Je, huu ni ukweli uliofichwa kwa miaka mingi?

Mwanzo 4:1
1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA
Kuielewa Biblia inahitaji kuwa na Roho Mtakatifu na Kuwa na imani kubwa sana, Kwanza Hapa wenye imani dhaifu umewayumbisha zaidi.. Biblia haisemi hivi hata kidogo ila hii ni tafsiri yako Potofu.. kwa Kiingereza Biblia inasema Adam made love to his wife Eve, and she became pregnant and gave birth to Cain.
She said, “With the help of the Lord I have brought forth a man.”

Hapa Chini ni Maneno ya Mstari Huo Huo Kwa Lugha ya Kiebrania ambayo Ndio Biblia imeandikwa nayo..Tafsiri yake kwa Kiingereza..

capturety-jpg.828635

Hakuna Mahali Biblia imeonesha Kama anavyosema mtoa Mada..
Kitu Kibaya sana nilichogudua watu Hupenda sana Kuamini Conspiracies Kuliko Ukweli..Hauwezi kumaliza list za conspiracies zipo nyingii Mno.. hasa kwenye haya Maswala ya imani ambayo sayansi Haiwezi Kuprove..Believe the Bible its Right.. it has No Contradiction..
Architectus
 
Adam aligundua alama au tofauti gani iliyopelekea Hawa kupata mimba? Kumbuka mimba inatajwa baada ya Adam kumjua (Kugundua tofauti) Hawa. Unaweza kuelezea kidogo uhusika wa Adam kwenye ujauzito wa Cain?
Alama yaani aligundua hawa ana mimba ya Cain..... Adam alitambua tu Hawa ana mimba basi ila zaidi ya hapo hakumpa manii yeyote na ndio maana nmeweka hapo mstari unaoonyesha seth ndio alikuwa na mfanano wa Seth na pia Hata agano jipya halimtambui Cain kama mtoto wa ADAM.
 
Kuielewa Biblia inahitaji kuwa na Roho Mtakatifu na Kuwa na imani kubwa sana, Kwanza Hapa wenye imani dhaifu umewayumbisha zaidi.. Biblia haisemi hivi hata kidogo ila hii ni tafsiri yako Potofu.. kwa Kiingereza Biblia inasema Adam made love to his wife Eve, and she became pregnant and gave birth to Cain.
She said, “With the help of the Lord I have brought forth a man.”

Hapa Chini ni Maneno ya Mstari Huo Huo Kwa Lugha ya Kiebrania ambayo Ndio Biblia imeandikwa nayo..Tafsiri yake kwa Kiingereza..

capturety-jpg.828635

Hakuna Mahali Biblia imeonesha Kama anavyosema mtoa Mada..
Kitu Kibaya sana nilichogudua watu Hupenda sana Kuamini Conspiracies Kuliko Ukweli..Hauwezi kumaliza list za conspiracies zipo nyingii Mno.. hasa kwenye haya Maswala ya imani ambayo sayansi Haiwezi Kuprove..Believe the Bible its Right.. it has No Contradiction..
Architectus
Mkuu nimeweka hapo tafsiri ya YADA na ETH kayatafute maana yake pia katafute biblia ya NEW JERUSALEM TRANSLATION inasema hivo hivo kama navyodai humu so mimi sijatunga chochote nmetoa kwenye hizo source nlizoziweka hapo. Unless NJT bible huitambui
 
Alama yaani aligundua hawa ana mimba ya Cain..... Adam alitambua tu Hawa ana mimba basi ila zaidi ya hapo hakumpa manii yeyote na ndio maana nmeweka hapo mstari unaoonyesha seth ndio alikuwa na mfanano wa Seth na pia Hata agano jipya halimtambui Cain kama mtoto wa ADAM.

Tukienda kwa muktadha wa kiuandishi, unafaham imeandikwa Kaini akamjua mkewe akamzaa Henoko..Mwanzo 4:17, hiyo unaielezeaje mkuu? Henoko hakua mtoto wa Kaini?
 
Natamani nijifunze na nijue zaidi ILA NAOGOPA ku-corrupt my mind na maandiko haya mengine ya ziada. Biblia jinsi ilivyo iwe ni summary of summary ya kile kilichotokea, basi yanitosha.

Wengine karibuni kwa mada
Bible nimeweka hapo mkuu haimtambui CAIN kama uzao za Adam

Pia biblia hyo hyo inasema kupitia NJT version kwamba Hawa alimtoa mtoto kutoka malaika wa Bwana na sio kwenye kiuno chake.

Labda tuanzie hapa mkuu je unakubaliana na quote hizi za biblia???
 
Mkuu baada ya Eva kula tunda alimpa na Adam akala,kama tunda hilo ni ngono au kuzini(kama unavyodai) je Adam alifanya kosa gani kwa kufanya ngono na Eva wakati alikuwa kapewa ruhusa ya kufanya hivyo na Muumba?
Hapana hyo hadithi ya TUNDA ni ngono haipo kwenye biblia hiyo imetoka kwenye vitabu vya kiyahudi niliyoquote hapo juu ambavyo havionyeshi Mungu alitoa hyo ruhusa ila kinaeleza hyo story ambayo inadai hawakuwa na ufahamu mambo ya ngono maana wangezaliana ila baada ya shetani kumwambia Hawa kwamba ukilala na mwanaume utazaa mtoto yaani utakuwa na uwezo wa kuumba mwanadamu kama Mungu ndio akabeba mimba ya Cain na ilipelekea Mungu kukasirishwa na kuwaadhibu.

Ila kuhusu ngono ya Nyoka na Hawa irrespective kama tunda ni ngono au Lah ndio nmeweka hyo mistari ya biblia

Ni vitu viwili tofauti mkuu
 
The Africans gave us the concept against murder. When the Shipwats at the Temple of Philos, a Greek word, which means Angelica, by the way, of the Goddess Auset, which the Greeks called Isis, and her son Heru, who the Greeks called Horus, and all the gods viewed the murder of Osiris by his brother Seth. A murder that preceded the Cain and Abel murder by thousands of years.
 
mpendwa zitto junior uzi wako fikirishi sana hasa unapotoka nje ya bible na kuna moja ya kitu umekielezea ambacho ni moja ya sababu iliopelekea kutokukubalika kwa baadhi ya vitabu hasa vya agano la kale (kutokukidhi canon ya palestina,kwa biblia ya kiebrania na canon ya aleksandria, kwa septuangita)

pia inazusha swali kwamba ni kwa nini vitabu vingine viliachwa havikujumuishwa ktk biblia ???
 
Tukienda kwa muktadha wa kiuandishi, unafaham imeandikwa Kaini akamjua mkewe akamzaa Henoko..Mwanzo 4:17, hiyo unaielezeaje mkuu? Henoko hakua mtoto wa Kaini?
Hata kama tutasema basi kumjua ina maana moja tu ila bado kwenye issue ya Adam na Hawa biblia inasema kupitia NJT kwamba alitokana na MALAIKA ila kwenye uzao wa Henoko sikuona Cain akisema HENOKO katoka kwa malaika sijui tofauti unaiona hapo mkuu
 
Mkuu zitto junior asante kwa kunikaribisha katika uzi wako mwingine tena. Lakini nitaandika kwa kifupi tu, ni hivi; hoja hiyo ya kusema eti lile halikuwa "tunda la mtini" bali lilikuwa ni tendo la ndoa mimi binafsi nakataa hasa kutokana na NENO la MUNGU halidanganyi. WARUMI 3:4 "MUNGU ajulikane kuwa mkweli na wanadamu wote waongo"..... Pia soma ZABURI 116:11

Kwa kuwa MUNGU siyo muongo na Musa alikiandika kitabu cha MWANZO kwa kuambiwa na MUNGU mambo yote yaliyotukia, hivyo yote yaliyoandikwa kwenye BIBLIA ni KWELI tupu pasipo shaka yoyote ile!

Ili tujue kwamba lile lilikuwa ni tunda la mti kweli na siyo vinginevyo hebu soma MWANZO 3:6 .."mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho nao ni mti wa kutamaniwa kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala".

Nime-highlight hayo maneno hapo juu kwa rangi nyekundu ili tuyajadili na kupata majibu...."ule mti wafaa kwa chakula"... sentensi hii inatosha kabisa kutonesha kuwa ule ulikuwa ni mti wa matunda kama miti mingine ndiyo maana Eva aliona unafaa kwa chakula. Kama tunda lingekuwa ni "uchi" wa Eva au "uchi" wa Nyoka, Je! uchi unafaa kwa chakula? Au tendo la ngono linafaa kwa chakula?

...."basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala"...hapa tunaona wazi kabisa ni kitu alikula kwa kutumia mdomo wake, maana baada ya kula alimpatia na mumewe naye akala. Je! kama tunda lingekuwa ngono angewezaje kula "uchi" wake na kumpa mumewe naye ale?

Kuna watu watabisha na kusema; "oooh, hiyo ni lugha tu ilitumika kuficha ukweli". Mimi nasema hapana, kama kitendo cha ngono kingefanyika basi BWANA MUNGU angesema kuwa ni ngono ilifanyika wala asingeficha ukweli. Ngono ilipofanyika kati ya malaika waasi na wanadamu BWANA MUNGU hakuficha bali alisema wazi;

Baadhi ya Malaika walipoacha viti vyao Mbinguni na kuja duniani kufanya ngono na binti za wanadamu, BWANA MUNGU alisema bila kificho, MWANZO 6:1-2 ..".........Wana wa MUNGU waliwaona hao binti za Wanadamu ya kuwa ni wazuri, wakajitwalia wake wowote waliowachagua". Tukubali tu kuwa MUNGU haufichi UKWELI.

Sasa hebu ona ushahidi mwingine kutoka kwenye Biblia kuwa lile lilikuwa ni tunda la mti na siyo tendo la ngono. Soma MWANZO 3:22-24 ... "BWANA MUNGU akasema basi huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya, na sasa asije akanyoosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima akala akaishi milele................akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga wa moto uliogeuka huko na huko kuilinda njia ya mti wa uzima".

Baada ya Adamu na Eva kula matunda ya mema na mabaya, kulikuwa na mti mwingine wenye matunda ya Uzima, ambao sasa ikabidi BWANA MUNGU auwekee ulinzi ili Adamu na Eva wasije wakaenda na kunyoosha mikono yao na kuchuma matunda yake na kula. Kwa mistari hii tunaona UKWELI ni upi na uongo ni upi. MUNGU hasemi UONGO hata siku moja, wala Biblia haijadanganya wala kuuficha UKWELI.

Shetani ni mjanja sana na anatumia ujanja wake kuwadanganya na kuwarubuni Wanadamu ili waone kuwa MUUMBA wao ni muongo. Lengo la Shetani ni kutuaminisha kuwa MUNGU ni muongo na alitumia ujanja huo huo kumfanya Eva amuone MUNGU ni muongo. Shetani amewasaidia Wanadamu kuandika vitabu vingi sana vyenye maudhui ya kupingana na Biblia ili tu kuwafanya wanadamu wamuone MUNGU ni muongo.

Vitabu hivi vyenye maudhui ya kudanganya vipo vingi sana na viliandikwa miaka mingi sana nyuma, enzi za mfalme Nimrodi wa Babeli ya kwanza kabisa. Hapa ndipo palipokuwa chimbuko la dini zote za KIPAGANI na maandiko yenye kupotosha.
 
mpendwa zitto junior uzi wako fikirishi sana hasa unapotoka nje ya bible na kuna moja ya kitu umekielezea ambacho ni moja ya sababu iliopelekea kutokukubalika kwa baadhi ya vitabu hasa vya agano la kale (kutokukidhi canon ya palestina,kwa biblia ya kiebrania na canon ya aleksandria, kwa septuangita)

pia inazusha swali kwamba ni kwa nini vitabu vingine viliachwa havikujumuishwa ktk biblia ???
Mkuu nimefurahi sana kuona umekuja kwenye nyuzi yangu hii maana siku hizi hupatikani kabisa.... Bila shaka uzi utakaofuata utazungumzia hoja uliyotaja hapo juu ili mje mtiririke na kutuongezea maarifa

Once again ubarikiwe sana kwa kuchangia
 
asante mkuu zitto junior kwa mada nzuri na yenye kufikirisha.
wazo langu nadhani kuendelea kujifunza haya mambo iya kiimani taratibu ili tusipotee moja kwa moja.
kwanza lazima tukubali kwa vyovyote vile alivyo Mungu yupo. na kama Mungu yupo, wapo na walikuwepo na watakuwepo wajumbe wake wakituelezea yanayo muhusu Mungu.
ila siku zote najiuliza na kukosa majibu kwamba kwanini baadhi ya habari za Mungu zimefichwa au zimepotoshwa na hali ya kua M ungu yupo na anaona mbali kuliko mwanadamu awae yote? je ni kwa ridhaa yake? au amekusudia jambo fulani ndio maana akaridhia hivyo?
kwa kua nilikosa jibu la maswali hayo basi nabakiwa na kile nilichofundishwa kwamba Hawa hakuzini na nyoka bali nyoka alimshawishi kula aina ya tunda la mti uliozuiliwa kuliwa matunda yake alipewa adhabu na kwa bahati mbaya mtoto wake wa kwanza alipata laana kutokana na makosa ya mama na baba yake .
 
Asee nipitiwa na huu Uzi ,ahsante mleta Mada kwa huu Uzi...ila mm bado nakua ktk utata hasa wa kile tutakacho kukifahamu ...uzuri humu humu JF kuna Mada huwa zinakuja kwa namna ile ile lkn ktk hali tofauti hasa linapokuja suala la hapo 'mwanzo' juu ya uumbaji

Kuna Mada huwa zina mtaja Adam na Eva/Hawa moja kwa moja na zingine zikimtaja Adam na 'so called' Lilith

Lakini pia kuna hizi zinamtaja Hawa /Eva na huyu nyoka , uzuri au ubaya ni zote zinalenga kumjua nani ni nani

Binafsi bado najiFUNZA zaidi toka kwa wajuzi wa humu JF ,tuko pamoja ,nafuatilia mjadala
 
Mkuu Son of Gamba nashkuru kwa nondo zako zilizoshiba nimekuelewa sana ila labda tungeeleweshana haya yafuatayo
1. Kwanini Biblia haimtambui Cain kwenye kitabu cha Yuda hadi kusema Henoko alikuwa mtu wa 7 na sio wa 8???

2. Kwanini hiyo biblia ya NJT inatafsiri tofauti kuwa Cain alitokana na MALAIKA na sio ADAM je biblia hii inakubalika duniani kote na wwe unaikubali au huikubali???

3. Kitabu cha apocalypse of Moses kinatumika na baadhi ya madehebu duniani kama mormons etc na kinatambua kuwa Lucifer alilala na nyoka je msimamo wako ni upi kuhusu kitabu hiki??

4. Je kwanni biblia inasema seth alikuwa na sura na mfano wa Adam ila haisemi hivyo kwa Cain

5. Kwanini adhabu zote za Hawa ziwe kwenye masuala ya ngono na sio masuala mengine

Tuanzie hapo mkuu, i appreciate your presence
 
Kuna topic moja mtu aliuliza, kwa mapokeo, tunaambiwa yule Cain mtotowa Adam, alipofukuzwa Eden, aliondokana kuoa mbalihuko.

Sasa kama Adamndiye mtu wa kwanza, huko mbali alioa nani?

Wataalam wakawa na majibu mawili.

Moja wakasema alioa dada yake. Jibu hili linaelezea habari kwamba Adamna Hawa walikuwa na watoto tofauti.

Lakini halijitoshelezi, tunaambiwa Adamna Hawa na uzao wao walikuwa Eden, kama walikuwa na watoto wao kabla ya Cain kufukuzwa, hao wangekuwa Eden nao.

Hao watoto wao waliofika nje ya Eden bila kufukuzwa walikuwa nani? Wlaifikaje huko? Mbona habari zao za kufika huko hazikuandikwa?

Kukatolewa jibu la pili, la kisomi zaidi kuliko kimapokeo. Wanasosholojia wanasemakwamba waandishi wa Kiyahudiwameandika mambo kingano zaidi ya ukweli. Kwamba si ajabu kwa watu wa kabila moja, wanapoandika hadithi za mwanzo wa kabila lao, kuandika mwanzo wa kabila lao kama mwanzo wa watu wote, na si ajabu, katika enzi hizo, watu waliokaa pamoja waliwahesabu watu wengine wa mbali nao kwamba si watu kamili.

Kwa hivyo, kulikuwapo na watu kablaya Adam wanaishi sehemu nyingine mbaona uzao wa Adam, ila watu wa uzao wa Adam haukuwahesabu hawa watu kama watu kamili, na Cain alivyofukuzwa Eden akaenda kuoahuko.

Hili jibu la pili lilinifanya niseme kwamba, hizindizohabari ninazosema mara kwa mara hapa.

Kwamba, hivi vitabu ni mythologies, si fact, watu wengi wanavisoma kama fact.

