Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

Unaweza kuisoma tabia ya mtu kwa kuangalia viashiria mbalimbali.

Lakini kuna masuala ambayo huwezi kuyajua kamwe. Siri zake, mipango yake, maamuzi yake wakati wa matatizo nk.
Kijana mdogo
Hapa tunazungumzia mawazo ya mtu sio tabia zake

Nitakuminya ☹️
 
kudai kujua moja kwa moja kilicho kwenye akili ya mtu: “Ananichukia,” “anaficha kitu,” au “anafikiria X.?

Hii hakuna anayeweza kufanya

Claim Vs Evidence
Kwanini unadhani hakuna anaeweza ?
 
Ukiona ni “mix,” basi tayari kuna distinction muhimu umeiona. 🙂 Tatizo ni kwamba mara nyingi watu wanachanganya kile kinachoonekana, signal yenyewe, na interpretation ya signal hiyo.
Kwa mfano, gesture ni movement fulani; nonverbal cue ni taarifa inayoweza kutolewa bila maneno; body language ni broader pattern ya posture/movement/expression; inference ni tafsiri tunayofanya kutokana na cues; na mind reading ni kudhani unajua moja kwa moja kilicho kwenye akili ya mtu.
Kwa hiyo si kila gesture ni ujumbe maalum, na si kila cue inatupa access ya moja kwa moja kwenye thoughts za mtu. Hapo ndipo tofauti kati ya observation, interpretation, na mind reading ilipo.
Asante kwa maoni mkuu
 
Kijana mdogo
Hapa tunazungumzia mawazo ya mtu sio tabia zake

Nitakuminya ☹️
Si ndio? Unaweza kumsoma mtu kupitia milango yako ya fahamu. Utaona anavyokwepesha macho na kuchezesha mikono, utasikia kigugumizi chake nk.

Kulingana na muktadha, unaweza kujua kitu flani. Mfano ukimuuliza jambo halafu ajibu kwa kupepesa macho, utahisi huenda anadanganya.

Lakini, kuingia moja kwa moja ndani ya akili ya mtu na kuona mawazo yake kama yalivyo(telepathy) haiwezekani, labda uingie upande wa pili kwenye mambo ya kiroho.
 
Yule mshikaji ana wivu sana na nilikuwa namjua vyema. Kukusaidia zaidi tafuta hiki kitabu , nilishawahi kuwa nacho mwaka 2014 sijui kilipotelea wapi lakini pale Efatha kwa Mwingira nadhani kipo na kipo na cha kiswahili

View attachment 3674138
Huyu mwandishi Iyke alikuwa ni Makamu wa rais wa Wachawi Africa, halafu huwa tunabishana sana kuhusu uchawi lakini ukikisoma hiki kitabu utajifunza na kufahamu mengi. Huyu Mwandishi alishaokokà na kuwa Pastor mkubwa sana na siri nyingi za uchawi amezianika wazi
Nitasoma kaka
Ila hapo kwenye umakamo wa
Rais wa wachawi najua ni chai 😄
 
1. inaweza ikawa ni direct au in-direct ili uweze kumsoma mtu ni lazima mjongeo wa mwili na sauti uwepo japo hata maiti inaweza kuzungumza ukitaka kuisoma:3Dance:
2. ndio inawezekana kabisa intelligency wengi wamezaliwa na huo ujuzi...ila ukisoma sana unaweza ukajiongezea maarifa ya kukuwezesha kuwajua watu na binaadam...
3. manabii wengi wamesoma au wamezaliwa na kipawa cha utambuzi...hivyo akikuona tu anaweza kukuelewa na kucheza na akili yako akakuvuruga ukamuamini...ila ni kitu kidogo tu watu wanadanganyika kwa kuambiwa mambo yao ambayo wanadhani wanayafahamu wenyewe....!
Shukran sana mkuu
Hapo kwenye maiti jazia kidogo nyama hata kwa uchache

Manabii wanatumia akili kubwa kucheza na akili za watu wale watu sio poa
 
Si ndio? Unaweza kumsoma mtu kupitia milango yako ya fahamu. Utaona anavyokwepesha macho na kuchezesha mikono, utasikia kigugumizi chake nk.

Kulingana na muktadha, unaweza kujua kitu flani. Mfano ukimuuliza kitu halafu ajibu kwa kupepesa macho, utahisi huenda anadanganya.
Hapa unatumia ishara zake kubashiri kwamba huenda anadanganya huyu
Lakini, kuingia moja kwa moja ndani ya akili ya mtu na kuona mawazo yake kama yalivyo(telepathy) haiwezekani, labda uingie upande wa pili kwenye mambo ya kiroho.

Huko rohoni unajua lolote ?
Unaweza ku share hapa
 
Kusoma mawazo ya mtu ni rahisi sana kama ukivuta ganja kiasi kwa mtu unaemfahamu

kwa mtu usiemfahamu vuta pia kiasi na uwe msikilizaji sana
Ni hayo tu!
Hii njia hua unatumia mkuu
Sio kwamba unatuingiza chaka😁
 
Kwanza finale wanawake wamepata mtu wa kuwatoa unyonge,maana siku za nyuma ilikuwa inasemwa mbona wanawake hawachapishi nyuzi?

Sasa walau wamepata mwakilishi wao,tena haandiki tu nyuzi kama nyuzi ili mradi awe ameandika ila ni nyuzi ambazo hata ukisoma hujutii kutumia muda wako kuzisoma

Hongera sana mto mada
Shukran mkuu
Karibu ndani ya mada
 
Manabii wanatumia akili kubwa kucheza na akili za watu wale watu sio poa
Kuna Nabii mmoja , aliniambia jina langu bila kumtajia, Mkoa na Wilaya niliyozaliwa mpaka tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa. Wewe Nabii huko uliko ulaaniwe 😆😆😆

Na hamna liloendelea 😏
 
KARIBU KWENYE MADA WANA GREAT THINKERS 🧠 ☕️

Unaweza vipi kusoma mawazo ya mtu mwingine au kujua kinachoendelea kwenye akili yake?

Unaamini kama kuna watu wanaoweza kusoma akili au mawazo ya watu wengine?

Unadhani ni nini huwa kinatokea pale mtu anapoona maandishi ya mtu au akiwa kwenye mazungumzo na mtu mwingine, halafu akagundua kwamba huyu mtu anawaza kitu fulani?

Na ajabu, unakuta baadae yule mtu anafanya kitendo au vitendo vinavyothibitisha kwamba yale aliyogundua mwanzo yalikuwa sahihi


Kisayansi hali hii inaelewekaje?

Hawa watu tunaweza kuwaita watambuzi.watu wenye intuition kubwa wenye uwezo mkubwa wa kuchanganua watu, au ni geniuses?

Na wewe binafsi unaamini unaweza kusoma akili ya mtu?

Kama ndiyo unafanya hivyo kwa namna gani?

Maoni yangu 👇

Kikawaida kabisa, naamini kuna watu wenye uwezo mkubwa sana wa kutambua mambo hata bila mtu kuyaeleza moja kwa moja

Sio kwamba wanatumia akili ya ajabu au wanaingia kwenye akili ya mtu mwingine bali kuna wakati mtu akiwa makini sana anaweza kuona signals ndogo ndogo ambazo watu wengine hawazioni

Hata kama mtu anajaribu kufake au kuficha mawazo yake kwa kuongea au kuandika kitu tofauti na anachohisi, ukiwa makini sana unaweza kugundua kuna kitu hakipo sawa

Ni sawa na mtu ambaye anaweza kukuonyesha kwamba amefurahi sana kwa sababu umepata kazi

Anaweza kucheka kukusifia na kukuambia:

Hongera sana ShesRise_1 nimefurahi kwa ajili yako umepata kazi

Lakini wakati huo huo kuna signals nyingine unaweza kuziona

Labda kwenye facial expression yake namna anavyocheka tone la sauti macho, movements za mikono, posture yake au hata namna anavyoendelea na mazungumzo
Unaona kabisa yeye wa ndani
Na yeye wa njee ni kama mifumo haisomani

Na kama wewe ni mtu ambaye una observation nzuri na ubongo wako unafanya kazi shap utagundua haraka sana

Huyu mtu kwa ndani hafurahii kama anavyosema

So patterns ukiziona unagundua huyu anawaza kwa namna nyingine kabisa tofauti na anachokionesha

Na kinachofanya jambo hili liwe interesting zaidi ni pale unapokuja kugundua kwamba baadae yule mtu anafanya kitu kinachothibitisha kile ulichohisi mwanzo

Swali la mjadala?👇

Hua najiuliza nimeisoma akili yake, au nilikuwa nimeisoma signals zake vizuri na kwa haraka?

Na kama kweli kuna watu wenye uwezo huu mkubwa wa kutambua kile ambacho wengine wanajaribu kuficha...

Uwezo huu unatokana na nini?

Ni intuition?
Ni experience?

Au kuna kitu kingine ambacho bado Labda wengi wetu hatujakifahamu kwa undani
Na kama kipo je ni kitu gani?

Nataka kusikia mawazo yenu🧠

Cc: Marcostilone

ShesRise_1 ✋️
Hali ya kuweza kujua mawazo ya mtu mwingine na kujua anafikiria nini inaitwa telepathy. Kijamii kuna watu (kama wewe mtoa post) wanaamini hilo jambo lipo na limawezekana, lakini mpaka sasa HAKUNA scientific proof ya uwepo wa telepathy!

Yaani kama vile Wabongo na maskini wengi wanvyoamini uwepo wa uchawi!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom