Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Unajua mkuu, binafsi sina shida kabisa na mtu anayemini chochote, either Mungu yupo au hayupo, kwangu mimi wote wako sahihi.

Sababu kubwa ni kwamba, wote, wanaoamini kuwa yupo na wale wasioamini kuwa yupo, hakuna mwenye uthibitisho wa 100%. Zote zinabaki kuwa ni imani.

Lakini shida inakuwa moja, mtu anataka kulazimisha imani ya kuwa yupo au hayupo ili hali hata kuthibitisha uwepo au ukutokuwepo wake hawezi.

Mi binafsi msimamo wangu kuhusu haya mambo ni huu, kwamba japokuwa ni muumini wa dini ya Kikristu, lakini kiuhakika siwezi kuthibitisha kuwa Mungu yupo au la!

Cha msingi ni kuwa, kila mtu asimame katika imani yake, na yupo sahihi katika hiyo imani yake. Ila asianze kudharau imani ya mtu!!
KAMA UNAFIKIRI KUHUSU UTHIBITISHO KIASI HICHO ULIKUWA NA HAJA GANI YA KUAMINI MUNGU?MAANA INAONESHA HADI SASA HAUJAONA HATA DALILI YEYOTE AU ATHARI YA KUAMINI MUNGU,SASA KWANINI UNAENDELEA KUAMINI?
 
KAMA UNAFIKIRI KUHUSU UTHIBITISHO KIASI HICHO ULIKUWA NA HAJA GANI YA KUAMINI MUNGU?MAANA INAONESHA HADI SASA HAUJAONA HATA DALILI YEYOTE AU ATHARI YA KUAMINI MUNGU,SASA KWANINI UNAENDELEA KUAMINI?
Mkuu, hata nisipoamini kuwa kuna Mungu ni sawa tu na kuamini kuna Mungu, hakuna tofauti yoyote ya kifizikia.

Mi nimemua kuwa mfuasi wa dini ya kikristu, kwa sababu kadhaa, lakini kubwa ni maamuzi tu binafsi!!

Lakini kwa maoni yangu, kuwa mfuasi wa dini au dhehebu flani angalau kunaleta ahueni na faraja kwamba shida tupitiazo yupo ambaye atatutatulia kwa imani.

Pia, kujumuika na watu kwa lengo flani, kunawafanya muwe na mahusiano ambayo yanaweza yakaleta matokeo chanya baina yenu, kama vile upendo, faraja, ushirikiano, n.k

Sababu hizo haziifanyi imani niliyonayo iwe ndio sahihi kuliko imani za wengine.

Na wala kiwa katika imani hii, hakuniwezeshi kuwaaminisha watu wasio wa imani yangu waamini, kumuona na kujua kuwa kweli Mungu yupo. Uwepo wa Mungu mimi siujui ukweli wake aisee!!

Bwana Tz mbongo, Je, imani yako ndio sahihi kuliko za wengine!?
 
Mkuu, hata nisipoamini kuwa kuna Mungu ni sawa tu na kuamini kuna Mungu, hakuna tofauti yoyote ya kifizikia.

Mi nimemua kuwa mfuasi wa dini ya kikristu, kwa sababu kadhaa, lakini kubwa ni maamuzi tu binafsi!!

Lakini kwa maoni yangu, kuwa mfuasi wa dini au dhehebu flani angalau kunaleta ahueni na faraja kwamba shida tupitiazo yupo ambaye atatutatulia kwa imani.

Pia, kujumuika na watu kwa lengo flani, kunawafanya muwe na mahusiano ambayo yanaweza yakaleta matokeo chanya baina yenu, kama vile upendo, faraja, ushirikiano, n.k

Sababu hizo haziifanyi imani niliyonayo iwe ndio sahihi kuliko imani za wengine.

Na wala kiwa katika imani hii, hakuniwezeshi kuwaaminisha watu wasio wa imani yangu waamini, kumuona na kujua kuwa kweli Mungu yupo. Uwepo wa Mungu mimi siujui ukweli wake aisee!!

Bwana Tz mbongo, Je, imani yako ndio sahihi kuliko za wengine!?
Basi wewe hauamini Mungu au hauna hakika na unachoamini na ndio maana unaamini Mungu bila dalili yeyote.
 
Kwa hiyo tunaweza kusema uwepo wa dhambi hautegemei uwepo wa shetani?

yaani shetani anajitegemea na dhambi inajitegemea?
Hata huyo shetani alifanya dhambi na ndio sababu ya hadi kuitwa shetani ila hakuumbwa akiwa ni shetani.
 
Hebu thibitisha kwamba Baba ni mwanaume?
Au mwenzangu baba yako ni mwanamke!?

Niambie, nifanye nini ili nikuthibitishie kuwa Baba yako ni Mwanaume!?

Maana mimi nimetaka unithibitishie kuwa Mungu yupo kwa kumuonyesha na kuonyesha nguvu zake!!!
 
Sasa kwanini katipa Challenge ilihali sisi ni kazi ya mikono yake!?


sisi ni kazi ya mikono yake lakini kati yetu kuna aliye bora zaidi ya mwingine, na huyo bora ni anayemwabudu, wewe unafikiri kwanini kuna pepo na jehanam, bila kipimo nani angekuwa wa peponi na nani angekuwa wa jehanamu?
 
Kwa aliyesema nidhibitishe kwamba malaika wabaya waliasi kabla ya binadamu kuumbwa, jibu ni kwamba Adam na Hawa walijaribiwa na shetani. That proves that the devil preceded them in history. I assume that you believe in revealed truth, otherwise there is no basis for our discussion here.

Ifahamike pia kuna nadharia sadifu kwamba kuasi kwa shetani kulikuwa kukataa kuabudu alipoonyeshwa umwilisho (ahead of time, as God exists outside time).
 
Nimekumbuka yule dogo aliyewashitaki wazazi wake kwa kumzaa mzungu badala ya mweusi


Hivi siku ya kiama haiwezekan kukata rufaa ukihukumiwa kwenda jehanam!?

Kwanza wewe hukuomba uumbwe ila yeye ndio alikuumba kwa malengo yake sasa kosa lako ni nini hadi upelekwe jehanam?
Ndio ushangae sasa " ... vitu vingine ni nonsense tu ... ujinga mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu hamjambo!

Kama kichwa cha Uzi huu kinavyouliza, Mimi nikiri kuwa naamini uwepo wa Mungu mmoja aliyeumba vyote vinavyoonekana na visivyoonekana pia.

Katika vitabu mbali mbali vya dini, tunaelezwa kuwa dhambi ilitokana na uasi alioufanya shetani dhidi ya Mungu, biblia inaenda mbali kwa kudai kuwa vita vilipiganwa huko mbinguni na shetani alishindwa na akatupwa duniani akiwa na theluthi ya malaika wakawa upande wake.

Maswali:

1. Ikiwa kabla ya shetani kuasi hakukuwa na dhambi yoyote ile, tena alikuwa mbinguni kwenye utakatifu wa MUNGU, je shetani alishawishiwa au alitoa wapi mawazo ya uasi Ikiwa hakukuwa na shetani yeyote mwingine?

2. Kama MUNGU hujua mwanzo hata mwisho wa viumbe vyake, INA maana alikuwa anajua kuwa shetani atakuja kuasi baadae na kusababisha dhambi, kwanini alimuumba?
Jambo la kufikiria hapa ni kuona kwamba MUNGU alimuumba shetani/Lucifer ( dhambi) mahususi ili kuja kuwa upande maovu. Dhana hii inadhihirisha kuwa MUNGU ndie aliyeumba dhambi.

3. Je, lengo la MUNGU lilikuwa mwanadamu aishi milele bila kufa?
Hapa kuna mazoea yalishajengeka hasa kwa wakristo na waislamu kuamini kuwa isingekuwa Eva/Hawa kudanganywa na Shetani basi Leo hii wanadamu wasingekuwa wanakufa ( immortal). Hii dhana haina mantiki hasa ukiwaza kuwa wanadamu wangezaliana na kuishi milele bila kufa nadhani dunia ingekuwa imejaa mabara na visiwa vyote.
Hivyo MUNGU akaamua kuleta mauti ili kudhibiti ( control) idadi ya wanadamu duniani isizidi uwezo wa rasilimali zilizopo, fikiri Leo hii watu wanauwana kugombania ardhi je ingekuwaje akina Adam na bibi yetu Eva wangekuwepo wote?

4. Je, Dini ni matokeo ya mwanadamu kumhofia shetani?
Tunaishi katika jamii ambazo kila MTU ana juhudi za kujikwamua kuondokana na shida Kama magonjwa, njaa, vita, ambazo Mara nyingi wanadamu wanahesabu kuwa hayo yote ni sababu ya shetani, na dini wanaona ndio kimbilio ili kumkwepa shetani asiwadhuru.
Lakini wao wanaamini kuwa wanasali ili kumtukuza MUNGU, lakini kiukweli dini ni hofu ( fear of unknown) isiyo na ithibati yoyote.

5. Je, Mungu anawapenda wanadamu? Hapa jibu laweza kuwa ni ndiyo, bahati mbaya sana ukiangalia uhalisia toka zamani kuna ugumu wa kusema ndiyo au hapana.
Tunaambiwa kuwa mbinguni kulikuwa na vita Kali sana, mwaishowe malaika aitwaye Mikaeli alimshinda shetani, Mungu akamtupa ibilisi huyo huyo duniani kwa wanadamu anaowapenda sana. Mungu hakuona sehemu nyingine ya kulitupa hilo joka ila duniani ambako ndio wanadamu aliwaweka. Hii ni sawa na kuwarushia watoto wako furushi lenye nge wengi huku umewafungia chumbani na kuwataka wajikinge wasing'atwe hata kidogo.

Nimekuja kuamini kuwa: MUNGU yupo ila dini zote ni michezo ya kukamata fikra za wanadamu tu, inawezekana kabisa kuwa dini ziluletwa na shetani mwenyewe ili kuwachonganisha wanadamu wasiishi kwa upendo na amani.
Angalia jinsi Palestine na Israel, syria , Iraq n.k wanavyouana kwa misingi ya dini.

Niishie hapo, naomba waumini/maswahaba mje mtueleze hizi hoja.

Cc: Mshana Jr
Cc: Kiranga
Na wanajamvi wote karibuni.
DHAMBI NI NINI?
Dhambi ni tendo, hisia, au wazo lolote linalopingana na viwango vya Mungu. Inatia ndani kuvunja sheria za Mungu kwa kutenda mabaya, au ukosefu wa uadilifu, kwa maoni ya Mungu. (1 Yohana 3:4; 5:17) Biblia pia inaeleza kuhusu dhambi ya kutofanya lililo sawa ingawa mtu anajua alipaswa kulifanya.—Yakobo 4:17.

Katika lugha za awali za Biblia, neno dhambi linamaanisha, “kukosa shabaha.” Kwa mfano, askari fulani katika Israeli la kale walikuwa na ustadi wa kutupa mawe kwa kombeo “bila kukosea.” Maneno hayo yanapotafsiriwa kihalisi yanamaanisha “bila kufanya dhambi.” (Waamuzi 20:16) Hivyo, kufanya dhambi ni kukosa shabaha ya viwango vikamilifu vya Mungu.

Kwa kuwa Mungu ndiye Muumba, ana haki ya kuwawekea wanadamu viwango. (Ufunuo 4:11) Tunawajibika kwake kwa matendo yetu.—Waroma 14:12.

CHANZO CHA DHAMBI / UOVU

Ingawa Yesu alikubali kwamba wanadamu wana uwezo wa kutenda maovu, alionyesha ni nani hasa aliye chanzo cha uovu, yaani, Shetani Ibilisi.

Kwa kusema kwamba Shetani “hakusimama imara katika kweli,” Yesu alifunua kwamba wakati mmoja kiumbe huyo wa roho alikuwa mtumishi mwaminifu wa Mungu lakini akapotoka kutoka katika njia hiyo iliyo sawa. Kwa nini Shetani alimwasi Mungu? Ni kwa sababu alijiona kuwa mtu wa maana sana hivi kwamba akatamani ibada ambayo Mungu tu ndiye anayestahili kupewa.*—Mathayo 4:8, 9.

Uasi wa Shetani ulifunuliwa katika bustani ya Edeni alipomdanganya Hawa ale tunda walilokatazwa. Kwa kusema uwongo wa kwanza kabisa na kwa kumchongea Yehova, Shetani alijifanya mwenyewe kuwa “baba ya uwongo.” Zaidi ya hilo, kwa kuwashawishi Adamu na Hawa wasitii, alifanya dhambi iwatawale, na hivyo kuwaongoza wao pamoja na wazao wao kwenye kifo. Kwa sababu hiyo, Shetani pia alijifanya mwenyewe kuwa “muuaji,” naye kwa kweli ndiye muuaji mkatili zaidi katika historia yote!—Mwanzo 3:1-6; Waroma 5:12.

Uvutano mwovu wa Shetani ulifika hata katika makao ya roho ambako aliwashawishi malaika wengine wajiunge naye katika uasi wake. (2 Petro 2:4) Kama Shetani, roho hao waovu walipendezwa na wanadamu kwa njia isiyofaa. Walivutiwa hasa na mahusiano mapotovu ya ngono, na hilo likawa na matokeo mabaya sana na yaliyo maovu.
 
Je, uumbaji wa Mungu ulikuwa na kasoro?
Kazi zote za Mungu ni kamilifu. Wanadamu na malaika waliumbwa na Mungu wakiwa na uwezo kamili wa kutii matakwa yake. (Kumbukumbu la Torati 32:4, 5) Mungu alituumba tukiwa na uhuru wa kuchagua kufanya mema au mabaya. Uhuru huo unatupa nafasi ya kuonyesha upendo wetu kwa Mungu.—Soma Yakobo 1:13-15; 1 Yohana 5:3.
 
3. Je, lengo la MUNGU lilikuwa mwanadamu aishi milele bila kufa?
Hapa kuna mazoea yalishajengeka hasa kwa wakristo na waislamu kuamini kuwa isingekuwa Eva/Hawa kudanganywa na Shetani basi Leo hii wanadamu wasingekuwa wanakufa ( immortal). Hii dhana haina mantiki hasa ukiwaza kuwa wanadamu wangezaliana na kuishi milele bila kufa nadhani dunia ingekuwa imejaa mabara na visiwa vyote.
Hivyo MUNGU akaamua kuleta mauti ili kudhibiti ( control) idadi ya wanadamu duniani isizidi uwezo wa rasilimali zilizopo, fikiri Leo hii watu wanauwana kugombania ardhi je ingekuwaje akina Adam na bibi yetu Eva wangekuwepo wote?

Adamu na Hawa walikataa kumtii Mungu kwa kula tunda walilokatazwa. (Mwanzo 2:17; 3:6) Kwa kuwa walitenda dhambi dhidi ya Mungu, hatimaye walikufa, kama tu Mungu alivyokuwa amesema. (Mwanzo 3:17-19)
Chanzo cha Kifo ni kutotii sheria /amri
Mungu anamamlaka ya kufanya apendacho kwa alichokiumba.

Kwanini amri ya kutokula tunda?
Nadhani kwa mamlaka yake aliweka mipaka midogo ambayo haikuwa migumu kwa binadam.

Kama unamiti 100 au zaidi ya matunda
Kwa nini utake 1 uliokatazwa

Nadhani pia, kwa sababu ya sifa ya binadam ya kupenda kuwa juu au mamlaka, uongo wa kuwa kama Mungu pindi watakapokula tunda uliwaingia barabara.

Mauti ilikuja kwa kutotii hata kabla ya ongezeko la watu.
Kama alihofia kuwa watu wangekuwa wengi kuzidi, na kwa kuwa Mungu=Upendo, kuua alichokipenda na kuumba sidhani kama ni suluhisho

Kwa kuwa anauwezo wa kuumba, kwa nini asingewaumba na uwezo wenye mipaka flani kimwili, yaan binadam awe na uwezo wa kuzaa mtoto mmoja au wawili na wengine wasizae kabisa, badala ya kufikiria kuwaua.
 
Back
Top Bottom