Je, kwa mara ya kwanza bajeti ya 2022/2023 kupitishwa na kura chache za wabunge wa CCM?

Jun 13, 2022
8
9
Tumezoea kuona mara nyingi inapofikia wakati wa kupiga kura kupitisha bajeti ya Wizara ya Fedha., wabunge karibia woote (99.9%) wa CCM huipigia kura ya NDIYOOO kuiunga mkono hata kama hoja zao za msingi hazikujibiwa kwa usahii, ukiachilia mbali wale wa upinzani (sio kwa bunge la sasa) ambao siku zote huwa wanapiga kura ya hapana( Naah).

Ila kwa jinsi nilivyoona uwasilishaji wa bajeti ya mwaka huu pamoja na kugusa maeneo mengi ya msingi, ila kwa jinsi alivyokuwa akijigamba Waziri wa Fedha kwa dhihaka na majivuno huku akijificha kwenye kivuli cha Mama (hasa siku ya leo asubuhi wakati wa hitimisho (Hakujibu kabisa hija za wabunge zaidi ya kupoteza mda mwingi kuzungumzia umuhimu wa Serikali kukopa na swala jingine dogo kabisa la kuondoa ada za kidato cha 5&6).

Ni matarajio yangu kuwa uenda kura za ndio zikapungua saana leo jiioni wakati wa kupiga kura ya kupitisha bajeti ya mwaka huu 2022/2023
 
Back
Top Bottom