nzalendo
Platinum Member
- May 26, 2009
- 13,062
- 15,134
MUNGU Yupo....na hajaruhusu mateso,,,,Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?
Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.
Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?
NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
Kwa kifupi sana...SISI WAAFRIKA NDIO KILA KITU...... NDIO WATEULE WA MUNGU.....KWA KUTOJITAMBUA NA KUVURUGWA..... NDIO YOTE HAYA YANATOKEA........TORATI IPO WAZI KABISA SOMA NA UIELEWE.