Je, kuna maisha mengine baada ya hapa duniani?

Je, kuna maisha mengine baada ya hapa duniani?

Swali zuri. Ndio kuna maisha baada ya kifo ambayo ni ya milele. Maisha hayo yanategemea uliishije duniani,ikiwemo utii wako kwa Mungu. Wengi wanapata ukakasi kuyaamini maisha hayo kwa sababu hayaonekani kwa macho yetu ya kibinadamu(yapo kwa jinsi ya Rohoni). Jiweke tayari maadam upo hai(Hii ndio nafasi pekee uliyo nayo)
Mkuu naona unaturudisha palepale tulipotoka kwenye hadithi za alinacha
 
Kwa mujibu wa Quran ndiyo kuna maisha mengine baada ya hapa na ninaamini hivyo.
 
Biblia ni historia halisi. Imebainisha ukweli mwingi sana unaojibu maswali makuu yote kuhusu maisha ya mwanadamu yaliyopita, ya sasa na baadaye.

Mtu anayeamini uwepo wa Mungu, anashindwaje kuwa na hakika ya maisha ya baadaye? Anashindwaje kutambua kwamba maisha ya dunia na kaburi siyo mwisho wa mambo?

Mungu aliumba kwa kusudi la kudumu milele kwa viumbe Wake.

Pamoja na kwamba mpango Wake umevurugwa na dhambi, lakini bado ameandaa njia ambayo kwayo mwanadamu anaweza kurejesha mahusiano yake kwa Muumba wake.

Iwapo Mungu ndiye msingi, basi mauti kamwe haiwezi kuwa ukuta wala ukingo. Kuna maisha baada ya Kiama.

Ni muhimu pia kujikumbusha kwamba si kila mtu ataonja mauti. Kuna watu watakaokuwa wangali hai wakati wa kuja kwa Kristu Yesu. 1 Thesalonike 4:16, 17

Usemi mashuhuri kwamba ^kila nafsi itaonja mauti^ unaenezwa na Shetani kupitia malaika wake, kwa lengo kuu la kuwapotezea tumaini watu ambao wamechagua kumpenda na kumtii Mungu.

^Amin, amin, nawaambia, yule alisikiaye neno Langu na kumwamini Yule aliyenipeleka, yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.^ ~Yohana 5:24
Reference za bible hapana, ni za kuandikwa na watu waliotumia zaidi ya miaka 500 wakiiandaa Bible ila waitumie kwa manufaa yao.

Kama kungekua na mbingu, maisha mapya, kula asali na maziwa basi wazungu wangeficha Bible zisifike africa, hakuna mzungu anatupenda watu weusi.

Kama mungu angekua na mpango wa binadamu kuishi milele, basi asingeshindwa kumzuia shetani asilete madhara kwenye mpango wake kwani yeye ni ndio mwenye ngunvu.

MAMBO YOTE YA BIBLE NI MAJIBU KWA AKILI ILIYOFIKA MWISHO KUFIKIRI. NI SILAHA KWA WAJANJA
 
Siyo kweli. Akiolojia na sayansi vinathibitisha juu ya ukweli na usahihi wa Biblia.

Habari zilizoandikwa kwenye Biblia ni mambo halisi, kama tusomavyo kuhusu matukio ya vita vya dunia, au hata migogoro ya sasa baina ya Palestina na Israeli.

Yaliyomo kwenye Biblia, siyo tu kwamba ni habari za kihistoria, bali pia ni uvuvio mtakatifu ulioandikwa na watu halisi wakiomcha Mungu, mfano Musa, Daudi, Sulemani, Daniel.

Watu hawa wote ni wahusika halisi katika historia, wala si wahusika dhahania (fictional characters).

Ujumbe wao mahususi wa uvuvio kutoka kwa Mungu umetufikia sisi kupitia Biblia.

Viumbe vinakufa kwa sababu ya dhambi, kwa sababu ya uchaguzi mbaya wa Lusifa ama Shetani, kwa sababu mwanadamu alikubali naye kufuata njia ya Lusifa, akamwasi Mungu.

Lusifa alitumia uhuru wake vibaya. Mwanadamu naye alitumia uhuru wake vibaya.

