Mkuu
lifecoded post yako imenifikirisha sana nafikiri ni wakati sahihi waafrika kuanza kutafuta ukweli nje ya hivi vitabu vya dini maana vina mkanganyiko kidogo kutoka kwenye uhalisia wa mambo. Ila ambacho sielewi ni kwanini sisi waafrica tulioletewa dini ndio tumeishika sana kuliko waliotuletea dini??? Na kipi kitatukomboa kutoka vifungo hivi??
Kuna topic moja mtu aliuliza, kwa mapokeo, tunaambiwa yule Cain mtoto wa Adam, alipofukuzwa Eden, aliondokana kuoa mbali huko.
Sasa kama Adam ndiye mtu wa kwanza, huko mbali alioa nani?
Wataalam wakawa na majibu mawili.
Moja wakasema alioa dada yake. Jibu hili linaelezea habari kwamba Adam na Hawa walikuwa na watoto tofauti.
Lakini halijitoshelezi, tunaambiwa Adam na Hawa na uzao wao walikuwa Eden, kama walikuwa na watoto wao kabla ya Cain kufukuzwa, hao wangekuwa Eden nao.
Hao watoto wao waliofika nje ya Eden bila kufukuzwa walikuwa nani? Walifakaje huko? Mbona habari zao za kufika huko hazikuandikwa?
Kukatolewa jibu la pili, la kisomi zaidi kuliko kimapokeo. Wanasosholojia wanasema kwamba waandishi wa Kiyahudi wameandika mambo kingano zaidi ya ukweli. Kwamba si ajabu kwa watu wa kabila moja, wanapoandika hadithi za mwanzo wa kabila lao, kuandika mwanzo wa kabila lao kama mwanzo wa watu wote, na si ajabu, katika enzi hizo, watu waliokaa pamoja waliwahesabu watu wengine wa mbali nao kwamba si watu kamili.
Kwa hivyo, kulikuwapo na watu kablaya Adam wanaishi sehemu nyingine mbaona uzao wa Adam, ila watu wa uzao wa Adam haukuwahesabu hawa watu kama watu kamili, na Cain alivyofukuzwa Eden akaenda kuoahuko.
Hili jibu la pili lilinifanya niseme kwamba, hizindizohabari ninazosema mara kwa mara hapa.
Kwamba, hivi vitabu ni mythologies, si fact, watu wengi wanavisoma kama fact.
Habari yenyewe imeandikwa kirefu zaidi hapa
Who Was the Wife of Cain? - Biblical Archaeology Society