Je, hii inawezekana kwa mtu kuwa msambazaji wa gesi ya kupikia (LPG - Liquefied Petroleum Gas) mitaani kwa njia ya Bomba !?..

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,339
Reaction score
1,493
Habari Tanzania !..

Habari yako EWURA, TRA, TPDC, mko poa !?..

Naomba kuwauliza na nyie wadau; eti naweza kupata kibali cha kuwa muuzaji wa Gesi kwa kutumia mfumo wa usambazaji wa gesi ya kupikia (LPG - Liquefied Petroleum Gas) mitaani kwa njia ya mabomba kuelekea majumbani (Piped Gas System).

Natamani kuwa muwekezaji kijana hapa Bongo maana hii njia wananchi mtaweza kununua Gesi kwa Tsh.5,000/= kwa mwezi. Au nyinyi mnasemaje wananchi !?.

Faida za Mfumo wa Mabomba Mitaani
1. Gharama nafuu: Kununua gesi kwa wingi (bulk) kwenye tanki kubwa ni rahisi kuliko kununua mitungi midogo midogo. Hapa wateja mtafurahia huduma vizuri.

2. Urahisi: Huna haja ya kubeba mtungi kwenda kujaza; gesi inapatikana saa 24 kama maji ya bomba. Yaani ni mwendo wa kulipia kwa simu au Bank mambo yanakuwa mepesi.

3. Nafasi: Huokoa nafasi jikoni kwani huna haja ya kuwa na mtungi ndani ya nyumba. Sasa hii kwanini uingie magharama makubwa ya mafenicha mara machuma kisa upate gesi. Oya nipeni moto niwe mwekezaji chaap kwa haraka.

Karibu kwa maoni yako. Nitazingatia kila hatua; lazima mnunue Gesi chini ya buku tano (Tsh.5,000/=).

NB
Jamani kwasasa mitungi ya gesi imekuwa kama uchafu hivi. Na haifanyi mazingira yetu yavutie mwe.
 
Hao wamelala usingizi wa pono mpaka wapate maelekezo kutoka mawinguni.
 
LNG (methane) inawezekana ila Lpg ngoja wataalamu waje
Inawezekana Kaka. Japo njia za bomba hasa gesi zinataka utaalamu; ila zinawezekana. Serikali waniite tukae chini tufanye biashara tufanye PPP (Wao wajenge tank na mipira; mimi na wanangu tuwauzie wananchi huduma). Mbona easy sana.
 
Kwa mtaji wa 2.5m mtu ashindwe huu uwekezaji; mpaka ajipeleke huko kwenye makuku buraza !?.
Bila shaka umesoma masomo ya sanaa ,,hujui kuhusu survey hujui kuhusu project management,hujui kuhusu safety,hujui kuhusu investment..pole sio kosa lako..hio 2.5 bet,kunywa bia,n.k
 
Wazo zuri sana Mkuu, ila sio rahisi wewe kupewa hicho kibali

Hivi si unajua kitendo cha wewe kupewa kibali cha kuwa msambazaji wa gesi kupitia mfumo wa mabomba kuna watu utakuwa unawaharibia biashara

Fikiria Oryx gas, Taifa Gas, Mihan n.k watapeleka wapi hiyo mitungi yao waliyoijaza nchini?

Changamoto ya Nchi yetu ni kuwa na Viongozi wafanya biashara wakiwa na hisa kwenye makampuni makubwa ya Mawasiliano , Nishati, Kilimo n.k

Kwahiyo hawataki kutoa nafuu kwa Wananchi wao zaidi ya kulenga faida zao binafsi

Kumbuka suala la Mkongo wa Taifa, hivi Serikali wangekuwa serious wananchi wangekosa internet ya bei nafuu kweli wakati asilimia 90 Mkongo wa Taifa umefika kila mahali

Kwanini, unakuta Viongozi wana hisa kwenye makampuni mengine ya mawasiliano ya airtel, Voda, Yas n,k ambao wanaendelea kuwanyonya raia wao kwa kuwauzia vifurushi vya Data kwa gharama kubwa
 
Liquefied Natural Gas ambayo inachakatwa Songosongo Lindi Pia Madimba mtwara Ambayo zinakutana Somangafungu nakuunda pipe moja Ambayo inaleta moja kwa moja gesi Hadi hapo kinyerezi.
Sasa hivi watu wengi wanaunganishiwa moja kwa moja Majumbani kwa gharama Nafuu.
Kutoka kinyerezi kuna pipeline ya inches 6 ambayo imeenda Mpaka Tegeta.
Mteja mkuu sasa Hivi ni Tanesco, Dangote, Twiga cement. Pia kuna kituo kikubwa tumeweka mlimani city cha kujaza gesi kwenye Magari. Hii miaka miwili kwa hapa Dar es salaam wateja wataongezeka maradufu maana nikama watanzania wanatoka kwenye usingizi wa pono sii tu majumbani hata kwenye vyombo vya usafiri.
Kikubwa safety inazingatiwa maana ni deadly high pressure ikitokea makosa kama leakages inakuwa hatari.
Ni ngumu kwa mtu kukabidhiwa hiyo kwa sababu ni ngumu kucomplay na standard za usambazaji.
Just imagine unaoperate around 50 bar halafu ajali itokee utatengeneza disaster kubwa hatari.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Bila shaka umesoma masomo ya sanaa ,,hujui kuhusu survey hujui kuhusu project management,hujui kuhusu safety,hujui kuhusu investment..pole sio kosa lako..hio 2.5 bet,kunywa bia,n.k
Umenipima kwa njia ipi rafiki !?. Mpaka ukahisi mimi ni nimesomea sanaa !?..
 
ile gesi ya mtwara mngetusaidia kutuleza imefikia wapi mapaka sasa, maana tuliambiwa kuna nyumba chache wananchi wameungiwa kutumia, maendeleo yapoje na gharama zipoje?
 
Liquefied Natural Gas ambayo inachakatwa Songosongo Lindi Pia Madimba mtwara Ambayo zinakutana Somangafungu nakuunda pipe moja Ambayo inaleta moja kwa moja gesi Hadi hapo kinyerezi.
Sasa hivi watu wengi wanaunganishiwa moja kwa moja Majumbani kwa gharama Nafuu.
Kutoka kinyerezi kuna pipeline ya inches 6 ambayo imeenda Mpaka Tegeta.
Mteja mkuu sasa Hivi ni Tanesco, Dangote, Twiga cement. Pia kuna kituo kikubwa tumeweka mlimani city cha kujaza gesi kwenye Magari. Hii miaka miwili kwa hapa Dar es salaam wateja wataongezeka maradufu maana nikama watanzania wanatoka kwenye usingizi wa pono sii tu majumbani hata kwenye vyombo vya usafiri.
Kikubwa safety inazingatiwa maana ni deadly high pressure ikitokea makosa kama leakages inakuwa hatari.
Ni ngumu kwa mtu kukabidhiwa hiyo kwa sababu ni ngumu kucomplay na standard za usambazaji.
Just imagine unaoperate around 50 bar halafu ajali itokee utatengeneza disaster kubwa hatari.
Sorry !
Hiyo uliyoisema ni Natural Gas na sio mfanano na gesi unayoitumia sasa wewe nyumbani kumbuka hilo.
 
Sasa ebu tuwe realistic wewe unazungumzia propane Ambayo ndio hiyo Liquified Petroleum Gas utakuwa unaitoa wapi?
 
Hiyo ni usd au hata kama ingekuwa usd bado huwezi fanya kitu chochote
Brother, hapa nazungumzia supply sio hizo mbaga nyingine ndio maana nikasema panakuwa na PPP (Public Private Partnership). Ukumbuke Serikali ndio mjenzi wa miundombinu ya Gas sababu ana interest na umma moja kwa moja upo.

Kwani hiyo Gesi hapo nyumbani wanaokuuzia wana mitaji ya US Dollar ($) ngapi mangi !?.
 
ile gesi ya mtwara mngetusaidia kutuleza imefikia wapi mapaka sasa, maana tuliambiwa kuna nyumba chache wananchi wameungiwa kutumia, maendeleo yapoje na gharama zipoje?
Achana nayo. Mimi nimezungumzia Gesi hii hii ambayo wewe unaitumia sasa hapo nyumbani inafanyiwa mabadiliko kiusafirishaji badala ya kuwa kwenye tank dogo kama sasa; inakuwa mpira sasa shida ipo wapi wapendwa !?.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Habari Tanzania !..

Habari yako EWURA, TRA, TPDC, mko poa !?..

Naomba kuwauliza na nyie wadau; eti naweza kupata kibali cha kuwa muuzaji wa Gesi kwa kutumia mfumo wa usambazaji wa gesi ya kupikia (LPG - Liquefied Petroleum Gas) mitaani kwa njia ya mabomba kuelekea majumbani (Piped Gas System).

Natamani kuwa muwekezaji kijana hapa Bongo maana hii njia wananchi mtaweza kununua Gesi kwa Tsh.5,000/= kwa mwezi. Au nyinyi mnasemaje wananchi !?.

Faida za Mfumo wa Mabomba Mitaani
1. Gharama nafuu: Kununua gesi kwa wingi (bulk) kwenye tanki kubwa ni rahisi kuliko kununua mitungi midogo midogo. Hapa wateja mtafurahia huduma vizuri.

2. Urahisi: Huna haja ya kubeba mtungi kwenda kujaza; gesi inapatikana saa 24 kama maji ya bomba. Yaani ni mwendo wa kulipia kwa simu au Bank mambo yanakuwa mepesi.

3. Nafasi: Huokoa nafasi jikoni kwani huna haja ya kuwa na mtungi ndani ya nyumba. Sasa hii kwanini uingie magharama makubwa ya mafenicha mara machuma kisa upate gesi. Oya nipeni moto niwe mwekezaji chaap kwa haraka.

Karibu kwa maoni yako. Nitazingatia kila hatua; lazima mnunue Gesi chini ya buku tano (Tsh.5,000/=).

NB
Jamani kwasasa mitungi ya gesi imekuwa kama uchafu hivi. Na haifanyi mazingira yetu yavutie mwe.
?
 
Back
Top Bottom