Kuna wakati nilisoma coment yako ukaonyesha wasiwasi wa kwamba dunia ingekuwa bila dini ingekuwaje.
Nina kawaida ya kufanya kuwaza na kuwazua sana, hivyo pengine ninapowaza na kuwazua unaweza kuona kama wasiwasi.
Mwalimu Nyerere aliwahi kuulizwa kama dini yake inamsukuma vipi katika maamuzi ya kisiasa, akajibu vizuri sana kwamba ni swali gumu kulijibu kwa sababu hawezi kurudi nyuma akue bila kuwa na dini ili ajione anaweza kuwa mtu gani bila dini.
Je dini imekuwepo siku zote hizo Unahisi ilianza anza vip?
Dini ilianza kwa watu kutaka kujipa majibu ya maswali ambayo hawakuwa na majibu yake. Watu wana kawaida ya kwenda wakiboresha majibu yao kadiri wanavyozidisha uelewa, kwa hiyo zamani watu waliokuwa hawayaelewi mazingira, waliona kuwa kama baba anavyozaaa mtoto na kumlea, au anavyojenga nyumba, basi lazima kuna baba mkubwa huko juu aliyeumba dunia na kuumba watu. Ni mawazo primitive. Ndiyo hizo habari za kusema radi ni sauti ya Mungu kakasirika.
Sasa hawa watu wa zamani hawakujua mengi katika sayansi, hawakujua umeme wa radi unafanya kazi vipi, hawa naweza kuwasamehe kwa sababu hawakuwa na internet.
Sasa kijana wa leo ana internet, tena kwenye simu ya mkononi, habari zote za sayansi anaweza kuzi Google, lakini bado anaamini habari za miujiza ya Mungu tu? Kama fact?
Huyu sina msamaha kwake kabisa.
Dunia nzima kwa sasa ina watu Billion 7.,,Almost Billion 5 wanasali japo sio kwa Mungu mmoja.Hivi idea ya kusali ndani ya binadamu Unaweza kuielezea vip?
Profesa Noah Yuval Harari ameelezea vizuri sana katika vitabu vyake "Sapiens: A Brief History of Humankind" na "Homo Deus: A Brief History Of Tomorrow" kuhusu kitu ambacho watu wana uwezo nacho sana, kinaitwa "manufactured reality".
Watu wana uwezo wa kutengeneza uongo kuwa ukweli, mpaka ule ukweli ukakubalika kabisa. Chukulia fedha za makaratasi. Noti ya US $ 100 ina thamani sana. Lakini thamani yake ni ya kutungwa na watu tu. Ukiwa katika kisiwa ambacho hakina watu, umetupwa huko, unapewa uamuzi uchague papai moja na $100, papai litakuwa na thamani kuliko $100. Maana $100 thamani yake si ya msingi, inategemea na mazingira. Ni ya kupachikwa tu na watu.
Idea ya kusali iliwekwa na watu waliokuwa na maswali ambayo hawana majibu yake, wakajipachikia majibu rahisi waliyoyajua wao.
Kwa nini ndani ya binadamu kuna uhitaji wa sala.??
Kuna watu wanahitaji madawa ya kulevya, wengine wanahitaji kununua nguo kila weekend.
Hilo lina maana gani? Madawa ya kulevya ni Mungu? Nguo ni Mungu?
Mimi sihitaji sala. Ulaya ya Kaskazini watu kibao hawahitaji sala, makanisa yako matupu.
Huoni hio inaonyesha kwamba kuna nafasi ndani ya binadamu inakuwa special kwa kutimiza ibada na mtu anahisi mkamilifu zaidi akisali.??
Sala ni therapy kwa watu masikini. Wenzetu matajiri wanaenda kwa therapists wanafanya therapy ya matatizo yao ya kisaikolojia.
Sala ni therapy kwa masikini wasio na therapists. Una mzigo wa matatizo yako, badala ya kwenda kwa therapist, unaenda kwa mchungaji kanisani au msikitini unafanya sala zako, unatua mzigo wako, unajisikia afueni.
Ni saikolojia tu.
Huoni kwamba Kusema hakuna Mungu ni ajenda ulioibeba ila ikiwa ni makusudio ya viumbe wasioonekana wenye kujua siri nyingi kushinda wewe??
Viumbe gani wasioonekana? Unaweza kuthibitisha wapo na si hadithi zako tu?
Huoni kwamba na wewe umekuwa mhanga wa kuamini kusudio hasi na wewe umelibeba kulieneza japo ulikusudiwa kuliamini tu?
Kama kusema Mungu hayupo na kama yupo athibitishwe ni kuamini, basi kunyoa kipara ni mtindo wa kusuka nywele.