Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Kwa wasomaji wapya, leo ni muendelezo wa sehemu ya pili ya somo la Ijue Katiba ya JMT kwa jicho la mtunga katiba. Sehemu ya kwanza wiki iliyopita ilitambulisha katiba ni nini, ni ya nani na ya kazi gani. Katiba ni mkataba wa watawala na watawaliwa ni ya wananchi na kazi yake ni kutoa maelekezo ya kila kitu kitakavyo fanyika, hivyo katiba iko juu ya kila kitu, hakuna aliye juu ya katiba. Pia nilionyesha jinsi baadhi ya viongozi wetu na mihimili yake valivyojiinua juu ya katiba na hata kuikiuka katiba yenyewe!

Leo katika sehemu ya pili najadili dhana ya "Katiba Ndio Sheria Mama".

Ibara ya 64(1) ya katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977, inatoa mamlaka ya kutunga sheria kwa Bunge la JMT
1694160649102.png

Ibara ya 64(5) Katiba inasema
1694160830240.png

Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni batili na ikitokea sheria nyingine yoyote ikakinzana na katiba, katiba ndio itasimama, kwa Kiingereza dhana hii inaitwa " The supremacy of the constitution" yaani hakuna aliye juu ya katiba, msimamo wa katiba ndio juu ya kila kitu.

Mfumo wa uongozi wa nchi yetu, ni kupitia mfumo wa mihimili mitatu, Serikali, Bunge na Mahakama. Mihimili hii yote mitatu kidharia iko sawa na inalingana, kila mhimili una wajibu wake, nguvu zake na mamlaka yake inayojitegemea, kwa kufanya kazi bila kuingiliana, Bunge kazi yake ni kutunga sheria na kuisimamia serikali, Mahakama kazi yake ni kutafsiri sheria na kutoa haki, serikali kazi yake ni kutekeleza sheria na kuzihudumia Bunge na Mahakama.

Wakuu wa mihimili hii, Rais ni Mkuu wa mhimili wa serikali, Spika ni Mkuu wa mhimili wa Bunge na Jaji Mkuu ni Mkuu wa mhimili wa Mahakama, wote wanakula kiapo cha kuongoza kwa mujibu wa katiba ya JMT na ku apa kuilinda na kuitetea katiba ya JMT, na kumuomba "Mungu nisaidie".

Waanzilishi wa mfumo huu, pia wakauwekea mfumo wa ukiranja, yaani checks and balance kwa kila mhimili kuwa kiranja wa mhimili mwingine usikiuke mamlaka yake au kuvuka mipaka. Kanuni hii kwa Kiingereza inaitwa "The doctrine of separation of powers, check and balance "

Hivyo katiba ndio kila kitu, na kwa vile katiba ni mali ya wananchi, ina maana wananchi ndio kila kitu!, viongozi ni watumishi wa wananchi, lakini kufuatia madaraka na mamlaka ya viongozi wetu, baadhi ya viongozi wamejiinua na kujiona wao ndio kila kitu, wengine kufikia hata kuikanyaga katiba!

Dhana ya katiba ni sheria Mama na sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni batili, dhana hii kwa jicho la mtunga katiba, alimaanisha.

Ikitokea ikatungwa sheria yoyote inayokwenda kinyume cha katiba, sheria hiyo inakuwa batili outright!. Anayebatilisha sheria hiyo sio Mahakama, sio Bunge, sio serikali, ni katiba yenyewe kupitia ibara hiyo ya 64 (5).

Kwenye sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, jukumu la Mahakama ni kutafsiri katiba na kutangaza sheria fulani ni batili, mara baada ya Mahakama kutangaza ubatili wa sheria fulani, tangu baada ya tangazo hilo, sheria hiyo inakuwa umebatiliswa na katiba na sio imebatilishwa na Mahakama!.

Sii mara moja wala mbili, serikali yetu imekuwa ikipeleka miswada Bungeni kutungwa kuwa sheria, baadhi ya miswada hiyo, ina vipengele batili vinavyokwenda kinyume cha katiba yetu. Swali la kujiuliza ni inawezekana vipi serikali yetu yenye wanasheria mabingwa wabobezi na wabobevu kutunga muswada wa sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba?. Jibu ni moja tuu rahisi, hao watunga miswada ya sheria, hawaijui vizuri katiba ya JMT kikamilifu!

Na baada ya serikali kutunga miswada ya sheria batili, Bunge letu Tukufu ambalo nalo limeshehenezwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, nao pia wanaitunga hiyo sheria batili na kumpelekea rais kuisaini na kuwa sheria!. Hapa swali la kujiuliza ni lile lile kama la serikali, inawezekana vipi Bunge letu Tukufu lenye wanasheria mabingwa wabobezi na wabobevu kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba?. Jibu ni moja tuu rahisi, hao wabunge watunga sheria wetu, nao pia hawaijui katiba ya JMT kikamilifu!.

Mtu pekee ambaye hana kosa katika hili la sheria batili ni Rais wa JMT kwa kusaini sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba kuwa sheria, kwasababu rais wetu ana wasaidizi anao waamini, hivyo sheria batili hizo zikifika mezani kwake yeye anaanguka tuu saini na zinakuwa sheria.

Kama watu waliopaswa kuijua katiba hawaijui, watu wanakula kiapo cha kuilinda na kujitetea katiba ya JMT ndio hao wanaikanyanga, unategemea nini kwa Mwananchi wa kawaida kuijua katiba? Hivyo elimu hii ya katiba ya JMT ni muhimu sana kwa wananchi kuijua katiba.

Baada ya Bunge kutunga sheria batili, kuna Mwananchi mzalendo wa kweli wa taifa hili, akafungua shauri Mahakama Kuu kupinga sheria batili hiyo, akashinda, Mahakama Kuu ukaitangaza ni batili, na kutoa amri ifutwe kwenye vitabu vya sheria.

Mzalendo yule hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua shauri jingine kupinga mabadiliko hayo, Mahakama Kuu ikampa ushindi, ikatangaza mabadiliko hayo ya katiba ya JMT ni batili!

Serikali yetu haikukubali ikakata rufaa Mahakama Kuu ya Rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, kutamka kipengele cha katiba ni batili.

Mahakama Rufaa
ikawaita manguli watatu wa sheria kuwa marafiki wa Mahakama, ambao kisheria huitwa "Amicus Curiae", na ndio ikatoa uamuzi wa ajabu kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya Mahakama zetu, ambao mimi nauita ni uamuzi sarakasi!

Kama mtakumbuka mwanzo nilisema mihimili hii mitatu ina wajibu wa kuheshimiana na kutoingiliana, ila pia kila mhimili ni kiranja wa mhimili mwingine kupitia kanuni ya "the doctrine of Separation of powers, Checks and Balance".

Serikali ikikiuka mamlaka yake inadhibitiwa na Bunge na Mahakama, Bunge lilikiuka mamlaka yake inadhibitiwa na Serikali na Mahakama, Mahakama nayo ikikiuka mamlaka yake inadhibitiwa na Bunge na serikali.

Kwa mujibu wa katiba yetu vyombo hivyo vyote vitatu viko chini ya katiba, na vyombo vyote vina wajibu wa kuilinda na kuitetea katiba ya JMT, hakuna chombo kinachoruhusiwa kuwa juu ya katiba au kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba!

Kitendo tuu cha serikali kupeleka Bungeni muswada wa sheria batili ni kosa, serikali yetu ilipaswa kuadhibiwa!.

Kitendo cha Bunge kutunga sheria batili, Bunge lilipaswa kuadhibiwa!

Swali ni nini kinachofanya mihimili hii yetu mitatu isifanyiane checks and balance?. Hii ni mada inayojitegemea.

Angalau Mahakama Kuu ya Tanzania, ilitimiza wajibu wake kwa kusema sheria hiyo ni batili na mabadiliko ya katiba kuiingiza batili hiyo ndani ya sheria zetu ni batili.

Mahakama ya Rufani ndio ikatoa kubwa kuliko!, Ikasema "The court is not the custodians of the will of the people". Hapa the will of the people ni katiba. Mahakama ya Rufani imejivua jukumu la kuilinda na kuitetea katiba ya JMT.

1. Imetungwa sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba
2. Mahakama Kuu imetangaza sheria hiyo ni batili
3. Serikali ikakata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kuibadilisha sheria batili hiyo.
4. Serikali ikashindwa, ikafanya mabadiliko ya katiba kwa kuichomekea batili hiyo ndani ya katiba yetu
5. Mahakama Kuu ikasema mabadiliko hayo ni batili.
6. Serikali ikakata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu.
7. Mahakama ya Rufani badala ya deal na ukiukwaji wa katiba yetu kwa kutungwa sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, yenyewe ikajikita kwenye kuangalia uwezo wa Mahakama kuliingilia Bunge kwenye uchomekeaji ubatili ndani ya katiba yetu!.
8. Ikatoa uamuzi wa ajabu kabisa kuwa Mahakama Kuu haina uwezo wa kuliingilia Bunge. Hivyo kama Bunge limetunga sheria batili, na kufanya mabadiliko batili ya JMT, ni jukumu la Bunge lenyewe, kutengua sheria batili hiyo na kutengua mabadiliko batili hayo ya katiba!.
10. Mpaka leo ninapoandika makala hii, Bunge letu Tukufu halijafanya lolote!. sheria batili hiyo bado ipo kwenye sheria zetu, ubatili uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu bado upo!. Hivi sivyo alivyo dhamiria mtunga katiba.
Jee sheria hiyo batili ni ipi, na ubatili wake ni upi na una madhara gani?. Tukutane wiki ijayo kwenye sehemu ya Tatu ya Ijue katiba ya JMT kwa jicho la mtunga katiba.

Paskali
 
Je suala ambalo haliko kwenye Katiba na linamaslahi kwa nchi ni sahihi kulitekeleza au kuliacha kwa kigezo Cha kuvunja Katiba iliyoko!?

Mukatadha wake ni pale hakuna namna (wakati) WA kuliingiza jambo hilo kwenye katiba
 
Paschal Mayalla, niwie radhi kwasababu nilijibu maoni ya Lucas aliyokutag nikidhani ni maneno yako. Tena nilitaka kushangaa, mtu kama wewe kuwaza katika ule muelekeo ni ajabu.
Mkuu mbussi , usijali nimekuelewa na kukupiga darasa la mchakato wa utengenezaji katiba bora. Mchakato huu wa Katiba ni umasikini wetu. Tujikubali, tuukubali, tuupigie kura ya ndio

Pia humu JF, najihesabu ni mmoja wa self made teachers wa katiba
P
 
Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni batili na ikitokea sheria nyingine yoyote ikakinzana na katiba, katiba ndio itasimama, kwa Kiingereza dhana hii inaitwa " The supremacy of the constitution" yaani hakuna aliye juu ya katiba, msimamo wa katiba ndio juu ya kila kitu.
Mbona kuna mambo mengi tu yanakiukwa na katiba ipo kimya? Tatizo ni nini?
 
Ibara ya 64(1) ya katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977, inatoa mamlaka ya kutunga sheria kwa Bunge la JMT
1694160649102.png

Ibara ya 64(5) Katiba inasema
1694160830240.png
Hili lingesimamiwa kikamilifu, tusingekuwa na sheria kandamizi.

Katiba yetu haina wa kuilinda kisawasawa, kusiginwa ni halali.
 
Kitendo tuu cha serikali kupeleka Bungeni muswada wa sheria batili ni kosa, serikali yetu ilipaswa kuadhibiwa!.

Kitendo cha Bunge kutunga sheria batili, Bunge lilipaswa kuadhibiwa!

Swali ni nini kinachofanya mihimili hii yetu mitatu isifanyiane checks and balance?. Hii ni mada inayojitegemea.
Mada kama hii ilisababisha wewe kuitwa Dodoma kuhojiwa baada ya kuuliza ikiwa kuna 'muhimili unajipendekeza'?

Huogopi tena kurudi huko kwa mahojiano ?
 
Back
Top Bottom