Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Mungu ni kila kitu ni mwanzo wa yote na mwisho wa yote. Kwa hata yale binadamu kwa utashi wake anayoyaona kuwa ni dhambi yameumbwa na mungu.
"Mungu ni mwanzo wa yote!”

Kwahiyo mkuu, unamaanisha pia Mungu ni mwanzo wa dhambi, shetani na maovu yote!?
 
Mkuu mimi nafikiri tungejikita kwenye sababu,,mfano kwa nini Mungu ajue kwamba huyu kiumbe Lucifer anaemuumba atakuja kuharibu kazi yake?? Ezekiel 28: ina majibu,,, kwamba Lucifer Alikuwa kaumbwa vizuri ila Alikuwa na tamaa,,,yako majibu kabisa kama ukiwa uko huru bila presha kutafuta majibu ya maswali yako.

Nimependa hapa uliposema anawajua walio wake toka kuwekwa misingi ya ulimwengu,,,mimi nikuulize kwamba wasi wasi wako ni nini kama labda hao walio wake mmoja wapo ni wewe?? Maana hakuwataja.
Ndio Unaweza ukawa na dhambi kama mimi na Baadae kumebaki dakika moja ufe ukatubu,,,nani anajua!
Ukisema Mungu maana yake anauwezo mkubwa sasa kwanini hakujua kuwa Lucifa atakuwa natamaa? Na kwanini asingeondoa hiyo tamaa kwa Lucifa ili aendelee kuwa kiumbe bora.
 
CREATION IS GAME WHERE BY GOD PLAY BY HIMSELF. Vitu vyote na matendo yote yameumbwa na Mungu. Tendo ni tendo tuu linaweza kuwa zuri au baya inategemea how the subject or object fills. Kuua (kutoa uhai) ni dhambi lakini imagine kama kusinge kuua. Sheria za maumbile zimewekwa na muumba lakini amefungwa nazo lazima azifuate kwani yeye ndie anayetenda na wakati huohuo ndio anayetendewa.
Wakuu hamjambo!

Kama kichwa cha Uzi huu kinavyouliza, Mimi nikiri kuwa naamini uwepo wa Mungu mmoja aliyeumba vyote vinavyoonekana na visivyoonekana pia.

Katika vitabu mbali mbali vya dini, tunaelezwa kuwa dhambi ilitokana na uasi alioufanya shetani dhidi ya Mungu, biblia inaenda mbali kwa kudai kuwa vita vilipiganwa huko mbinguni na shetani alishindwa na akatupwa duniani akiwa na theluthi ya malaika wakawa upande wake.

Maswali:

1. Ikiwa kabla ya shetani kuasi hakukuwa na dhambi yoyote ile, tena alikuwa mbinguni kwenye utakatifu wa MUNGU, je shetani alishawishiwa au alitoa wapi mawazo ya uasi Ikiwa hakukuwa na shetani yeyote mwingine?

2. Kama MUNGU hujua mwanzo hata mwisho wa viumbe vyake, INA maana alikuwa anajua kuwa shetani atakuja kuasi baadae na kusababisha dhambi, kwanini alimuumba?
Jambo la kufikiria hapa ni kuona kwamba MUNGU alimuumba shetani/Lucifer ( dhambi) mahususi ili kuja kuwa upande maovu. Dhana hii inadhihirisha kuwa MUNGU ndie aliyeumba dhambi.

3. Je, lengo la MUNGU lilikuwa mwanadamu aishi milele bila kufa?
Hapa kuna mazoea yalishajengeka hasa kwa wakristo na waislamu kuamini kuwa isingekuwa Eva/Hawa kudanganywa na Shetani basi Leo hii wanadamu wasingekuwa wanakufa ( immortal). Hii dhana haina mantiki hasa ukiwaza kuwa wanadamu wangezaliana na kuishi milele bila kufa nadhani dunia ingekuwa imejaa mabara na visiwa vyote.
Hivyo MUNGU akaamua kuleta mauti ili kudhibiti ( control) idadi ya wanadamu duniani isizidi uwezo wa rasilimali zilizopo, fikiri Leo hii watu wanauwana kugombania ardhi je ingekuwaje akina Adam na bibi yetu Eva wangekuwepo wote?

