua Mungu hayupo, watafanya fujo sana.
5. Ni sehemu ya kwenda kutoa sadaka ili ujisikie umelipia mabaya yote uliyofanya. Ni therapy hata ya matajiri. Wezi na wauza madawa ya kulevya kibao wanaenda makanisani kutoa sadaka kubwa tu Mungu awabariki katika kazi zao. Angalia historia ya Mafia Mob na kanisa uone wakubwa wa Mafia walivyo Wakristo wazuri.
 
NANDERA

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,029
2,000
Amri za Mungu zilishushwa duniani baada ya dhambi kuingia. Anyways, dini/imani kwangu kwa sasa haina mashiko.
Amri ni sheria. Dhambi ilikuwepo kabla Adam na Hawa hawajawa wafuasi wa mdhambi wa kwanza shetani na ndiyo maana walipewa sheria ya kutokula tunda. Walipovunja sheria wakawajibishwa.

Ila thatha .... umeacha imani kabitha?? Imani ina nafasi yake bwana ilimradi usifukie akili chini.
 
NANDERA

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,029
2,000
Yule Musa aliemtokea Yesu wakati alipopanda mlimani na baadhi ya wanafunzi wake unajua alitokea wapi?? Hivi unajua nabii Musa alizikwa na Mungu kwa jinsi alivyokuwa anampenda.Musa alienda pazuri kushinda hao walioingia kanaani.
Sawa. Hoja ya msingi ni kuwa hatma ya mtu haiamuliwi na kiwango cha mema au mabaya. Hilo la Musa kumtokea Yesu hata Samweli alitolewa katika wafu na mganga sijui mwaguzi akaongea na Sauli kuhusu matokeo ya vita kisha akarudishwa kwa wafu. Yaani Samweli na unabii wake wote ule anatolewa alikolala mauti na nguvu za 'giza'. Sasa sielewi paradiso imekaakaaje kwa kweli.
 
Eli79

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
26,528
2,000
Amri ni sheria. Dhambi ilikuwepo kabla Adam na Hawa hawajawa wafuasi wa mdhambi wa kwanza shetani na ndiyo maana walipewa sheria ya kutokula tunda. Walipovunja sheria wakawajibishwa.

Ila thatha .... umeacha imani kabitha?? Imani ina nafasi yake bwana ilimradi usifukie akili chini.
Imani haina mashiko NANDERA, ni mkusanyiko wa hadithi za watu waliokuwa na akili nyingi zamani hizo!!
 
ManchoG

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,510
2,000
You seem to be so slow. Yani miaka yote hii tunabishana ndiyo leo unafikiria swali hili?

For real? Nakuona unajongea Mzee wa Annunaki.

Kwanza nitamuuliza, anakubali kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo? Tulimalize la hiyo kabla ya kurukia lingine.

Akikataa hatuanzi kujadili lingine kabla ya kumaliza hilo.

Akikubali Mungu huyo hayupo, nitamtaka atoe ushahidi na uthibitisho wa kuwepo kwa huyo dubwana anayemsema yupo.

Zaidi, dubwana huyo si Mungu, kwa sababu ana mapungufu ya upendo. Mungu hana mapungufu yoyote.
'Mzee wa annunaki'.. hizo stori ni za lifecoded mimi huwa nampa fagio tu

Ila mkuu ni dhahiri kuwa hakuna atakayeweza kuyathibitisha hayo juu yako_eneo ulilosimamia ni gumu hakuna wa kukubadili labda utake mwenyewe

Ila juu yangu Sijui ni kwa nini ninaposoma aina ya mtazamo kama wako napata picha Kama mmea wenye mizizi mikubwa lakini wenye uchache wa majani 'sijui niite mbuyu'..!

Hausumbuliwi na mabadiliko ya kimazingira kwakuwa upo dhabiti kwelikweli na unaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi_ila u mkiwa kwakuwa malisho hauna..!

Ndege Ni ngumu kutua kwake unawezaje pata nyimbo nzuri za kuvutia ukipumzika chini yake..!

Ni mtazamo au muonekano ambao naona si mzuri Sana kwa afya ya akili zetu usiku_hii ni kwa Mimi lakini
 
Kiranga is a singularity.
 
Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Dec 1, 2013
1,196
2,000
Kuhusu samweli kupandishwa juu kuna maswali mengi sana magumu.ila kuhusu musa na kutokea kwake pamoja na Elia ambae hakufa bila shaka walitokea sehemu nyengine ila sio chini kwenye bottom less pit.Na isitoshe walikuwa na Yesu asiekuwa na dhambi au ushirikina.
Sawa. Hoja ya msingi ni kuwa hatma ya mtu haiamuliwi na kiwango cha mema au mabaya. Hilo la Musa kumtokea Yesu hata Samweli alitolewa katika wafu na mganga sijui mwaguzi akaongea na Sauli kuhusu matokeo ya vita kisha akarudishwa kwa wafu. Yaani Samweli na unabii wake wote ule anatolewa alikolala mauti na nguvu za 'giza'. Sasa sielewi paradiso imekaakaaje kwa kweli.
 
