Wabunge badilisheni mbinu za kuomba kura uchaguzi ujao

utukufu mwanjisi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
2,834
2,422
Nashangaa tena nashangaa sana wanasiasa wenzangu ambao mpaka sasa ni wabunge wa majimbo mbalimbali bado wanafanya siasa za miaka ya 90's huko wakati tupo kwenye ulimwengu wa wapiga kura waelewa na wasomi wengi tofauti na kipindi cha nyuma.

Mwanasiasa kijana tena wa kileo bado anaanzisha mashindano sijui nani nani cup, sijui nagawa kanga kwa wamama sijui natoa mashindano ya ng'ombe mara mbuzi, huko kote ni kupoteza nguvu tu.

Tafuteni watu wenye mawazo mapya namna ya kufanya majimboni ili muwe na uhakika wa kubakia 2025 bila wasiwasi wowote bila hivyo mtapoteza hayo majimbo kwa kufanya siasa za miaka ya 90 kwa kipindi hichi.
 
mojawapo ya virus natamani wagombea waitoe vichwani mwa wapiga kura ni kuwaaidi kufanya jambo lolote linalohusu kodi na idhini toka serikal kuu/mitaa isipokuwa tu kutoka mfukoni mwao!
Hiki kitu kinawatafuna sana wanapopa,mbana kwenye wizara husika bila mafanikio.
Waseme tu ...nitaisisitiza serkali kufanya hili na lile .. na sio ..nitajenga barabara x na kujenga shule kadhaa
wanajibebesha lawama na kuiacha serkali inapumua!
 
Back
Top Bottom