Kufa kwa viumbe haina maana kwamba mpango wa kuishi milele umetoweka. Kifo kimekuja kwa sababu ya dhambi.

Lakini pia mauti siyo mwisho wa mambo. Kuna maisha baada ya mauti, kwa wale ambao wamechagua kuufuata mpango wa Mungu wa wokovu kupitia Yesu Kristu.

Alijua. Mungu anajua mwisho toka mwanzo. Anajua yote. Isaya 46: 9, 10. Kila kitu ki wazi mbele Yake. Ebrania 4:13.

Hii ndiyo maana Biblia inasema mpango huo uliandaliwa muda mrefu tangu kuwekwa misingi ya dunia. Ufunuo 13:8

Kutokea kwa dhambi haina maana kwamba mpango Wake umezuiwa. Dhambi katika mpango wa Mungu, ni sawa mfano wa njia mbovu kwa msafiri.

Mungu hakushtukizwa na dhambi wakati akimuumba Lusifa, malaika walioasi na hata mwanadamu ambaye ameanguka.

Alijua na aliliona hilo mapema, ndiyo maana akaandaa mpango mahususi, mkamilifu ili kukidhi hali hiyo ya dharura kabla ya kutimia kwa mpango Wake.

Ukamilifu wa mpango huo uko katika makusudi husika, namna ya utekelezaji na hatimaye matokeo yake.

Mungu angeweza kutumia njia nyingineyo, lakini uchaguzi Wake wa kuanza kushughulikia dharura ya dhambi ndilo jambo bora zaidi ambalo lingekuwa na manufaa kwa viumbe Wake wanadamu kwa malaika, milele na milele.

Kuasi kwa Lusifa kuliambatana na hoja zake mahususi (incendiary postulations) dhidi ya Mungu ambazo pekee zingeweza kujibika kikamilifu mazima milele (completely & finally forever), kwa mujibu wa silika takatifu na yenye upendo ya Mungu, kwa kuwaruhusu viumbe Wake wenye utashi huru japo ^wachungulie^ ng'ambo ya pili na kuhabiri maisha nje ya Mungu.

Kwa maneno mengine, kuasi kwa Lusifa ilikuwa fursa ya Mungu kumthibitishia vinginevyo dhidi ya fikra zake kinyume na Muumbaji.

Unapozungumzia Mungu mwenye upendo timilifu na mwanadamu (au hata malaika) mwenye utashi huru, ni rahisi kutambua kwa nini viumbe wenye uwezekano wa kutenda dhambi waliumbwa.

Ni kana kwamba Mungu, ili kudhihirisha upendo Wake wa juu zaidi kwa mwanadamu na malaika na viumbe Wake wengine wenye nadhari za juu za maarifa, aliamua kuumba nafsi zenye utashi huru zikiakisi utashi Wake Mwenyewe.

Mwanadamu ameumbwa katika sura na mfano wa Mungu. Huo ndio upeo wa upendo wa Mungu.

Kudai kwamba Mungu alishindwaje kuumba dunia isiyo na uwezekano wa kufikwa umauti ni kutotambua silika na baraka kuu ya Mungu kwa viumbe Wake -- upendo.

Pia, kudai kwamba Mungu alishindwaje kuumba dunia isiyo na uwezekano wa kufikwa na dhambi na mauti ni sawa na kudai kwamba kwa nini Mungu asingetuumba tukiwa watii tarasili (automatic obedients), tulio radhi wakati wote, na tusio tayari katu wala wenye uwezekano wowote kabisa wa kubadili msimamo huo -- watii halaki (blind obedients), unaweza kusema.

Kama hilo angelifanya Mungu, basi tusingekuwa tumeumbwa katika ^sura na mfano Wake.^

Kwa namna hiyo, tusingekuwa tunamtumikia kutokana na moyo wa upendo, bali kwa kusukumwa na hulka asili ndani yetu iliyotarakibiwa awali (intrinsically preprogrammed nature) -- tungekuwa mithili ya roboti.

Matokeo yake, tungekosa utashi huru, ambayo ni tunu bora zaidi miongoni mwa amana alizotubarikia Maulana.

Pamoja na tunu hii kuu, ukaja pia uwajibikaji kwa upande wa mwanadamu kuhusu matumizi husika. Na ndipo hatari kuu ikafuatia. Lakini huo haukuwa mwisho wa mambo.

^Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.^ ~ 1 Korintho 15:22

Mungu hajashindwa kitu, na wala kushindwa hakupo katika asili Yake takatifu.

Ubongo wa mwanadamu ndio unakataa kukubali mambo jahara aliyoyafunua Mungu kuhusu mpango Wake kwetu.

Hivi inawezekanaje Mungu wa milele, aliyeumba vitu vyote, hata ahusishwe na msamiata wa kushindwa?

Ni wazi kwamba kudai Mungu ameshindwa, hilo tu kwa lenyewe ni kumkufuru.

Kila jambo analotenda Mungu, kila kitu anachoruhusu kitendeke, huwa kina kusudi maalumu.

Na ndiyo maana dunia, baada ya dhambi, wadhambi, Shetani na malaika zake kutokomezwa milele, bado itakuwa sehemu ya kutimizia lengo hilo la awali la Mungu

^1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, Naye atafanya maskani Yake pamoja nao, nao watakuwa watu Wake. Naye Mungu Mwenyewe atakuwa pamoja nao.

4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

5 Na Yule aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.

6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yule mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.

7 Yule ashindaye atayarithi haya, Nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.

27 Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yule afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo.^ ~Ufunuo 21
Yaan mm mtu akianza ku quote Bible tu naona walewale wasoma kitabu kimoja na kukariri. Amka wewe hicho kitabu kimetungwa na watu kwa manufaa yao
 
Yaan mm mtu akianza ku quote Bible tu naona walewale wasoma kitabu kimoja na kukariri. Amka wewe hicho kitabu kimetungwa na watu kwa manufaa yao

Sawa hivyo vitabu vingine unavyosoma wewe vimeandikwa na Malaika sio The Bible is the most sold book duniani. Watu wana kiu ya kupata Hekima iliyomo ndani ya kitabu hicho. Hakuna Mwanadamu anayeweza kuandika kitabu kikaendelea kuhitajika na mamilioni ya watu kwa karne na karne. HAKUNA!
 
Reference za bible hapana, ni za kuandikwa na watu waliotumia zaidi ya miaka 500 wakiiandaa Bible ila waitumie kwa manufaa yao.

Kama kungekua na mbingu, maisha mapya, kula asali na maziwa basi wazungu wangeficha Bible zisifike africa, hakuna mzungu anatupenda watu weusi.

Kama mungu angekua na mpango wa binadamu kuishi milele, basi asingeshindwa kumzuia shetani asilete madhara kwenye mpango wake kwani yeye ni ndio mwenye ngunvu.

MAMBO YOTE YA BIBLE NI MAJIBU KWA AKILI ILIYOFIKA MWISHO KUFIKIRI. NI SILAHA KWA WAJANJA

Unahoji kitoto sana mkuu. Dhamira ya Mungu haiwezi kushinda dhamira ya Mwanadamu. Hakuna anayeweza kuzuia neno la Mungu lisifike mahali popote. Soma historia uone namna gani injili imepigwa vita mahali pengi lakini bado imepenya. Tafuta kitabu kinaitwa BREAKTHROUGH (kinazungumzia safari ya kusambaza Injili)
 
Uongo Tu, yule jamaa si alimuamsha kutoka usingizini

Watu wakisinzia wanalala makaburini sio? maana historia inajieleza Wakati Yesu anaelekea kumfufua Lazaro, alikua kaburini tayari yapata siku tatu.
 
Unahoji kitoto sana mkuu. Dhamira ya Mungu haiwezi kushinda dhamira ya Mwanadamu. Hakuna anayeweza kuzuia neno la Mungu lisifike mahali popote. Soma historia uone namna gani injili imepigwa vita mahali pengi lakini bado imepenya. Tafuta kitabu kinaitwa BREAKTHROUGH (kinazungumzia safari ya kusambaza Injili)
Yan mungu alete Dini, watu Fulani Tu 😂, alafu wengine wabaki kupokea mapokeo Tu,
Huyo mungu ni mchoyo Sana wa elimu, halafu ni mbaguzi
 
Back
Top Bottom