4. Je, Dini ni matokeo ya mwanadamu kumhofia shetani?
Tunaishi katika jamii ambazo kila MTU ana juhudi za kujikwamua kuondokana na shida Kama magonjwa, njaa, vita, ambazo Mara nyingi wanadamu wanahesabu kuwa hayo yote ni sababu ya shetani, na dini wanaona ndio kimbilio ili kumkwepa shetani asiwadhuru.
Lakini wao wanaamini kuwa wanasali ili kumtukuza MUNGU, lakini kiukweli dini ni hofu ( fear of unknown) isiyo na ithibati yoyote.

5. Je, Mungu anawapenda wanadamu? Hapa jibu laweza kuwa ni ndiyo, bahati mbaya sana ukiangalia uhalisia toka zamani kuna ugumu wa kusema ndiyo au hapana.
Tunaambiwa kuwa mbinguni kulikuwa na vita Kali sana, mwaishowe malaika aitwaye Mikaeli alimshinda shetani, Mungu akamtupa ibilisi huyo huyo duniani kwa wanadamu anaowapenda sana. Mungu hakuona sehemu nyingine ya kulitupa hilo joka ila duniani ambako ndio wanadamu aliwaweka. Hii ni sawa na kuwarushia watoto wako furushi lenye nge wengi huku umewafungia chumbani na kuwataka wajikinge wasing'atwe hata kidogo.

Nimekuja kuamini kuwa: MUNGU yupo ila dini zote ni michezo ya kukamata fikra za wanadamu tu, inawezekana kabisa kuwa dini ziluletwa na shetani mwenyewe ili kuwachonganisha wanadamu wasiishi kwa upendo na amani.
Angalia jinsi Palestine na Israel, syria , Iraq n.k wanavyouana kwa misingi ya dini.

Niishie hapo, naomba waumini/maswahaba mje mtueleze hizi hoja.

Cc: Mshana Jr
Cc: Kiranga
Na wanajamvi wote karibuni.
 
Endelea kujiuliza majibu yapo tena ndani yako wala sio maandishi. Jiulize nani alikufundisha kutambua Rangi.
Kuna Vitu Vingi Huwa Najiuliza Kama Hivi Nakosa Majibu Sahihi.
Ila Maandiko Yanasema Hekima Ya Mwanadamu Ni Upuuzi.
 
Now you agree that God created everything be it Good or bad ones, and even sin is there coz God is there too! are you in that logic?
CREATION IS GAME WHERE BY GOD PLAY BY HIMSELF. Vitu vyote na matendo yote yameumbwa na Mungu. Tendo ni tendo tuu linaweza kuwa zuri au baya inategemea how the subject or object fills. Kuua (kutoa uhai) ni dhambi lakini imagine kama kusinge kuua. Sheria za maumbile zimewekwa na muumba lakini amefungwa nazo lazima azifuate kwani yeye ndie anayetenda na wakati huohuo ndio anayetendewa.
 
Endelea kujiuliza majibu yapo tena ndani yako wala sio maandishi. Jiulize nani alikufundisha kutambua Rangi.
Unajua mkuu, binafsi sina shida kabisa na mtu anayemini chochote, either Mungu yupo au hayupo, kwangu mimi wote wako sahihi.

Sababu kubwa ni kwamba, wote, wanaoamini kuwa yupo na wale wasioamini kuwa yupo, hakuna mwenye uthibitisho wa 100%. Zote zinabaki kuwa ni imani.

Lakini shida inakuwa moja, mtu anataka kulazimisha imani ya kuwa yupo au hayupo ili hali hata kuthibitisha uwepo au ukutokuwepo wake hawezi.

Mi binafsi msimamo wangu kuhusu haya mambo ni huu, kwamba japokuwa ni muumini wa dini ya Kikristu, lakini kiuhakika siwezi kuthibitisha kuwa Mungu yupo au la!

Cha msingi ni kuwa, kila mtu asimame katika imani yake, na yupo sahihi katika hiyo imani yake. Ila asianze kudharau imani ya mtu!!
 
Kilichobaki tunatakiwa kuishi kwa imani tu..Kwa hakika mimi naweza Kusema Mungu ana upendo sana na anatupenda sana.

Na hata mtu ukafa ukaenda motoni au paradise hakika unastahili sana unapoenda.Maana unastahili kulingana na ulichokuwa unafanya hapa duniani.
Nimecheka sana hii comment, so hata tukienda Motoni tufurahi tu kwa sababu Mungu ni pendo?Hakuna anayependa moto na hakuna ajuaye makosa mangapi yanastaili mtu kwenda Motoni ila tunaishi kwa kuomba utakaso kila inapoitwa leo
 
Kama kweli Mungu alimaliza kuumba, kila alichoumba aliona ni chema kabisa. Hakukuwa na uasi juu ya uso wa dunia, Lucifer alikuwa msafi, asiye na dhambi.

~Nani alimuingia Lucifer aliyekuwa anaishi patakatifu ili aasi?

~Kama kweli Mungu ni alpha na omega, maana yake alijua kuwa dhambi itaingia ulimwenguni, kwa nini aliruhusu hiyo dhambi iingie?

~Kwa wakristo, kabla ya Yesu kuja kutufia, walikuwa wakiteteteza sadaka(kondoo) ili kusamehewa dhambi zao, kwa nini kondoo aliye mnyama wa kawaida auwawe kila siku ili tu mimi nisamehewe?

~Mungu mwenye rehema, upendo kwa nini aruhusu mwanadamu aishi maisha ya dhiki kiasi hiki? Maradhi, kifo, vita nk.

Why?
Why?
Why?
Kweli hizo hadithi zinachanganya, lakini huoni anatafuta majibu kwa njia isiyo sahihi. Umemfananisha mungu na binadamu, umemuweka mahali pataitwa mbinguni na pia umemuwekea muda na imekuwa historia. Mwili na akili haziwezi kumjua mungu kama ilivyo vigumu kumuelezea tuu. Mwili na akili na matokea ya chakula, hewa na maji ulioanzishwa na umbaji uliofanywa wazazi, ukaatamiwa tumboni kwa mama kwa miezi ya mimba, then kupitia kula, kunywa, na kupumua chakula kilimwacho ardhini mwili na akiri vinakuwa na kuzeeka na baadae kufa. Mwili na akili haviwezi fanya hizo process zote bila UHAI. Uhai ndio kitu constant hakibadiliki toka kinaungana mwili wako mpaka kinaachana na mwili. Ni njia isiyo sahihi kama tukitafuta majibu ya mungu kwa kutumia miili na akili zetu badala kujua sisi ni uhai ( Roho) ndio ilioumbwa na mungu. Mwili unatenda kwa kushawushiwa na akili wakati Roho inapata impression its injoy joy and pain. Roho hata bila mwili haifi, haichomeki, iko huru. Swali kwa nini ije iteseke kwenye mwili? Hili ndio fumbo kuu.
 
Hilo swali la kwanza liko tough,,ila kwa Kusema kawaida bila reference nawaza kwamba Mungu alikuwa akitafuta mshindani mwenye nguvu ila ambae kamuumba mwenyewe na ambae hawezi kumshinda.Maana kamchukulia Mungu malaika wake kwa kuwadanganya na pia hawa malaika wamekuwa chini yake akaweza kuanzisha ufalme.

Kuhusu Mungu kuwajua walio wake,,kila mmoja ana probability ya kuingia mbinguni.Ndio maana Suleiman Anasema kwenye mhubiri kwamba usiwe na haki sana wala usiwe na dhambi sana.Fanya mambo sahihi ya kukupa furaha ila usivuke mipaka.

Kuna mtu anafundisha dini namkubali sana,,,kuna siku alikuwa akifundisha kuhusu selection inayofanyika hapa duniani kwamba Mungu anatafuta watu wakaikae ile sehemu walioondoka malaika walioumeza uongo wa Luci.idadi ni hesabu ya 1/3 ya malaika wote waliokuwa mwanzo.Kwa hio hapa duniani tuko wengi ila mchujo unafanyika.kikubwa Jitahidi ufurahi Maana hujui kwamba wewe ni x,y au z
Leobs naomba uniangalizie huo mstari ktk Mhubiri unipe nami nisome, usiwe wa haki na usitende dhambi nyingi
 
Mimi pia nina swali hapo,

Je, kabla Mungu hajaumba kitu chochote, alikuwa anakaa wapi!?

Makazi yake yalikuwa wapi!?

Tunaomba mtuelimishe wale waaminio!!
MUNGU anaketi mahali pa sirini, mathayo 6:6
 
It depends, Good or bad ones are different qualitie of one did, depend on how you translate it in wha level of existance of being. Qualities are transalation of our minds while God exit beyond that.
Now you agree that God created everything be it Good or bad ones, and even sin is there coz God is there too! are you in that logic?
 
Kama kweli Mungu alimaliza kuumba, kila alichoumba aliona ni chema kabisa. Hakukuwa na uasi juu ya uso wa dunia, Lucifer alikuwa msafi, asiye na dhambi.