Habari yenyewe imeandikwa kirefu zaidi hapa

https://www.biblicalarchaeology.org/daily/biblical-topics/hebrew-bible/who-was-the-wife-of-cain/
mpendwa kwanza kabisa napenda kukushauri kidogo jinsi ya kuisoma Biblia Takatifu.

Biblia Takatifu ikisomwa kwa kunyofoa nyofoa vifungu fulani bila kuhusianishwa na vifungu vingine au ikisomwa kwa kukatishwa katishwa, labda juu ya simulizi fulani, unaweza kuibuka na maswali mengi na hata kufikia kwenye utata usio wa lazima.

Kwa mfano hivo mistari vichahe ulivovisoma ndugu yangu na kukuzushia hayo maswali jibu lake lipo sura ya tano aya zile tano za mwanzo kabisa, ungeweza kugundua kuwa Adamu na Eva hawakuwazaa watoto hao watatu tu unaowafahamu wewe, yaani Kaini, Abeli(Habili) na Sethi.

Sura hiyo ya tano angalau aya za mwanzoni zinaonyesha bayana kuwa Adamu na Eva walizaa watoto wengi wa kiume na kike.

Ninanukuu sehemu hiyo ya Biblia:

"hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku zile mungu alipoumba mtu, kwa sura ya mungu alimfanya; mwanamume na mwanamke aliwaumba,akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa. Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi. Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana waume kwa wake. Mwisho wa kunukuu, kitabu cha Mwanzo 5:1-4.
 
asante mkuu zitto junior kwa mada nzuri na yenye kufikirisha.
wazo langu nadhani kuendelea kujifunza haya mambo iya kiimani taratibu ili tusipotee moja kwa moja.
kwanza lazima tukubali kwa vyovyote vile alivyo Mungu yupo. na kama Mungu yupo, wapo na walikuwepo na watakuwepo wajumbe wake wakituelezea yanayo muhusu Mungu.
ila siku zote najiuliza na kukosa majibu kwamba kwanini baadhi ya habari za Mungu zimefichwa au zimepotoshwa na hali ya kua M ungu yupo na anaona mbali kuliko mwanadamu awae yote? je ni kwa ridhaa yake? au amekusudia jambo fulani ndio maana akaridhia hivyo?
kwa kua nilikosa jibu la maswali hayo basi nabakiwa na kile nilichofundishwa kwamba Hawa hakuzini na nyoka bali nyoka alimshawishi kula aina ya tunda la mti uliozuiliwa kuliwa matunda yake alipewa adhabu na kwa bahati mbaya mtoto wake wa kwanza alipata laana kutokana na makosa ya mama na baba yake .
Mkuu kuhusu hilo swali lako nafkiri Biblia ilishasema watatokea manabii wa uongo hivyo sio kila tukisomacho, tukionacho na kukisikia ni ukweli hivyo ni heri tushike imani kuliko KITABU!! Mfano ukisoma biblia kuna incosistence nyingi ambayo labda ni makosa ya waandishi tu lakini unajiuliza kwanni Mungu ameruhusu watu wafanye makosa kwenye kitabu kinachoshikilia imani ya ukristo mifano iko mingi na inastahili uzi wake hivyo jibu ni kwamba Mungu karuhusu ila inatakiwa kabla hatujasoma mstari wowote basi tumuombe Mungu atufunulie tafsiri sahihi ya maandiko

Tukirudi kwenye mada niliyochokoza nachojiuliza kama hakukuwa na ngono kati ya nyoka na hawa kwanini haya masuala yanaibuka

1. Kwanini Biblia haimtambui Cain kwenye kitabu cha Yuda hadi kusema Henoko alikuwa mtu wa 7 na sio wa 8???

2. Kwanini hiyo biblia ya NJT inatafsiri tofauti kuwa Cain alitokana na MALAIKA na sio ADAM je biblia hii inakubalika duniani kote na wwe unaikubali au huikubali???

3. Kitabu cha apocalypse of Moses kinatumika na baadhi ya madehebu duniani kama mormons etc na kinatambua kuwa Lucifer alilala na nyoka je msimamo wako ni upi kuhusu kitabu hiki??

4. Je kwanni biblia inasema seth alikuwa na sura na mfano wa Adam ila haisemi hivyo kwa Cain

5. Kwanini adhabu zote za Hawa ziwe kwenye masuala ya ngono na sio masuala mengine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom