Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Kuna MTU mmoja alishawahi kusema hivi. Kwa Uwezo alionao binadamu, Kuhoji kuhusu Mungu Ni sawa na kuchimba kashimo kwa Mkono pembezoni mwa bahari na kutaka kuhamishia bahari yote katika kale kashimo.

Ova and Out.
Watu wanashindwa kuelewa tu kwamba kuna elimu/ujuzi na kuna akili,tunapokwenda shule sio kwamba hatuna akili au hatuzitumii akili zetu. Ila ajabu mtu anataka apate kujua kuhusu Mungu kwa kutumia akili tu ila ajabu mtu huyohuyo hakukaa tu nyumbani na akili yake kwa kutegemea kupata kujua yale yenye kufundishwa shule kwa akili tu.
 
Ndani ya bustani ya eden Mungu aliweka mti wa mema na mti wa mabaya. sasa mti wa mabaya wa nini wakati dhambi ilikuwa bado? Inaonekana Mungu aliiumba dhambi before
 
Mungu "aliumba" vitu, na dhambi sio "kitu". Sheria pia sio kitu. Mungu alitupatia sheria, hakuumba sheria. Tutumie neno "kuumba" kwa usahihi.

Maoni hasi dhidi ya dini yanatokana zaidi na kutokuwa na msingi mzuri wa kuanzia kwenye kumwelewa Mungu. God is infinite while we are finite. We cannot fully fathom Him, not even when we enter His Kingdom. Ni kama mende kujaribu kumwelewa binadamu. Hana huo uwezo.

Mungu ni UPENDO. That's biblical. Hampangii mtu ubaya. But as He exists outside of the limitation of time, He knows all the good and bad choices that we will make in our lives.

Si mpango wa Mungu tutende dhambi. Ni uamuzi wetu, na Mungu anafahamu, tangu mwanzo wa nyakati, kwamba tutaamua kufanya nini. Ametuumba tukiwa na uhuru wa kuchagua mema au mabaya. Hatulazimishi kwani kupenda hakulazimishwi.

Malaika waliumbwa wakiwa na uhuru wa kuchagua mema na mabaya pia. Waliochagua kumwasi Mungu ni mashetani. Uelewa wao ni mkubwa, so they understood perfectly what they were doing. Ndiyo maana hawakukombolewa kama sisi.

Kiburi tunachokionyesha hapa cha kudhani tunaelewa kila kitu ni hatari sana. Tuwe wanyenyekevu na tujue sisi sio miungu.
 
Yeye alijuaje kama mawazo hayo ni sahihi!?

Kwa sababu lazima kuwe na reference ambayo ndio ukweli!!
 
Watu wanashindwa kuelewa tu kwamba kuna elimu/ujuzi na kuna akili,tunapokwenda shule sio kwamba hatuna akili au hatuzitumii akili zetu. Ila ajabu mtu anataka apate kujua kuhusu Mungu kwa kutumia akili tu ila ajabu mtu huyohuyo hakukaa tu nyumbani na akili yake kwa kutegemea kupata kujua yale yenye kufundishwa shule kwa akili tu.
Mkuu, hapa unamaanisha nini!?

Kwamba yahitaji uwe na nini ili umjue Mungu!?

Au labda wewe mkuu Tz mbongo, umemjua Mungu kupitia nini!?
 
Ndani ya bustani ya eden Mungu aliweka mti wa mema na mti wa mabaya. sasa mti wa mabaya wa nini wakati dhambi ilikuwa bado? Inaonekana Mungu aliiumba dhambi before
Na kwanini aliuweka huo mti wa mabaya!?

Au ndio ulikuwa mtego kwa akina Adam!?
 
Mungu "aliumba" vitu, na dhambi sio "kitu". Sheria pia sio kitu. Mungu alitupatia sheria, hakuumba sheria. Tutumie neno "kuumba" kwa usahihi.

Maoni hasi dhidi ya dini yanatokana zaidi na kutokuwa na msingi mzuri wa kuanzia kwenye kumwelewa Mungu. God is infinite while we are finite. We cannot fully fathom Him, not even when we enter His Kingdom. Ni kama mende kujaribu kumwelewa binadamu. Hana huo uwezo.

Mungu ni UPENDO. That's biblical. Hampangii mtu ubaya. But as He exists outside of the limitation of time, He knows all the good and bad choices that we will make in our lives.

Si mpango wa Mungu tutende dhambi. Ni uamuzi wetu, na Mungu anafahamu, tangu mwanzo wa nyakati, kwamba tutaamua kufanya nini. Ametuumba tukiwa na uhuru wa kuchagua mema au mabaya. Hatulazimishi kwani kupenda hakulazimishwi.

Malaika waliumbwa wakiwa na uhuru wa kuchagua mema na mabaya pia. Waliochagua kumwasi Mungu ni mashetani. Uelewa wao ni mkubwa, so they understood perfectly what they were doing. Ndiyo maana hawakukombolewa kama sisi.

Kiburi tunachokionyesha hapa cha kudhani tunaelewa kila kitu ni hatari sana. Tuwe wanyenyekevu na tujue sisi sio miungu.
Mkuu Augustine Moshi , watu wasioamini kuwa Mungu yupo, ni kwa sababu ya sifa anazopewa kuwa ni zake. Kwa hiyo watu wanatumia sifa zile kuonyesha kuwa hayupo.

Sasa, kabla haujawaambia takwa la Mungu kwa wanadamu, basi kwanza uwathibitishie kuwa ni kweli yupo.

Kwa, mfano Mungu anayetajwa kuwa ndio kaumba kila kitu!
Lakini wewe kwenye aya ya kwanza tu, umesema kuwa kaumba 'vitu' tu (ila hapa sikukuelewa kama unamaanisha tangible au vipi).

Kadiri yako ni kwamba kuna baadhi ya vitu(sijui nitumie neno gani hapo ili kuonyesha utofauti) ambavyo havikuumbwa, mfano sheria!!

Sasa hapa watu watataka uwaeleweshe kuwa, kumbe Sheria haikuumbwa na Mungu.

(Note: naomba kuuliza, hivi kuumba na kutengeneza, ni sawa kuyaexchange?)
 
Lengo la kumpima sio kujua mapungufu yake hapana,,,ila ni kuthibitisha kwamba kaumba mtu mkamilifu anaeweza kuhimili jambo fulani.Hata Yesu alijaribiwa ila haikuwa na maana ana mapungufu,,lakini kulikuwa na lengo kwamba kuona kwa upana njia aliokuwa akiiendea,,kwamba kulikuwa na jaribu la nafsi yake lilitokana na Njaa,,kukawa na Jaribu la kuhusu lengo lake,,kumsujudia shetani,,na la tatu kukufuru kwa kujirusha chini.
Na aliposhinda haya majaribio ya Lucifer alithibitisha kwamba yeye ndie mwana wa Mungu na kuendelea kulisimamia kusudi lililo mleta kulifanya.

Swali ni je! Huyo Yesu ambae hakuwa binadamu kujaribiwa na Lucifer huoni Kuna kitu kilichokuwa zaidi ya tunavyofahamu.
Sijui kama umeelewa nilichokuuliza. Unampimaje binadamu kwa kumpa mtihani ilihali huyo huyo anayepima ndio huyo huyo aliyemuumba mpimwaji. Kwahiyo kamuumba makusudi awe na mapungufu ili afeli mitihani? Kwani alishindwa nini kumuumba huyo mtu akiwa mkamilifu? Ikiwa wewe ni designer wa magari, umeunda gari kisha ukalipeleka barabarani kwajili ya kulifanyia majaribio na ukagundua gari linamapungufu kwenye matairi lakini hukurekebisha hayo mapungufu. ukaliacha gari litumike hivyo hivyo. Je ikitokea gari limesababisha ajali wewe designer utalilaumu vipi gari wakati wewe ndiye chanzo?
 
Mimi siwezi kujua feature ya mwanangu ila Mungu anajua mwanzo mpaka mwisho wa lolote, Kwanza ulilenga nini?

Namaanisha, Mungu alituumba na utashi (free will) ambayo yeye hakushurutishi. Pia, Mungu anatuwazia na kututakia mema hivyo kutenda mabaya inakuwa ni utashi wako
 
Nimemjua Mungu, kupitia Biblia!!
Hiyo ndio naita ni elimu kwamba ndani ya Biblia kuna elimu yenye kumuelezea Mungu kwa maana nje ya hapo hauwezi kumjua Mungu kwa kutumia akili tu ambayo ni mawazo binafsi ya mtu.
 
Lakini mkuu, kuielewa biblia si nimetumia akili!? Au!?
Sahihi kabisa kwa sababu hayo ni matumizi sahihi ya akili,ila matumizi ambayo sio sahihi ya akili ni pale mtu anapotaka kumuelezea Mungu au kumjua kwa kutumia tu akili bila kupata elimu kwanza ya kumjua huyo Mungu.
 
Uko sawa!!

Sasa, Je, ni kwenye biblia pekee ndio kuna elimu ya kumjua Mungu!?

Vipi kuhusu Quran!?
 
Hujajibu chochote rudia mkuu.
Nitajibu Kwa muongozo wako namba 3, kuhusu watu kujaa kwenye uso wa dunia, unadhani tusingekufa milele kuna madhara labda yangetokea??? Mi Siamini kwamba kifo control ya population
 
Duhhh! umekaba hadi kooni complex paradox
Kwahiyo hapa unakubali kwamba kuna vitu Mungu hakuumba, kama vile space.

Na kama unakubali au kuamini kuwa space haiumbwi, kwanini usiamini au kukubali pia kuwa ulimwengu hauumbwi?

Na pia swali lingine, kwa kabla ya kuumba ulimwengu huu(ambao kitheologia unakadiriwa kuwa na umri wa miaka 6000 tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa). Hapo kwenye space Mungu alikuwa anafanya nini kwa makarne na makarne?!
 
Mkuu asante kwa jibu lako fikirishi lakini naweza kujibu kama ifuatavyo:

La kwanza, kama kweli Mungu amekuwepo milele na milele maana yake kabla ya kuumba kitu chochote amekuwepo hapo kwenye space(kadiri ya mdau mmoja hapo juu, kuwa Mungu alikuwa kwenye space kabla ya kuumba chochote) kwa muda infinity(maana yake hana mwanzo). Sasa swali linakuja kwa wanaomuamini, katika Muda huu infinity, Mungu alikuwa anafanya nink hapo kwenye space peke yake? (Kumbuka hiyo ni kabla hajaumba chochote hata malaika)

La pili, mkuu hauwezi ukasema kuwa Mungu yupo pasi na kutanabaisha sifa zake. Yaani sifa ni kama identity ya uwepo wake, kwa mfano, wewe unaamini kuwa mungu ni chanzo cha vitu vyoote. Tayari hiyo ni sifa unayoamini anayo, na hapohapo swali linazuka, Je kama Mungu ni chanzo cha vyoote, je Mungu ni chanzo cha shetani, dhambi na uovu uliomo duniani!?
Nadhani utaona ni jinsi gani watu wanatumia sifa wampazo Mungu kupinga uwepo wake!
Duhhhh!! aiseee unajua kujenga hoja mkuu!
Umeeleza/kuuliza kama ambavyo nia yangu ilikusudia mkuu.
 
Hiyo choice ya kuchagua "Mema" na "Mabaya" inaonyesha kumbe hayo mawili yaliwekwa kwa makusudi na Mungu?

Back
Top Bottom