~Nani alimuingia Lucifer aliyekuwa anaishi patakatifu ili aasi?

~Kama kweli Mungu ni alpha na omega, maana yake alijua kuwa dhambi itaingia ulimwenguni, kwa nini aliruhusu hiyo dhambi iingie?

~Kwa wakristo, kabla ya Yesu kuja kutufia, walikuwa wakiteteteza sadaka(kondoo) ili kusamehewa dhambi zao, kwa nini kondoo aliye mnyama wa kawaida auwawe kila siku ili tu mimi nisamehewe?

~Mungu mwenye rehema, upendo kwa nini aruhusu mwanadamu aishi maisha ya dhiki kiasi hiki? Maradhi, kifo, vita nk.

Why?
Why?
Why?
ukisoma sala ya baba kuna mstari unasema " mapenzi yako yatimizwe duniani hata mbinguni" kama sijakosea.
Hvyo basi kwa mapenzi yake yeye aliye mtukufu ndo yote hayo uliyouliza mzizi wake mungu.
 
Kwa mujibu wa Iman ya dini yangu, dhumuni kuu la Mwenyezi Mungu kutuleta duniani ni ili tumwabudu, sasa kama dhambi zisingekuwepo ni nini kingekuwa kipimo cha anaemuabudu na asiye muabudu, hivyo basi Mungu anao uwezo wa kuitokomeza dhambi lakini kwa makusudi aliamua kuiacha kwa makusudi kwa maana ya kama challenges kwetu ili kufikia kwenye kumuabudu kwa ukweli!!!!
 
It depends, Good or bad ones are different qualitie of one did, depend on how you translate it in wha level of existance of being. Qualities are transalation of our minds while God exit beyond that.
Fine! you've absolutely admitted that some of attributes of faith especially bad/sins or goods are measured by the standards of human( subjective intuitions) but not by the reference of God?

Namaanisha kwamba, umesema baya/dhambi au zuri hupimwa kulingana na mhusika anavyolitafsri jambo kwa utashi wake binafsi na SIO kwa sheria au kanuni za Mungu?

kama ni hivyo ni ipi nafasi ya shetani kusababisha dhambi na ni ipi nafasi ya Mungu katika kudhibiti dhambi ikiwa mwanadamu yuko huru namna hiyo kuamua lipi jema na lipi baya?

jibu mkuu!
 
Kwa mujibu wa Iman ya dini yangu, dhumuni kuu la Mwenyezi Mungu kutuleta duniani ni ili tumwabudu, sasa kama dhambi zisingekuwepo ni nini kingekuwa kipimo cha anaemuabudu na asiye muabudu, hivyo basi Mungu anao uwezo wa kuitokomeza dhambi lakini kwa makusudi aliamua kuiacha kwa makusudi kwa maana ya kama challenges kwetu ili kufikia kwenye kumuabudu kwa ukweli!!!!
Ufikiria kwa niaba ya mungu au ndio ufahamu wako.
 
Kwa mujibu wa Iman ya dini yangu, dhumuni kuu la Mwenyezi Mungu kutuleta duniani ni ili tumwabudu, sasa kama dhambi zisingekuwepo ni nini kingekuwa kipimo cha anaemuabudu na asiye muabudu, hivyo basi Mungu anao uwezo wa kuitokomeza dhambi lakini kwa makusudi aliamua kuiacha kwa makusudi kwa maana ya kama challenges kwetu ili kufikia kwenye kumuabudu kwa ukweli!!!!
In short umesema kwamba Mungu ndiye kaiumba dhambi na ndiye anayetoa ruhusa ya dhambi iwepo! si ndiyo?
 
"DHAMBI" Ni kukiuka maagizo ya mwenyezi mungu,kwenda kinyume na sheria za mwenyezi mungu,kufanya mambo ambayo Ni chukizo mbele za mungu.hapo mwanzo hakukuwako na dhambi, Before human creation dunia ilikua inakaliwa na viumbe wanaitwa majini,majini wameumbwa na mwenyezi mungu na wapo wema na wabaya,majini Ni viumbe visivyoonekana Kwa macho Ila kutokana na maandiko matakatifu Ni kwamba wameumbwa Kwa moto,Kubwa lao ndilo Hili tunalisikia linaitwa "lucipher",yeye alipewa uwezo mkubwa Sana na mwenyezi mungu juu ya viumbe vyote vilivyokuwa duniani na mbinguni ambavyo mungu aliviumba, Kwahyo majini waliishi muda mrefu Sana Hapa duniani kabla ya Adam "binadamu wa kwanza"
MWANZO WA DHAMBI
viumbe hao wa Kwanza kuishi duniani walianza kufanya dhambi ya "kulawitiana" na walizidi Sana kufanya dhambi ndipo mwenyezi mungu akawaangamiza kabisa katika uso wa dunia lakini "lucipher" hakuangamizwa Kwa sababu hakushiriki katika dhambi ya kulawiti/kulawitiana.
Ndipo mwenyezi mungu akaamua kuumba kiumbe chenye ujuzi na akili kuliko viumbe vya mwanzo "majini "akamuumba Adam ili aje atawale dunia na vilivyomo lakini suala hili lilipingwa na Jini lucipher ndipo ilipozaliwa dhambi Kwa Mara ya Kwanza Kwa maana alipinga matakwa ya mwenyezi mungu ambaye anapoamua jambo hashauriani na yeyote.
Kwahyo mwenyezi mungu akamuumba Adam na akampa akili na uwezo wa kutawala vitu vilivyomo duniani,na akamweka edeni.
Lucipher Yule jini mkuu akalaaniwa na kutupwa duniani lakini Bado alikua na uwezo Ule ambao aliumbwa nao,
Baadaye mungu akaona si vyema Adam awe binadamu peke yake duniani akamfanyia "msaidizi" ili atawale pamoja Naye lakini akawapa masharti akawaamuru wale matunda yote katika Ile bustani ambayo aliwaweka isipokuwa tunda LA mti wa katikati mti wa ujuzi wa mema na mabaya (pale bustanini palikuwa na mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya)
Ndipo Yule jini aliyetupwa duniani akawaonea wivu Adam na Eva akaandaa mpango wa kuwashawishi watende dhambi ili asiwe peke yake katika laana ya mwenyezi mungu.
Yule jini ndiye Yule nyoka tunaemsoma katika HOLLY BIBLE wapendwa, akamtokea Hawa Wakati Adam akiwa usingizini akamshawishi kufanya dhambi ya kulawitiwa naye, kisha Adam kumlawiti mkewe Hawa, Hapa ndipo binadamu wa Kwanza alipofanya dhambi Kwa muumba wake. Kwa hivyo kuna mambo watu wanaumiza Sana vichwa kuyajua
1.bustani Ni mwili wa mwanamke
2.mti wa ujuzi wa mema na mabaya Ni tendo la kulawiti/kulawitiana/kulawitiwa
3.mti wa uzima Ni Ile njia ya tendo LA ndoa ambayo Ni imehalalishwa na mwenyezi mungu pale tu unapofanya ki utaratibu ambao mungu anaukubali
4.nyoka Ni Yule jini luciopher
Nikipata muda nitaeleza haya mambo vizuri ili tuyaelewe kutokea katika maandiko pia tukumbuke kwamba maneno ya mungu mtu yeyote anaweza kuyasoma lakini sio kuyaelewa
.....ngoja nifuatilie mkeka wangu....
Achimwene hayo yote umeyatoa wp? Kulawiti kulianza pale sodoma ila walikatazwa wasile tunda la katikati
 
Hakuna shetani hapa, upo wewe na Mungu. Mwili, Akili na Roho. Mwili unatenda kwa kushawishiwa na akili. Roho huvuna dhahibu ya matendo. Kama kuna shetani katika tendo lolote basi ilaumiwe akili.
Fine! you've absolutely admitted that some of attributes of faith especially bad/sins or goods are measured by the standards of human( subjective intuitions) but not by the reference of God?

Namaanisha kwamba, umesema baya/dhambi au zuri hupimwa kulingana na mhusika anavyolitafsri jambo kwa utashi wake binafsi na SIO kwa sheria au kanuni za Mungu?

kama ni hivyo ni ipi nafasi ya shetani kusababisha dhambi na ni ipi nafasi ya Mungu katika kudhibiti dhambi ikiwa mwanadamu yuko huru namna hiyo kuamua lipi jema na lipi baya?

jibu mkuu!
 
Kwa hiyo dhambi haitokani na shetani? kwa hivyo mtu aweza kutenda DHAMBI bila ya shetani kuhusika?
Hakuna shetani hapa, upo wewe na Mungu. Mwili, Akili na Roho. Mwili unatenda kwa kushawishiwa na akili. Roho huvuna dhahibu ya matendo. Kama kuna shetani katika tendo lolote basi ilaumiwe akili.
 
Back
Top Bottom