Bonded35

Member
Jul 11, 2019
50
125
Huo uhuru unakujaje ilihali wakati anamleta binadamu hakukuwa na makubaliano ya kuchagua kwamba unataka uletwe duniani au hutaki?
2. Umezungumzia swala la utashi, je binadamu wote wana utashi ulio sawa au unatofautiana?

3. Je Mungu anapenda na kufurahia binadamu watende dhambi? Mfano wakati anamuumba k2206 alijua kabisa kabla hata ya kumleta duniani kwamba kwa utashi niliyomwekea huyu k2206 atachagua mambo kadhaa wa kadhaa ambayo yatampeleka motoni. Je hapo k2206 akija duniani
atakuwa kinyume na matarajio ya Mungu au atapita mule mule kama Mungu alivyotaraji?

4. Je wewe kwa ridhaa yako unapenda kutenda dhambi? Na je Ukijitathmini toka asubuhi kunakucha hadi usiku unapolala hakuna kosa lolote ulilotenda kinyume na Mungu? Kama lipo, je unadhani kuna nini ndani yako kinachokupelekea kutokuwa mkamilifu kwa asilimia 100?

Sent using Jamii Forums mobile app
We kiumbe sio wakawaida..... kwamaswali hayo akikujibu kwaufasaha kesho najinyonga.
 
Bonded35

Member
Jul 11, 2019
50
125
You seem to be so slow. Yani miaka yote hii tunabishana ndiyo leo unafikiria swali hili?

For real? Nakuona unajongea Mzee wa Annunaki.

Kwanza nitamuuliza, anakubali kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo? Tulimalize la hiyo kabla ya kurukia lingine.

Akikataa hatuanzi kujadili lingine kabla ya kumaliza hilo.

Akikubali Mungu huyo hayupo, nitamtaka atoe ushahidi na uthibitisho wa kuwepo kwa huyo dubwana anayemsema yupo.

Zaidi, dubwana huyo si Mungu, kwa sababu ana mapungufu ya upendo. Mungu hana mapungufu yoyote.
Kiranga, kunamuda huwa nikisoma post zako, natamani nikuchue nikutie mfukoni, ilimladi ikitokea naitaji kukusoma nakutoa mfukoni nakusoma. Alafu nikichoka kukusoma nakutia tena mfukoni, wewe mtu nikichwa mbayaa,,
 
Namichiga

Senior Member
Jun 1, 2017
159
250
Nyie ndo mnaitwaga bendera fuata upepo. Sasa ume comment nini?
Wengine dini wamerithi waache tu!, wanashindwa hata kujiuliza kwamba binadamu wote tumeumbwa na huyo mungu sawa,sasa iweje sisi Waafrika hadi aje mtu mweupe (mwarabu+mzungu) kutufundisha namna ya kuabudu kwani sisi sio watu wake?
 
NANDERA

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,029
2,000
Kuhusu samweli kupandishwa juu kuna maswali mengi sana magumu.ila kuhusu musa na kutokea kwake pamoja na Elia ambae hakufa bila shaka walitokea sehemu nyengine ila sio chini kwenye bottom less pit.Na isitoshe walikuwa na Yesu asiekuwa na dhambi au ushirikina.
Ni ishara kuwa Paradiso ni dhana. Mbingu ni roho na dunia ni maada. Sasa Elia na Yesu sielewi waliendaje huko paradiso na maada iharibikayo na sisi tunasubiri miili yetu ibadilishwe kutoka iharibikayo kwenda isiyoharibika.
 
Mwanambugulu

JF-Expert Member
May 26, 2017
562
1,000
Kwahiyo mkuu kwa lugha nyepesi Mungu alichokifana ktk hii dunia ni sawa na mtu kununua au kudondoa muvi ya vita na kuanza kuitizama na kuifurahiya? Yani aliiumba dunia na kuiweka ktk matatizo ya Vita, njaa, umasikini ili akae chini ashuhudie huku ana popcon pembeni?
Kwaio mungu anakula popcorn taratibu huku sisi tunakomaa kupambana na shetani
 
Mr chaz

Member
Aug 29, 2018
23
45
As Christian nijuavyo dhambi ni uasi uasi ni kwenda kinyume /against God sasa kwanin shetan alitoka wapi ...? One thing Shetan ni jina la laana kabla hapo alkua lusfa... Lusifa then shetan huyu hakwenda against sheria za Mungu bali kutak utawala kabisaa yaani kumpindua Mungu utawala wake apa sasa ndio matokeo ya kulaaniwa lusfa adi shetan lakin haya yote before creating earth and human being so binadam anakuj kuumbwa kwa mfano wa Mungu lakin tiar shetan ameshaadhibiwa ni suala la muda tuu everything is over
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom