Je, Marais wa Siku hizi wa Afrika Kujisifia kuwa Saa 8 za Usiku nao hukesha kama Popo ni vyema au ni Uthibitisho wa Kufeli Kwao Kiuongozi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,721
109,153
Madaktari Bingwa wengi wa Akili wanasisitiza na Kutusisitiza mno Wanadamu ( Watu ) kuwa pamoja na kwamba tupo busy na Maisha ila Usiku kuanzia Saa 4 hadi Saa 11 ni lazima tuwe tumelala vya Kutosha Kwa Afya ya Miili yetu na Akili pia.

Wataalam hao wakaenda mbele pia na kusema kuwa Mwanadamu anayekosa Usingizi au asiyependa Kulala mida hiyo tajwa hapo juu basi moja kwa moja atakuwa na shida ya Akili ambayo inaweza hata Kuathiri Ufanisi wake wa Kiutendaji.

Kwa miaka ya hivi karibuni 2020 na hata 2022 GENTAMYCINE kwa Masikio pamoja na Macho yangu haya haya niliwahi Kuona na Kusikia Marais kadhaa wa Afrika ( kwa sasa nimewasahau ila huko mbeleni nikiwakumbuka nitawataja ) wakisema tena kwa Kujiachia kabisa Ili Waonekane kuwa Wanazikeshea nchi zao kuwa Wao Usiku wa Manane huwa hawalali kabisa Mmoja akisema Yeye huwa anasaini Mafaili hiyo mida na Kusikiliza Simu za jinsi Watendaji wake Wanavyotongozana na Mwingine nikamsikia akisema Yeye mida hiyo ndiyo huwa anaitumia kwa Kuchati na kujibu Arafa ( Meseji ) za Wateule ( Watendaji ) wake.

Je, hii tabia ni Sawa / ni Upuuzi mno?
 
Severe depression + Insomnia.
Hivi na Marais akina Joe Biden na Vladimir Putin nao huwatangazia kwa Kujimwambafai Wananchi wao Wamarekani na Warusi kuwa na Wao huwa hawalali Saa 8 za Usiku wanakesha kama Popo Wakichati, Wakijibu Meseji na Wakikesha Jamiiforums Kumsoma GENTAMYCINE na 'Critics' wengine?
 
Picha ya kusindikizia uzi tafadhali
Ipi sasa? Ya aliyesema hukesha Usiku Kusaini Mafaili na Kusikiliza Maongezi ya Wateule wake au ya anayekesha Usiku kama Popo kujibu Meseji na Kuchati Umbea tu?
 
Hivi na Marais akina Joe Biden na Vladimir Putin nao huwatangazia kwa Kujimwambafai Wananchi wao Wamarekani na Warusi kuwa na Wao huwa hawalali Saa 8 za Usiku wanakesha kama Popo Wakichati, Wakijibu Meseji na Wakikesha Jamiiforums Kumsoma GENTAMYCINE na 'Critics' wengine?
Hao wanajielewa. Wanajua wajibu wao na uzito wa dhamana waliyopewa na wananchi wao. Hata wasipolala mwezi mzima hawawezi kusema. Labda akija kustaafu ndio anaweza kuelezea maisha aliyoishi akiwa ofisini.

Tatizo hawa wakwetu wanakuwa sio machaguo ya wananchi hivyo hata hawaogopi kujimwambafai.
 
Sasa kuna maana gani ya kuwa macho saa nane za usiku huku vitu vinazidi kupanda bei!!???
Labda ndiyo huwa anakesha Kuchati nao Wapandisha Bei Ili wapunguze ila nao Wanamkazia huku wakimshangaa kwanini Saa 8 za Usiku halali?

Mkuu kwani na Wewe tupo hapa Northern Malawi niishipo GENTAMYCINE na huyo Rais Mkeshaji au upo kwa Biden na Putin huko?

Northern Malawi kuna Vituko mno tu.
 
Hao wanajielewa. Wanajua wajibu wao na uzito wa dhamana waliyopewa na wananchi wao. Hata wasipolala mwezi mzima hawawezi kusema. Labda akija kustaafu ndio anaweza kuelezea maisha aliyoishi akiwa ofisini.

Tatizo hawa wakwetu wanakuwa sio machaguo ya wananchi hivyo hata hawaogopi kujimwambafai.
Mkuu kwani nawe unaishi hapa Northern Malawi kama Mimi GENTAMYCINE?
 
Itakua wanadhihirisha kufeli kwao.nakumbuka marehemu aliyefariki machi 17 alisema huwa anakesha akipekuwa mafaili.
 
Itakua wanadhihirisha kufeli kwao.nakumbuka marehemu aliyefariki machi 17 alisema huwa anakesha akipekuwa mafaili.
Anatokea hapa Northern Malawi ( tulipo wana JamiiForums wengi ) au labda ni wa kutokea nchini Burundi?
 
Back
Top Bottom